JINSI ROHO YA YEZEBELI (roho chafu) INAVYOBOMOA KANISA, WATUMISHI, WATEULE NA WATOTO WA MUNGU
Somo: *jinsi roho ya yezebeli inavyobomoa kanisa, watakatifu, watumishi na wateule wa Mungu kwa siri*
#. Kuna masomo si rahisi kuyaongea mbele za watu unatamani ungemfundisha mtu binafsi basi.
#.Somo hili la kipekee sababu nitaenda ongea mambo ya ndani sana, mengine ni siri za mtu kati ya yeye na moyo wake.
#.Nataka tujue hakuna kilichojificha mbele ya Roho Mtakatifu
#.Somo hili kama si wewe basi ninahakika siku moja utamsaidia mtu mwingine aliye kwenye kifungo.
Halleluyaaaah!
#. ROHO MTAKATIFU ANISAIDIE KUNENA KWA UJASIRI WOTE.
#. ROHO MTAKATIFU AKUSAIDIE KUELEWA KWA UNDANI WOTE.
#.BAADA YA KUELEWA ROHO MTAKATIFU AKUPE NGUVU NA UJASIRI WA KUFUNDISHA WENGINE
#.SIWEZI FIKIA KILA MTU LAKINI NAAMINI KWA WEWE KUELEWA NA KUFUNGULIWA MACHO BASI KUNA WATU 100 YAKO WATAFUNGULIWA KUPITIA WEWE.
Halleluyaaaah
Bwana Yesu asifiwe. Neno la Mungu linasema watu wangu wanangamizwa kwa kukosa maarifa.
Hosea 4
6 Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
Shetani anapinga na maarifa! Stephano aliuwawa sababu ya maarifa Mungu aliyoweka ndani yake, hakuuwawa kwa ajili ya upako, no! aliuwawa sababu ya maarifa ya miungu, anachopingana nacho shetani ni
maarifa ya Mungu, kama unafikiri shetani haogopi upako, kumbuka yeye mwenyewe alikuwa mbinguni kabla ya kukosa adabu, kutupwa kuzimu, shetani anaogopa upako utokanao maarifa Halleluyaaaah. kwanini ya
leo tuangalie roho ya yezebeli? ni sababu ndio roho inayohusika
i.kuangusha watumishi kupitia uzinzi na uasherati. ukiona hayo basi ujue yezebeli yupo nyuma yake.
ii.ukisikia watu wanajichua (masterblation) iyo ni roho ya yezebeli nyuma yake.
iii.ukiona mawazo ya watu yamechafuka siku hizi hata ndani ya kanisa mtu anawaza uchafu basi jua nyuma yake yupo yezebeli.
iv.ukisikia roho ya kusagana (lesbian spirit) uyo ni yezebeli.
iv.ukiona mtumishi anatembea na waumini wake bila hata hofu ya Mungu.jua yezebeli yupo nyuma yake.
v.ukiona mtu anangalia video chafu (pornography) anajaribu kuacha anashindwa, jua yezebeli yupo nyuma yake.
vii.roho ya matamanio kupita kiasi (spirit of lust) jua yezebeli yupo nyuma yake.
Halleluyaaaah, Bwana Yesu asifiwe. niliwahi pata email wako wapendwa walikuwa wakilalamika na kutaka ushauri wakisema, mtumishi naomba unisaidie maana ndoa yangu inapelekea kubaya nimeshaomba
hata nimemaliza, kila kitu sijapata mpenyo, anasema shida yangu mimi kubwa ni mme wangu, mme wangu anatabia ya ajabu na ni kama hawezi kuacha, nikamuuliza ana tabia gani?, akaniambia mme wangu anafanya
masterblation kaadhirika mpaka hawezi anashindwa tendo cha ndoa, samahani kwa lugha ya leo, nisiposema ukweli na waziwazi kanisa tutaanguka ngoja nifundishe waziwazi ili Mungu atusaidie na roho hii ni
mbaya sana, mwisho wa somo hili utajua kwanini tumefundisha mambo ya ndani hivi, Halleluyaaaah Bwana Yesu asifiwe, mmoja wa wale wanaolalamila alikuwa ni mke wa mchungaji, akaniambia mtumishi ajabu yeye
anafungua watu ila yeye anashindwa kujifungua. nikamwambia anahitaji neema ya Mungu, ndipo ikabidi nifunge na kuomba kumuomba Roho Mtakatifu anifundishe ili niweze kuomba, nimepitishwa sehemu
nyingi na Roho Mtakatifu ili kuelewa vizuri, Embu tuangalie Yezebeli katika agano la kale.
