YESU NI MKATE UNAONGEZEKA
Bwana Yesu asifiwe. Tunamshukuru Mungu anayetupa pumzi na mda wa kuendelea kujifunza miguuni pake. Halleluyah. Leo tutaenda kujifunza nguvu ya kuongeza kingereza wanaita "power to multiply" halleluyah!
MESSAGE: "YESU NI MKATE UNAONGEZEKA"
Yes! Bwana wetu Yesu Kristo yeye ni mkate uongezekao. Na sio upunguao. Watu wengi wanaomba kwa Mungu na ni waombaji wazuri tuu. Sio kwamba Mungu hawapi anawapa lakini baada ya kupata kwa Mungu hawaridhiki na hawafurahii ivyo wanaendelea kuomba na kuomba na kuomba. Wanasahau mandiko ya Mungu aliposema nendeni duniani mkazaliane. Mkaongeze halleluyah halleluyah. Embu tujikumbushe!
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;-Mwanzo 1
Wapendwa watu wengi wanabarikiwa na Mungu kawapa ila hawajui jinsi ya kuongezeka. Wengi wameomba kazi wakapata kazi let say mshahara wake ni 200,000/= lakini kutokana na misukosuko na mambo ya dunia hii. Iyo pesa wamekuta haitoshi! Wanaendelea kulalamika na kumsumbua Mungu na Mungu amekuwa akiwashangaa. Kwann alikubariki mwaka juzi na mpaka leo unapokea mshahara wa 200,000/= Mungu alitegemea ufikie mshahara wa 2mil. Lakini wewe unaendelea kumsumbua Mungu. Naye Mungu anakushangaa maana alishakamilisha kila kitu zile siku 7. Na sasa Mungu anakazi moja tuu. Kusikiza maombi kujibu. Kusikiza maombi kujibu. Lakini katika kutengeneza na kuongezeka Mungu ashakamilisha. Umeomba mtaji kwa Mungu. Mungu kafanya njia umepata mtaji mil10. Lakini toka upate mtaji hujaongeza. Na Mungu alikuambia ukaongezeke. Wengi formula hii wanafikiri haipo kuwa kila mara lazima urudi kuomba kwa Mungu more and more. Wengine wanajua lakini hawakutilia maanani. Ila njoo leo tuangalie principal za kuongeza na Yesu alifundisha kabisa lakini sema tuu labla husomi biblia yako au unaisoma hujawahi ijua kuwa kuna formula ya Mungu yakuongezeka. Ni kweli alikubariki akakupa amri ya kuongezeka lakini kuna utaratibu. Watu wengi wanasahau kila ahadi kwa Mungu inautaratibu. Kuna utaratibu wa kutoa sadaka. Mfano usiwe n dhambi yoyote. Wala usiwe na adui. Kuna taratibu za kufunga. Kuna taratibu wa kuomba kuna utaratibu wa kusoma neno. Kila kitu cha Mungu kinautaratibu. Na ukikosea hupati majibu. Kama ulikuwa unafikiri Mungu hana utaratibu Mungu anao utaratibu. Tena uko vizuri sana. Ukiufuata kama inavyotakiwa basi mambo yote ahadi zote. Ni za kwako. Halleluyah. Hata Mungu akitaka kukubariki kuna utaratibu. Mungu akitaka kukukilinda kukupigania kuna utaratibu wake. Kuna utaratibu wa hata jinsi ya kutunza baraka ya Mungu. Twende kwenye maandiko.
14 Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.
15 Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.
16 Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula.
17 Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili.
18 Akasema, Nileteeni hapa.
19 Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano.
20 Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa.
21 Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.
Mathayo 14:14
5 Basi Yesu alipoinua macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia Filipo, Tununue wapi mikate, ili hawa wapate kula?
6 Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda.
7 Filipo akamjibu, Mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu.
8 Wanafunzi wake mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia,
9 Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa?
10 Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao.
11 Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka.
12 Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee cho chote.
13 Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula.
14 Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.Yohana 6
Bwana Yesu asifiwe. Umeona siri hii imeongelewa mara (2) katika biblia kitabu cha Mathayo na kitabu cha Yohana. Nataka usome kwa makini maana ukielewa hapa jua kuwa wewe utaenda kuongeza. Kuongezeka ni lazima. Vigezo na masharti kuzingatiwa. Nitazungumzia sana kitabu hicho cha Yohana. Kwa kuuliza maswali yafuatayo..
1.Kwann Yesu aliwaambia wanafunzi wake wawalishe na huku anajua kabisa hawana kitu cha kuwalisha watu?
2.Kwann Yesu aliwambia mna nn mkononi?
3.Kwann Yesu alijua wanafunzi wake hawana chakula na akawaambia wawalishe watu?
4.Kwann Yesu alichukua mkate na samaki mikononi mwao kwann asingefanya miujiza akaleta mikononi mwake?
5.Kwann alichukua kwao mikononi akavibariki alafu akawarudishia akawaambia wawape watu wale?
Halleluyah nikimaliza kujibu maswali hayo somo limeisha na sasa utaenda kuongeza. Bwana Yesu asifiwe sana. Soma biblia yako vizuri alafu ndo uje kwenye maswali ili upate point yangu vizuri.
Swali la 1.
Jibu: Yesu alitaka kuwafundisha wanafunzi wake kuwa wao hawana kitu. Ila mpaji ni yeye. Kwa siku zote lazima ujue chochote ulichonacho amekupa Mungu. Ivo usije ukajisahau ukapata kiburi au ukajiinua. Vitu vyote viliumbwa na Yeye na yeye ndio neno lenyewe na yeye ndio aliyeviumba.
Swali la 2.
Jibu: Yesu aliwauliza wakina Petro wana nini mkononi manake Alitaka kuwambia ya kuwa iko nilichowapa kinawatosha wala huhitaji kingine. Mimi ndio niliyokupa ivo sikukosea kukupa sababu mawazo nikuwaziayo binadamu ni mazuri si mabaya. Ivo mpendwa icho Mungu alichokupa kinatosha. Mshahara Mungu aliokupa unatosha. Mtaji Mungu aliokupa unatosha. Huna haja ya kutafuta excess. Wafilipi 4:6 inasema msijisumbue kwa neno lolote bali katika kuomba kusali na kushukuru. Kipaji ulichonacho hichohicho kinatosha. Uwezo wako wa kuongea aliokupa Mungu. Uwezo wako wa kushawishi aliokupa Mungu. Ikoiko ulichonacho ndicho Mungu anaenda kukitumia kukuongeza. Bwana Yesu asifiwe sana.
Swali la 3.
Jibu: Yesu ujumbe aliokuwa anatupa hapa kwanza vyote anavyokupa Mungu ni kwa ajili ya kuwalisha watu. Yani katika vitu vyote unavyovipata kuna sehemu yako ya kuwalisha watu. Leo hii wale wanafunzi 13 na yule mmoja aliyepigiwa kura hawapo ivo wewe sasa ndo mwanafunzi wa Yesu. Ivo ni wajibu wako kuwalisha watu wake. Pili aliwaambia kuwa wawalishe watu manake alitaka kuwaongezea imani yao. Ya kuwa si kwamba huna kitu mkononi ila unacho isipokuwa kimeshikiliwa na Yesu. Kwa iyo mkate wako upo tayari ila inakubidi uongeze imani yako kuchukua. Inabidi uongeze imani yako kupata unachokitaka. Ndo akawaambia wambie wakae na muwanawishe mikono. Alitaka aongeze imani yako. Kwa iyo cha kwanza kabisa katika wewe kuongezeka lazima uamini katika akili yako kuwa ninacho. Fedha ninayo. Gari ninazo duka ninalo. Kuchukua kwa Yesu wala hajakuzuia. Wala hakukatazi sema imani yako kidogo tuu ndio. Itakuwezesha kuchukua kwa Yesu. Yesu anakila kitu kila kitu amevishika mkononi mwake. Anasubiri uchukue lakini wewe huchukui. Ongeza imani yako. Jana nimeongelea kuusu imani. Halleluyah. Tatu. Yesu anatufundisha jinsi ya kuomba. Njia nzuri ya kuomba baraka ni kuomba kwa njia ya kuwasaidie watu wa Mungu. Mungu nijalie pesa sehemu ya iyo pesa ni ya yatima. Hapa tunafundishwa kuomba katika mapenzi ya Mungu. Tunafundishwa kuomba katika program ya Mungu. Lazima ujifunze haya mambo. Omba kwa nia ya kuwalisha watu wa Mungu.
Swali4
Jibu: Yesu alichukua samaki na mkate mikononi mwao ili tunakuja ile sheria ya kuongezeka sasa. Ilia aviongeze ndipo akupe. Kwa iyo vitu vyote haviwezi kuongezeka ni mpaka umkabithi Yesu aviongeze maana yeye ni mkate uongezekao. Na sio upunguao halleluyah. Yesu alikuwa anatoa siri kwa watu wake ya kuwa ukitaka kuongezeka kwa lolote lazima umkabithi mikononi mwake abariki akishabariki ndipo kiongezeke. Nina maana gani Yesu ndio aliumba dunia hii na program ya kuumba chochote ilitoka kwake. Na hata program ya kuongezeka ipo kwake. Kwa iyo unapomkabithi yeye muumbaji yeye aliyebuni kanuni za kukuumba jinsi ulivyo ndiyo yeye anayo kanuni ya kukuongeza. Sasa kwann kanuni hii isiweke wazi haijawekwa wazi kwa sababu ingekuwa wazi shetani angeeiba ila kujiongeza. Kwa iyo sasa hii program ameiweka siri yake yeye. Its ina safe place. Mtu yoyote anayetaka kuongezeka lazima amjulishe. Anamjulisha vip? Anamjulisha kwa kumpa kile anachotaka kukiongeza kwa kumuwekea mikononi pake. Halleluyah halleluyah. Nampenda huyu Yesu.
Swali.5
Jibu:
Alichukua kwao kuvibariki kuwarudishia na wao wawape wengine. Sababu. Moja akishabariki Mungu hiko kitu hakipungui. Kwa iyo ile nguvu ya kuongezeka itakuwa ndani yako. Hutamsumbua kila mara Mungu fanya njia Mungu fanya njia wakati ameshafanya njia. Yeye atasubiri tuu umshitakie kuwa shetani ameanza kunisumbua kile ulichonipa anataka kuninyanganya. Ndipo yeye amkemee shetani. Kwa iyo yeye akiweka program ya pesa kwenye uchumi wako jua ya kwamba. Uchumi wako hautashuka. Vigezo na masharti kuzingatiwa. Alifanya iyo kusudi wale pia unawapa wale watu wa Mungu ile nguvu ya kuongezeka pia unawapa unapowapa. Iko hivi ukimsaidia mhitaji wa Mungu. Mfano umempa mtaji. Ile shukrani atakuwa nayo kwa Mungu ndivyo jinsi ile nguvu ya kuongezeka ambayo imetoka kwa Yesu ikapita kwako. Ndivyo jinsi itatoka kwako kwenda kwa yule mhitaji ili na yeye akawalishe wengine wasirudi tena kwako halleluyah.Najua umenielewa tena zaidi ya sana. Asante roho wa Mungu kwa kazi nzuri. Sasa unafanyaje kumkabithi Mungu. Yes! Swali zuri 1. Jifunze kussuport kazi za Mungu popote ulipo. Mwambie "Mungu hii ninakukabithi mkononi mwako naomba unibariki ili nikalishe wengine" halleluyah umesikia maombi hayo. Chochote Mungu anachokupa kama ni mkate wa mwilini nazungumzia baraka za mwilini. Kitu cha kwanza kufanya chukua mkabithi Mungu kwa kusaidia yatima. Wajane. Wazee wasiojiweza wahitaji wote ambao unajua huyu ni mhitaji yani anamsuburi Mungu amsaidie. Support kazi za Mungu maana unasaidia uinjilisti. Support watumish wa Mungu. Alafu mwambie Yesu hii ni samaki wawili na mikate mitano ninakukabithi mkononi mwako. Naomba unibariki nikabariki wengine. Naomba unabariki nikalishe wengine. Iyo ndo siri ya kuongezeka. Na unapofanya haya acha kujihesabia haki. Juu unachokifanya. Fanya kwa imani. Maana haitaji siku kukubadilishia maisha yako. Anitaji sekunde tuu. Akikohoa mambo yamebadilika. Mungu akujalie neno hili liwe hai ndani ya maisha yako Ameen.
Josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment