MUNGU HABADILIKI HATA DAKIKA YA MWISHO!
Bwana Yesu asifiwe tuendelee kumlisha mtu wa ndani maana anavyoshiba ndivyo anaweza kukupigania bila hata wewe kujua. Wangap wanajua siri hii? Unaposhiba neno la Mungu kuna uvita vingine vinaondoka vyenyewe bila hata kukemea. Ivo twende pamoja. Kama Mungu amekujalia pumzi. Na riziki umeshiba vizuri jioni ya leo. Una afya. Mambo yako mazuri. Au hata kama kuna sehemu umepitia basi tumia jioni hii kumlisha mtu ndani usimlishe tamthilia tuu za wafilipino. Usimlishe majuto bali mlisho neno lake halleluyah
Message; Mungu habadiliki hata dakika ya Mwisho.
Bwana Yesu asifiwe!Wapendwa Mungu katupa neema ya kujifunza kutoka kwake.kwa mara ingine tena. Ujumbe nazungumza na mtu ambaye ameomba mda mrefu haoni kama Mungu anamjibu. Nazungumza na mtu ambaye jinsi anavyozidi kuomba anaona ndo kwanza majaribu yanazidi. Nazungumza na mtu ambaye anaomba anaona kama vile hata mambo hayasogei. Hakikisha unaomba katika mapenzi ya Mungu. Hakikisha unapoomba kuna uwepo wa Mungu zile kanuni za kuomba kupata majibu hakikisha zote unazifuata. Nina hakika wote mnazijua. Maana tushaangalia sana. Kama unaombea uchumi tafuta maandiko kuusu uchumi yasome usiku na mchana alafu yakiri. Na baada ya mda imani yako itaongezeka. Wewe ambaye umeeomba kwa kanuni zote. Lakini unaona hata baada ya kutoa sadaka unaona mambo ndo kwanza yamezidi. Mambo ndo kwanza hayasogei. Na kama umeanza kuchoka. Hili neno litakutia moyo. Hili neno leo litakuinua katika jina la Yesu Twende Pamoja. Daniel 3:16-30
16 Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili.
17 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.
18 Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.Tanuri Liwakalo
19 Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto.
20 Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.
21 Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.
22 Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego.
23 Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto.
24 Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme.
25 Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.
26 Kisha Nebukadreza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye juu, tokeni, mje huku. Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto.
27 Na maamiri, na manaibu, na maliwali, na mawaziri, waliokuwa wamekusanyika pamoja, wakawaona watu hao, ya kuwa ule moto ulikuwa hauna nguvu juu ya miili yao, wala nywele za vichwa vyao hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu ya moto haikuwapata hata kidogo.
28 Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.
29 Basi mimi naweka amri ya kuwa kila kabila ya watu, na kila taifa, na kila lugha, watakaonena neno lo lote lisilopasa juu ya huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watakatwa vipande vipande, na nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.
30 Kisha mfalme akawakuza Shadraka, na Meshaki, na Abednego, katika wilaya ya Babeli
Halleluyah! Twende mstari kwa mstari nataka ujue Mungu habadiliki hata dakika ya mwisho. Hata katika jaribu ambalo umeona Mungu ameshakuacha umeteketea. Mungu amekuacha umeaibika. Yani kama ushafedheheka. Ushaingia hasara. Ni kama vile umejisumbua kufunga. Umejisumbua kuomba. Umejisumbua kutoa sadaka. Umejisumbua kuomba. Yani mambo kwa macho yako yameshabaribika. Leo nataka kukuambia "MUNGU HABADILIKI HATA DAKIKA YA MWISHO". Bwana Yesu asifiwe! Twende kwenye neno. Shedrack Meshack na Abednego walikataa kumtumia ibilisi yan mfalme ni kama wewe jinsi unakataa kuwa katika vifungo vya umasikini. Vifungo vya dhambi. Unataka kufunguliwa. Na huku ibilisi. Anataka umwabudu yeye. Yani utafute ela kwa njia za uwongo. Anataka utapeli! Anataka utoe hongo! Anataka uchukue hongo. Anataka ufanye uasherati ufanye uzinzi ili uifurahishe nafasi ya ibilisi. Hataki kukuona ukitoka katika kumwadubu wewe. Biblia inasema mstari 18 hatutakubali kutumikia miungu yako. Ni sawa na wewe unapofanya maombi kupinga yale ya ibilisi. Biblia inasema ndipo mfalme Nebukadreza akajaa ghadhabu. Ni sawa na ibilisi anapokuona unapotaka kuvunja maagano ya ukoo wako. Maagano ya familia yako. Anakasirika. Maana umengangana katika maombi halleluyah! Basi mstari huohuo wa 19. Anasema Nebukadreza akaamuru moto ule wa tanuru uchochewe mara saba. Ni sawa na wewe sasa baada ya kuomba unaanza kuona vitisho mara saba ya vile vya mwanzo. Mateso yanazidi. Magumu yanazidi. Huelewi kumbe hujui mfalme nebukadreza kakasirika. Yani mapepo yamekasirika. Roho za ibilisi zimekasirika unaanza kujiuliza imekuwaje ninaomba alafu naishia kupata majaribu mazito.inakuwaje. usiulize imekuwaje jua ya kwamba mfalme Nebukadreza amekasirika. Mstari wa 20. Akawaamuru watu wa majeshi yake. Kuwatupa katika tanuru la Moto. Ni sawa na wewe sasa baada ya kuomba unaona umeingia sehemu ambayo hata huelewi hivi vita vinatoka wapi? Huelewi imekuwaje? Unaona mambo yameharibika na yanazidi kuharibika. Halleluyah halleluyah. Nampenda uyu Yesu simwachi.sikiza Mungu anaweza kukuacha mpaka ulingie jaribu. Mpaka imani yako ianze kumdaught Mungu kama kweli yupo na kama yupo kama kweli anakusikia maombi yako. Au wewe unaoomba vibaya. Anaweza kukuacha mpaka ukate tamaa ya kuomba na hujui tena ufanyaje.