1 wafalme 18
4 kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji.
☆Yezebeli alihusika kuuwa watumishi wa Mungu. yeye alikuwa anawawinda watumishi wa Mungu ili awanyamazishe, anapambana na watumishi wa Mungu ili awauwe. ili wasieneze injili ya Mungu.
1 Wafalme 19
1 Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga.
2 Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.
☆ Umeona hapa Yezebeli aliitaka roho ya Eliya, alimtishia Eliya kumchinja, Na Eliya alitishika akaamua kukimbia.
1 Wafalme 19
3 Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko.
4 Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.
☆Eliya anajiombea afe sababu ya kutishwa na yezebeli, usishangae kuona watumishi wanatamani kufa, ukiona mtumishi anatamani kufa jua kabisa ni roho ya yezebeli ipo nyuma yake.
yezebeli siku hizi hapigani kimwili tena bali anapigana kiroho, anapambana na fikra zako, kukuingizia fikra chafu, kukuingizia mawazo machafu, ili wewe mwenyewe ufungue mlango. nitazungumzia addiction
of masterblation kifungo kilichowafunga hata watakatifu, utakuta mtu ananena kwa lugha lakini bado ana msukumo wa kufanya masterblation msukumo haujakatika, anafanya maombi yenye mpenyo akitoka
hapo anaingia katika masterblation, anafunga ili aache akimaliza kufunga tuu anarudi kwenye iyo dhambi, ashamuuliza Mungu why this mpaka amechoka, ameombewa na kila mtumishi anafunguliwa
mwezi huu,mwezi unaofuatia yuko palepale. mpaka anafika sehemu anaanza kuwaza labla sijaokoka vizuri, labla upako wa mtumishi haufanyi kazi, labla Yesu ameshindwa, kunifungua pengine sasa upo mbioni na
ameanza kutafuta nauli ili kwenda kwa watumishi duniani huko wenye majina ili akafunguliwe,inawezekana na mafuta, maji, bracelet, kitambaa, umepewa na 3 kavu,
umefunga ,7 kavu umefunga, na siku 14
umefunga ya kawaida, hakuna ambayo hujaacha 14 umefunga, Siku 21 umefunga, siku 40 umefunga, siku 70 umefunga lakini bado ile hali inakata ukiwa rohoni, na upako ukianza kurudi chini, wazo likimjia tuu mtu
hawezi kukataa anajikuta tayari ameingia katika masterblation, inamsumbua mpaka
amefikiria kumwacha Mungu, akijisemesha nimeokoka lakini nafanya uchafu, watu wananieshimu lakini nikiwa chumbani
kwangu, nikiwa mwenyewe namtumikia shetani ameshajaribu kila kitu na sasa
amekata tamaa, amechoka na hiko kifungo Halleluyaaaah, Leo nitakuambia kwanini hufunguliwi pamoja na jitihada zote. leo
kweli itatuweka huru. ukiona mtu yoyote
hafunguliwi kwenye kifungo kama hiki ni sababu amekuwa addicted ni sababu hiko kifungo alifungua mlango yeye mwenyewe aliingia yeye mwenyewe na alipo ingia tuu
roho ya yezebeli, roho chafu ikamfunga
akaingia kwenye agano,kajiingiza kwenye kiapo yeye mwenyewe, kwaiyo amedakwa amekamatwa. lakini alijipeleka yeye mwenyewe, wenye udhaifu wa kufanya
masterblation huwa wana tabia pia ya kuangalia pornography, msukumo wa kufanya masterblation huja baada ya kuangalia pornography (video chafu za uasherati) masterblation ni kitendo cha mtu
kushiriki tendo la ndoa yeye mwenyewe. bila kuwa na jinsia nyingine tofauti, anaweka picha akilini ya jinsia nyingine kisha hujichua, ni kitendo kina madhara makubwa sana na watu wanafikiri ni kawaida,
kimeathiri watu wengi pamoja na watoto wa Mungu, watumishi wa Mungu, wateule wa Mungu, na hii ndo roho ya unabii wa uongo kitabu cha ufunuo inaelezea, roho ya unabii imekaa kwenye mapenzi inahubiri mapenzi,
miziki inahubiri mapenzi, tv zinahuburi mapenzi, vitabu vinahubiri mapenzi, akili za watu zimewekewa sumu ya mapenzi, ndo huwezi kukuta watu wenye rika moja ambao hawamjui Mungu ambao hawana hofu ya
Mungu wamekusanyika pamoja huwezi kosa story za mapenzi, story za ngono, wacha tuongee kweli ili Roho Mtakatifu akutenge na mtandao wa yezebeli uliofunika dunia nzima na mawazo fikra akili za
uasherati na uzinzi tuu, toka asubuhi akili ya mtu inaweza uasherati na uzinzi haina nafasi ya kumtafakari Yesu, haina nafasi ya kulitafakari neno la Mungu. Halleluyaaaaah. wacha tuongee waziwazi na leo fikra zako,
akili yako, mawazo yako yatakombolewa kwa damu ya Yesu, leo yezebeli atakuacha moyo wako. roho ya yezebeli ni roho chafu ya machafu yote uliyowahi kusikia, ukisikia mtu katembea na mama yake uyo ni
yezebeli, ukisilkia baba katembea na mtoto wako iyo ni yezebeli, ukiona kuna uzinzi na uasherati kanisani uyo ni yezebeli, yezebeli anawadanganya wateule, watakatifu,watoto wa Mungu, walokole kuzini,ukiona mtu
mzima anamtamani mtoto wa umri wa kumzaa mara mbili uyo ni yezebeli, roho ya uzinifu, roho ya uasherati, roho chafu za matendo ya sodoma na gomora zimetupwa duniani kuwaangusha watakatifu,
kuwangusha watumishi, kuwangusha wateule, kuwangusha watoto wa Mungu,
Ufunuo 2
22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;
23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
shetani anajua kabisa akishakukamata basi utakuwa unaupako, utakuwa unachemka kiroho lakini ndani yako hakuna kitu, utakuwa unaomba sana lakini ndani yako nguvu za Mungu zimekuacha (ikabodi)
sababu umezini na yezebeli.
1 samweli 4
21 Akamwita mtoto, Ikabodi, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.
roho ya yezebeli haiwezi kuja tuu isipokuwa imepata mlango. ipo milango ambayo roho hii hupita
i.upo mlango wa uchungu
☆kuwa na uchungu moyoni
ii.upo mlango wa kutokusamehe
☆husababisha hasira
iii.upo mlango wa kutokujiamini
☆hasa baada ya mtu kuachwa vibaya, kusalitiwa,mahusiano kuvunjika
iv.Upo mlango wa kutendewa mambo mabaya ya kudhalilishwa
☆mfano kubakwa
v.upo mlango wa upweke
☆ni rahisi shetani kukushawishi kufanya machafu
vi.upo mlango wa kukaa idle,
☆kutokuwa na kazi ya kufanya, wanasema idle mind is devil workshop, usikae bila kazi tafuta shughuli ya ya kufanya hata hapo nyumbani kwako.
vii.zipo roho chafu zinazokufuatilia ili kukuharibu fikra zako (monitoring spirit)
☆kupitia miziki inayohusu love affairs
☆kupitia video zinazohusu love affairs
☆kupitia story zinayohusu love affairs
☆kupitia watu waliokuzunguka
☆kupitia mitego ya kukunasa kwenye uovu
◇kama hutaona basi utasikia kama hutasikia basi utasoma ndo mana tunasema dunia imefunikwa na love affairs dunia imefunikwa na mawazo ya yezebeli, fikra za yezebeli, akili ya yezebeli kila mahali kila
kona si watoto si watu wazima, fikra zao zimeshachafuliwa na kufungwa na mambo
ya mapenzi, na mawazo machafu ya ngono, ndo mana tunakuambia usome biblia kila siku ili kuingiza kitu cha Mungu kila siku. (to renew yourmind) usipofanya hivyo akili yako itadakwa ikishadakwa utajikuta
kwenye mitego ya yezebeli sasa kwa waliokoka ni mbaya sababu ya hofu ya Mungu wanaogopa kuzini na kufanya uasherati ila shetani atatawasukuma kuangalia pornography kisha atawasukuma
kufanya masterblate wakidanganywa na yezebeli kuwa wewe hujafanya dhambi, wewe hujazini, imeandikwa hivi..
Mathayo 5
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
yezebeli asikudanganye, ukiangalia pornography wewe umeshazini tena na mapepo, ukifanya masterblation wewe umeshazini na pepo la ukahaba yezebel.
