IMANI YA HAKIKA NI IPI?
Bwana Yese asifiwe wapendwa, Ninamshukuru Mungu Baba wa mbinguni kwa kutupa nafasi ingine tena ya kujifunga neno la imani, sifa na utukufu kwa Yesu pekee.
"IMANI YA HAKIKA"
WAEBRANIA 1:11
1 Basi imani ni
kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
* embu leo
tuangalie lugha tofauti ya hili neno.
Imani ni hakika. Hakika baina ya mambo yasiyoonekana. Yani hayapo.
Nikuulize swali
unalala usiku kesho unapanga mipango yako. Kitendo hiko manake ni hakika. Tena iyo hata waislamu
wapagani wana iyo imani.
Ukisema ninaweza kuruka juu una miguu miwili. Una afya, iyo
siyo imani inayoongelewa hapo juu. Bali Yule mtu asiyekuwa na miguu! Au hawezi
kusimama akisema nina
hakika nitaruka juu baada ya kuombewa ikatoka moyoni mwake basi iyo hakika basi
ndiyo imani yake.
Ukisema nina hakika nitanunua gari na ela unayo iyo siyo
imani inayoongelewa hapo juu. Maana
ela unayo. Imani ni hii huna pesa kabisa. Au pesa haiwezi hata
kununua baiskeli. Alafu inatoka moyoni unasema
nina hakika kwa neno hili la Bwana nitanunua gari. Na ukaamini na kukubali
moyoni mwako.
Ukiwa unafanya
kazi kazini ukasema nina hakika mwezi huu nitapata mshahara iyo siyo imani
inayoongelewa hapo. Maana kama una kazi ni kawaida utalipwa tuu.
Imani ni hii mtu asiyekuwa na kazi kusema nina
hakika mwezi unaokuja nitapata kazi nitapokea mshahara na nitatoa fungu la 10.
Imani ni kuzungumza kitu ambacho huna hakipo. No
possibilities. Ila unaongea sababu neno
limesema na ukaamini lile neno. Imani ni hii kiwete anayetembea chini.miguu
hainyooki kabisa. Kabla ya kwenda kwenye maombi anashona full sute ya mtu mzima
na kusema nikitoka huko nakuja kuvaa
na kutoka out kwa miguu yangu. Imani ni
hii kipofu asiyeona kabisa kabla ya kwenda kwenye maombi atabeba biblia atasema
baada ya kuombewa tuu nitasoma biblia yangu. Imani ni kuwa na
hakika katika vitu
ambavyo havipo. Wengi tunaweka imani katika mambo ambayo yapo kwenye uwezo
wetu. Au ndugu zetu. Imani ni hakika ya mambo
ambayo kwako
hayawezekani na hayapo na unaona kabisa haiwezekani. Lakini iyo haiwezekani
imebadilishwa uliposikia neno la Mungu na unaamini kwa mazingira ya
nje haiwezekani ila kwa neno la Mungu tuu. Kuwa
kwa hili neno Hakuna lisilowezekana. Imani ni kutokusikiliza ndani mwako
kunasema nini au watu wanasema nini. Yani kama
kupingana na dunia
ionavyo! Watu walivyozoea! Au kawaida au utaratibu.au maneno ya watu. Imani ni
kama uchizi flani! Wehu flani wa kiroho! Kuamini
katika taratibu za
dunia watu hawaamini. Kuona vitu ambavyo watu hawavioni. Kusikia vitu ambavyo
watu hawawezi kusikia, imani ni kama kujitenga na msimamo wako bila kurudi
nyuma. Ni
kama kubaki mwenyewe
tuu unayeona njia wakati wengine hawaoni njia Yani wewe unaenda tofauti. Ni
kuamini kile kisichowezekana. Labla nikupe mfano huu!
Luka
30 Malaika
akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto
mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye
juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na
ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno
hili, maana sijui mume?
35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu
atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa
sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
36 Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye
amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita
kwake yeye aliyeitwa tasa;
*Hapa tunaona jambo lisilowezekana kwa akili za Mariam!
Lisilofikirika!hata angewaambia wengine wangembishia ni
yeye na moyo wake!
Offcourse aliguna moyoni, akifikiri akaona haiwezekani! Angalia maswali
anayouliza? Litakuwaje jambo hili? Kitu nachotaka uone hapo malaika hakumwachia
ni mpaka
ameelewa asingeelewa
na kukubali ile mimba isingeingia, ya roho mtakatifu. Angalia jinsi malaika
anamuelezea! Tena tazama jamaa yako Elizabeth yule aliyetasa amechukua mimba
tena ya
uzeeni! Naye ana mimba ya miezi sita. Mariam
akazidi kishangaa! Hee Elizebeth kachukua mimba? Akafikiria Elizabeth ni mzee
alafu tasa alikuwa mzee wa miaka 80, akazidi kushanga sana.
Akasema moyoni kama
mwanamke mzee miaka 80 tena aliyechukua mimba na alikuwa tasa. Basi jambo hili
unaloniambia basi pia kwangu litawezekana, imani kuwa na
hakika na mambo
ambayo katika akili, fahamu, macho masikio haviwezekani, hakika huwa haipigi
hesabu itakuwaje kuwaje hii si kazi yako. Hesabu jinsi
itakavyofanyika anayo
Mungu. Nikuulize swala Musa alikuwa na hesabu ya kugawanya bahari ? Musa
alikuwa na
hakika. How? When?
Siyo maswala yako, wewe unachotakiwa kuamini yasiyowezekana kwako lakini kwa
neno linawezekana. Imani itafanya kazi baada ya kukubali!
Ukishapata hakika
niliyoongelea hapo juu. Basi lazima sasa ndani mwako itakuja kukubali yes!
Inawezekana. Sio mdomoni no ndani kwako. Yani nafsi! Nafsi ndio adui mkubwa wa
imani. Unachokisoma
kwenye biblia nafsi
inasema haiwezekani, inakuonyesha mazingira ya nje, au hali yako halisi ya
sasa! Inakukumbusha ya zamani. Sasa dawa yake ni kuongea ulichokiamini.
Kuijibisha nafsi! Kwa neno
la Mungu. Ikisema angalia hali yako ya sasa! Ikikukumbusha
ya nyuma! Ikitumia macho yako! Au mazingira uliyopo iongeleshe nafsi yako kwa
neno itasikia. Sema ni kweli lakini neno la Mungu linasema hivi. In long run,
au baada ya mda mfupi nafsi yako itanyamaza kimya itakaa kimya baada ya kukaa kimya. Sasa
ile hakika
yasiyowezekana. Itakuwa juu. Hakika ikishakua juu moyo utakubali. Katika
kiwango hiki sasa lolote mdomo utakao tamka kwa jina la Yesu inakuwa
ivyo. Hata baada
kutamka kuendelea kukiri ulichotamka no matter what situation. Haijalishi
mazingira yataendelea kukuzonga. Kutamka mpaka umepata kile ulichokikiri. Kumbuka
baada ya kukiri tuu
kutakuja mawazo,
maneno ndani yako. Au watu wa nje au mazingira ya kukupinga kile unachokiamini.
Sasa what it matters ni kile unachokiri kukimaintain kwa mda
wote. Kama umekiri
cha shetani malaika wa shetani anafanyia kazi hapohapo. Kama umekiri cha Mungu
malaika wa Mungu anafanyia kazi hapohapo. Iyo ndio siri ya imani. Bwana Yesu
asifiwe sana.
kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment