IMANI INAFANYA KAZI KWA KUTAMBUA MAMLAKA ILIYO KATIKA JINA LA YESU
Bwana Yesu asifiwe.
Tupandishe imani zetu kwa neno hili na
tafakari yake. Neno unalijua tuangalie lugha ya neno ya leo.Nimshukuru Mungu wa BWANA WETU YESU KRISTO.ni mda mwingine tena wa kujifunza neno la Mungu
Luka 7
2 Na mtumwa wake
akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa; naye ni mtu aliyempenda sana.
3 Aliposikia habari
za Yesu, alituma wazee wa Wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa wake.
4 Nao walipofika kwa
Yesu, walimsihi sana wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili;
5 maana, analipenda taifa letu, naye
alitujengea sinagogi.
6 Basi Yesu akaenda
pamoja nao. Hata alipokuwa si mbali na nyumba yake, yule akida alituma rafiki
kwake, akamwambia, Bwana, usijisumbue, maana mimi sistahili wewe uingie chini
ya dari yangu;
7 kwa hiyo nilijiona
sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona.
8 Kwa maana mimi nami
ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia
huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.
9 Yesu aliposikia hayo alimstaajabia,
akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli
sijaona imani kubwa namna hii.
10 Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani,
wakamkuta yule mtumwa ni mzima.
*Halleluyah halleluyah! Neno hili watu wengi wanalijua na
wameshalisoma nachotaka kukuuliza kwanini akida alisema sema neno moja tuu.
Tatizo si imani aliyokuwa nayo!
Tatizo Ni nini
kilimsukuma kusema vile !?. Ukijua kilichomsukuma kusema ilo neno "sema
neno moja tuu" ukikijua hicho kilichomsukuma basi imani yako itatoka
sehemu moja kwenda sehemu ingine.
Imani si kusikia tuu Bali na kuamini, wengi kusikia tunasikia.
Lakini hatuamini. Ile hakika ya mambo yatajariwayo huwa haikamiliki pamoja na
kusikia neno. Imani
huja kwa kusikia.
Wengi tunasikia. Imani ni hakika ya mambo yatajariwayo! Hapo ndipo tunakwama.
Umeamka huna hata 100 mfukoni. Kukiri kusema mpaka ifike saa 10 jioni nitakuwa
na mil 1, mfukoni.
Ndani mwako ukisema ni kama Kuna Moto unakurudia! Siyo? Iyo
inataka imani ya hakika . Hatuamini mambo yatarajiwayo sababu kutokujua au
kutambua mamlaka ya jina la Yesu.
Kupitia kusikia kwa
neno. Ngoja niongee lugha rahisi. Ni hivi bila kutambua mamlaka ya jina la Yesu
huwezi amini kinachotaka kutokea kutokea.
Angalia hapo juu kwenye ilo neno anapomuelezea Yesu mstari
wa 8, Mimi nami ninamamlaka yangu nikimwambia uyu Nenda huenda. Uyu njoo naye
anakuja. Akida alitambua mamlaka ya
Yesu,ndo mana
akajifananisha yeye na Yesu kwa hapa duniani, Mamlaka iliyobebeshwa kwenye
ardhi, katika anga na bahari na mbingu zote,soma waefeso 1-17-23.kilichofanya Yesu akasema sijaona imani
kubwa namna hii ni hakika ya kutambua mamlaka
na kuijua kuwa Yesu
Hana limitation kuwa anaweza kufanya lolote.Yes! Iyo ndo ilimfanya Yesu
amshangae! Ivyo hata tatizo lake haliitaji Yesu afike kwake! No! Sababu tayari
hata kwenye sauti ya Yesu
tuu akitamka lile
tatizo linasikia haijalishi yupo au hayupo. Kuna mamlaka. Ndo mana huitaji
kumuona Yesu unahitaji jina lake ulitumie kwa imani.Unajua kila kitu kinasikia
sauti ya Mungu. Ndio maana watumishi
wakisema pokea
uponyaji lile neno linatoka na mamlaka Yesu yani nafasi katika kuponya linaenda
kwenye ugonjwa. Ugonjwa ndio unaisikia lile neno sio masikio ya kichwani. Ugonjwa una
masikio,Biblia inasema Bwana hulituma neno lake, kuwaponya. Kinachomponya mtu
wewe kusikia na masikio yako. No ni ile situation
imesikia ile mamlaka
ya jina la Yesu na siyo masikio yako ya binadamu. Kama ni masikio inakuwaje
unasikia kwa masikio then unapona mgongo? Hili ni somo lingine tutaangalia
another time. katika
ulimwengu wa roho
lile tatizo linasikia. Kinachofanya watu wengi wasiamini neno au wazoee neno,
au neno walione ni kitu cha kawaida ni kutokutambua
mamlaka ya Yesu kwa
uzito.YANI HILI NENO LIMEBEBA MAMLAKA
KIASI GANI AU NAFASI KUMALIZA TATIZO LANGU?
SITUATION YANGU? yani nafsi ya ilo neno katika shida yako iyo ndo shida
ya wengi katika imani , kumbuka mfano wa
Bahresaa kule juu. Ni
kama vile mtu akitaka kukusaidia utataka ujue uwezo wake kwanza, anafanya nini?
Mfano Raisi akisema nitakusaidia utakuwa na hakika.sababu ya nafasi aliyonayo.
Watu wasio na imani si kwamba
hawasomi neno, si
kwamba hawataki kuliamini neno hapana.si kwamba hawaombi hapana Its simple huwezi kulipa tatizo lolote uzito
Ni mpaka liwe na uzito kwenye akili
yako. Hujanielewa! Kwenye mioyo Yao Yao hakuna hakika
kama mamlaka ya jina la
Yesu itamtoa kwenye magumu,yani hawaamini ilo neno kweli Lina mamlaka ya
kumaliza shida yake iyo ndo tatizo.jinsi anavyoamini ndio matokeo
anayopata,majaribu anayopitia,
hawana hakika ya
mamlaka iyo isiyoonekana kama kweli itamsaidia kwenye tatizo lake.ingawa neno
wamelisikia. Ukisema Bahresaa, Ni tajiri
unamwelezea mtu
mwingine ule uzito
unaojua wewe kwa mwingine hawezi amini. Chukulia Bahresaa humfahamu kabisa
alafu
anakuambia mtu kuhusu
bahressa, utasikia lakini hutaamini kwa uzito ule jinsi yeye anavyomuamini ni
mpaka pengine uanze kuona bidhaa zake kwa wingi masokoni, ukiona azam
television, ukiona magari ya bahressa yakienda mkoani.
Ukiona miradi yake mikubwa ndipo Utaamini.Kwa iyo ukiwa na shida ya mil 10,
ukaambiwa bahressa kaelezewa tatizo lako unatakiwa ukaonane naye, kesho saa
tano! Je hutakuwa na hakika
tatizo lako kuisha? Jibu ni ndiyo! Iyo hakika
imetoka wap? Iyo hakika imetokana na wewe kuujua uwezo wa bahressa. Nafasi
ya bahressa! Kama wengi tungeenda kwa
Yesu kwa nafasi yake
katika neno lake la ahadi! Au la agano kwa kuitambua hakika ya mamlaka ya Yesu,
juu ya tatizo tulilonalo basi tungesogeza milima mikubwa mbele yetu.ukiwa
unaitambua unaijua na
unaikubali mamlaka ya
Yesu juu ya ilo neno kwenye biblia! Na ilo tatizo lako basi mambo Mengi
ungeyavuka. Na utapokea kila ahadi bila wasiwasi na itatokea kwako hata kama
imekawia hutakuwa na mashaka.
IMANI = kusikia neno+
kuwa na hakika ya mambo yatajiriwayo haina ya mambo yasiyoonekana + kuamini
mamlaka inayoenda kutekeleza mambo yatajiriwayo.
Embu tuangalie watu waliokuwa na matatizo ya kuijua mamlaka,
kuitambua na kuiamini.
Marko 9:23
23 Yesu akamwambia,
Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.
24 Mara babaye yule kijana akapaza sauti,
akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.
25 Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika
mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi
nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.
*wengi stori hii mnaijua. Huyu Baba haukuitambua nafasi ya
Yesu ya Kimamlaka . Kule juu ndo mana alisema ukiweza unaweza nisaidia, akasema
yote yawezekana kwake aaminiye. Ndo mana wanafunzi wa Yesu
walishindwa kumtoa
yule pepo kwa yule kijana. Tatizo halikuwa kwa wanafunzi wa Yesu tatizo
lilikuwa kwenye imani aliyoibeba yule Baba mwenye mtoto. Alivyotambua ilo ndo
mana akamwambia Yesu nisaidie kutokuamini kwangu.
Mathayo 8-23-27
23 Akapanda chomboni,
wanafunzi wake wakamfuata.
