MAANA WAKATI UMEWADIA AMBAPO HAIMPASI KUKAWIA MAHALI WAPENYAPO WATOTO
Somo: Maana wakati umewadia ambapo haimpasi kukawia mahali wapenyapo watoto- Hosea 13-13
Bwana Yesu asifiwe!
Si kusudi la Mungu ukawie katika muujiza wako, Si mpango wa Mungu ukae mda mrefu ukisubiri jambo moja litokee. Jina la Bwana libarikiwe Sana. Hapo juu anaposema haimpasi kukawia mahali wapenyapo watoto hapa Mungu alikuwa anaongea wana wa Israeli.
baada ya kutolewa Misri na kustareheshwa walijisahau! Na kuanza kufanya mambo Yao nje na maagizo ya Mungu. Misri inaweza kuwa kukosa kazi,kukosa mtaji,
inaweza kuwa kutokuwa Na amani, Inaweza kuwa uchumi mbovu.kusubiri uponyaji, Inaweza kuwa biashara inayoenda kufa,kutokupanda cheo, mshahara hautoshi,
inaweza kuwa mambo yako kukwama. Kutokutoka! Kuchelewa kuwa na ndoa yako,kuchelewa kupata mtoto, inaweza kuwa madeni, Kutokuwa na nyumba yako, kutokuwa na gari yako!Halleluyah yani kila mtu huwa ana misri yake!
Kila mtu huwa ana jambo lake moyoni. Sasa ndo anaelezea kuwa haimpasi mtu kukawia mda mrefu mahali wapenyapo watoto.watoto maanake ni kaanani yako, ushindi wako,victory yako! Bwana Yesu asifiwe Sana. Maana kukawia huku kunachosha si ndio wapendwa?
Sasa nini husabisha? Mtu kukawia?
1. Mauti
2. Kuabudu sanamu
Mauti kivipi? HOSEA 13-14
14 Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.
* nitawakomboa na nguvu za kaburi na mauti. Bwana Yesu asifiwe! Kumbe Kuna nguvu za kaburi na nguvu za mauti ni vitu viwili tofuti kumbe mauti ndio inayoanza. Kaburi inahakikisha hautoki, yenyewe inakumeza ili usije ukainuka.
Na mauti inatoa mapigo Bwana Yesu asifiwe! Na kaburi inaharibu. Kama ni mtu anapigwa kwanza akishapigwa kazi ya kaburi sasa ni kuharibu ule mwili wa mtu. Basi hivi viwili ndivyo vinavyoshirikiana hivi vitu viwili sasa geuza katika maombi au ulimwengu wa roho. Pigo la mwisho la ibilisi kwako wewe au mambo
yanayokuzunguka ni mauti na kaburi.Hata Yesu mtihani wa mwisho kuushinda ilikuwa Ni mauti na kaburi otherwise angeweza ondoka tuu na kupaa. Ndo mana alijua atakufa akasema imekwisha. Yani mission accomplished Kuna
watu wanajisikia vibaya, no! Lazima uujue kweli, tuchukulie mfano ibilisi anataka akupoteze kabisa usifikie ndoto yako ya kuwa Proffessor alishajua hatima yako ni Proffessor ukiwa mtoto atauwa kipengele chako cha kumbukumbu hutaweza soma.
Au atafanya jinsi yoyote usisome. Hapo ndipo tunaita mapigo ya mauti. Maana inauwa ile mbegu ya kisababishi cha u proffessor. Sasa nguvu ya kaburi hapa inakuja
kukufanya wewe usije ukarecover ibilisi atakutupia roho ya ukichaa, au kuvuta madawa ya kulevya. Bwana Yesu asifiwe. Iyo ndo uharibifu kabisa ili usije unapata chance hata ya kujitambua.
Sasa watu wengi wanateseka kwa sababu ya hatima nzuri ya maisha Yao Mungu aliowaandikia. Shetani ameziuwa kwa nguvu ya mauti na nguvu ya kaburi. Bwana Yesu asifiwe sana,Lakini ashukuriwe
Yesu. Sasa unaifahamu kweli. Nayo iyo kweli utaijua na itakuweka huru. Kwa iyo sababu ya vipengele vingi vineuwawa katika maisha Yao hii inawapelekea kutokufikia hatma za maisha Yao. Au kukawia Sana kufika.
Au Kupata result kidogo, kidunchu, Bwana Yesu asifiwe. Ndo mana anasema nitakukomboa na nguvu za kaburi Na nguvu mauti. Alafu
anauliza ewe mauti yako wapi mapigo yako. Ewe kaburi yako wapi kuharibu kwako? Anasema kujuta kutafichwa machoni pako.
Kuna watu baada ya kujua vizuri hili neno wanaanza kujuta usijute Yesu anasema kujuta kwako kutafichwa. Kutafichwa Yes, hii kuijua tuu hii siri
tayari vifungo vya mauti na kaburi vinakukimbia na macho yangu. Macho ya nani Mungu ndo anaongea hapo.
Nini husababisha mauti sasa Katika mwanadamu?
Kuabudu sanamu. HOSEA 14:3
3 Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.
Kuabudu sanamu kivipi? Sanamu ni nini? Ni kile kinachokupa amani ya uongo, furaha ya uongo. Unayoipata kwenye vitu au watu, mazingira. Ndo
mana anasema Hosea 14:3 wala hutaiambia tena kazi ya mikono yetu. Ninyi ndinyi miungu yetu. Pesa Si sanamu, rafiki si sanamu.
Sanamu inakuja vipi? Sanamu inakuja pale unaponunua gauni, suti nzuri, simu nzuri, unapojenga nyumba nzuri, unapomiliki na kuendesha gari nzuri, unaponunua
kiwanja, cheo kizuri, kazi nzuri, faida nzuri ya biashara, mke mzuri, Mme mzuri, watoto wazuri, rafiki mzuri,mshahara mzuri alafu usije kusahau
kuunganisha neno alafu ukapoteza maana alafu ukaviabudu au vikaendesha moyo wako, fikra zako, unavigeuza kuwa source ya amani
na furaha yako. Vikiyumba na wewe unayumba, vikiwa sawa na wewe unakuwa sawa. Yani vinakuendesha wewe, vinaamua direction yako wewe.
badala ya wewe kuviendesha kupitia neno la Mungu. Iyo ndio inaitwa sanamu. Kutegemea gari, nyuma, fedha iliyoko bank kama source ya furaha na amani iyo ni sanamu. Sanamu ni kile kitu
kinakuja kabla ya Mungu Katika moyo wako. You can imagine unapenda vitu vingap kabla ya kumfikiria Mungu Katika moyo wako? Mungu anataka nafasi ya kwanza. Hata tatizo ulililo nalo lisigeuke sanamu.
Tatizo lisichukue nafasi ya moyo wako kuliko uyo Mungu. Yani unawaza tatizo kuliko hata uyo Mungu.Hichi ndicho kinatuchelewesha. Ukiamua kwenda nenda usiende na kurudi. Usiende na kurudi. Kama umeamua kumfuata
Yesu mfuate kikweli kweli. Acha kutafuta misaada ya pembeni! Acha kutegemea watu, au vitu, vitaharibu focus yako.Bwana Yesu asifiwe! Mtafute kikweli kikweli acha kumchanganya Yesu na sanamu. Bwana Yesu asifiwe sana.
Nini ahadi za Mungu kama tukimfuata kwelikweli? HOSEA 14-5
5 Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza mizizi yake kama Lebanoni.
6 Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni.
7 Na wao wakaao chini ya uvuli wake watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni.
8 Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako.
* Mwisho Hosea anasema HOSEA 14-9
9 Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za Bwana zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
*Kwa maana njia za Bwana zimenyooka, njia zipi? KUTOKUABUDU SANAMU, anasema wenye haki watakwenda katika njia hizo, ila wasio wataanguka katika njia hizo wataanguka wap? Katika "MAUTI NA KUKAWIA MAHALI WAPENYAPO WATOTO"
Bwana Yesu asifiwe? Sasa umeijua kweli kwa habari ya nguvu ya mauti na nguvu ya kaburi. Kwa habari ya sanamu na vipi vinausika katika kukawia kwako sehemu ambayo watoto wanapita. Ndo mana anasema katika HOSEA 14: 1-3
1 Ee Israeli, mrudie Bwana, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.
2 Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng'ombe.
Jina lake Mungu libarikiwe.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment