ARDHI IMEBEBA ROBO TATU YA MAISHA YA BINADAMU
Bwana Yesu asifiwe. nimrudishie Mungu utukufu kwa neno lake. naomba Mungu akupatie kitu cha kukusaidia unapoanza kufuatilia somo hili. Na akupe ujasiri wa kufanya yakupasayo!
Somo: "Ardhi imebeba robo tatu ya maisha ya
binadamu"
Kwanini ardhi? Na
sio maji? Au Anga?
Mwanzo 12
1 Bwana
akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba
yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na
kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye
akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
4 Basi Abramu akaenda, kama Bwana
alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka
sabini na mitano alipotoka Harani.
*pigia mstari neno HARANI. nitaja kukuonyesha huko mbele.
*Mungu akikuita
ni lazima atakuahidi kitu. Amekuita uokoke jua kuna kitu atakupa.
Amekuita kwenye huduma yoyote jua kuna kitu Mungu atakupa. Mungu ni Mungu wa
mipango na maagano ya kweli si umeona hapo juu Mungu aliingia mkataba na
Abramu, ndipo Abramu akakubali kutoka nyumbani mwa Baba yake.
Tuendelee....
7 Bwana akamtokea
Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu
Bwana aliyemtokea.
8 Kisha akaondoka
huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema
yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki,
akamjengea Bwana madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana.
9 Naye
Abramu akasafiri, akazidi kwenda pande za kusini.
*Abramu
alimjengea Mungu madhabahu. Alijenga wapi? juu ya ardhi.
Tuendelee....
Mwanzo 28-10-13
10 Yakobo akatoka
Beer-sheba, kwenda Harani.
11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku
kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale
akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale.
12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa
juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu
wanapanda, na kushuka juu yake.
13 Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema,
Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii
uilalayo nitakupa wewe na uzao wako.
*Yakobo mjukuu wa Abramu naye akaenda HARANI sehemu ile ile
Babu yake aliyoijenga madhabahu!
*kilichomtoa Yakobo mpaka Harani mimi na wewe hatujui.
Lakini cha kushangaza ikawaje Yakobo akaenda kulala sehemu ileile Babu yake
aliyomjengea Mungu Madhabahu. Wakati huu Mungu bado hajajitambulisha kama ni
Mungu wa Yakobo. Bado alikuwa anaitwa Mungu wa Abramu.
*Alivyolala Yakobo aliota ndoto, kazi imetoka pale alipolala
kuelekea mbinguni. Tena malaika wanapanda na kushuka.
*Ilikuwa imepita zaidi ya miaka ishirini kumbuka
*Mungu akamtokea Yakobo katika ile madhabau, Mungu akaahidi
katika ile madhabau.
*Nataka nikufundishe kitu ulimwengu wa roho wowote haufanyi
kazi bila madhabahu. Uwe ulimwengu wa ibilisi au wa Mungu Yehova lazima kuwe na
madhabau ya kuwapa nguvu au maagizo hao watumishi wa iyo madhabau.
*unauliza nimejuaje? Jiulize kwanini Mungu asiongee kote au
asiahidi kote ni mpaka kwenye ile madhabahu. Na madhabau ile ilijengwa katika
ardhi. sababu binadamu yoyote mambo yote yalianzia kwenye ardhi.
Hata mwili wako ni udongo. Vitu vyote juu ya ardhi vyote
vimejengwa na ardhi. Kwa iyo ardhi ni mbegu ya Mungu. Mwingine atauliza ardhi
ilitokea wap? Ardhi ni pumzi
ya Mungu. Iyo pumzi
moja tuu ya Mungu ndiyo iliyotengeneza kila kitu. Juu ya ardhi, simu
unayoisoma, makaratasi, pesa, nyumba unayoishi kila kitu juu ya ardhi
kilitokana na udongo. Bwana Yesu asifiwe sana.
Tuendelee...
Mwanzo 28-16-19
16 Yakobo akaamka
katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.
17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha
kama nini! Bila shaka, hapa ni
nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.
18 Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa
lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na
kumimina mafuta juu yake.
19
Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza
uliitwa Luzu
*Yakobo akasema
BILA SHAKA HAPA NI NYUMBA YA MUNGU,NAPO NDIPO LANGO LA MBINGUNI
*tutafakari neno
hilo hapo sehemu hii pangekuwa kuna madhabahu ya ibilisi je ingekuwaje? Yakobo
pengine angeota
anakimbizwa na wanyama, nyoka,au ndoto zozote
zile za kutisha. na angeona ngazi imeanzia juu ya ardhi kushuka kuzimu. Kushuka
chini ndiko kuzimu. Lakini ameota malaika wanapanda ngazi na kushuka kuelekea
mbinguni.
*ardhi nyingi
tunazoishi zina madhabau ya ibilisi. Labla si wewe uliyeweka lakini aliyekuuzia
na aliyemuuzia aliwahi kuweka madhabau za ibilisi.
Angalia mda ambao Abram alijenga madhabahu
mpaka Yakobo alipoenda palepale. Ivyo madhabahu haina mda.
Inaweza ishi milele. Ndo mana nyumba nyingi
hazina utulivu. Ndio maana mwana wa Mungu ukienda kukaa sehemu yenye madhabau
ya ibilisi lazima upate vita.
Tuingie ndani
kidogo....
Nia ya Mungu ni
nini?
ISAYA 32:18
18 Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na
katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu.
*masakani manake
ni mahali unapoishi, Mungu kasema watu wangu watakaa kwa amani na kupumzika
penye utulivu.
*Ilo neno
linazungumzia ardhi ile yenye madhabau ya Mungu. Ardhi ambayo ina madhabau ya
ibilisi huwezi kuwa kuna utulivu, hakuishi magonjwa, hakuishi ugomvi, hakuna
amani. Watu wanaoishi
nyumba iyo mapito hayaishi. Ni vita baada ya vita baada ya vita. Unaweza kuta familia
nzima inaisha kwa pressure au cancer au kuumwa kichwa watu wanakufa hawajui
kumbe ardhi waliyokalia kuna ngome alifukiwa mzima,
kuna jogoo alifukiwa mzima wakishafanya ivyo
manake wamemkaribisha pepo au wamefungua mlango wa kuzimu. Na iyo tayari ni
madhabau, kuna mbuzi mzima alifukiwa,
kuna kondoo mzima alifukiwa kitendo cha kufukia
tuu tayari pepo linakuja linakaa kwenye iyo ardhi, panakuwa madhabau na watu
sasa wanatii sheria za yule pepo bila kujijua.
Mahali popote
penye madhabau ya ibilisi juu yake lazima ilo
anga aje mkuu wa giza ili
kucontrol hao watu. Ndo anawasukuma kufanya matambiko. Kumwaga damu. Watu
wanakuwa
controlled kupitia iyo madhabau, kwa iyo
madhabau sasa ndo inayowapa wachawi, waganga wa kienyeji nguvu ya kutawala ilo
eneo nguvu.kwa iyo unaweza kukuta mtaa mzima kuna nyumba moja tuu ipo madhabau
ya ibilisi!
Serikali yote ya
ibilisi ya huo mtaa lazima waende hapo kupewa maelekezo au kupewa nguvu. Sasa
wewe mpendwa hujui A wala B umeenda
kukodisha, au kupanga au kukaa,kununua tayari ile madhabau inaanza kukupiga
vita.haufanikiwi katika lolote. Kwa kuwapa wale margent wa kuzimu nguvu za
kukushambulia.
Tuingie ndani
zaidi....
Ufunuo 2-12-13
12 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo
andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.
13
Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika
sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi
wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
*Nataka nikupe
siri ili uone utamu wa biblia kitabu cha ufunuo ni majibu ya makanisa yale saba
(7) ya Kristo! Ndio maana unasikia anasema na malaika wa Pergamo andika,
malaika wa Efeso, Filipi haya ni makanisa Yesu alikuwa anajibu
majibu yao, Yesu alikuwa anawaita malaika
anawambia andika uwapelekee majibu hayo. Ndio maana anasema andika anawapa
majibu hayo ili wawapelekee makanisa hayo ndio maana anasema andika!
Anasema napajua
ukaapo ndipo penye kiti cha enzi cha shetani! Anasema najua umeshika sana jina
langu, hukuikana imani yangu, hata Antipa shahidi yangu, aliyeuwawa kati yenu
akaapo shetani. Yesu alikuwa anawaambia kuwa hapo
mnapokaa kuna kiti cha enzi cha shetani, kuna
madhabau ya shetani! Ilo ndilo tatizo. Yani manake iyo ardhi mnapoishi kuna
madhabahu ya shetani. Kwa iyo ili kanisa lilikuwa linapata vita alafu alijui
vita inatoka wapi,
sasa ndo wanamuuliza Yesu maswali magumu
hawaelewi. Ni kama wewe jinsi ulivyokazana na wokovu lakini bado unapata
vita.... Haviishi. Haya majibu yametolewa mpaka kwenye kanisa la leo, watu
hawasomi biblia tatizo. Bwana Yesu Asifiwe.....
Tuingie ndani
sana sasa.....
Ufunuo 13-1-2
1 Kisha nikaona
mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya
pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa
chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha
simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
*Wote tunafahamu
fahamu stori hii uyu alikuwa ni mnyama wa ajabu aliyotoka chini ya bahari. Ni
mnyama ambaye Ibilisi akampa nguvu zake na kiti cha enzi na uwezo mwingi.
Ndio maana kuna
sehemu unaweza ukalala ukaota unakimbizwa na wanyama mara dubu, simba, chui jua
kwamba hapo ulipolala kuna viti vya enzi vya ibilisi. Sasa nikupe siri ingine
hivi vitu haviji kama kuja tuu.
Wakitaka kuweka
kiti cha enzi cha shetani watazika kitu kizima, na kwa manuizo ya maneno ya
maagano. Si kila kaburi ni kaburi makaburi mengine ni madhabahu!
Kabla ya kuzika mtu pengine walitanguliza
mbuzi mzima au kuku mzima. Mizimu ni watu waliokufa. Wanawasiliana nao kwa
kupitia mapepo. Mambo haya yanatisha lakini lazima tuyaongee ili ujue uzito wa
ardhi, ardhi ya namna hii au ukoo wa namna hii wewe mtakatifu wa Mungu ni
lazima upigwe vita. Joka atampa yule mnyama nguvu ya kukupiga vita. Kukufanyia
makufuru.
*Mstari 1 anasema
mwenye makufuru mengi, ndio maana ukoo wowote au familia yoyote mtu akiokoka
tuu wanamtenga unafikiri ni kwa nini?si wao! Hata kama hawamwambii lakini kuna
mipaka flani utaiona tuu baina yako wewe
na wao. Ni sababu ya uyu mnyama wa ibilisi.
Unaweza ukaokoka na ukapigwa vita na kila mtu! Kumbuka anayekupiga vita ni
ibilisi maana kwa wewe kuokoka manake utaweza kuzuia madhabahu kwa upande wa
Baba yako zisifanye kazi. Kwa upande wa Mama yako zisifanye kazi.
Hapa ndipo
unaposhangaa vita haziishi, ndipo wapendwa huwa wanapata shida hasa tena wewe
ndio wa kwanza kuokoka.
Kwa iyo ile madhabahu ya uyu mnyama
inatengeneza chuki na watu waliokuzunguka hata ndugu zako au Baba yako ili
wakupige vita.utaona tuu kwa matendo hata kama hawasemi. Na kuna baadhi ya vitu
hutashirikishwa.
Ibilisi anawawekea hasira ili wakumalize.
Kinacholindwa ni wewe usije gusa ile madhabahu maana ukigusa tuu umeharibu ndo
mana unapata vita katika kila kitu. Hawana nguvu tena.
Kuna shuhuda
moja; dada mmoja toka mwanza alikuwa mwislamu mbegu ya Kristo ikamdondokea
moyoni mwake si unajua kunatofauti ya kuokoka kwa kuombewa (kusukumwa kwa
maombi) na mbegu ikidondoka moyoni sasa uyu dada aliyekuwa kwao mwislamu
kabisa.
mbegu ya Kristo ilidondoka, akawa anaenda
kuomba na baibui lake kanisani. Sasa Baba yake ambaye ni mkubwa wa mizimu kuna
namna wale mapepo walimjulisha maana mambo yao yalikuwa hayaendi tena,
basi
wakamchunguza kupitia shangazi yake wakamkanya yule Dada. Yule Baba akamwambia
mtoto wake ukienda tena kusali huko wewe si mtoto wangu tena. Kama unavyojua
mbegu ya Kristo ikikudondokea huwezi
jizuia akaenda
tena. Yule mzee alijua maana kila akienda ile
madhabahu ya yule mzee haifanyi kazi. Akakasirika akachukua bunduki akaikoki
ile anataka kufyatua yule dada akasema kuna mwanga mweupe ukaja mbele ya ile
bunduki kwenye lile tundu la kutolea risasi, akifyatua haitoki.
Akilenga juu inatoka. Kwa iyo ndo ikawa pona yake. Sasa
jiulize kwanini mtu aombe tuu mwingine atake kumuuwa? Jua hili limnyama
linauwezo wa kumbebesha mtu hasira au watu hasira wakawa adui zako.
Na utashangaa ukibomoa tuu iyo madhabahu ya uyu mnyama watu haohao waliotaka kukuuwa
wanakuwa tena upande wako. Madhabahu kwenye katika ardhi ni kitu kina nguvu sana.
*Shetani huzipa nguvu madhabahu zake ili kufanya vita na
watakatifu.pamoja na wewe
*ukiona unaenda sehemu unapata vita unaenda sehemu ingine
hupati vita jua hapo unapopata vita chini kuna madhabahu ya ibilisi.
*ukiona vita haviishi, vinajirudia kila mara au tatizo
linamwendelezo jua katika iyo ardhi unayokaa kuna madhabau ya ibilisi
*90% ardhi ya Tanzania ardhi yake haiko salama kuna madhabau
za ibilisi. Vitu vingi sana vimezikwa
katika ardhi ya Tanzania. Mtumishi mmoja aliwahi toka Kenya kuelekea
Tanzania alipofika mpakani akawa anagawa vikaratasi vya ujumbe wa neno la
Mungu,
anasema alipokuwa
anagawa Tanzania walikuwa wanamtukana matusi ya nguoni kabisa. Alipokuwa
akienda upande wa kenya akigawa watu walikuwa wanamshukuru na kumbariki.
Mungu akamwambia
ardhi ya Tanzania si salama kama ya Kenya. Sehemu nyingi ni malango ya ibilisi. Ndo mana alikuwa anatukanwa
kilichokuwa kinamtukana si wale watu ni
yule
mnyama kupitia
madhabahu ambazo sisi watanzania tumezijenga toka enzi na enzi. Anga letu bado
halijafunguka kama la Kenya.
* Kufanikiwa kwa mtu inategemea na mahali anapokaa. Kwa iyo
vita nyingi wanayopata wapendwa 100% inatokana na ardhi ya kwenu, kwa Baba
yako, kwa mama yako. Ulipopanga, uliponunua. Kama kuna madhabahu za giza hizo
ndizo zinakupiga vita.
Unachokiona wewe katika maisha yako ni matokea ya vita za
izo madhabahu. Ndo mana unaweza lala nyumba moja chumba hiki ukalala kwa raha.
Chumba hiki kingine ukaota ndoto mbaya. Unakimbizwa na simba au kuna mnyama
hata
asiyeeleweka anayetisha.Sasa
kufanya vita na matokeo huwa hakumalizi tatizo. Ni mpaka ardhi iponywe. Ni
mpaka iyo madhabahu kupitia iyo ardhi ivunjwe. Vitu vya enzi vibomolewe. Kuna
mambo utayaombea utavuka lakini Kuna vitu vingine vimefungwa kupitia ardhi.
Inapovunjwa basi
wafalme wa giza wanakosa nguvu, wachawi wanakosa nguvu maana hakuna kitu
kinachofanya kazi bila madhabahu. Ndo mana mtu anaombewa anawekewa mikono na Mtumishi mwenye annoiting kubwa
lakini baada ya mda vita vinaibuka tena.
Ukiona ivyo ujue ni
vita vya madhabahu kupitia ardhi iliyounganika au unganishwa na wewe kwa njia
moja au nyingine. Au jiulize kwanini ukiwa kanisani unasikia
amani sana na hewa
nyepesi hutamani hata kuondoka. Na kwanini ukirudi nyumbani husikii iyo amani
ushawahi jiuliza? Jibu ni kwamba kanisani kumejengwa madhabahu ya Yesu na kwako
hujajenga. Anga halijafunguka.
*Vita vya kiuchumi, ndoa, kutokupata watoto, kazi,
umasikini, na yanayofanana na hayo inategemea sana na ardhi ya maisha yako
ikoje.
Ardhi inaponywa na
kufunguliwa jinsi inavyofunguka ndivyo jinsi wewe unaanza kuona wepesi katika
sehemu zilizokuwa zinakupa wakati mgumu. Ndo mana kuna maeneo ukienda utapata
shida sana
unaweza fikiri hakuna
wokovu. Mfano mtu aliyewahi enda
zanzibar au aliyewahi enda India kule utapata shida sana kuomba au kusoma neno.
Arshi ya kule imeshikiliwa na viti vya
enzi vya ibilisi.
Jinsi ya kuomba
sasa kibiblia ungana nami part B ambayo ndo muhimu kupita yote. Kuombea ardhi
unapoishi, au ardhi ya kwenu. Na jinsi ya kuombea sehemu za kazi au biashara
pia kuna maombi yake tofauti. Tutaelekezana. Jina la Bwana libarikiwe
josephntandu@gmail.com,0713297066
Ubarikiwe mno nimelipenda somo la Kuombea Ardhi kwakweli nimefunguliwa mno, Ubarikiwe mno kwa ufafanuzi huu leo ninaamini nimekuwa mpya katika Jina la Yesu ardhi ninayokaa inaenda kutakaswa kwa Damu ya YESU🙏🏿
ReplyDelete