PART B-MFAHAMU ROHO MTAKATIFU VIZURI ILI UPATE MSAADA KATIKA NJIA ZAKO ZOTE
Bwana Yesu asifiwe!
Part B tutacover maeneo manne
*Dhumuni la Roho Mtakatifu
*Faida/kazi za Roho Mtakatifu
*ninampokeaje Roho Mtakatifu
*Nitajuaje Nina Roho Mtakatifu
DHUMUNI LA ROHO MTAKATIFU
.kuwa msaidizi
.kuwa pamoja na wewe
.kuwa rafiki
Roho Mtakatifu haji kuharibu mipango yako. Roho Mtakatifu huja kufanya hizo kazi tatu. Roho Mtakatifu huja kukusaidia wewe kutimiza kusudi la Mungu. Tatizo laWakristro
wengi waliokoka hawajui kusudi Lao kwa Mungu. Kila mtu anakusudi aliloletewa hapa duniani. Iyo ni shule ingine sitaigusa Leo.Kwaiyo sababuhawajui kusudi au wako nje ya kusudi Roho Mtakatifu
wanamtumia sehemu moja tuu. "katika ibada" katika maisha mengine ya kawaida hawamtumii. Roho
Mtakatifu kazi mojawapo ni kukusaidia wewe kufanikisha huo mpango wako.
Haji kukuharibia mipango yako.Watu wengi wanafikiri wakimkaribisha Roho Mtakatifu atakuja kuharibu mipango Yao. Matokeo yake wanamfungia nje alafu wanakomaa wenyewe. Wamesahau lile neno "hamwezi neno lolote pasipo huyo Roho.
Bwana Yesu asifiwe.
Yohana 15:5
. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
*nataka nikufungue macho maana ya ilo neno na ukiijua hii siri haitakutoka moyoni mwako wala hutakaa husahau na itakujengea imani utakayoenda nayo mpaka mbinguni. "kwanini Yesu alisema hamwezi neno lolote pasipo Mimi" ?Wote tunakumbuka nini kilitokea baada ya Yesu kubatizwa na Yohana ubatizo wa maji Mengi? Roho Mtakatifu alishuka juu yake. Na mbingu zilimfunukia.Yesu ni
Mungu binadamu hapa duniani kubatizwa ubatizo wa Roho Mtakatifu. Hata wale waliokuwa wanabatizwa na Yohana Mbatizaji walikuwa wanabatizwa kwa ajili ya ondolea la dhambi (maji) but ubatizo wa Roho Mtakatifu ulifanyika kwa Mara ya kwanza kwa Yesu. Kwa wengine ni chakula kigumu. Roho Mtakatifu akusaidie. Ni hivi baada ya kuokoka mtu hubatizwa kwa maji Mengi ili
kukamilishahaki yote. Then kipo kitendo cha kujazwa Roho Mtakatifu Kwa Mara ya kwanza huo
ndio ubatizo wa Roho Mtakatifu. Bwana Yesu asifiwe. Wengine wanaita ubatizo wa Moto.
Nakufundisha maandiko sikufundishi jambo jipya!
Yohana 1:31
. Wala mimi
sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana *mimi nalikuja nikibatiza kwa maji.*
Yohana 1:33
. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye
ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, *huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.*
SASA TUJE KWANINI YESU ALISEMA HAMUWEZI NENO LOLOTE PASIPO MIMI?
Tuangalie Roho Mtakatifu alipomshukia
Mungu-binadamu wa kwanza Yesu Kristo alifanya nini?
-Aligeuza maji kuwa wine
-Aliponya magonjwa
-Alifufua wafu
-Alitoa pepo
-Alirudishia wasiona kuona
-Viziwi walisikia
-Alizuia upepo wa Bahari
-Alitembea
juu ya maji
-Aliwalisha watu maefu mikate na samaki wachache na wote wakashiba wakasaza
-Alifundisha neno kwa hekima haijawahi tokea hapa duniani
-Alijitoa uhai Na kujirudishia uhai
*Kama Yesu alifanya
Yote hayo kupitia Roho Mtakatifu kama yeye alimuhitaji Roho Mtakatifu wewe unamuhitaji Mara 100.na maana ya lile neno
Marko 16:17
. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu
watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
Marko 16:18
. watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Marko 16:19
Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu
*Hapa Yesu alikuwa anazungumzia Roho Mtakatifu. Bwana Yesu asifiwe Sana.manake mkiwa Na Roho yule yule ambaye Mimi nilikuwa naye mtafanya haya na zaidi ya haya.
Yohana 16:7
. Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.
*Mimi nisipoondoka huyo msaidizi hatakuja kwenu. Kwanini Yesu alizungumza haya maneno? Jibu its simple
Yesu alimpokea Roho Mtakatifu wote. Na
alipompomkea alifanya kazi aliyotakiwa kuifanya. ila tatizo la Yesu ilikuwa liko hapa.
.Mda
.Mazingira(eneo)
.jinsi ya kujigawa kila mahali
.Jinsi ya kumuhudumia kila mtu
.Jinsi ya kumfundisha Kila mtu
.watu waliomuamini walikuwa wengi Sana
Wote wanamuhitaji! Na yeye anahitaji awahudumie wote
Yesu akapiga hesabu siwezi kuwa Africa the same time niwe America au Ulaya nipite kila mahali niponye!
Nifanye muujiza! Nifundishe akaona simple way ni
kufanya kazi Kwa kila mmoja kupitia Roho Mtakatifu. Ndio maana ile sheria ya Musa zile amri 10 zipo moyoni mwako uwe umeokoka au hujaokoka unazijua.
Kwa iyo
sasa Yesu ana Roho Mtakatifu alimchukua (whole from heaven) sasa kwanini Yesu alisema inanibidi Mimi niondoke. It's simple Roho Mtakatifu alikuwa ndani ya
mwili wa Mtu mmoja tuu ambaye ni
Yesu. Kwa iyo kusudi atoke ndani yake aje kwetu lazima amtoe kwenye mwili kwa kumtoa kwenye mwili kwa yeye kuondoka
kurudi katika UUNGU yani (Roho) Kwa iyo Roho Mtakatifu Atahitaji mwili tena wa
binadamu ili aendelee Ku operate hapa duniani. Ivyo ndio maana akawambia
wanafunzi kaeni humu ndani msiondoke mpaka aje Roho Mtakatifu awavike uwezo. Yani uwezo uleule aliokuwa nao Yesu. Bwana Yesu
asifiwe Sana. Kwa iyo
Sasa kwa kufanya hivyo Yesu tayari amesolve matatizo Yale pale juu. Anaweza kuponya akiwa Africa na America at same time. Anaweza kufungua watu akiwa Asia
na Europe at same
time. Maana tuko wakristo waliokoka na kujazwa Roho Mtakatifu zaidi ya 1bil sasa. Kwa iyo tatizo la Muda. Tatizo la mazingira. Tatizo la
kujigawa! Tatizo la usafiri amelisolve sasa badala ya Roho
Mtakatifu kutumia mwili mmoja wa Bwana Yesu anatumia miili bil 1 kufanya kazi zilezile za Yesu. Manake ni
Nini huhitaji Yesu akufuate nyumbani kwako kama Lazaro maana yupo moyoni mwako. Huhitaji
Yesu aje akufundishe habari ya hukumu haki Na dhambi yupo
Moyoni mwako kwa iyo huhitaji kufanya jambo kisha jiuliza hii ni dhambi au sio dhambi no hiyo unaijua vizuri. Iyo unaifahamu vizuri. Bwana
Yesu asifiwe.
Na ndio maana Yesu akasema hivi
Yohana 16:8
. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
Ona hapo juu Yesu alikuwa anajizungumzia yeye.
Ona hapa chini pia
Yohana 16:16
. Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.
Ushawahi jiuliza hii manake yake nini? Maana yake ni hii mda si mrefu hamtaniona
katika mwili. Mda si mrefu mtaniona Katika mioyo yenu. Kwa iyo
Ni kweli ule usemi unaosema Jesus never say goodbye. Yesu hajaondoka. Anatawala kupitia Roho wake Mtakatifu. Ni Roho huyo huyo
Mtakatifu aliyekuwa naye Yesu
ndie kawachia wanafunzi wake. Na ndio huyo huyo anayeishi ndani yako. Bwana Yesu asifiwe Sana
SASA TUNAPOSEMA ROHO MTAKATIFU NI MSAIDIZI TUNAMAANA GANI?
*Roho Mtakatifu Ni Mungu sio kijakazi. Watu wakisikia msaidizi kinachowajia kichwani mwao Ni picha ya Housegirl
/houseboy. Kumbuka zile kazi za Yesu
alizokuwa anazifanya. Tofauti ya
Yesu Na wanafunzi wake wakati ule ilikuwa Ni nini? Ilikuwa Ni "Roho Mtakatifu" kwa iyo Roho Mtakatifu humtumikishi Bali yeye
Anakutumikisha, Roho Mtakatifu humwagizi Bali yeye anakuagiza, anachokuja
kukifanya ni kukusaidia kufikia malengo yako, kuwa Na malengo au kujua
Kusudi la Mungu haina maana umefanikiwa no! no! no! Bado unamuhitaji Roho Mtakatifu akusaidie. Kwanini unamujitaji Roho
Mtakatifu
akusaidie ni sababu yeye ni Mungu anavyovitu vya kukusaidia ufanikiwe kwa wepesi ambavyo wewe huna. Bwana Yesu asifiwe. Unaweza kuwa na pesa za
kujenga kiwanda na idea ya product lakini haina maana tayari umefanikiwa bado utahitaji wataalamu wa sheria, wataalamu wa mazingira, wataalamu
utawala, wataalamu wa uhasibu, wataalamu wa manunuzi, utahitaji engeneers, wa chemicals! Na
industrial mechanical, utahitaji wataalamu wa store,
utahitaji wataalamu wa mauzo, tena ukiwa umeokoka Una hofu ya Mungu utahitaji watumishi wa kuja kuombea eneo lako kabla ya ujenzi hata baada ya
ujenzi. Wataalamu wa Muundo au designers wa jengo, yani bado unahitaji vitu vingi. Sasa Roho Mtakatifu Ni Mungu
ambaye anavitu vyote hapo juu na vya ziada. Ukimpata Yeye umepata vyote. Bwana Yesu asifiwe Sana! Na ndio maana ya lile hamwezi lolote pasipo mimi
.Roho Mtakatifu Ni mbunifu
.Roho Mtakatifu Ni mzalishaji wa vitu yeye ndio anayetoa Rohoni kuja mwilini
.Roho Mtakatifu ana hekima ya
hali ya juu
.Roho Mtakatifu ana maarifa ya hali ya juu
.Roho Mtakatifu ana ufahamu hali ya juu
.Roho Mtakatifu ndo anaye multiply vitu
.Roho Mtakatifu anaona vitu vya Rohoni
.Roho Mtakatifu ana
sensitivity ya hali ya juu yani manake ana predict kinachokuja
Iyo ni mifano michache tutaingia ndani kule mbele. Kwa iyo unachohitaji wewe ni plan. Ukiwa na plan yeye anakuja kukuonyesha jinsi ya
kuimpliment. Watu
hawaelewi kwanini Mungu anaweza kukuonyesha mwanzo na mwisho wa jambo jinsi itakavyokuwa. Mfano nini kusudi lako? Kusudi Langu hapa duniani ni
kufundisha neno la Mungu. Nini maono
yako? Maono yangu ninaona ipo siku nitafundisha watu laki 3 kwa Mara moja. Lakini utafikaje katika maono yako don't
worry iyo anayo Roho Mtakatifu anayo jinsi ya kufika. Mungu anakuonyesha wewe ni
tajiri Sana ni kweli huko ni mwishoni but katikati hapa pana Roho
Mtakatifu. Mungu anakuonyesha unabiashara kubwa, umeolewa, anakuonyesha katika ndoto mambo mazuri well and good hapa Katikati Una
Muhitaji Roho Mtakatifu. Mungu amekutolea unabii kupitia Nabii thank you Jesus but unahitaji vitendea kazi! Vitendea kazi anavyo Roho Mtakatifu
Kwa iyo Roho Mtakatifu hakwepeki. Unaweza kukomaa
kufanya mwenyewe sikatai lakini mwisho wake utafika umechelewa Sana, umechoka hata haina
Maana tena maishani mwako, bila Roho Mtakatifu utakata tamaa! Sababu mwenye hekima za kupita kwenye Hilo
tatizo kirahisi ni Roho Mtakatifu sio
wewe. Mwenye maarifa ya kuondoka kwenye ilo tatizo ni Roho Mtakatifu sio wewe, mwenye ufahamu ya mambo ya Rohoni na mwilini ambayo unayatafuta
maisha yako yote
ni Roho Mtakatifu. Kwa iyo Roho Mtakatifu anavyovifaa vya kazi vya kukufanya ufike kwa wepesi kule unakoenda. Bila kuchoka. Na saa ingine
ukifanya kila kitu wewe unachoka unakata tamaa unaamua
kuachana navyo. Tatizo la binadamu akisoma kidogo anafikiri amepata vitendea vyote vya kazi vya
Kutatua matatizo. Kwa iyo Roho Mtakatifu Ni mtatua matatizo katika mipango yako. Roho Mtakatifu ni
mwondosha changamoto katika mipango yako. Roho
Mtakatifu ni mwezeshaji katika mipango yako. Roho Mtakatifu ni mtiaji nguvu katika mipango yako nguvu zote, nguvu za mwili, nguvu za akili, nguvu za kiuchumi
Nguvu za maarifa, nguvu za hekima, nguvu za ufahamu juu ya jambo flani. Bwana Yesu asifiwe Sana. Roho Mtakatifu ana vifaa vyote vya kazi vya kuhakikisha
Umefikia maono yako kwa iyo ni
msaidizi Roho Mtakatifu. Jina la Bwana libarikiwe.
Zaburi 32:8
. Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
TUNAPOSEMA ROHO MTAKATIFU KUWA PAMOJA NA
WEWE TUNA MAANA GANI?
Manake ni hii! Wazungu wanaita companion yani unaweza kusikilizana na mtu lakini asiwe pamoja na wewe. Unaweza kuishi na mke au Mme ndani
Lakini asiwe pamoja na wewe. Laiti
Mungu angekufunulia mioyo ya watu uangalie jinsi inavyokuwazia ungeshangaa Mme anaweza kukupenda au mke
na kukuhudumia lakini ikifika maamuzi flani akakataa kuwa pamoja na wewe. Mfano kitendo
mwanaume kuleta ndugu zake ndani ya nyumba ingawa anampenda
Mme wake mke anaweza asiwe pamoja Na yeye. Utasikia mtu anasema "kwa ilo siko pamoja na wewe kabisa". Mke anaweza anzisha maneno maneno
mtaani
Kwa kukosa hekima labla akasababisha watu wakatenga. Case ikaja kwa Mme wake akamwambia mke wake Katika hili sipo pamoja na wewe. Au mke kwa wivu
tuu akajikuta ameuwa mtu kwa tetesi tuu hapo
Mme wako akamwambia katika hili upo mwenyewe sipo pamoja na wewe. Bwana Yesu asifiwe Sana. ROHO
MTAKATIFU Ni mtu pekee anayeweza kuwa pamoja na wewe no matter what! Anaweza kuwa pamoja na wewe ukiwa
gerezani! Au watu wote wamekugeuka Na
Kukucheka au wamekukimbia Roho Mtakatifu atakuwa pamoja na wewe. Roho Mtakatifu atakuwa pamoja na wewe hata kwenye mambo madogo Sana mfano
Unajaribu kuwaelezea
watu kitu Na wanakubishia Roho Mtakatifu atawafanya wale watu wakusikize. Roho Mtakatifu Hata kwenye mpira atakuwa pamoja na
wewe.atashangilia na wewe Unajua interest zinatofautiana Kati ya mtu na
mtu. Mfano Mme anaweza kuwa anapenda mpira mke hapendi mke
anapenda kwenda kutembea kutoka out
Kuna vitu ambavyo huvipendi na ambavyo unavipenda binadamu ana limit Sana Katika vitu ambavyo havipendi
anaweza kukutenga kuwa mbali na wewe ila katika
Vitu ambavyo vina interest zake anaweza kuwa pamoja na wewe. Kwa iyo Roho Mtakatifu si mnafiki. Yeye yupo pamoja
na wewe no matter what. Hata kwenye
Kutenda dhambi yupo pamoja na wewe kukumbusha habari ya hukumu haki na dhambi. Na kukuletea huzuni na
kuhakikisha umekosa amani mpaka
Umetubu. Binadamu mpe nafasi Katika moyo lakini usimpe moyo
wako. Moyo wako mpe Roho Mtakatifu maana yeye
Hana upendo wa kinafiki. Binadamu wote wanahitaji mtu wa kuwa pamoja naye no matter what! Binadamu kwenye aibu atakukimbia! Binadamu kwenye
kuhukumiwa
atakukimbia! Binadamu kwenye fedheha atakukimbia! Binadamu kwenye matatizo atakucheka atafurahi! Atakuwa pamoja na wewe huku
anakungonga lakini si Roho Mtakatifu! No matter What! Roho Mtakatifu
atakuwa pamoja na wewe. Lakini sasa ninajua kwanini watu huwakimbia watu au
kuwapa migongo wakati wa matatizo. Ni sababu hawana tools za Roho Mtakatifu, yeye ana kumbatio, yeye anafariji, yeye
anarudisha tumaini, yeye anakuletea
tabasamu, uyo ni Roho Mtakatifu yeye ana kutia nguvu, yeye anakuombea, yeye anakutia moyo, yeye anakufungua macho no matter what! Kwa kweli ukimjua Roho
Mtakatifu you will fall in love with him. He is true companion. More than your husband, more than your wife, more than Friend, more than your Children. More
than your neighbour, hawa wengine
wanaweza kuwa pamoja na kwa mda tuu. But yeye Roho Mtakatifu yupo pamoja na wewe hata ukienda kuoga atakufuata ataanza kuongea na wewe! Unashangaa
ukimaliza kuoga jibu ulilokuwa unatafuta tayari
umelipata. Roho Mtakatifu Ni zaidi ya kiu ya maji. Ni kweli hatuwezi bila yeye. Ana tools zote binadamu anazozihitaji
hapa duniani. Zoote zipo kwake. Kuzipata lazima uambatane naye. Bwana Yesu
asifiwe sana. Roho Mtakatifu yupo pamoja na wewe.
TUNAMAANA GANI TUNAPOSEMA ROHO MTAKATIFU NI RAFIKI?
Rafiki ni mtu wa karibu ambaye mnaelewana na mko huru kushirikishana baathi ya mambo au mambo
yote. Kipo kitu kinachofanana ambacho kilishaabiana
ndani mwenu. Ambacho ndicho kilichowaunganisha. Kwa iyo urafiki huanzia moyoni kibali cha urafiki huanzia moyoni. Wako waliokuwa marafiki sababu
ya interest zao zimefanana. Mfano wote wanapenda mpira. Wote wana watoto mapacha. Au wote ni weupe wafupi. Au wote hawapendi mtu kuonewa, au wote
wanapenda neno la Mungu aidha Ni mazingira au Ni
sababu zimewakutanisha but lazima kuwe Kuna kitu kinaitwa common interest. Kwa saa ingine
unaweza kuwa huru Sana kushare mambo yako kwa uhuru au siri zako kwa rafiki kuliko mme au mke. Au ndugu au
wazazi. Rafiki saa ingine anaweza chukua nafasi
ya watu muhimu katika maisha yako. Na watu wasikuelewe. Bwana Yesu asifiwe! Kwa wewe na Roho Mtakatifu haina tofauti. Interest yako wewe ni interest
yake yeye. Kivipi?
Yohana 16:14
. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
Yesu anatukuzwa Katika maisha yako na anapopata sifa pale mtu anapoona ahadi za
Mungu zimekuwa kweli katika maisha yake. Baada ya mapambano ya mda
mrefu ukafikia ushindi wako ukamiliki kile ulichokuwa unaomba Yesu huwa anatukuzwa katika mdomo wako. Midomo ya waliokuzunguka.
Kwa iyo kazi
Ya Roho Mtakatifu Ni kuhakikisha kwamba Yesu anatukuzwa sasa Yesu anatukuzwa vip? Anatukuzwa kwa kukusaidia wewe upate unachotakiwa
Kukipata. Sawasawa na zaburi 32:8 Bwana Yesu asifiwe.
Sasa rafiki haiishi hapo tuu rafiki pia anaweza shear na wewe siri. Roho Mtakatifu huwa anashear na sisi siri
Yohana 16:13
. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye
kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Katika vipengele ambavyo Roho Mtakatifu huwa nampenda kama
rafiki huwa always mambo yanayokuchanganya au mambo unapatashida kufanya maamuzi au
mambo usiyoyaelewa Roho Mtakatifu kazi yake atakutia katika kweli yote manake atakufunulia kila kitu. Yeye si ni
rafiki basi hufanya mambo kwako kwa mwingine
hawezi kufanya. Rafiki anaweza mkopa rafiki mwingine hata mil200 kwa kumuamini tuu. Bila hata dhamana ya kitu chochote sasa Roho Mtakatifu kwako
Ni zaidi
ya rafiki! Kwa iyo yuko tayari kukuibia siri za ufalme wa Mungu kukuambia. Yuko tayari kukutoa katika giza. Yuko tayari kukujulisha ukweli
Yuko tayari kukuambia yanayokuja. Mfano mimi nikitaka
habari zako sitazitafuta kwa watu nitachukua jina lako nitajifungia nalo ndani nakumuuliza Roho
Mtakatifu yeye atanifunulia kila kitu kuhusu wewe. Nikitaka kujua habari za uyu mtumishi nitajifungia
ndani nitafunga na kuomba na Mungu atanifunulia nitajua
Tatizo wengine wakijulishwa basi wanaanza kuropoka ukifanya hivyo Roho Mtakatifu hataongea tena na wewe. Unless amekuambia uongee kama
hajasema dont talk. Mfano mimi napokuwa Rohoni ninapoongea na wewe Roho Mtakatifu hudownload habari za mtu zoote kabisa. Ila siwezi kusema wala
Kukuambia tena ni mpaka Roho Mtakatifu aseme aruusu
Bwana Yesu asifiwe. Kwa iyo rafiki anaweza kukutendea mambo ya ziada ya wengine. Jina la Bwana libarikiwe
Kwa iyo tukitumia advantage ya urafiki wetu na Roho Mtakatifu utajikuta wewe unajua mambo
mengi. Una majibu mengi. Na mambo yanayokuja tayari unayajua
Hata yakitokea unajua kabisa Mungu aliniambia. Nabii wa kwanza wa maisha yangu mimi ni Roho Mtakatifu. Holly Spirit is wonderful
atakupeleka chanzo cha
tatizo atakuleta kwenye situation uliyopo sasa na atakuambia nini cha kufanya. Bwana Yesu asifiwe. Uyu Bwana mkubwa kuwa rafiki yako ni sawa kuwa na tochi
Katikati ya giza
nene unaona kutambua kuelewa vitu wengine wanaona giza, wengine hawana iyo tochi iyo ila wewe unayo. ingawa haya nayokuambia kuyapata lazima uwe
.mnyenyekevu
.Mtii
.uvumilivu
Roho Mtakatifu huwa hana
haraka. Yeye ni Mtaratibu. Na mstaarabu. Si kwamba anashindwa but akitumia spidi yake katika maisha yetu tunaweza tusi survive.
Sababu its most poweful being on heaven and on earth. Tatizo Roho
Mtakatifu tunamtumia may be 1% tena katika kusifu na kuabudu au neno la Mungu. But yeye
He is multpurpose anafanya vitu vingi sana beyond your thinking Bwana Yesu asifiwe.
FAIDA/KAZI ZA ROHO MTAKATIFU.....
1.kukuvika uweza utakao juu
Luka 24:49
. Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.
Uweza maana yake "ability to do" Mungu amekupa kila kitu kasoro uweza wa
kufanya hivyo vitu. Huo uweza ukiupata ndipo mambo yanaenda kwa wepesi
ndipo mambo yanaenda kwa uraisi Bwana Yesu asifiwe. Timu ya mpira ina wachezaji 11 inakuwaje katika timu yote mastaa utakuta
ni wawili au watatu? Ni sababu
wamevikwa uweza. Wa kuwa staa. Yani kwao kucheza mpira kukimbia kupiga chenga kufunga goli hawa struggle kama wengine kwao ni automatic! Sio kitu cha
kutafuta au
kujifunza kipo kwao automatic. Sasa huu uweza ukija sehemu mbalimbali za maisha yako ndipo unakuta mahali ulikuwa umekwama unapita kwa
wepesi. Uweza si kwa ajili ya kuhubiri injili tuu. Uweza
utokao juu unacover sehemu zote katika maisha Bwana Yesu asifiwe sana. Ukiona wewe unaenda hatua zako
kwa ugumu. Huna wepesi jua nyuma yako hakuna uweza ukusaidio. Uweza huu unaposhuka na unapovishwa basi utakuta mazingira yanalazimishwa kuwa upande
wako. Watu wote wanakuwa upande wako. Wakati watu wanaleta nyanya zao mfano sokoni hawauzi nyanya zinaoza ukileta wewe unauza zote na zinaisha na
watu wanagombania nyanya zako. Ukimaliza wewe ndipo wengine wanauza. Ukiona ivyo jua upo uweza uliovishwa juu. Yako na uweza ninaozungumzia hapa ni
uweza wa Mungu. Unakuta mtu anajaribu
kujenga nyuma miaka 7 na bado haijaisha ila wewe ile kuanza msingi tuu nyumba iyo iyo mara baada ya miezi mitatu nyuma
imeisha na kiukweli si kwamba ulikuwa umeweka akiba ila unashangaa tuu kila
ukitoa ela zinaingia nyingine. Kila ukitoa ela zinaingia nyingine unashangaa. Ukiona
ujue huo ni uweza utakao juu. Ukifanya kitu kwa struggle manake ni moja tuu haujavikwa uweza utakao juu.. Huu
uweza wa Kimungu unakusaidia kufanya
unachokifanya ufanye kwa wepesi kabisa. Sasa mwenye kazi ya kuvika watu uweza ni Roho Mtakatifu. Bwana Yesu asifiwe! Sasa angalia hapa. Wanafunzi wa Yesu
walikaa na Yesu miaka 3! Wakijifunza pamoja na kujifunza kwa kuona na kupractice na imani yao kuwa kubwa sana Bado Yesu anawaambia no! Msianze kazi
Petro! Msianze kazi Yohana! Subiri Paulo mkishavikwa uweza utakao juu ndipo mtaweza. Uweza wa Mungu kazi yake ni kumsukuma adui nyuma ili wewe uweze
kupita. Uweza wa Mungu ukivikwa kila kitu kitalazimishwa kukutii. Na kuwa upande wako.
Uweza wa Mungu ni special nguvu za Mungu za kukusaidia ufanye kitu
flani kwa wepesi. Uweza huo ndo unamfanya mtu awe mwalimu wa kutegemewa. Doctor wa kutegemewa. Wakili wa kutegemewa. Uweza huo ndo
una mfanya mtu awe staa. Uweza huo ndo unamfanya mtu awe mwanasayansi hatari. Uwezo huo ndio unaomfanya mtu awe engineer wa kutisha. Uweza huu wa
kimungu ndo unamtofautisha mtu mmoja na mwingine
wanachokifanya. Mtumishi na Mtumishi. Mchezaji na Mchezaji. Msusi na Msusi. Kwa iyo ukiona unastruggle
eneo lolote katika maisha basi ujue hujavikwa uweza utokao juu katika ilo eneo. Mungu kabla
ya kukuvika anangalia icho unachokifanya je alikuambia
ukifanye? Je ni mpango wa Mungu ufanye biashara? Je ni mpango wa Mungu ufanye kazi? Je ni mpango wa Mungu uwe Mtumishi kama ni mpango wa Mungu
katika ilo unalolifanya basi atakuvika uweza wake. Hii ipo hata kwenye ndoa kama ndoa ni ya Mungu basi Mungu atakupa uweza utokao juu maarifa na
hekima ya kuishi na uyo mwanamke na uyo mwanaume.
Bwana Yesu asifiwe. Kwa iyo hakuna ambacho hakivikwi uweza. Sasa kazi hii ni ya Bwana mkubwa ROHO
MTAKATIFU. Ndo mana Roho Mtakatifu ni Muhimu sana hapa duniani kuliko hata Roho yako. Watu wengi
sana wanaishi katika giza mateso na shida na taabu.
Sababu hawamjui Roho Mtakatifu. Au wanamjua lakini wanamdharau. Kila kitu chako hapa duniani kimefungwa kimekuwa packed kwa Roho Mtakatifu.
Utaruka ruka tuu na kukimbia but kumkataa Roho Mtakatifu ni kumkataa Mungu. Kumkataa Mungu ni kujiangamiza. Bwana Yesu asifiwe.
Yesu hajaondoka duniani bado yupo anatawala kupitia Roho
Mtakatifu.kutomtambua Roho Mtakatifu ni kutomtambua Yesu. Halleluyah
2. Msaidizi
Yohana 14:16
. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine,
ili akae nanyi hata milele;
Yohana 14:17
. ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani
yenu.
Roho Mtakatifu
-anaona mambo ya Rohoni
-Anajua yote,ana majibu yote
-Ana nguvu na uweza wote
-Ni mbunifu
-Ana hisi vitu
-Anajua siri za Mungu
-Anajua yanayokuja
-Mtengenezaji njia
-Mnyooshaji njia
-Ni Muongezaji
-Mzidishaji
-Ana nguvu ya kuanza jambo
-Ana nguvu ya kuendeleza jambo
-Ana nguvu ya kumalizia jambo
-Ana nguvu ya kuumba tena jambo
-Ana nguvu ya kutowesha jambo
-Ana nguvu ya kurudisha jambo
-Ana nguvu ya kuwahisha jambo
-Ana nguvu ya kuchelewesha jambo
-Roho Mtakatifu muwezeshaji wa yote
-kukutengenezea mipango
-kukumbusha mambo muhimu
-Roho Mtakatifu ni mtengenezaji structure
- Roho
Mtakatifu ni muondoaji vikwazo
Kazi kubwa ya Roho Mtakatifu ni kuhakikisha kwamba jambo unalolifanya unalifanya bila kukwama kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Bwana Yesu. Yeye ni msaidizi katika
-kazi
-biashara
-ndoa
-Miradi
-Shule
-Huduma
Chochote unachokifanya kiongozee hapo kazi ya Roho yeye atakichukua mwanzo mpaka mwisho atakukabithi tayari kimekamilika alafu bado ataendelea kukufuatilia Bwana
Yesu asifiwe. Roho
Mtakatifu haji kukuvurugia mipango yako anakuja kuhakikisha kwamba mipango yako inasimama na inakamilika. Bwana Yesu asifiwe. Yeye ni rafiki, yuko pamoja na wewe. Yeye ni
msaidizi uyo ni Roho Mtakatifu.
3.Mwalimu
Zaburi 32:8
. Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Roho Mtakatifu
kazi yake kubwa kwa binadamu ni kumfundisha binadamu ili aweze kufanikiwa. Bwana Yesu asifiwe! Ile ministry ya kufundisha iliyokuwa ndani ya
Yesu ilitoka kwa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu
atakufundisha kila kitu. Sijapata kuona mtu kama Roho Mtakatifu. Mtu ni nafsi ya Mungu. Bwana Yesu asifiwe
-Roho Mtakatifu atakufundisha kuishi na wakorofi
-Roho Mtakatifu atakufundisha jinsi ya kukaa na mme,mke na watoto
-Roho Mtakatifu atakufundisha jinsi ya kuishi na watu wasikukimbie
-Roho Mtakatifu atakufundisha kusamehe na kusahau
-Roho atakufundisha na kukumbusha jinsi ya kufanya usafi
na kuwa msafi
-Roho Mtakatifu atakufundisha jinsi ya kuongea mbele ya watu jinsi ya kubehave
-Roho Mtakatifu atakufundisha hata mambo ya chumbani kwa wanandoa.
-Roho Mtakatifu anakuonyesha out of you atakuonyesha watu wanakuchukuliaje ili ujirekebishe
-Roho Mtakatifu atakufundisha kufanya kazi, kufanya biashara,huduma
-Roho Mtakatifu atakufundisha jinsi ya kupanga ratiba
-Roho Mtakatifu atakufundisha kuvaa kupendeza
-Roho Mtakatifu atakufundisha kuwa wewe (original)
-Roho Mtakatifu atakufundisha kuchagua marafiki
-Roho Mtakatifu atakufundisha mambo yote ambayo huyawezi na utayaweza
-Roho Mtakatifu atakufundisha ku plan
-Roho Mtakatifu atakufundisha jinsi ya kuheshimu watu
-Roho Mtakatifu atakufundisha jins ya kujishusha
-Roho Mtakatifu atakufundisha jinsi ya kutokuwa bored
-Roho Mtakatifu atakufundisha ujasiri
-Roho atakufundisha jinsi ya kuongea na mtu akukubali
-Roho Mtakatifu atakufundisha jinsi ya kukaa na boss mkorofi
-Roho Mtakatifu atakufundia hata jinsi ya kutembea
-Roho Mtakatifu atakufundisha hata jinsi ya kupika
-Roho Mtakatifu atakufundisha jinsi ya kushinda au wap pa kuanzia mradi wako
Roho Mtakatifu anafundisha KILA KITU ni wewe tuu. Bwana Yesu asifiwe.
Kuanzia mambo makubwa sana na madogo sana. Ya siri na yasiyo ya siri. Ya Rohoni na ya
mwilini. Kusudi ufanikiwe inakupaswa uombe akufundishe. Shida inakuja hapa tunatabia ya kumwaharakisha Roho
Mtakatifu hatumfuati kama Mungu
tunamfuata kama mjakazi. Uyu ni Mungu kabisa. Bwana Yesu asifiwe.lazima umfuate kama Mungu.
4. Mwongozaji
Zaburi 32:8
. Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Kukufundisha ni jambo moja. Mtu anaweza kukufundisha bado ukawa huna
ujasiri wa kuanza. Bwana Yesu asifiwe. Roho Mtakatifu hatakufundisha tuu no!
Bali atakuongoza hapo anasema nitakuonyesha njia utakayoiendea manake atakutangulia atakushika mkono Bwana Yesu asifiwe
sana. Kumkosa Roho
Mtakatifu ni kukosa kitu kikubwa sana maishani mwako. Mwongozaji pia njiani katika safari anaendelea kukushauri kuhusu safari yako. Sioni jinsi Mkristo
anaweza ishi bila Roho
Mtakatifu sijui anapata wap iyo nguvu ya kushinda vita bila uyu Bwana mkubwa. Bila uyu Bwana mkubwa utakwama katika kila kitu unachokifanya Bwana Yesu asifiwe sana.
5. Mlinzi
Zaburi 32:8
.Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Hapo anaposema jicho langu litakutizama manake nini nitakuangalia ili usije jiingiza katika makosa. Watu
walikosea kufanya maamuzi. Walikosea kufanya maamuzi katika kuchagua
-mahali pa kuishi/alipopangisha
-eneo la biashara alipo
-mtu wa kuolewa/au kumuoa
-course ya kuchukua chuo
-kazi anayofanya
-marafiki
-maamuzi ya kununua vitu
-Biashara ya kufanya
-Shule aliyompeleka mtoto/watoto
-mahali alipojenga nyumba
- ramani ya nyumba iliyojengea nyumba
-Maamuzi kuhusu pesa
Kuna maamuzi mengi sana
binadamu tuliyafanya na ndio yametufikisha hapa tulipo. Kazi ya Roho Mtakatifu ni kukulinda ili usifanye maamuzi mabaya
Ili usije kujutia baadae maana gharama ya kufix kitu na Mungu ni gharama
kubwa. Hasa ambako kitu ambacho hukumshirikisha Mungu. Au ulijua wrong
ukachagua Kuendelea anyway. Bwana Yesu asifiwe. Katika section ambayo inagharimu watu ni decision. Ndo mana Roho Mtakatifu
ameshuka ili yeye afanye
decision kwa niaba yako ili usije pata hasara. Bwana Yesu asifiwe sana.
6. Kutupasha habari kwa habari ya haki,hukumu na dhambi
Unaweza kuokoka na bado ukaishi katika utumwa. Utumwa wenyewe ni upi ni kuishi katika sheria. Unakuta mtu tokea asubuhi anajichunga asifanye dhambi.
Anajichunga afanye haki, anajichunga asihukumu vibaya.
Bwana Yesu asifiwe! Anasahau tunaishi katika neema. Sasa ukiwa na Roho Mtakatifu ukienda wrong
kwa habari ya hukumu haki na dhambi hapo hapo atakujulisha. Pili huna haja ya kujichunga yeye mwenyewe
atahakikisha huendi kufanya makosa mambo ambayo
hayampendezi Mungu. Utakuwa unasikia uzito wa kunywa pombe! Uzito wa kuzini! Uzito wa kufanya uasherati. Uzito wa kudanganya! Uzito wa kuiba! Uzito
wa Kusengenya. Uzito wa mizaha inayotoa uwepo wa Mungu. Bwana Yesu asifiwe sana. Kwa iyo kazi mojawapo Ya Roho Mtakatifu ni kuhakikisha ilo lango linakaa
sawasawa. Bwana Yesu asifiwe. Kuna watu
wanahangaika wanasema nataka niwe mtakatifu. Utakatifu unakuwa controlled na Roho Mtakatifu na sio
Na Mwili huu. Kazi mojawapo ya Roho Mtakatifu ni kukusaidia ili uweze kukaa sawasawa. Bwana Yesu
asifiwe.
Yohana 16:8
. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
7. Mpashaji habari wa mambo yanayokuja
Yohana 16:13
. Lakini yeye atakapokuja, huyo
Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Kama unataka kujua
mambo yanayokuja kuhusu
-Mahali unapoabudu
-Familia yako
-mme,mke,watoto wako
-Ofisini kwako
-Serikalini
-Katika ulimwengu wa Roho
-Biashara,kazi unayofanya,huduma
-Mwaka husika
Au whats ever its simple
ukinyenyekea Roho Mtakatifu atakuambia mambo yatakayokuja. Alimradi tuu unauliza kwa nia nzuri ya ki Mungu si sababu zako au
interest zako. Roho Mtakatifu ni mwaminifu tena atakuambia hata
usiyouliza. Ukitaka kuyajua uliza utayajua. Kama unataka uambiwe na watu basi
ngoja wakuulizie kisha wakuambie. Bwana Yesu asifiwe sana. Jina la Bwana libarikiwe.
8. Anafumbua mafumbo ya Mungu
1 Korintho 2:10
. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
Jambo lolote fumbo katika maisha yako lisikupe
shida mshirikishe Roho Mtakatifu mwombe Roho Mtakatifu akufungulie. Funga omba msihi Roho Mtakatifu
akufunulie atakufunulia. Fumbo ni pamoja na mambo usiyoyaelewa. Siri usiyoielewa. Jambo lenye
utata Roho Mtakatifu
anauweza wa Kutrace case iyo kukufunulia chanzo. Sehemu iliyopo na nini kinatakiwa kifanyike uyo ni Roho Mtakatifu.
9. Hutuweka katika kweli yote
Yohana 16:13
. Lakini yeye
atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Kukuweka katika kweli yote manake kukufungua macho kuhusu swala flani. Ukimwambie Mungu niweke katika kweli yote kwa maana nyingine Mungu afungue
macho yako na masikio yako ya Rohoni.ili uweze
kuona kwa iyo badala ya kuhisi watu, kudhania watu mwombe Roho Mtakatifu afunue kweli. Akupe ukweli
wenyewe. Jina la Bwana libarikiwe.
10. Mkamilishaji au mtendaji Mkuu/coordinator wa mambo ya
Rohoni kuja mwilini.
Mwanzo 1:2
. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Mwanzo 1:3
. Mungu akasema, Iwe
nuru; ikawa nuru.
*Roho ikawa juu ya maji akasema iwe nuru Roho akafyatua nuru. Hii manake yake nini? Manake ni hii Roho Mtakatifu ni msababishaji wa vitu.au producer wa
vitu Kama ni msababishaji
wa vitu au mzalishaji wa vitu na wewe unahitaji ivyo vitu basi ujue kabisa bila yeye huwezi vipata. Kabla hata ya kumjua amekua
akikutengenezea na vingine unavyo je si zaidi ukawa karibu naye?
Utakuwa mshindi kila kona ya maisha yako. Bwana Yesu asifiwe sana. Roho Mtakatifu tuna
Mwitaji kuanzia utosi hadi uwayo. Tena katika kila kona ya maisha yetu na si sehemu ya ibada tuu. Bwana Yesu
asifiwe
Ni Muhimu kuliko hata Roho yako.
NINAMPOKEAJE ROHO MTAKATIFU....
Bwana Yesu asifiwe!
Zipo njia tatu za kumpokea Roho Mtakatifu
1. Kuwa na kiu na Roho Mtakatifu kumkaribisha aingie ndani
yako.njia wewe kuomba.
-mfano mimi nilijazwa na Roho Mtakatifu chumbani kwangu! Nilikuwa na kiu nilimuomba Mungu anijaze Roho wake
Mtakatifu aniwezesha niseme kwa lugha mpya. Nilikiri sala ya toba
chumbani na kujazwa Roho Mtakatifu chumbani.
Luka 3:21
. Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;
*ONA HAPO NAYE ALIOMBA! ROHO MTAKATIFU
ANAWEZA KUJA KWAKO KWA KUOMBA AJE KWAKO NA AKUJAZE.
Hii mara nyingi ni Mungu huwa anasukuma watu au mtu. Kunakuwa na automatic ndani yako ya kiu unajikuta
umeomba mwenyewe na umejazwa.
Ukiona
msukumo huu ndani yako basi jua Ni Mungu.Wengine walijazwa bafuni. Wengine jikoni. Wengine wakitembea. Wengine usingizi. Wengine wakisifu na kuabudu.
2. Neno linapofundishwa
Matendo ya Mitume 10:44
.Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.
Matendo ya Mitume 10:45
. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na
Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 10:46
. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu,
Matendo ya
Mitume 10:47
. Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?
Kama hivi kwa kusoma habari za Roho Mtakatifu anaweza kuja juu yako kukujaza na
ukanena kwa lugha mpya. Neno
Likimgonga Sana mtu moyo unafunguka Roho Mtakatifu ataangalia ile kiu iliyopo ndani basi kama moyo umefunguka anakujaza.Bwana Yesu asifiwe Sana.
3.Kuwekewa mikono na Mtu
aliyojazwa Roho Mtakatifu
Matendo ya Mitume 19:1
. Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;
Matendo ya
Mitume 19:2
. akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
Matendo ya Mitume 19:3
. Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa
ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.
Matendo ya Mitume 19:4
. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.
Matendo ya Mitume 19:5
. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
Matendo ya Mitume 19:6
. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza
kunena kwa lugha, na kutabiri.
Ingawa ni muhimu Sana kuwa na hakika ni nani anakuwekea mikono. Ikibidi funga kwanza omba umjue uyo Mtumishi. Usitishwe na ishara maajabu
yanayofanyika Mungu alisema
muichunguze kila Roho. Msikubaliane Na kila Roho. Soma maandiko funga. Mwombe Mungu akufunulie kuhusu uyo Mtumishi kabla ya kupeleka kichwa chako
kuwekewa mikono mikono mingine inamuunganiko wa
kipepo akikuwekea tuu mikono tayari anaku connect na kuzimu. Bwana Yesu asifiwe. Sasa Mtu
Aliyejazwa Roho Mtakatifu akikuwekea mikono akiomba wewe ujazwe Kuna kuwa na Impartation ya Roho Mtakatifu
gafla na wewe utaanza nena kwa lugha mpya. Bwana Yesu asifiwe.
*KITU MUHIMU KATIKA YOTE KATIKA HAYO MATATU HAKIKISHA UMETUBU. KAMA HUJATUBU NA UNANENA KWA LUGHA BASI JUA YA KWAMBA HIYO SIO
LUGHA YA ROHO MTAKATIFU. SAA INGINE UNAWEZA NENA KWA LUGHA UKAFIKIRI UNANENA KWA LUGHA KUMBE UNANENA KWA LUGHA YA MAPEPO.
HIVYO NI MUHIMU SANA KUSOMA NENO! KUSIFU KUABUDU KUTUBU KISHA NDIPO UNENE KWA
LUGHA. KITU KINGINE
CHA MSINGI UKIJAZWA MARA MOJA IMETOSHA YAKUPASWA UENDELEE KUNENA UNAPOZIDI KUNENA ILE LUGHA INAENDELEA KUBADILISHWA. NA KUWA YA KWAKO.
Swali nitajuaje kama Roho Mtakatifu yupo ndani
yangu au nitajuaje ninaye?
Jibu it's simple
Utaangalia vile vitu ambavyo Roho Mtakatifu anavyo kama na wewe unavyo yani tabia za Roho Mtakatifu au Matunda ya Roho Mtakatifu kukaa ndani ya Mtu.
Ukiwa na Roho Mtakatifu utajua si swala la kuhisi. Mabadiliko utayaona ndani mwako Kwa kiasi kikubwa kuanzia ndani mpaka nje. Maneno yako yatakuwa
ushuhuda wa Kristo. Matendo yako yatakuwa ushuhuda wa
Kristo, mawazo yako yatakuwa ushuhuda wa Kristo. Bwana Yesu asifiwe Sana.
Wagalatia 5:18
. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
Wagalatia 5:19
. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo
haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
Wagalatia 5:20
. ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
Wagalatia 5:21
. husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na
hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
ROHO MTAKATIFU AKIINGIA NDANI YAKO HAYO MATENDO HAPO JUU
HAMU YAKE INAKATWA INAKUWA DISCONNECTED.
HAITAKUWA MARA MOJA BUT KIDOGO KIDOGO MWISHOWE INATOKEA ILE HALI YA KUCHUKIA HAYA MATENDO NA YANAYOFANANA NA HAYO.
Wagalatia 5:22
. Lakini tunda la Roho ni
upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
Wagalatia 5:23
. upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
HAYO HAPO JUU NI MIFANO MICHACHE YA MATUNDA YA ROHO MTAKATIFU.
IVYO UNAWEZA TUMIA IYO KAMA TESTER. INGAWA ROHO MTAKATIFU
AKIWA NDANI YAKO HUNA HAJA YA KUAMBIWA NA MTU WA NJE ATAKUSHUHUDIA NDANI YAKO NA UTAJUA KABISA UNAYE ROHO MTAKATIFU.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066/0765377506
Comments
Post a Comment