WAKRISTO WENGI SANA WANA TATIZO KWENYE IMANI YA KUPOKEA
Bwana Yesu asifiwe Mungu katupa neema tena ya kujifunza neno lake. Mda wa kumlisha mtu wa ndani. Tunamshukuru yeye sifa na heshima ni za kwake yeye Tunamrudishia Ameen
Message: WAKRISTO WENGI SANA WANA TATIZO KWENYE IMANI YA KUPOKEA.
Bwana Yesu asifiwe! Niombe macho yako ya rohoni hapa maana ukielewa hapa na ukavuka tayari wewe utakuwa umeruka kitanzi cha wakristo wengi wanachotembea nacho. Bwana Yesu asifiwe sana.
Wakristo wengi wanaomba lakini hawapokei majibu. Yes! Nasema hawapokei majibu. Yani manake wanaomba vizuri sana majibu yanakuja lakini majibu yanapokuja hawajui jinsi ya kupokea hayo majibu. Nazungumzia "IMANI YA KUPOKEA" wakristo wengi wanaimani ya kupeleka manake wakiomba watapokea, lakini si kwamba majibu hayaji majibu yanakuja. Majibu yanakuja lakini hawajui jinsi ya kupokea majibu. Kuna mtu bado hanielewi. Ngoja nitoe mfano; wakristo wengi wana imani ya kupeleka maombi manake ni sawa na wewe unayocheque mkononi kivipi? Baba yetu ibrahimu si alibarikiwa na kukabithiwa kila kitu? Iyo ndo cheque unayo mkononi. Na cheque iyo ni ya pesa nyingi. Wana imani ya kwenda mpaka bank kwenda mpaka kwa cashier alafu baada ya kumkabithi wanageuka wanaondoka wanaacha ela bank. Iyo ndo imani ya wakristo wengi halleluyah! Halleluyah!
Wakristo wengi wanakwama hapo na wanabaki kulalamika why! why! why! Yesu alifundisha jinsi ya kuomba na kupokea. Twende kwenye maandiko sasa!
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. - Wafilipi 4:19
Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. - 1 Yohana 5:14,15
Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; - Isaya 1:19
Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. - Mathayo 21:22
na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. - Yohana 3:22
Yes! Kama unavyoona maandiko Yesu alitufundisha kuomba na kupokea. Kuomba na kupokea lakini yote hayo bila imani hakuna lolote tunalolifanya, angalia mstari Yohana 3:22 anasema lolote tuombalo twalipokea kwake kwa kuwa twazishika amri zake. Na kuyatenda yapasayo machoni pake. Omeona sheria ya kupokea. 1.kishika amri zake? Amri zipi yale aliyoyandika katika biblia sio kuyashika tuu maana wengi tunayashika na kuyajua na tunayaimba. Na hayo tunayoyashika tunayaweka katika matendo ndo mana anasema na kuyatenda yapendezayo machoni pake. Nikupe mfano umemuomba Mungu kwa imani. Manake umeshika amri zake. Ukitoka kuomba tuu unaanza kuwaza njia za shetani za kupata ela kwa kutapeli,kudanganya ofisi,kuzulumu-unakopa kisha hurudishi. Unatumia shortcut. Tayari mawazo yako. Matendo yako. Maneno yako yameendana kinyume na kile ulichoomba wapendwa hapo ndipo wakristo wengi wanapoanguka. Hapo ndipo shetani anapopiga wakristo wengi hataangaika na wewe ukiomba. Hataangaika na wewe ukifunga. Hatahangaika na wewe ukitoa sadaka. Yeye ataanza pale baada ya kukamilisha imani iyo ya kutoa. Atakachofanya atakuletea majaribu ili imani yako ya kupokea iendane kinyume na kila ulichokuwa unaomba. Na hapo ndipo kuna fumbo la imani. Unaomba pesa lakini ushafikiri uibilisi. Jinsi ya kupata ela baada tuu ya kuomba. Iko mianya ya kupata ela kazini kwa njia za uongo tayari umeanza mchakato. Tayari matendo yako yamekinzana na kile ulichokitoa katika imani. Ndo mana nikasema imani ni matendo. Biblia inasema imani pasipo matendo matendo ni vigumu kumpendeza Mungu. Embu tuangalie neno tena.....
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. - Waebrania 11:1
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. - Warumi 10:17
Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa. - Yakobo 2:26
Angalia waebrania 11:1 mimi ninaita ni imani ya kupeleka. Iyo wakristo wengi tunayo anasema ni kuwa na uhakika na mambo yatarajiwayo.
Angalia Yakobo 2:26 hiyo ninaiita imani yakupokea hapo ndipo wengi sana wanachemka. Hapo ndipo wakristo wanapiga marktime, unaomba kila siku unavunja unaharibu unaangamiza lakini baada ya hapo unashindwa iweka imani yako katika matendo. Halleluyah halleluyah. Omeomba kuusu uchumi mzuri umekiri maneno yote ya biblia. ulifunga. ukatoa sadaka. Baada ya hapo manen yako "maisha magumu" "sujui kama nitatoka" "nimeomba mkopo sijui kama nitafanikiwa" tayari hata baada ya kuomba maombi yako huonekani kupokea bado mnyonge. Bado mawazo yako hayakubaliani kile ulichoomba. Ni kama mtu unaomba tuu alafu unasubiri. Yani unaomba lakini huna uhakika wa kupokea. Maneno yako. Matendo yako. Mawazo yako ni tofauti na maombi yako. Ni tofauti na kukiri kwako. Ni tofauti na neno unalosoma na kuamini. Sasa umeanza kunielewa nachoongelea kuwa wakristo wengi hawana shida na imani ya kutoa isipokuwa wamekwama kwenye imani ya kupokea. Hawajui kupokea. Iko hivi! Ukishatoa imani. Kuweka imani ya kupokea manake matendo yako maneno yako. Mawazo yako ya support kile ulichokitoa katika imani? Wangap wananielewa? Ukivuka hapa utashangaa miaka uliyopoteza kuombea kitu kimoja halleluyah. Sema maneno ya biblia wakati wa shida. Mfano Mungu ndio mwanzo na mwisho kwa iyo ili nalopitia pia analijua. Ninayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu hata hili naliweza. Yesu ni njia hata hili atanifanyia njia. Fedha na dhahabu yote ni mali ya Bwana ivo sina wasiwasi Nitapata fedha kwa Mungu wangu. Yesu ni maji ya uzima. Yesu ni njia. Yesu ni jibu. Yani kukiri namna hii wakati kila kitu kinakupinga wakati unaona giza kutoka moyoni huko ndiko imani ya kupokea. Ukijifunza haya mambo utashangaa jinsi utakavyobadilika mwilini na rohoni. Sasa kuna aina mbili za imani muhimu sana kuelewa ili
1.imani haba
2.imani dhaifu
Imani haba- manake inatokana na mtu kutokuwa na taarifa za kutosha kuusu ufahamu wa Mungu. Juu ya swala husika hiyo ndo imani haba. Ngoja tuangalie maandiko tena.
Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. - Mathayo 17:20
Bwana Yesu asifiwe. Angalia hapo juu Yesu kawambia nyie mmeshindwa kuambia mlima huu ngoka si sababu hamna imani ni sababu imani yako ni haba. Yani pungufu. Wengi wakristo si kwamba hatuna imani bali tuna imani pungufu manake nini? Ufahamu wako wa jambo husika mfano uchumi na Mungu anasema nini ni mdogo. Biblia inasema imani huja kwa kusikia si ndio wapendwa. Kama unashida ya uchumi hakikisha kwanza imani yako kuusu uchumi wa Mungu uko juu. Tafuta maandiko ya kuusu uchumi. Hata mia (100 )yasome yarudie na kuyarudia usiseme nishayasoma endelea biblia inasema imani huja kwa kusikia. Unavyosoma lile neno linatendency ya kuongea na wewe. Kile unachokisikia baada ya kusoma neno la Mungu ndio imani. Na kila unaposoma ujue unatapa message nyingi sana. Tafuta mahubiri kuusu uchumi mengi sana. Tafuta vitabu vya watumishi wa Mungu wanazungumzia uchumi vs Mungu sikiza audio. Angalia video.over and over and over again. Mpaka uanze kupata ile amani. Mpaka uanze kuona maana kwa kusikia huko kwa bidii sana ndipo imani yako inakuwa kubwa. Halleluyah wengi hatuna utaratibu wa kutafuta ufahamu wa Mungu. Ndo mana shetani amekufunga na facebook. Twitter na ujinga wote. Mapicha ili haya yote usiyaelewe. Kuna vitabu vingi sana vinaelezea imani! Mpaka leo umesoma vingap? Umefanya ili kuongeza ufahamu wako? Hii inaitwa imani haba.
Imani dhaifu; iko hivi ni kufahamu kitu vizuri kabisa alafu kutokueka katika matendo wakristo hawa watafundisha. Watashuhudia lakini hawataka weka imani yao katika matendo halleluyah! Wengi pia wanatatizo hapa. Wanajua biblia kutokea mwanzo mpaka ufunuo. Wanajua historia yote. Wanajua matukio yote hata ukimwamsha usiku ukimsomea neno atakuambia imetokea katika kitabu gani lakini watu hawa kuweka kile wanachokiamini katika matendo ni shida. Mfano anahubiri kumtegemea ndugu ni laana lakini baada ya hapo anakubomu ela. Anahubiri uponyaji baada ya hapo anampigia simu Dr. Kuwa anawasiwasi na hali yake. Anachoshuhudia. Anachohubiri. Anachofundisha sicho anacho kiwaza wala kutenda wala kusema anapokutana majaribu. Bwana Yesu asifiwe sana. Sasa utanielewa ninaposema Wakristo wengi wanatatizo la imani ya kupokea halleluyah. Mtu uyu ataenda kila semina. Atasoma vitabu. Atasikiza mahubiri lakini anachotafuta ni kufuraisha nafsi yake wakati ule. Anachotafuta kupata amani wakati ule. Ndio wengi wanapenda nyimbo za dini kuliko mabubiri kwa nini ni sababu wanatafuta faraja ya mda. Wanatafuta kusikia amani ni sawa ni nzuri lakini sasa yako wapi?matendo baada ya hapo. Halleluyah halleluyah glory to God. Nampenda Yesu. Wapendwa nina hakika Mungu leo kakuvusha.
Sasa tunafanyaje? Tengeneza mapungufu hayo ambayo leo Mungu amekuonyesha. Bwana Yesu asifiwe sana.
Kama hujaokoka hakikisha unaokoka hakuna jinsi utamshinda ibilisi kama haujasurrender kwa Yesu. Mpe Yesu maisha yako. Kuokoka ni kuruusu Yesu Yesu aishi maisha yako. Ivo muhimu sana kama unataka kuona mabadiliko hayo hapo juu jikabithi kwa Yesu kwanza. Na hutajuta.
Maombi:
Roho mtakatifu,Roho wa Mungu
Ewe msaidizi wangu,ewe rafiki yangu
Siwezi imani hii bila wewe,imani bila matendo ni machukizo kwa Mungu. Nisaidie roho mtakatifu. Katika jina la Yesu. Roho wa Mungu nijalie kile nachosoma kwenye biblia. Kila ninachoomba nikiweke katika matendo katika jina la Yesu. Matendo yangu maneno yangu mawazo yangu yasikinzane na imani yangu ya kutoa imani yangu ya kupokea katika jina la Yesu. Tutie nguvu roho hata majaribu yanapokuja nisibadilike katika jina la Yesu.Roho mtakatifu nisaidie Yesu mwana wa Mungu nisaidie katika jina la Yesu. Nisaidie juu ya imani yangu haba. Nisaidie juu ya imani yangu dhaifu niende hatua ingine katika jina la Yesu.Kwa utukufu wa jina lako. Katika jina la Yesu ibilisi asinishinde katika jina la Yesu. Bwana Yesu asante kwa kuwa nimepokea ushindi leo na umeniweka huru asante Yesu. Katika jina la Yesu nimeomba amen.
josephntantandu@gmail.com
0713297066.

Asante sana kwa somo zuri limenivusha kutoka nilivyokuwa,watu wengi tumekwama hapa ila sasa nimevuka.jina la YESU lipewe sifa.ubarikiwe Mtumishi Joseph
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteUBarikiwe mtumishi wa Mungu maana nimejengeka katika Imani
ReplyDelete