Kumbuka Mungu hajakuacha Mungu hajakuacha. Isipokuwa Mungu alitaka kujitukuza. Mungu alitaka watu watambue Mungu wanayemtukia wakina Meshack Shedrack na Abednego. Mungu alitaka awarudishie heshima watumishi wake. Ndio maana akaruusu mpaka waingie kwenye tanuru la moto. Ni sawasawa na wewe unapoomba alafu unanikuta kwenye majaribu mazito. Lakini kumbuka moto haukuwachoma wala haukuagusa watumishi wa Mungu. Ni kama wewe jaribu lako unalopitia baada ya kuomba si kwamba Mungu anataka kukuteketeza. Hapana Mungu alichokuwa anatafuta kipo mstari wa 28. Nebukadreza akasema na abudiwe Mungu wa meshack Shedrack na Abednego ndicho anachokitafuta kwa wale wanaotumika na ibilisi. Kukuletea mateso. Waje watamke wenyewe halleluyah. Mungu anachotafuta angalia mstari wa 30. Nebukadreza aliweka amri kwa mataifa. Basi ndivyo itakavyokuwa kwa ibilisi atawaambia mapepo majini. Roho chafu mimi ibilisi ninaweka amri kwa nyie watumwa wangu kuwa atakaye wagusa meshack shedrack na abednego atakatwa vipandevipande. Na ndipo utakuwa huru. Mpendwa iko mifano mingi tuu inayosema Mungu habadiliki hata dakika ya Mwisho angalia Masihi wetu Yesu alionewa. Alidhalilishwa.alifedheheshwa. shetani akamuimulia maadui mpaka alipomuingiza kaburini. Mpaka pale nguvu za ibilisi zilipofika mwisho kabisa. Ndipo mwanaume akainuka. Sasa hana jipya tena kwa maana shetani alifika mwisho Yesu ndo kwa kwanza akaanza kazi halleluyah halleluyah. Ivo mpendwa Mungu habadiliki hata dakika ya mwisho. Haijalishi unapitia nini? Haijalishi jaribu ndo linaanza au lipo katikati au ushalivaa au unaona kabisa hili ni tanuru. Mungu habadiliki akisema amesema. Ivo simama katika neno lake hata mambo yote yabadilike. Hata dunia yote ibadilike lakini ujue ya kwamba Mungu habadiliki hata dakika ya mwisho. Nikupe mfano mwingine. Wana wa Israeli waliomba zaidi ya miaka 40 watoke misri hatimaye Mungu akawasikia Musa akapewa jukumu la kuwaongoza misri wakavuka vikwazo vyote. Wakavuka ukuta wote. Walipofika bahari ya shamu imoani yao ilitikiswa pengine walianza kurudi nyuma. Pengine walikata tamaa. Ni sawa na wewe inafika sehemu unapoa. Inafika sehemu mpaka una mdaught Mungu. Lakini Musa akawaambia ngoja muone Bwana atakavyowapigania
nanyi mtakaa kimya. Ivo Mungu hakubadilika hata dakika ya mwisho. Ivo nawe mpendwa usibadilike hata dakika ya mwisho halleluyah halleluyah.
"BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya."
Kutoka 14:14
Na biblia inasema Mungu akafanya njia katikati ya bahari ya Shamu ndivyo hivyohivyo itakavyokuwa kwako katika jina la Yesu. Bahari ya shamu ni jaribu ndani ya jaribu ilo Mungu atafanya njia. Na njia ambayo walipita. Wana wa Israeli wamisri watakapokuja na majeshi na mfalme wao. Hawatafanikiwoa maana ile njia ilikuwa maalumu kwa ajili ya wana wa Israeli.Biblia inasema majeshi ya wamisri nyuma walijaribu kupita njia ileile waliyopita wana wa Israeli walipita na bahari ikawameza. Ndivyo itakuwa kwa wote wanaokufuatilia. Kuna watu baada ya Mungu kukufanikisha watatamani kukuangusha lakini kwa kuwa wapo chini ya Nebukadreza hawana ufahamu wa MUNGU. watatumia au watataka kutumia njia iyoiyo ili kukufuatilia kukuangusha kukuangamiza. Biblia inasema walipojaribu kufuata ile njia bahari iliwameza. Na wakangamia wote.
Mungu awabariki wote.
josephntandu@gmail.com,0713297066

Mtumishi Mungu akubariki kwa kuanzisha hii blog, itatusaidia kueneza injili.
ReplyDelete