MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
Yoeli : 2 : 25 - Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
Hesabu : 23 : 23 - Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
√Tuangalie tafakari fupi!
Tuangalie hili neno ili uliangalie kwa tafsiri ya ndani au nzito, popote utakapokutana nalo basi upate hasira ya roho Mtakatifu! Tunutu , nzige, madumadu, parapare hawa ni aina ya mapepo katika ulimwengu wa roho! kazi yao kubwa ni kuvujisha au kutoa fuko lako la baraka, kukuchelewesha, usipowadhibiti utakutana nao tuu.
√ Tunashinda katika ulimwengu wa roho si sababu tumeokoka au tunaomba sana tunashinda sababu roho mtakatifu moja kakufungua ukagundua nina tatizo, pili kakupa neno la kufungua ilo tatizo, tatu umeamini na ukaomba kwa bidii. niliwahi kusema biblia ni program ya matatizo yote huku duniani. lakini program hizi zinafungua tatizo by its own program! mfano ufunguo wa sebleni hautafungua jikoni. ingawa bado ni funguo.Halleluyah!
√ Kwann tuangalia mambo ya uchawi correspondence with Tunutu , viwazi, nzige, parare ni sababu hao ndio aina ya mapepo wanaotumwa na wachawi kumrudisha mtu, nyuma shetani ukimpiga ukafanikiwa kuanza kazi, kuanza biashara mradi au chochote huwa tumahawa aina ya mapepo pasipo wewe kujua,kwa kutumia wachawi, kwanza atafanya maagano na wewe ya kimtego utaingia katika dhambi, kisha sasa ataanza kukutoboa taratibu. uchawi upo na ukitumwa inategemea ulimwengu wako wa roho uko vip wakati huo, kama taa zimezima utakupata, shetani haogopi wewe kuokoka, anaogopa wewe kujua tatizo na ufumbuzi yani neno na kulitumia kwake.
√ mapepo hawa si chuma ulete tuu ni kitu kikibwa sana ni pamoja na kutumiwa uvivu, uchovu wa kupindukia, hizi ni roho kabisa za ibilisi. Mungu alipoanza kuongea nami nilishangaa, kutokuwa na maamuzi ya haraka, yale mambo yote yanayokuchelewesha kufika pasipo hata wewe kujua, mfano kuchelewa katika appointment za muhimu, kuhairisha mambo, uzito wa kuamua, marafiki wa baya wanaokunyonya nguvu zako za kiroho, yale mambo unayopenda kufanya kupoteza mda au kustarehe ambayo hayana u Mungu ndani yake zote hizo ni roho za ibilisi,
√ kukata tamaa, uzito katika akili, tunutu ni laana la eneo kuna maeneo kusudi ufanikiwe lazima uvunje laana za hapo mahali, hizo roho si chuma ulete tuu ni vile vitu vyote ambavyo wewe ni vigumu kuvigundua lakini vitakusababishia uchelewe katika maendeleo yako, mfano watanzania wengi tumekumbwa na tunutu wa mda Mungu atufungue, mambo haya hayaonekani kwa jinsi ya uzito wake lakini ndivyo hutufanya miaka yetu kuliwa, kususa zote hizi ni roho za ibilisi, sasa iko mipango ya siri ya wachawi ya kuhakikisha kwamba, huendelei icho unachokipata kikurudishe
√ nyuma! zipo master plan ambazo zinatengenezwa kuzimu zinasubiri mda na majira ya utekelezaji wake, ndo mana mtu anaeenda mara anakwama, anakaaa hapo mda mrefu kisha anaaanza tena kisha anakwama, kumbe hajui wako wachawi wanakaa usiku wanachora ramani kukumaliza, Kwa sisi tuliokoka lazima tujue adui jinsi anavyopambana na sisi ili kuweza kumshinda sasa leo tutaenda kuharibu hizi network na ramani zote za kutuchelewesha, ambazo zinatushambulia kama nyuki, na mipango yote master plan za ibilisi ya kukushambulia, unapofanya hivi unajiwekea mazingira ya kuwa salama familia yako, juu ya magonjwa, kazi yako juu ya madeni, biashara yako juu ya hasara, ndoa yako juu ya utenganifu, na mambo kama hayo! kwa iyo weka kichwani hawa ni mapepo yaliyoachiliwa kuja kukuchelewesha au kukutia hasara mahali flani. ili ukawie kufika. Halleluyah!
tukaombe sasa!
√Baba katika jina la Yesu, ninakushukuru kwa kunikumbusha asante kwa ufunuo huu pia, ninakutukuza katika jina la Yesu, nami nimejua kua baraka zangu zingine zimechelewesha na nzige, tunutu, viwavi, parare, nimeju pia izi plan huwa zinapangika kule kuzimu na kutekelezwa duniani, na
√nimejua pia nimejua shetani hufanya maagano ya siri ili Kupata mlango wa kuchelewesha baraka zangu, kupata mlango wa kutoa baraka, nami katika jina la Yesu Ee Mungu Baba wa kweli ninakuja kwako kwa utakaso kamili, ninaomba unisamehe katika jambo lolote nilikukosa Baba, unirehemu katika njia
√zangu zote zilizoenda kinyume na maagizo yako na sheria zako, naomba pia unisamehe katika laana yoyote iliyonipata na kuifuta laana iyo kwa damu ya Yesu, katika maisha yangu, Baba nimekuwa chanzo cha baraka zangu kuchelewa mimi mwenyewe, Baba nimekuwa chanzo uharibifu wangu mwenyewe sababu kutokusikia sauti yako, na kutokufuata sheria zako Mungu wa kweli na
√uliye hai, leo hii Mungu unitakase kwa damu ya mwanao Yesu, unitakase kwa damu ya Yesu katika jina la Yesu, rehemu ata ardhi ya asili yangu katika jina la Yesu, rehemu kisababishi chochote katika maisha yangu kilichosababisha mimi kuchelewa kufika na si tuu kuchelewa bali kuendelea kurudi nyuma kuliko sababishwa na mapepo na roho za parare nzige tunutu na
√ viwavi katika jina la Yesu, ninaingia katika ulimwengu wa roho sasa naharibu kila master plan zote zilizopo kuzimu hata katika masijala zote za kuzimu ya mipango yote ya uharibifu juu yangu katika jina la Yesu Kristo, naharibu kwa moto wa roho mtakatifu katika jina la Yesu, kila kilichopandwa katika maisha ili kunichelewesha leo nakiongoa kwa jina la Yesu, leo pepo la marafiki wabaya, pepo la uvivu, pepo la kupoteza mda, pepo la kufunika akili yangu na giza, pepo la bumbuwazi, pepo la kutokufanya maamuzi, pepo
√ la chuma ulete, pepo la matukio ya gafla ya kunirudisha nyuma, pepo linalojenga mazingira ya kunikataa, leo nawaharibu wote kwa moto katika jina la Yesu, ewe pepo mauti, pepo konokono, pepo kobe, pepo vikwazo, pepo la kusababisha tabia za ajabu ajabu ndani yangu, ndani yangu, pepo la kunitenga na fursa, pepo la kuziba masikio yangu ya rohoni, pepo la kuziba macho yangu ya rohoni, pepo la kunikwepesha na watu sahihi,
√ pepo lililo tumwa na wachawi, magano yote ya kuzimu, maagano ya kichawi maagano yote ya siri yaliyoniingiza katika vifungo vya kuchelewa pasipo kujua kwa damu ya Yesu, kwa jina la Yesu, ninawashika wote mateka, kwa damu ya Yesu ninawatupa katika shimo la Moto nawayeyusha hadi mauti katika jina la Yesu Kristo! nawasambaratisha kwa jina la Yesu, shetani toa mkono wako katika uchumi wangu, hatua
√ zangu, toa mapepo yako yote uliyoyaagiza kunichelewesha kwa jina la Yesu nakuapisha kwa jina la Yesu toa hila zako zote, mipango yako yote ya kuchelewa nimeifuta kwa damu ya Yesu, nimeiharibu kwa jina la Yesu, umeanguka ibilisi na watoto wako wote, toka katika maisha yangu kwenu nyie ni shimo la giza na ziwa la moto toka achia maisha yangu, rudi kuzimu ninaamuru wote mshikwe mtumipiwe katika shimo la mateso msirudi tena duniani kwa jina la Yesu na damu ya Yesu, leo ninakiri Mungu kunirejeshea furaha, amani, fedha, utajiri,
√ kampuni, ndoa yangu, afya yangu, biashara yangu, kazi yangu, kila kitu kilicholiwa kinarejeshwa na faida juu sasa na neno la Mungu kwa jina la Yesu, nakukaribisha Roho wa Bwana wa marejesho njoo juu yangu sasa unirejeshee, Karibu sasa! karibu uje juu yangu uniatamie nakupokea sasa Roho wa Bwana katika jina la Yesu! Baba kama jinsi wana wa Israeli walivyorejeshewa wakatoka na kila kitu ndivyo jinsi neno pia ni kweli na amina katika maisha yangu na Roho wa Mungu wa marejesho yuko juu yangu sasa kunirejeshea, kunifidia , kwa jina la Yesu. Asante Bwana Yesu maana umekuwa. Ameen.
rudia mara 7*
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
Muhimu:
Mungu amenipa maono ya kwenda live kupitia radio, na televison, ili masomo haya na maombi tuyapate live, yaani audio na video tutaanza na online radio, online tv, kupitia internet, Pia tutakuwa na live prayer line ya kuhudumia watu, Mungu amesema nami kwa habari ya studio kwa ajili ya huduma iyo. Nikupe nafasi ya kupanda mbegu yako kwa ajili ya studio hiyo. Na Mungu atakukumbuka sadaka yako injili itakapoenda duniani kote. kufungua, kuponya, kuokoa, kuinua. Kama unataka kushiriki baraka hizi uko ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. basi tumia hizo namba hapo chini kutuma sadaka yako. kama uko nje ya Tanzania tumia izo namba nitakupa maelekezo
josephntandu@gmail.com,+255713297066, +255765377506
#Mtumishi Joseph Ntandu
#Wanamaombi Group
Nashukuru sana mtumishi kwa mafundisho mazuri yanayofungua.yananibariki sana
ReplyDeleteBwana Yesu na akutie nguvu sana uwezekutoa maneno yake na mafuandisho yake katika taifa la Mungu
ReplyDeleteAmina nimefunguliwa
DeleteAmen.Mungu akubariki mtumishi.Pia nina tatizo naomba unisaidie.Kila popote niendapo hiwa situlii natamani kuondoka.Mfano nikipata kazi nikikaa mwenzi mmoja huwa nachoka na hiyo kazi natamani kurudi nyumbani.Nikirudi nyumbani tena sikai naanza kuitamani ile kazi niliyoiacha.Mi sijui ni nini inanisumbua
ReplyDeleteJustine Elicki unahitaji maombi ya kufunguliwa ili uwe huru. Kufanya maamuzi sahihi. Fikra zako, maamuzi yako yamebanwa. Nitafute kwa ushauri na maombi
DeleteBwana Asifiwe.Niko kenya kwa sasa.Nifanyeje ndio tuwasiliane.Ama si ungeniandikia maombi hapa tafadhali
Delete+255713297066 nipigie what's app call
DeleteAmen mtumishi ninasumbuliwa sana na roho za kunirudisha nyuma na sasa nimekwama kabisa kiuchumi na sioni njia ya kutokea.je baada ya maombi haya nifanye kitu gani cha ziada?
ReplyDeleteBube ubarikiwe yapo maombi ya kuvunja maagano na adui. Yapo maombi ya ukombozi kupitia ardhi yapo hapahapa. Endelea kufuatilia yatakusaidia
DeleteMtumish maomb yako ni mazur yameniingia had nmetoa machoz mtumish Nina shda naomba nipate kaz niondolewee nuks na kupata mtu aliyesahihi kwang yesu kristo aniogoze na kunionyeshs njia iliyosahihi
DeleteAmina mtumish nimefunguliwaaa
ReplyDeleteAmen mtumishi maombi yako mazuri sanaa ila mim ni mvivu wa kuomba sanaa
ReplyDeleteAmina Mungu amenikutanisha na blog hii hakika ni mpango wake,nimebarikiwa naanza kufanyia kazi
ReplyDeletehakika Mungu ni mwaminifu sana
DeleteWoow,Mungu anao watumishi wake,yaani nambariki Mungu kwa ajili yako,asante kwa kummtii Roho Mt yaani huduma hii imenibariki na nimenza kuomba naona jinsi ninavyohudumiwa
ReplyDeleteAmen mtumishi ngoja nianze kuyafanyia kazi maombi naimani muda si mrefu nitaleta ushuhuda baada ya Mungu kutenda
ReplyDeletemtumishi nimebarikiwa ila niko na shida mtoto wangu anazimia alianza miezi tisa mpaka saii anamiaka miwili lakini mahali nimeolewa wazazi hawataki niende kwa maombi ilijiiba nikaenda wakajua sasa ata sina amani hatapia na mume wangu maana anasikiza wazazi nifanyaje nisaidie
ReplyDeleteAsante mtumishi,ubarikiwe kwa maombi na mafunzo
ReplyDeleteAsante mtumishi nimebarikiwa sana na nitaanza kuyafanyia kazi kuanzia sasa nataka nibadilike na mungu haonekane pia kwa namna moja naamini sasa mungu anakwenda kutenda na ntaleta ushuhuda
ReplyDeleteMungu WA Mbinguni akubariki Sana So powerful, Blessing and Useful amen.
ReplyDeletehakika
DeleteMungu akubariki Mtumishi wa Bwana.Nimeanza maombi Haya,hakika nimewekwa huru katika Jina la Yesu.Amen.
ReplyDeleteMungu akubariki limenvushaaa mno
ReplyDeleteShukran kwa maombi yako kuna wepes nmepataa Ameeeen
ReplyDeleteAhsanteee nimefunguliwaaa
ReplyDeleteNimependa sana mafundisho yako mtumishi barikiwa!
ReplyDeleteMUNGU akutie nguvu kupitia sala hii naona kufunguliwa
ReplyDeleteBwana Yesu asifiwe, maombi haya ni mazuri sana... Mungu anipe neema kurudi kushuhudia utukufu wa Mungu. Asante mtumishi kwa knowledge kama hii. Pia tungefurahi zaidi kwa wale waliofanya maombi haya na kufunguliwa kuja kushukuru Mungu mahali hapa. Ili watu walio wachanga kiroho wakiingia kwenye hii blog na kuomba watiwe nguvu na shuhuda zetu. Inapendeza zaidi tukivuka sehemu tuliokwama sehemu tukaja kushuhudia kuonesha utukufu wa Mungu ju ya maisha ya watu wake, tusisahau wapendwa.
ReplyDeleteNapenda mafunzo yako mtumishi wa Mungu shadrack Abunga mkenya
ReplyDeleteNimebarikiwa sana sana
ReplyDeleteNasubiri kushuhudia mahali hapa na kwa nyumba ya MUNGU,keani yamekuwa..
ReplyDeleteHebral 19:36,tunaishi kwa imani
Mungu baba akubariki mtumishi wake nahisi kufunguliwa kwa kusoma tu hata kabla ya kuomba.Naamini nitafunguliwa na kuwekwa huru katika vifungo nlivyofungwa
ReplyDeleteMtumishi Mungu akubariki popote pale ulipo
ReplyDeleteU
ReplyDeleteb
x
Barikiwa sana mtumishi wa Mungu
DeleteAwesome prayers much thanks for all and may Almighty Father God grant your Prayers too in Jesus Might Loving Name Ameeeeeeeeeen
ReplyDeleteBarikiwa sana
ReplyDeleteBwana Yesu asifiwe, nimefurahi kupata ufunuo huu kwa wakati sahihi, Mungu akuinue zaidi kwa viwango vyake katika utumishi wako, Barikiwa .
ReplyDeletenamtukuza Mungu wa Mbinguni kwaajili yako Mtumishi ,Roho Mtakatifu Amenivusha ,HALELUYAH
ReplyDelete