24 Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo
kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.
25 Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha,
wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia.
26 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa
imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.
27 Wale watu wakamaka wakisema, Huyu ni mtu wa
namna gani hata pepo na bahari zamtii?
* hapa wanafunzi wa Yesu hawakutambua nafasi ya Yesu ya
kimamlaka ndio maana walihangaika. Walivyoona wameshindwa ndipo
akamwamsha, si
unaijua hii stori ya mawimbi yaliyotikisa mtumbwi baharini na Yesu akiwa ndani
yake? Yesu akawaambia mbona mmekuwa waoga wenye imani
Haba? Manake nini
kwanini hamkuniamsha mda wote huo! Hamkuniamini ni mpaka mmeshindwa. Kitabu cha
Luka stori hii inaelezea jinsi ilivyokuwa walikuwa
wakitoa maji kwenye
mtumbwi kabisa. Fuatilia stori hapo juu. Ni mpaka walipotambua nafasi ya Yesu
ya kimamlaka.katika mtumbwi. Ndio mana wakasema uyu ni mtu wa aina gani hata
pepo zinamtii?
SASA TUANGALIE WATU WALIOKUWA WENYE IMANI NA WALITAMBUA
MAMLAKA YA YESU. AU NAFASI YA YESU KATIKA KUWAPONYA
Marko 9-27-31
27 Yesu alipokuwa
akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema,
Uturehemu, Mwana wa Daudi.
28 Naye alipofika nyumbani, wale vipofu
walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili?
Wakamwambia, Naam,
Bwana.
29 Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri
ya imani yenu mpate.
30 Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza
kwa nguvu, akisema,
Angalieni hata mtu mmoja asijue.
31
Lakini wakatoka, wakaeneza habari zake katika nchi ile yote.
*Nataka uone imani yenye hakika ya kutambua nafasi ya
kimamlaka aliyonayo Yesu Katika kutatua tatizo Lao. Hao vipofu walikuwa
hawaoni. Sembuse wewe unayeona na kusoma biblia na kuangalia
shuhuda. Kutokuona
manake Ni kutokujua njia ya jawabu ya tatizo lako. Wao walikuwa hawaoni kabisa
macho ya damu na nyama. Kwa iyo imani Yao
ilijengeka kwa
kusikia baada ya kusikia mioyoni mwao wakatambua nafasi ya kimamlaka aliyonayo
Yesu,ingawa hawaoni unauliza nimejuaje? Yesu
aliwauliza mnaamini
kuwa naweza kufanya hivi? Yani manake mnatambua kuwa ninayo mamlaka ya kuponya?
Mnahakika mamlaka yangu yanaweza kuwaponya? Iyo ndo maana yake!
Wakamwambia naamu
Bwana. Sasa angalia! Wasingetambua Yesu asingewaponya! Wasingeijua nafasi ya Yesu wasingeponywa. Na
wasingeikubali nafasi ya Yesu pia wasingeponywa. Wengi
leo hii aidha unaijua
unaitambua lakini hatuikubali nafasi ya Yesu katika matatizo yetu. Hatukubali
neno la Yesu katika kutusaidia. Kuijua ni kitu kingine, kuitambua ni swala
lingine bali kuikubali.
Kuikubali ndio
connection yako wewe na Yesu. Manake unaweza soma neno alafu wewe mwenyewe
umelielewa lakini akili yako haikubaliani kuwa ili neno kweli linaweza kungoa
huu mlima. Na hii
hutokea sababu ya
wewe kulinganisha maneno. Badala ya kulinganisha mamlaka. Kinakujia cha kwanza
ni ukubwa wa tatizo, ugumu wa tatizo, au historia ya tatizo. Kinachotakiwa cha
kwanza ni
uwezo wa mamlaka ya
Yesu. Kisha neno la Yesu limesema
nini. Baada ya kutambua sasa ndipo jina la Yesu litafanya kazi vizuri kwa imani
Hili ndilo tatizo kubwa katika imani zetu siku hizi. Huwezi kukivalue kitu
kama hujui thamani yake. Huwezi tambua uwezo
wa jina la Yesu kama hujui mamlaka zake. Kama hujui nafasi ya
mamlaka katika tatizo lako. Ukiwa unajua
nafasi ya mamlaka katika tatizo lako. Au nafasi ya Yesu kupitia neno lake. Basi
nakuambia utaangusha milima. Jina la Bwana libarikiwe.
kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment