KWANINI NI MUHIMU KUAMBATANISHA NA KUJIUNGANISHA NA SADAKA YA YESU KWA NJIA YA SADAKA?






Somo fupi: Umuhimu wa kuambatanisha na kujiunganisha maombi yako na sadaka kwa Yesu Kristo.

Wote mnakubali Yesu ni sadaka kwetu. Yeye alifanyika sadaka kwa Mungu kwa ajili yetu na sisi tukakubalika mbele za Mungu. Sasa kwanini unaunganisha maombi yako na sadaka? Tunaunganisha maombi yetu na sadaka kwa sababu tunataka kujiunganisha na sadaka ya Yesu. Sadaka inayotambulika mbele za Mungu ni ile ya Yesu. Ivyo kwa wewe kutoa sadaka mbele za Mungu ni kitendo cha wewe kujiunganisha na damu ya Yesu,  kujiunganisha na madhabahu ya Yesu. Kwanini tunafanya hivyo, tunafanya hivyo sababu sadaka pekee inayokubalika mbele za Mungu ni ya Yesu Kristo. Kwa iyo sadaka zote lazima zipitie katika mikono ya Yesu ndipo ziende kwa Mungu Baba. Haki yetu sisi tunaipata kupitia Yesu. Bila Yesu hatuna haki. Bwana Yesu asifiwe sana!

Tuangalie neno;  fuatilia taratibu ni stori nzuri ya kufundisha sana. Soma mpaka mwisho.

Hesabu 23
2  Na Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori.
3  Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa Israeli.
4  Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile.
5  Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi.
6  Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.
7  Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki.

12  Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa.
22  Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa Bwana akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye.
 23  Na yule punda akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, na upanga wake mkononi mwake amekwisha kuufuta; punda akageuka upande ili kuiacha njia, akaingia shambani. Balaamu akampiga punda ili kumrejeza njiani.
 24  Kisha malaika wa Bwana akasimama mahali penye bonde, katikati ya mashamba ya mizabibu, tena penye kitalu upande huu na kitalu upande huu.
 25  Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajisonga ukutani, akamseta Balaamu mguu wake, basi akampiga mara ya pili.

 26  Malaika wa Bwana akaendelea mbele akasimama mahali pembamba sana, hapakuwa na nafasi ya kugeukia mkono wa kuume, wala mkono wa kushoto.
 27  Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake.
 28  Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?
 29  Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi.
 30  Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La!
 31  Ndipo Bwana akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi.
 32  Malaika wa Bwana akamwambia, Mbona umempiga punda wako mara tatu hizi? Tazama mimi nimekuja ili kukupinga, kwa sababu njia yako imepotoka mbele zangu,

 33  punda akaniona, akageuka upande mbele zangu mara tatu hizi; kama asingejiepusha nami, bila shaka ningalikuua wewe, nikamwacha yeye hai.
 34  Balaamu akamwambia malaika wa Bwana, Nimefanya dhambi; maana sikujua ya kuwa wewe umesimama njiani ili kunipinga; basi sasa, ikiwa umechukizwa, nitarudi tena.

* wapendwa katika mstari huu unaona jinsi Mungu alivyokuwa akiwatetea wana wa Israeli. Ibilisi alitaka awashinde kwa njia ya uchawi lakini uchawi huo haukupata nafasi. Swali kwanini Walipata ulinzi kiasi hiki? Kumbuka wana wa Israeli walikuwa wana shida kama wewe? Waliomba kama wewe? Walifunga kama wewe? Na Mungu aliwaahidi kuwatoa misri kwa wajumbe wa Mungu, kwa maono, kwa ahadi, kwa maagano aliyoyafanya kwa neno kupitia Ibrahimu kama wewe ilivyo sasa haina tofauti, Unavyosimamia mistari ya biblia kilichofanya Mungu awatoe ni baada ya wao kutoa sadaka ya pasaka, kama jinsi walivyoelekezwa na Musa. Mpendwa unapoomba vitu vikubwa katika ulimwengu wa roho,maombi ya ukombozi au delivarence unapohitaji ufunguliwe kitu kikubwa lazima uambatanishe na sadaka, sadaka manake ni kujiunganisha na madhabahu ya Mungu aliyehai. Lazima kiwepo kitu cha kukuunganisha ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho! Bwana Yesu asifiwe!

Wapendwa watu wa duniani wanapoenda kwa waganga au kutaka kukudhuru kwa uchawi wakienda kwa waganga huwa wanaenda na sadaka mf. Ngombe 21, sadaka kubwa wanatoa ili wewe ufungwe kiuchumi, ili wewe usifunguliwe ukapata mme, usipate kazi. Na kadhalika wa kadhalika, watesi wetu sisi ni wachawi, ndio wanafanya maisha yanakuwa yalivyo, nakueleza ili upate ufahamu wa Mungu,Sasa wengi wanasema Yesu alifanyika sadaka kwetu mbele ya Mungu ni kweli lakini wewe umejiunganisha vip na Yesu? Mungu alituumba sisi ni viumbe wake lakini alijiunganisha na sisi kupitia sadaka ya mwanawe wa pekee. Kwa iyo Maombi makubwa yoyote ya ukombozi muhimu kujiunganisha na sadaka. Najua unajua ila nakukumbusha uone umuhimu wake. Pamoja na kufunga tatu kavu, pamoja na maombi yako. Chukua sadaka iunganishe na 

damu ya Yesu. Iunganishe na madhabahu ya Yesu ili ikakupiganie. Bwana Yesu asifiwe. Wengi tunaomba alafu hatuna sadaka maalumu ya kujiunganisha na maombi hayo maalumu. Au hiyo sadaka unaitoa tuu bila nayo kuiombea Bwana Yesu asifiwe! Angalie ile sadaka ya pasaka ya wana wa israeli ilikuwa inataratibu zake na siku yake. Ivyo usipeleke sadaka yako kavukavu kama unaitupa pata mda wa siku hata moja kuifungia kuiombea kuitamkia, na kuiunganisha na damu ya Yesu. Matokeo yake ni kama unayaona hapo juu kwenye neno, narudia tena uchawi upo na ni vita yetu sisi tuliokoka kila siku.kazi ya uchawi ni kukudhoodisha kwanza, kukupunguza makali yako ya imani au kuomba, kisha ndiyo wanapiga, utauliza nimejuaje angalia hapo juu kwenye neno. Watu wa ulimwengu huu wana maarifa kuliko sisi wa rohoni. Wanapeleka sadaka kubwa na kuiunganisha na madhabahu zao za kukufunga wewe. Wanakufunga ufahamu,ndoa yako, kipengele cha ndoa,uchumi,mikono yako ya uzalishaji, nyayo za miguu yako ya kumiliki, wanakutupia mikosi balaa, kutokufanikiwa, kuzaa mapooza n.k Na wewe toa sadaka kuiunganisha na damu ya Yesu na madhabahu ya Yesu. Kama kuna kitu umepata mrudishie Mungu utukufu.



JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu


josephntandu@gmail.com,0713297066


 

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA