UPONYAJI WA UCHUMI

✝️

Day 2️⃣

*"KWA KUPIGWA KWAKE  NIMEPONA TOKA KWENYE MADENI"*

💡Isaya 53 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

⁵ Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

✍🏽Kumuamini Yesu ni jambo la kwanza!kuamini kuwa Yesu anauwezo wa kukulipia madeni na kuondoa roho ya madeni hilo ni jambo la pili.Usiishie tuu kumuamini Yesu ana uwezo wa kumuokoa mtu kwenye dhambi na huyo mtu akaokoka!Ila uende mbali zaidi.Yesu anayemsaidia mtu kwa damu yake hata akaokoka ana uwezo wa kumsaidia mtu akaondoka kutoka kwenye kifungo cha madeni!na madeni yenyewe!JINA LA BWANA LIBARIKIWE!

▶️Biblia inasema hivi nayo dhambi ikishachukua mimba huzaa mauti,madeni ni mtoto wa mauti!mauti ni adhabu itokanayo na dhambi iliyotendeka,na dhambi ni uasi!mauti kwenye uchumi haiwezi kuja tuu itakuja kupitia mlango wa makosa.Kwa mfano ukikosea aina ya (Mungu) wa kumwabudu,ukaabudu miungu,mauti lazima itapata mlango wa kupiga uchumi wako!gafla unaanza kutembea na roho madeni!unakuwa na madeni yasiyo isha.roho ya mauti haiwezi kuja tuu ikamharibia mtu pasipo mlango.Iko hivyo hivyo roho ya madeni haiji tuu kwako ikakuchagua wewe ukaanza kuwa na madeni NO!Lazima itakuwa imepata mlango.

*➡️YESU ALILIPA KILA DENI KILA MASHITAKA,KILA LAANA KILA ADHABU YA MAUTI NA UHARIBIFU KWA HABARI YA UCHUMI WAKO KWA DAMU YAKE.*

(Ili wewe uwe huru na uchumi wako uwe huru!lakini je unamwamini kiasi gani kwamba yeye ni mwaminifu?!unaamini uwezo wake katika kuondoa na kufuta madeni kwa kiasi gani?!).

*️⃣Unakuja kugundua shida si Yesu,shida si uwezo na mamlaka na nguvu,shida ni imani yako,shida ni mashaka yako,shida ni hofu yako,shida unamwamini kisha humwamini,shida ni kiwango unachomwamini na kumpa,shida ya madeni si deni lenyewe shida ya deni ni imani yetu juu ya Mfuta madeni.SHIDA HATUAMINI NENO LAKE,HATUAMINI AHADI YAKE,SHIDA NI SISI NA SI YESU.

*Mfano:*

✔️Wakolosai 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹³ Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;

¹⁴ ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.

⏸️Wangapi wanaamini hilo neno ni la kwao na ni ahadi ya Mungu,kwa habari ya maisha yao ya kiroho na kimwili?!

⏸️Wangapi wanaamini kwamba nguvu za giza zinatakiwa zisiwasumbue sababu hawako kwenye hizo madhabahu au hizo sadaka kwa kuwa wamehamishwa kutoka huko?!

⏸️Wangapi wanaamini kwamba Yesu alilipa mauti yake ili wao wasipatikane na mauti,Yesu alikufa ili uchumi wao usife?!Yesu aliwanunua kwa damu yake (aliwalipia fine au dhamana) ili miungu isiwafuatilie?!Ili wao na uchumi usitiwe gerezani?!

*➡️WANGAPI WANAAMINI KWAMBA HAWADAIWI DENI NA SHETANI,WALA HAWAHUKUMIKI NA UFALME WA GIZA SABABU YESU  AMEWALIPIA ILI WAWE HURU?!*

💡Isaya 53 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³ Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.

⁴ Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

⁵ Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Amesema waziwazi!!!

1️⃣Alidharauriwa
2️⃣Alihuzunishwa
3️⃣Alisikitishwa
4️⃣Alijeruhiwa
5️⃣Alichubuliwa

✍🏽Adhabu ya amani yetu kwa habari ya uchumi ilikuwa juu yake.Ina maana kila adhabu shetani anayokupa kwa habari ya uchumi wako na wewe mwenyewe!hiyo adhabu imeshalipiwa cash na Bwana Yesu kwa mauti na damu yake.Na sababu hiyo kwa kupigwa kwake uchumi wako umepona.*LAKINI JE UNAAMINI HAYO?!* 

✍🏽Kwanini nafafanua hapa!sababu mwingine atasema mtumishi kwetu kuna uganga,kwetu kuna uchifu,kwetu kuna matambiko,kwetu kuna mazindiko,au zamani niliwahi kwenda kwa waganga,au nilitoa mimba je uovu huo wote,na dhambi zote,na makosa yote.JE YESU KAYALIPIA PALE KAIVARI?! *JIBU NI YES.* Kwa kupigwa kwake adhabu ya hayo makosa!adhabu ya hiyo dhambi,adhabu ya huo uovu ulio urithi wewe umepona.💡JINA LA BWANA LIBARIKIWE

*➡️JE YESU AMEWAHI MLIPIA MTU DENI KWENYE BIBLIA?!AMBAYE ALIKUWA AKISUMBULIWA NA MADENI NA UMASIKINI?!*

*️⃣NDIO....

Mathayo 17 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁴ Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa.

²⁵ Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni?

²⁶ Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru.

²⁷ Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.

✔️Hadithi hii ya Yesu inaeleweka isome taratibu!kitu kikubwa nilichokuwa natamani ukione!YESU KAMLIPIA PETRO MADENI YA KODI,na hii si mara ya kwanza,Yesu aliwahi msaidia Petro tena akapata samaki wengi karibia boti ya samaki izame.

✔️Kabla ya Petro kukutana  na Yesu inaonekana kabisa alikuwa ni mtu asiyekuwa na matokeo!alikuwa ni mtu mwenye uchumi mgumu!alikuwa anaweza kwenda kuvua asirudi na samaki hata mmoja.Maana yake kama ni mfanyabiashara akienda dukani haji mteja hata mmoja.Ni mtu ambaye alikuwa akizaa mapooza!utasa!uharibifu kwenye uchumi!mauti kwenye uchumi.MPAKA PALE ALIPOKUTANA NA YESU NDIPO ALIPOANZA KUYAONA MATOKEO.

*️⃣Ikiwa shida ya umasikini na shida ya madeni ya Petro ilitatuliwa na Bwana Yesu,basi uwe na hakika anaweza kukusaidia hata wewe!uwezo na mamlaka anayo.Utajiri anao!Biblia inasema anao utajiri usiopimika!biblia inasema alifanyika masikini kwa ajili yetu ili sisi tuwe matajiri.Shida si Yesu!Shida  si Neno lake!Shida si Roho wake Mtakatifu.

▶️SHIDA NI IMANI.NDIYO INAYOTUKWAMISHA.
Tumekwama kwenye imani!madeni yanakusumbua si sababu yanakusumbua ila sababu huna imani,huna maarifa ya kutosha,huna hekima ya kiungu ya kutosha.HUNA NENO LA MUNGU KUTOSHA LA KU DEAL NA KUKUTOA KWENYE ROHO YA MADENI NA UMASIKINI.MAANA YAKE HUNA UFUNUO SAHIHI YESU NDO JIBU PEKEE KWA HABARI YA UMASIKINI NA MADENI.*LAKINI JE UNAAMINI?!*

✴️Endelea kutafakati part 🅱️ ya siku ya pili inakuja... kisha siku ya tatu maombi

#.Wanamaombi Online Ministry
#.Mtumishi Joseph Ntandu
#.0765 377506 / 0713 297066

*©️WOM-2025*

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA