ROHO YA UTASA
Somo: "Roho
ya utasa" (Part A)
PART B
Bwana Yesu
asifiwe Sana!
Yohana
8-31-32
31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi
waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli
kweli;
32 tena
mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Mpendwa
ibilisi hatishwi na ulokole wako, hatishwi na kutembea na biblia, hatishwi au
kujua nyimbo zote za kuabudu na kusifu au tenzi za rohoni.
Hakuna
shetani anayeondoka katika maisha yako isipokuwa kwa kupingwa. Soma mwanzo
mpaka ufunuo lazima apingwe ndipo aondoke,haondoki tuu hivihivi lazima apingwe.
Mpingeni shetani naye atawakimbia. Ivyo Kuna vitu vya kufanya uvuke hapo ulipo.
ndipo akuachie ibilisi, aachie maisha yako. Shetani haindoki tuu kwa kuwa wewe
umeokoka. Au umeshiriki katika ibada. Shetani huogopa wewe kuijua kweli. Kuijua
haki yako kupitia neno. Neno linasema nini kwa habari ya iyo haki iliyoibiwa?
Yani kuzijua na kuzidahi haki zako ibilisi alizozozichukua, haki ya kufanikiwa
kikazi, kibiashara, kuwa na kiwanja, kujenga, haki ya kuwa na amani, haki ya
kusoma kufika mbali, haki kuwa na afya njema, haki ya kuwa katika ndoa, ya kuwa
na watoto. Kama kwenu hakuna anayevuka form 4, ukijua kuwa mlifungwa na maagano
ya kafara. Iyo ni moja pili sasa lazima uidai ile haki.
Yohana 15-7
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu
yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Kukaa ndani
ya Yesu ni hatua moja, hatua ya pili ni maneno ya Yesu kukaa ndani yetu. Umeona
formula ya kupokea. Wengi tuko ndani ya Yesu ndio tumeokoka lakini maneno ya
Yesu hayapo ndani mwetu. Anasema Ombeni lolote mtakalo mtatendewa. Hoja nzito
ni maneno ya Yesu. Kuna sehemu biblia inasema leteni hoja nzito tuhojiane
tusemezane. Watu wengine hoja nzito wanapeleka mawazo Yao. Biblia inasema nawe
utaijua kweli nayo kweli itakuweka huru. Biblia haijasema kweli itakuweka huru.
Kitakachokuweka huru ni kitendo cha wewe KUJUA. Baada ya kujua ndipo sasa kweli
itakuweka huru. Hicho ndicho shetani anaogopa.
Mungu
ameongea nini kuhusu utasa?
Kutoka
23:26
26 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala
aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.
27
Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu
wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo
yao.
Roho ya
utasa ni hali ya kutokifanikiwa katika kipengele flani kwa mda mrefu. Watu
wengi wapo kwenye utasa na hawajijui kama wamefungwa katika utasa. Mungu
hakukuumba ufanikiwe kidogo, Mungu hakukuumba uende kwa kuotea, Mungu
hakukuumba uwe na matokeo madogo, Mungu hakukuumba ubahatishe, Mwanzo 1-27-28,
ni mapenzi ya Mungu ufanikiwe. Maana kufanikiwa kwako kunamletea Mungu utukufu,
kama hufanikiwi eneo lolote iyo sehemu Kuna utasa. Iyo roho ya utasa ikaa
mahali hata ufanyaje huwezi kufanikiwa ni mpaka uivunje na udai haki yako kwa
jina la Yesu ndipo utakapo ona matunda yakikaa. Ukitanuka, ukiendelea. Kama
umefanya kazi mda mrefu mafanikio yako hayalingani Na kazi yako huo ni utasa,
kama umefanya biashara miaka 10 huna hata nyumba ya kwako huo ni utasa. Utasa
upo wa aina nyingi.
Aina za
utasa
1. Utasa wa
mwili- hukaa kwenye tumbo la uzazi-kutokuzaa huleta vimbe za tumbo hizi roho za
utasa, mikono(uzalishaji wa mtu hutegemea nguvu ya mikono katika ulimwengu wa
roho) miguu(miguu imepewa umiliki katika ulimwengu wa roho)
2. Utasa wa
kibali(kutokukubalika, hata mazingira kutokukubali, maeneo kutokukubali
hufanikiwi kwa lolote ilo eneo)
3. Utasa wa
biashara(madeni, kufilisika, kutokupata wateja, kutokuuza)
4.Utasa wa
kazi(kutokupata kazi, kufukuzwa kazi,kutokupanda cheo,kukandamizwa, kuchoshwa
kufanya kazi)
5.Utasa wa
mawazo,ufahamu (huwezi buni wazo la kuzalisha, kutegemea akili ya mtu
mwingine,kufikia mwisho wa kufikiri, kushindwa kufanya maamuzi)
6. Utasa wa
kiroho(kushindwa kuelewa neno, kusoma biblia, kushindwa kuomba, kushuhudia
wengine, kubaki mtoto kiroho hukui kila siku, kutegemea kulishwa kila Mara
kutafuniwa kupewa, kwenda kwa hamasa na
sio neno)
7. Utasa wa
ndoa(ndoa haifanyi kazi pamoja na jitihada zote,malumbano yasiyoisha, ushindani
usioisha,tatizo la mahusiano la mda mrefu lisiloisha hata baada ya jitihada
zote)
Na mwingine
mwingi...
Roho ya
utasa huwa inasimamia wap?
1. Katika
Kuzaa
2.katika
kuongezeka
3.katika
Matunda ya mwanzo yanaliwa hayawezi kujua
*kuzaa
mtu
mwingine hazai faida au matunda mema, anazaa mapooza. Anazaa balaa, mikosi.
Roho ya utasa inakaa sehemu kwenye mimba. Mimba Si ya mtu tuu. Mimba za
kiuchumi. Mimba za ndoa, mimba za wazo la biashara, mimba ya kiroho,mimba ya
uchumi, mimba ya mahusiano, kila kitu huwa kinaanza kama mimba katika ulimwengu
wa roho. Mimba ya marafiki wema, mimba ya watu wa msaada katika maisha yako.
Mimba ya biashara. Mungu anapoitunga tuu kama kitu au wazo. roho ya utasa huja Na kuharibu iyo mimba.
Watu wangap walipata mimba nzuri za idea au mwanzo mzuri gafla kama ni wazo. Au
ni mtu. Au chochote ambacho kingesaidia mimba iyo kuzaa kinakufa. Piga picha
katika maisha yako vitu vingap vimekufa mwanzoni? Na ulijua ni bahati mbaya? Au
kawaida?
*Kuongezeka
Sasa mimba
imeenda kwa misukosuko je swali litakuja itaongezeka? Ni ile mtu anasoma hapati
kazi, ni ile mtu anafanikiwa kupata mtaji biashara haiendelei, ni ile mtu
anafikia umri wa kuolewa alafu anakuja mtu ila haposi. Wanakuja wanaondoka. Wanakuja wanaondoka. Iyo ni roho ya
utasa.
*Matunda ya
mwanzo yanaliwa hayaongezeki.
Hii sasa
ndo ile tunaita kudumaza kitu, kama ni kitu kimevuka kuzaliwa, kimevuka
kuongezeka sasa unahitaji Ayo mafanikio yakae mda mrefu hayakai. Unahitaji
kwenda level za kimataifa, unahitaji kustaafu vizuri, unahitaji kuwa na
security gafla matokeo Yale uliyopata Mara ya kwanza yanaondoka kabisa. Alafu
inabaki stori. Alikuwa na hiki, alikuwa na kile.
Bwana Yesu
asifiwe Sana. Kuna matunda ya watu wengi Sana ibilisi kayapukutisha na hayapo
yamefutika.
Roho ya
utasa imekalia watu wengi Sana na wanabaki kujiuliza kwanini siendelei, kwanini
sivuki hapa. Tayari kuomba umeomba mlango umefunguka. Dalili zinaanza kuonekana
gafla roho wa utasa anakuja kuharibu mimba. Kama mimba ikifanikiwa kuzaliwa
utasa unakuja ili isiongezeke. Na kama itaongezeka basi matokeo ya kwanza utasa
huzuia kwa kuyala Yale matokeo. Au
kuyapoteza ili mtu uyo abaki Na histori.
Jinsi ya
kushughulikia roho ya utasa? Na maeneo gani makubwa roho ya utasa hukaa na
kutawala maisha ya binadamu kwa robo tatu ya maisha ya mwanadamu. Fuatana nami
kesho katika part B ya somo hili.
Bwana Yesu
asifiwe Sana!
Yohana
8-31-32
31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi
waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli
kweli;
32 tena
mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Ninyi
mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu. Nyie mmekuwa wanafunzi.
Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. Mpendwa Kuna kweli Mungu
anataka uijue. Ili iyo kweli kupitia neno ikuweke huru.
Kwanini
nizungumze kuhusu roho ya utasa? Jana kwanini Leo nizungumze kuhusu nyayo za
miguu?
Mwanzo
25-24-25
24 Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama!
Mapacha walikuwamo tumboni mwake.
25 Wa
kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita
jina lake Esau.
26
Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino.
Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa.
Wapendwa
wengi utasikia wakisema Yakobo tapeli Yakobo tapeli. Bila kujua Yale
yaliyoandikwa katika kitabu cha mwanzo 25-24..... Ni mambo ya ulimwengu wa
roho. Nataka ungalie uhusiano wa nyayo zako za miguu na nafasi yako ya uchumi,
nafasi yako ya ndoa, nafasi yako ya kufanikiwa, nafasi yako ya kuwa mtawala,
nafasi yako ya kuwa msaada kwa wengine, nafasi yako katika ulimwengu wa roho
Kuna uhusiano gani Kati ya nyayo za mguu na hatua za mtu? Au nafasi ya mtu?
Nikurudishe hapo juu mstari wa 26, biblia inasema Yakobo wakati anazaliwa
alimshika Esau kisigino! Manake nafasi ya uzaliwa wa kwanza haikuaanzia pale
Esau alipobadilishana na chakula hapana. Ilianza pale tuu aliposhikwa kisigino.
Manake Yakobo alichukua nafasi ya Esau tokea tumboni mwa mamaye Pale ndipo
aliponyanganywa nafasi ayo uliyoyaona baadae ni matokeo ya rohoni. Ni kama vile
wewe unavyoomba mambo yanaanzia rohoni kuja mwilini.
Kwa iyo
Yakobo hakudanganya bali alikuwa anasema kweli alipomuambia Baba yake mimi ni
mzaliwa wa kwanza alikuwa anamaanisha wala alikuwa hatanii.ile ilikuwa ni lugha
ya kimamlaka lugha ya ulimwengu wa roho ndio mana kule chini ukiendelea kusoma
mlango huo Mwanzo 27-18-29.....hata Baba yake baada ya kugundua alishindwa
kufanya kitu sababu ya lugha ya ulimwengu wa roho inamamlaka. soma hiyo stori
iyo, ISAKA alimuuliza mara mbili Yakobo maana alikuwa haoni akamuuliza lakini
kweli wewe ni Esau mzaliwa wangu wa Kwanza? Akasema ndio, akamwambia nisogelee
nikuguse maana Esau alikuwa na manyoya kwenye mikono. Na Yakobo alivaa ngozi
yenye manyoya mikononi, Isaka akasema mwili huu ni kama wa Esau lakini sauti ni
kama ya Yakobo. Pamoja na kuwa na daught Isaka hakuweza kufanya lolote na
akambariki, na hakuweza fanya lolote sababu Yakobo tayari alichukua nafasi
tokea alipomshika Esau nyayo za miguu ya Esau. Katika ulimwengu wa roho.
Yote
yaliyoonekana nje ulikuwa ni utiisho wa ulimwengu wa roho,Maana utawala na
hatua na nafasi ya mtu ipo katika nyao za mguu. Nyayo tunazozizungumzia hapa Si
nyao hizi unazoziangalia kwa macho na damu zipo nyayo katika ulimwengu wa roho
ambazo zimepewa mamlaka. Ndio mana wachawi wakitaka usifanikiwe katika hatua
zako zozote Wao wanacheza na nyayo zako, wanachukua sehemu ulipokanyaga, au
kutuma ma urgent wakikushika tuu tayari wameacha madhara ndo mana mambo ya
Mungu yanatambulika rohoni. Kwa macho ya kawaida watasema aaah uyo mshamba
mfano kusuguliwa miguu, kuoshwa miguu ni hatari wala si kwamba mimi ni mshamba
sababu anayekusugua miguu hujui hata historia yake, hujui ukoo aliotoka , hujui
wametokea ufalme gani? Wa Giza au wa Mungu. Wengi wanaopenda kupendeza
watalipinga jambo hili. Ila baada ya kuwa tasa katika mambo flani flani kwa mda
mrefu ndipo ataelewa haya mambo ya rohoni. Nyayo Maana zimebeba nafasi,
zimebeba hatua zako, zimebeba mamlaka ya kutiisha falme za Giza, mamlaka za
Giza, wakuu wa Giza.
Mpendwa kila mahali unapoishi lazima Kuna
falme za Giza za huo mtaa, Kuna wachawi wa huo mtaa, Kuna mizimu ya huo mtaa,
Kuna jeshi la pepo wa baya huo mtaa, Kuna wanga, Kuna wasoma nyota, Kuna ma
urgent wa kuzimu bahati mbaya wanatembea katika maumbo ambayo wewe ushayazoea
kuyaona ivyo Si rahisi kuwagundua kama huna Neema iyo. Mtu akitaka kukufunga
wewe kitu chochote usiendelee atadili na nyayo zako.
Luka 1:19
19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na
nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Anasema
nimewapa mamlaka ya kukanyaga. Kwanini anasema kukanyaga? Kwanini hasemi
kunyonga, ushawahi jiuliza? Kunyaga kwa sababu nyayo ndiyo zimepewa
mamlaka,huwezi kukanyaga na mikono Bali nyayo, kukanyaga nyoka Na nge nyoka ni
ibilisi mwenyewe katika ulimwengu wa roho, nge ni wale maurgent wa ibilisi
mapepo mizimu, roho chafu, walinzi wa kipepo hao ndio nge, hizi ni lugha za
ulimwengu wa roho, Bwana Yesu asifiwe Sana! Nataka uone uzito wa nyayo za miguu
ili ujue kuwa nyayo zinabeba mamlaka, zinabeba nafasi, zinabeba hatua kwa iyo
zimebeba roho tatu ya maisha yako.
Yoshua
3-15-16
15 basi hao waliolichukua hilo sanduku
walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa
katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika
wakati wote wa mavuno),
16
ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa
chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale
yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu
wakavuka kukabili Yeriko.
*Biblia
tena neno nyayo zimetumika kutiisha maji yakagawanyika. Biblia inasema makuhani
wa Mungu walipokanyaga walipotia nyao zao ukingoni maji yalitengeneza njia na wana wa Israeli
wakapita. Na ukiendelea kusoma utaona kuwa ilibidi wale makuhani wasiondoke
mpaka wote wamevuka mto Jordani. Tunaona nguvu ya utiisho katika nyayo.Bwana
Yesu asifiwe kama jinsi nyayo za mtu zilivyokuwa na uwezo na mamlaka ya
kutiisha falme za Giza, mamlaka za Giza kama jinsi Esau alivyonyanganywa haki
zake kwa nyayo ndivyo jinsi nawewe pia unaweza kunyanganywa nafasi yako tokea
mimba yako ilipotungwa kwa kupitia nyao. Au kuguswa nyayo zako, kwa njia yoyote
na mitego yoyote, ibilisi anajua siri hii ndio maana anamiliki hatua za watu na
watu wanakuwa na utasa, utasa wa hatua mchawi akitaka usisonge mbele, usitoboze
anakuwahi kwenye nyao. Watu wanaona ni fashion kuosha miguu lakini hawajui
jinsi wanavyoharibu maisha Yao, hawajui jinsi wanavyouza nafasi zao, hawajui
jinsi wanavyoondoa mamlaka zao za kutiisha. Ili uishi kwa amani ni lazima hapo
unapokaa wewe uwe juu ya wachawi, wanga, wakuu wa Giza,wachawi falme na mamlaka
za Giza usije sema mtaani kwetu hakuna wapo. Kwa iyo utiisho wa hao ma urgent
wa kuzimu upo kwenye nyayo zako katika ulimwengu wa roho. Na wanatesa watu,
wanahangaisha watu. Watu hawasogei, hawaendelei, kumbe siri ndogo tuu ni wewe
kuondolewa kwenye nafasi yako, wewe kuondolewa mamlaka yako, wewe kuondolewa
hatua zako. Na unakuwa tasa. BWANA Yesu asifiwe Sana!
Ushahidi
kwamba ibilisi hupiga hatua za mtu, mamlaka ya mtu, nafasi ya mtu kupitia
nyayo.....
Ayubu
18-7-8
7 Hatua zake za nguvu zitasongwa, Na shauri
lake mwenyewe litamwangusha chini.
8 Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake
mwenyewe, Naye huenda juu ya matanzi.
*anasema
hatua za mtu zitasongwa,kwani ametupwa wavu katika miguu yake mwenyewe, naye
huenda juu ya matanzi. Matanzi ni uchawi wa mafundo. Kuwekewa nyavu ni kutegewa
mitego katika miguu ili usikimbie Kuna watu katika ulimwengu wa roho hatua zao
zimewekewa Tanzi, zimewekewa wavu ndo mana anakuwa na utasa katika maisha yake.
Vitu vinakufa, haziongezeki, matunda ya kwanza nayo yanakufa.
Maombolezo
4-18
18 Wanatuvizia hatua zetu, Hata hatuwezi kwenda
katika njia zetu; Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia; Maana mwisho
wetu umefika.
*wametuvizia
katika hatua zetu, hata hatuwezi Nenda katika njia zetu. Mwisho wetu
umekaribia. Bwana Yesu asifiwe Si Mimi ni biblia inaongea maneno haya, hatua
inamaanisha miguu. Miguu ndiyo inayofuata njia. Ndo mana mwisho anasema maana
mwisho wetu umekaribia. Wapendwa watu wengi Sana wamefungwa hatua zao,
wamechukuliwa nafasi zao wengine wamekuwa omba omba, ma house girl kumbe nafasi
zao zimechukuliwa kupitia nyao. Wengine wanamekuwa ma professor lakini Si vya
kwao wamechukua nafasi za watu. Mpendwa huwezi kujua Mungu alikupa nafasi gani
hapa duniani na uyo unayemwomba msaada pengine alichukua nafasi yako kwa kujua
au kutokujua. Halleluyah! Au uyo anayeuza aliyefanikiwa pengine alichukua
nafasi ya hatua zako, mamlaka yako ya kutiisha kwa kupitia nyayo, ulimwengu huu
ni wa mapambano anayeshinda ndiye anayemiliki. Bwana Yesu asifiwe Sana.
Baada ya
kuelewa mpaka hapa sasa tunafanyaje?
*Damu ya
Yesu ya kwenye miguu iliachiliwa ili wewe urudishe nafasi yako katika ulimwengu
wa roho, ya kutawala, ili upige hatua, ili uwe na mamlaka katika nyayo zako.
Bwana Yesu asifiwe. Inawezekana umekamatwa toka tumboni mwa mama yako kama
Esau, au wamechukua alama za nyayo zako, kwa kujua au kutokujua. Hata ukawa
tasa kiuchumi, kindoa, kazi, biashara, kiroho, kujenga, ukawa tasa kila mahali.
Hufanikiwi umezungukwa na utasa kila mahali. Pengine ulikamatwa kupitia ardhi
ya kwenu, kupitia uchawi, unahitaji ukombozi wa miguu kipengele cha nyayo.
Ukombozi ni kila siku. Hasa baada ya kujua siri kubwa kama hii. Katika ufunuo
10-1-5 tunaona malaika wa Mungu alipotaka kumpiga ibilisi mguu mmoja aliuweka
katika bahari, kwa kumaanisha kutiisha mamlaka za bahari. Mguu mwingine aliweka
katika ardhi kwa kumaanisha kutiisha mamlaka za ardhini wachawi, mizimu na mikono
akainyoosha juu kwa kumaanisha kumiliki mamlaka za anga. Vitu muhimu Sana hivi
kujua mpendwa. Soma mwenyewe. Kwa iyo la kufanya omba rehema kwa nafasi
ulizopoteza kama Esau, mamlaka ulizopoteza, na hatua zako zilizofungiwa tanzi,
na kutegewa wavu. Kisha achilia damu ya Yesu ya miguuni . Ukiunganisha damu ya
Yesu ya miguuni. Ukiachilia katika nyayo zako. Fanya ukombozi huo katika nafsi
hizi zilizopotea aidha unazijua au huzijui. Fanya ukumbozi katika mamlaka
zilizopotea, na hatua zako zilizo zongwa kwa utasa. Unganisha mambo hayo kwa
damu ya Yesu ya miguu na ukombozi huo.
Fanya deliverance ya kumaanisha(self delivarence) utaanza kutembea tena,
kumiliki nafasi yako tena,na kutawala tena.
Nawe
utaijua kweli. Na iyo kweli itakuweka huru.
JINA LAKE
MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka
nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako
biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni
kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige
hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande
wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi
ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment