"MADHARA YA KUTOA KITU NA KUPOKEA KITU KWA LAWAMA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO"
Bwana Yesu asifiwe wapendwa!
Nilikuwa sijui how serious is it neno "lawama" mpaka Mungu aliponifunulia na maandiko! Wapendwa Kuna madhara ya kutoa kitu kwa lawama, na kupokea kitu kwa lawama kina impact kubwa Sana.katika ulimwengu wa roho. Pia Ni hatari kama hujajifunza kufuta hizo lawama kwa damu ya Yesu.
Katika ulimwengu wa roho. Tutaenda angalia situation mbili katika biblia za mtu aliyetoa kitu kwa lawama na mtu aliyepokea kitu kwa lawama. Na kama usipofuta iyo kitu Katika ulimwengu wa roho shetani atakufunga. Na unaweza kuwa unaeenda ikifikia sehemu flani ya kufikia hatima yako unakwama.
Neno lawama ni pana inaweza ikawa Ni maneno. Au pia inaweza kuita mashitaka ya lawama. Zipo case nyingi lawama zinaweza kuwa ni wewe unamlalamikia Mungu kutokuridhika na jambo flani iyo inageuka laana katika maisha yako.
Lawama inaweza kuwa zimetoka kwa wazazi wako. Ndugu zako, jirani zako, watu unaofanya nao kazi wanakulaumu, lawama zinaweza toka kwa wazee wakubwa zako pengine huwaheshimu watu wazima-wazee, huwajali! Lawama zinaweza kuwa kwa wadogo au watoto
wako, wakilalamika mbele za Mungu kitu chochote cha haki kwako inageuka laana, lawama inaweza kuwa kwa mwenza wako, Mme au mke akilalamika jua anakufungia vibali vyako. Hata wateja wako wakikilalamikia kutokuridhishwa na huduma labla inakufungia njia zako. Watu wanaokudai wakilalamika wakinungunika
kwako inageuka laaana, lawama inaweza kuwa ziliongelewa kwa mama yako wakati mjamzito izo lawama zinawafuatilia. Ndio maana Kuna watu Ni wa kulaumiwa kwa kila kitu na kila mtu anamlaumu! Lawama ni kifungo, manunguniko ni kifungo! Lazima ujifunze kufuta lawama katika
maisha yako. Pia wewe kulaumu watu pia ni kujifungia malango yako ya Baraka, maana ilipaswa usamehe kama vile Mungu hakulaumu Bali anakusamehe!unapoomba msamaha! Kuna baathi ya watu lawama zipo karibu Sana na midomo Yao kuliko kusamehe. Hiko Ni kifungo! Badala ya kutafuta jibu watu wanakimbilia kulaumu, ukilaumu na wewe utalaumiwa tuu mahali.
Tuangalie neno- madhara ya kutoa kitu kwa lawama
Mwanzo 4-3
3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
*tuangalie neno stori ya Habili na kaini. Karibia wengi tunaijua. Lakini swala dogo kwanini sadaka ya kaini ilikataliwa? Ushawahi jiuliza? Ni wazi kabisa moyo wa kaini ulibeba malalamiko, unauliza umejuaje? Usingekuwa na malalamiko asingemtolea Mungu sadaka kilema,
moyo wake ulijawa na uchoyo, na ubinafsi ikampelekea moyo kumlamimikia Mungu pengine moyo ulisema "unampa Mungu vyote hivi why?" Ile sadaka ilibeba malalamiko ndo mana Mungu hakuitakabali. Ndio maana mtu akikikupa kwa malalamiko, akikupa ela kwa malalamiko angalia nafsi yako
itakavyoinama! Angalia kama utafanikiwa, malalamiko ni roho, usipoifunga roho iyo inaenda kutengeneza mazingira ya wewe kulalamikiwa unashangaa kila unalolifanya unaishia malalamiko. Hufanikiwi.
Ndio maana watumishi wengine wanaojua siri hii. Kuna pesa utampa atakaa kuipokea sababu anajua Ina malalamiko na iyo Roho itamfuatilia. Ndio maana Ni muhimu chochote unakitoa moyo wako ukibariki, usikitolee malalamiko. Ukitoa sadaka kwa malalamiko hayo
malalamiko hayendi tuu kule inakoenda Bali hata wewe mwenyewe itakurudia na itakuvuruga. Unauliza umejuaje? Angalia hapo juu stori hii kwenye biblia ile dhambi ya malalamiko ilimfanya Kaini akamuua ndugu yake Habili. Sasa angalia Mungu anachosema baada ya Habili kuwawa,mstari 10- anasema Mungu damu ya ndugu yako
inanililia kutoka Katika ardhi. Damu ya Habili ilikuwa inalalamika kwa Mungu. Angalia kilichotokea baada ya hapo. Kaini alilaaniwa. Ndo mana Ni hatari Sana kutoa kitu kwa malalamiko. Si sadaka tuu Bali kila kitu. Hata zawadi usitoe kwa moyo wa malalamiko. Wengine wamesomeshwa kwa malalamiko! Angalia maisha ya hao watu waliosomeshwa wanaishije?
Lawama na zile laana zinawafuata kila mahali. Sasa haendi tuu kwa yule aliyepokea Bali hata kwa wewe uliyetoa kwa moyo wa malalamiko. Angalia mtu anayepewa pesa kwa malalamiko, chochote cha malalamiko kimebeba laana nyuma yake. Ndo mana Si kila zawadi ni nzuri wakati wa harusi! Zawadi zingine
zimebeba malalamiko. Angalia iyo ndoa itakuwa na kulaumiana katika kila kitu. Sasa hii inaenda hadi kwenye tumbo la uzazi wa mwanamke, inaenda hadi kwenye kiuno cha uzazi wa mwanaume. Kama Kuna kitu walikipokea kwa malalamiko hao wazazi! Angalia kama iyo Roho itawaacha watoto. Roho izi zinafuatilia. Chochote kinachotolewa kwa malalamiko hakikai, hakidumu! Ni mpaka
umeingia katika ulimwengu wa roho umefuta mashitaka hayo kwa damu ya Yesu. Moyo wa malalamiko hauridhiki, moyo wa malalamiko unatoa malalamiko tuu. Hii Ina affect kuanzia ndoa, biashara, elimu, uongozi pia unakuwa kiongozi wa kabeba malalamiko, kazi, kila kitu na malalamiko yanavunja moyo na kubomoa mausiano, usitoe kitu chochote kwa malalamiko maana iyo Roho itakurudia wewe angalia kaini ilimsababisha akauwa, na akalaaniwa.
Tuangalie situation ya kupokea Kitu kilicho na malalamiko.
Mwanzo 27: 34-35
34 Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu.
35 Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako.
41 Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo
Malango wa 29
25 Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda?
26 Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa;
27 timiza siku zake saba, nasi tutakupa huyu naye kwa utumishi utakaonitumikia, miaka saba mingine.
28 Yakobo akafanya hivi, akatimiza siku zake saba. Naye akampa Raheli binti yake kuwa mkewe.
*Nimefupisha stori lakini tunaona kwamba pamoja na Yakobo kuchukua cheo cha uzaliwa wa kwanza kwa hila. Na Esau moyo wake ulikuwa na malalamiko makubwa, na uchungu mkubwa pia Yakobo ilimsababisha kulipa gharama.
Aliyeumia si Esau tuu. Hata Yakobo alifanyiwa Hila ya kubadilishiwa mke, na ikambidi atumike miaka 7 mingine. Kumpata Rahel na hii ndivyo inavyokuwa ukipokea kitu chenye lawama itakucheleweshea kibali chako maana ile roho itakufuatilia. Tuu.
Usipojifunza kufuta mashataka ya malalamiko ndivyo inavyokuwa. Swali linakuja mambo mangap? Umeyapokea kwa malalamiko? Mambo mangap umeyatoa kwa malalamiko? Iyo ni roho mashitaka ya malalamiko kama nilivyosema roho hii ya mashitaka ni halisi
ukipokea pesa yenye malalamiko zawadi yenye malalamiko, Baraka zenye malalamiko. Wish toka kwa mtu ya malalamiko, chochote chenye malalamiko Ni roho ya mashitaka na itakufuatilia aidha umepokea au umetoa. Bwana Yesu asifiwe Sana!
Ivyo muhimu kufuta malalamiko yote kwa damu ya Yesu. Wakubwa, wadogo, wafanya biashara wenzako, mfanyakazi wako wa ndani, wafanyakazi wenzako, wote wanaokulaumu jua wanafunga ulimwengu wako wa Roho. Kama hukutenda haki jua unafunga ulimwengu wako wa Roho.
Kama ulitumia cheo, wadhifa wako, uongozi wako, au nafasi uliyonayo kuonea mtu yoyote akalalamika jua pia anafunga malango yako. Malalamiko ni roho na yanafunga vibali vyako au kuchelewesha vibali vyako. Huwezi jua nani kalalamika au nani alikufurahia na huwezi kumbuka kila kitu right?
Ivyo usiku wa Leo ingia katika ulimwengu wa roho achilia damu ya Yesu ya kufuta mashitaka ya malalamiko Anza na wewe, kisha watu wote waliokuzunguka kuanzia mimba yako ilipotungwa, shule ulizosoma, ardhi ya kwenu, sehemu ulizo wahi kukaa
au watu waliowahi kukuzunguka, omba rehema kwa ajili yako, omba rehema kwa ajili Yao. Achilia damu ya Yesu ya kufuta malalamiko. Futa mashitaka yote ya malalamiko. Katika ardhi, bahari na anga. Jina la Bwana libarikiwe Sana. Na Kadiri roho wa Mungu atakavyokukumbusha.
Jina la Bwana libarikiwe
Maombi:
Baba katika jina la Yesu Kristo ninakuja mbele zako mtakatifu wa Israeli, ninaomba rehema Bwana katika jina la Yesu ninaomba unitakase dhambi zangu zote baba wa utukufu,kwa damu ya mwanao yesu Kristo ninaomba unirehemu Mungu kwa kutoa jambo lolote kwa malalamiko, na kupokea jambo lolote kwa malalamiko, ee Bwana nimetambua ya kwamba nilijiunganisha au kuunganishwa na milango ya adui ninaomba rehema Bwana kwa damu ya mwanao Yesu Kristo, ninaomba unisamehe sasa Bwana katika jina la Yesu Kristo, aidha nimetoa au kupokea chochote kupitia mawazo, maneno, au matendo naomba unirehemu katika jina la Yesu, kuna mahali pengine nilipokea malalamiko,kwa kupokea vitu nilipokea roho ya uchungu, roho ya kilio,utasa,mapooza bila kujijua ikasababisha laana katika maisha yangu ya kiroho na kimwili ee Mungu mtakatifu wa Israeli ninaomba unisamehe sasa katika jina la Yesu!ninaomba pia uwarehemu wote waliohusika kwa jina la Yesu, mahali pengine nilitoa kwa malalamiko, nilitoa kwa moyo wenye uchungu,nilitoa kwa moyo wa uchoyo,au moyo usiopenda kutoa,au maneno yasiyo na baraka, Bwana nikasababisha watu wengine kupata laana naomba unirehemu Mungu katika jina la Yesu, na sasa roho ya kutokufanikiwa inaniandama, kukaa sehemu moja mda mrefu,roho ya mapooza, roho ya utasa inanifuatili na kuniandama kila mahali katika biashara zangu, ndoa yangu, mahusiano yangu, kazi zangu, hatua za zangu za mafanikio hazisogei,mahali pa kupita ninakwama ee mfalme, mahali pengine Mungu tulitoa malalamiko kwako wewe mwenyewe sababu ya majaribu kwa kutokujua na kwa binadamu, mahali pengine tulipokea malalamiko au mashitaka kwa kuyasikia au kutoyasikia na yule mwovu ibilisi akayachukua na kuyafanyia kazi katika ulimwengu wa roho, sehemu ingine Mungu ilikuwa ni kwa njia ya mawazo, Baba wa mbinguni mlango wowote ule laana ilipoingilia ninaomba rehema kwa malango ayo laana izo kupitia hizo roho katika ardhi, anga na mbigu zake, au bahari au chini ya bahari malango yangu yote ninamwaga damu ya Yesu ya kufuta laana zote na kumbukumbu zake zote damu ya Yesu yenye pembe saba na macho saba ninaachilia sasa katika ivyo vifungo. na kwa neno hili ninaruusu moto wa roho mtakatifu kuunguza mashataka yote duniani na ulimwengu wa roho, ninaruusu mvua ya damu ya Yesu juu ya vifungo vyote vikafunge sasa katika jina la yesu, ninaruusu mvua ya acid ya mungu juu ya vifungo vyote vilivyonifunga vya kutokufanikiwa pamoja vya mapooza, utasa na kutokufanikiwa kwa aina yoyote katika jina la yesu, ninajitoa katika mtego huo kwa jina la yesu, ninachomoka katika mduara huo kwa moto wa roho Mtakatifu kwa jina la yesu, ninaruusu moto wa roho mtakatifu ukasambaratishe na kuwaangamiza mapepo yote ya laana maishani mwangu kwa jina la yesu na kwa damu ya yesu. roho Mtakatifu ninaungana na wewe sasa katika vita hivi kwa damu ya Yesu, hadi kuwa huru kwangu katika mafanikio ya juu Mungu aliyonipangia katika jina la yesu na damu ya Yesu ninakiri kuvuka kwangu amen.
endelea kuomba mpaka umepata amani ya Yesu............
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
Muhimu:
Mungu amenipa maono ya kwenda live kupitia radio, na televison, ili masomo haya na maombi tuyapate live, yaani audio na video tutaanza na online radio, online tv, kupitia internet, Pia tutakuwa na live prayer line ya kuhudumia watu, Mungu amesema nami kwa habari ya studio kwa ajili ya huduma iyo. Nikupe nafasi ya kupanda mbegu yako kwa ajili ya studio hiyo. Na Mungu atakukumbuka sadaka yako injili itakapoenda duniani kote. kufungua, kuponya, kuokoa, kuinua. Kama unataka kushiriki baraka hizi uko ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. basi tumia hizo namba hapo chini kutuma sadaka yako. kama uko nje ya Tanzania tumia izo namba nitakupa maelekezo
josephntandu@gmail.com,+255713297066, +255765377506
josephntandu@gmail.com,+255713297066, +255765377506
Comments
Post a Comment