Ufunuo wa yohana 17
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
umeona hiyo amewekewa mvinyo wamepewa, yani manake hawawezi kufikiria kitu kingine zaidi ya uchafu tuu. Halleluyaaaah, Shetani sasa hafanyi vita vya mwili na watakatifu bali vita vya roho,
anachofanya anachilia nguvu itakayokudaka
kukushawishi mambo machafu ndio maana utaona movies,tamthilia,miziki,picha, video maongezi ya watu yametawaliwa na uchafu,mapepo ya sodoma na gomora
yanazidi kuvuvia watu uovu,katika watu 10 inawezekana watu 2 ni wahanga, tayari wameshaathirika, shetani anachotafuta usipate mda wa kusoma biblia usipate mda wa kuomba, kama ukiomba basi usiwe na
nguvu, Halleluyaah ndio tuna mamillion ya watu wanaofunguliwa leo kesho wamerudi nyuma, kesho hawana tena nguvu za Mungu, utakuta mtumishi kasimama madhabahu lakini amekauka kabisa hana
tena nguvu za Mungu. sababu ya uchafu wanaosikiliza, uchafu wanaousema na kukiri, uchafu wanaosikiliza, na ukiwakumbusha wanakuwa wakali, watakuambia utakatifu ni ndani si nje haya
mavazi hayakuusu, hajui hayo mavazi ndo yanamletea vishawishi vyauzinzi, vishawishi uasherati wa kila aina, ushawishi wa kuangalia pornography, ushawishi wa kutizama masterblation roho ya unabii wa
uongo, roho ya yezebeli inatudanganya, mpaka kanisa, mpaka watakatifu, Mungu atusaidie, yezebeli ametakeover kila mahali kuhakikisha kwamba mawazo machafu yanabaki kwenye moyo wako, yanabaki
kwenye akili yako, yanabaki fikra zako, yanabaki kwenye macho yako, yanabaki kwenye masikio yako ili uwe rahisi kukuvuta kwenye dhambi,ili atakapo kuambia chepuka hutabisha, atakapo kuambia
tembea na mke wa mtu, tembea na mme wa mtu basi hutabisha.shetani hakuwashawishi kwa siku moja. inawezekana aliwashawishi toka utoto wao na sasa ameweka mizizi HALLELUYAAAAH
Bwana Yesu asifiwe, kupitia iyo milango hapo juu shetani atamshawishi angalia pornography kidogo, do masterblation kidogo,na akifanya hivyo biblia inasema anajiangamiza nafsi yake.
Mithali 6
32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Jina la Bwana libarikiwe, kwa iyo tatizo la masterblation limetokana na pepo, si kitu cha kawaida, kama hali iyo inakusumbua basi kaa ukijua si kawaida ni kifungo tena kifungo kibaya sana. Halleluyaaaaaah
Ufunuo 2
18 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika;Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.
19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
☆☆☆
Ufunuo 2
21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, *wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake*
23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. *Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.*
24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, *wasiozijua fumbo za Shetani*, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.
25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja.
hata kanisa la Thiatira liliambiwa lilionywa kuhusu roho ya yezebeli, ni roho ya nabii wa uongo. angalia mstari wa 20 anasema *nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na*
*kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwasanamu.*
,umeona hapo "yule mwanamke yezebeli akiwafundisha na kuwapoteza watumishi
wangu ili wazini", mtu utakuta ameokoka kabisa lakini utakuta anashiriki mambo yote machafu kama ya wakati wa sodoma na gomora, anashiriki uchafu wote, kifungo hiki kipo kwenye nafsi ni kifungo cha ushawahi
mara utasikia kwanini usifanye uchafu, kwanini usijaribu na uchafu huu, wewe unapitwa na wakati, wewe uko nyuma na wakati wenzako wanafanya uchafu huu, wewe unakosa vitu vizuri. ndo mana
anaitwa nabii wa uongo kazi yake ni kushawishi watumishi, wateule, watoto wa Mungu, kazi roho ya yezebeli ni kushawishi umuache Mungu sio moja kwa moja no! kwa mtego ile roho inayokuambia angalia
pornography, inakuambia fanya masterblation, inayokuambia jaribu michezo michafu, jaribu dhambi hii, kwani ukishajaribu si utatubu, Fanya kidogo tuu kisha utatubu, sasa kwa kuwa umekamatwa
nafsi, umekamatwa hisia, umekamatwa utashi, umekamatwa moyo, umekamatwa mawazo, umekamatwa fikra, umekamatwa akili, unajikuta nguvu ya kipepo imekushika unafuata unafanya uasi , na kila ukiombewa
haufunguliwi kwa sababu wewe mwenyewe ulifungua mlango, wewe mwenyewe umeingia kwenye mtego, wewe mwenyewe unashiriki tendo la ndoa na yezebeli mkuu wa pepo wachafu, kwa iyo kutoka hapo
lazima itoke moyoni, ndiyo ubaya wa kifungo hiki, sababu utakuta mwingine huku anatamani aendelee kutenda dhambi, huku anatamani atoke, kwa iyo nguvu mbili zinashindana, ili kutoka lazima toka moyoni
uamue kutoka, kama vile toka moyoni ulivyoamua kuingia. hivi si vifungo vya kusukumiwa uingie, ni vifungo vya kushawishiwa wewe kuingia. ukiona watu wanavaa nusu utupu jua ni roho ya
yezebeli, ukiona watu wanapiga picha za nusu utupu au zinaonyesha maungo yao ya siri jua roho ya yezebeli ipo nyuma yao, ukiona watu wazima kabisa na akili zao tendo la ndoa ambalo ni faragha ya
wanandoa wawili wanajirekodi video jua ni roho ya yezebeli, ukiona watu wanacheza ngoma wanavua nguo hadharani jua ni roho ya yezebeli, ukiona kwenye kitchen party watu wanafundisha michezo michafu iwa
matendo, wengine wanavua nguo iyo ni roho ya yezebeli, vitabu vyote vyenye hadithi za mapenzi iyo ni roho ya yezebeli, shetani anataka ulimwengu wote ufikirie mambo mchafu, uongee macho machafu, uone
mambo machafu, utamke mambo machafu ili Kristro YESU asipate nafasi, kwenye akili za watu, kwenye fikra za watu, kwenye mawazo ya watu. unakuta mtu tokea asubuhi mpaka jioni akili yake inafikiria
mambo machafu matupu. Leo nitakuonyesha madhara ya kufanya masterblation na madhara ya mtu kuangalia pornography au picha chafu au video chafu. ukishajua ukaelewa kama ni mhanga wa
kifungo hicho cha kipepo leo utapata nguvu ya kukataa toka moyoni, yako madhara mengi ila tuangalie machache.
i.kuharibu hali yako kiroho
☆kila mara mtu anapofungua pornography, kila mara anapofanya masterblation, anapoteza nguvu za rohoni, anapoteza upako, anajiingiza katika ulimwengu wa roho wa giza, nafsi yake anakuwa amemkabithi shetani.
ii. Shetani ana muibia , ana mharibu, ana uwa
☆kila mara uyu mtu anapokaribia kupata breakthrough, kupata mpenyo, kupata baraka ndio mda ambao atangalia mambo machafu, atafanya michezo michafu, akifanya hivyo tuu, shetani atapata mpenyo na atamwibia huo ushindi, atauwa huo ushindi, atauharibu huo ushindi
iii.kuharibu mwili wako
☆kurokuridhika na tendo la ndoa (spirit of dog) mpaka u masterblate, unakuwa muhanga wa kutokufurahia tendo la ndoa, sababu ya addictions.
iv.roho ya matamanio kupita kiasi au roho ya uzinifu inakuja kukaa juu yako
☆unaanza kuwa na tamaa kila kilichoko mbele yako, unamfungulia mlango kila aliye mbele yako. unajikuta unafanya vitu unavichukia na umeokoka.
v.inaleta mikwamo kila wakati
☆kuangalia picha chafu, video chafu kunasababisha kukwama kila wakati, huwezi kupiga hatua ni sababu kila mara unapoangalia mambo machafu au unapofanya matendo machafu hata kwa siri, shetani anapata nafsi anakuvuruga unakuwa husogei, ukitaka kusogea anakusukuma kwenye hivyo vifungo unarudi tena nyuma.
vi. masterblation na pornography inauwa kabisa baraka.
☆ni kwa sababu kwa kufanya hivyo unajiunganisha na shetani, ukijiungamanisha na shetani Mungu anakuacha kwa muda mpaka utubu.
vii. Masterblation na pornography inauwa kabisa macho ya rohoni na masikio ya rohoni, sababu moyo wako umeunganishwa na shetani. (yezebeli spirit), masterblation na pornography inauwa uwezo wa kufikiri, inauwa ufahamu wa rohoni na mwilini, inauwa mawazo ya Mungu ndani yako, inauwa utashi wa Mungu ndani yako, inauwa akili ya Mungu ndani yako, inapofusha macho unakuwa huoni tena rohoni, inaondoa hamu ya kusoma biblia, inaondoa hamu ya kusoma, inazuia we kumsikia Mungu na kumtii Mungu.
☆KWA KIFUPI NI UHARIBIFU MTUPU, KUNA VIFUNGO VITAFUNGUKA KWA KUJUA KWELI SI KUOMBEWA TUU, BALI KUPATA MAARIFA YA MUNGU, ULE UONGO UKISHAONDOKA KWENYE MOYO WAKO KWA KWELI YA MUNGU, BASI UNAKUWANA UHURU WA KUSEMA ENOUGH IS ENOUGH I DONT WANT THIS ANYMORE. AND I MEAN IT, UKISHASEMA IVYO SHETANI ANAONDOKA MAANA IMEANDIKWA
Yakobo 4
7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
_NINI CHA KUFANYA KUISHINDA IYO HALI_
1.Kupata ufahamu wa kina kama hivi.
◇Yohana 8
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
2.kuamua kutoka moyoni kutoka kwenye kifungo maana haina afya kiroho wa kimwili ni maangamizo matupu.
◇Mithali 16
1 Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.
3.kusulubisha mwili kwa kufunga kila mara na kuomba.
◇Mathayo : Mlango 17
21 Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.
4.kungoa jicho lako kwenye uovu.
◇Mathayo 5
29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling?oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
5.Kufungulia fikra zako na mawazo yako nuru kwa kusoma neno la Mungu kila siku.
◇Warumi 12
1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
6.Kuomba kila siku kwa Lisaa limoja
◇Mathayo.26
40 Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja.
7.Kuziteka nyara fikra zako, mawazo yako kuweka chini ya jina la Yesu, na kufunga kwa damu ya Yesu kila elimu ijinuayo kinyume na Mungu.
☆Kila upatapo mawazo machafu, ushawishi mchafu funga iyo elimu ya kipepo kwa damu ya Yesu. funga kwenye fikra zako, funga kwenye mawazo yako, funga kwenye akili yako.
2 Wakor 10
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
#BANDIKA MKONO KWENYE KICHWA CHAKO FUNGA KWA DAMU YA YESU, FIKRA NA MAWAZO MACHAFU TOKA KWA yezebeli, kwa kumuambia imeandikwa msomee andiko funga hayo mawazo don't entertain, anakuambia ufanye michezo ya dunia hii kama walimwengu kataa funga hayo mawazo. huanza kidogo kidogo usipoyakemea yanazidi na kusudi mwisho unayafuata, usimpe. shetani nafasi. amua kutoka huko.
#INAWEZEKANA KUTOKA KWENYE KIFUNGO HICHO AMUA TUU TOKA MOYONI.
#KIFUNGO KINAFUNGULIWA KWA DAMU YA YESU
#HAITOSHI TUU KUTUBU NA KUOMBA BALI INGIA KATIKA MAOMBI UHARIBU ROHO IZO CHAFU KWA KUWA UMETAKA TOKA MOYONI MUNGU ATAKUFUNGUA
Muhimu:
Mungu amenipa maono ya kwenda live kupitia radio, na televison, ili masomo haya na maombi tuyapate live, yaani audio na video tutaanza na online radio, online tv, kupitia internet, Pia tutakuwa na live prayer line ya kuhudumia watu, Mungu amesema nami kwa habari ya studio kwa ajili ya huduma iyo. Nikupe nafasi ya kupanda mbegu yako kwa ajili ya studio hiyo. Na Mungu atakukumbuka sadaka yako injili itakapoenda duniani kote. kufungua, kuponya, kuokoa, kuinua. Kama unataka kushiriki baraka hizi uko ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. basi tumia hizo namba hapo chini kutuma sadaka yako. kama uko nje ya Tanzania tumia izo namba nitakupa maelekezo
josephntandu@gmail.com,+255713297066, +255765377506
#WANAMAOMBI GROUP
#MTUMISHI JOSEPH NTANDU
ubarikiwe mtumishi, asante
ReplyDelete