MAMBO MATATU (3) YA KUFANYA KIBALI CHAKO KISIYEYUKE" KIDUMU MDA WOTE.

Somo: "Mambo matatu (3) ya kufanya kibali chako kisiyeyuke" kidumu mda wote.

Bwana Yesu asifiwe Sana!

Maelezo mafupi;

*watu wengi Sana pamoja na Mimi vibali vyetu havikai, vinakuwa Ni vya mda tuu. Kama ni neno la Mungu litakaa wiki tuu,lifutika moyoni kama ni maombi yatakaa siku tatu tuu, Kama ni mlipuko wa ndani utakaa wiki tuu. Mlipuko au Moto wa roho mtakatifu. Ni kama vile Moto wa karatasi. Unaanza kwa nguvu hauchelewi kuzima. Na ndivyo hata maisha yetu mafanikio yetu yalivyo. Kama Moto wa makaratasi


*Limenisumbua mda mrefu, nikamuuliza Mungu why? Kama ni kibali kwa mke wako, au Mme wako kinakuwa cha mda, yani hakija automatic! Kitaletwa na jambo flani ilo jambo kiliisha na kibali hiko kinatoweka. baada ya mda mnarudi kwenye commitment, yani inabaki sheria.kutimiza wajibu. kama ni biashara inakuwa ya mda tuu.wateja watakuja kwa wingi wiki, wiki inayokuja unahesabu kwa shida Sana. Mafanikio ni ya mda tuu. Wateja ni wa mda tuu. Kama Ni amani itakaa kwa masaa tuu, hata siku haimalizi, kicheko ni cha mda tuu, Ni kama vile tunaazima vitu baada ya mda mwenyewe anavitaka. Ni kweli tuko duniani hatuwezi pata 100% but maisha tunayoishi hata 2% hatupati.


*Amani kazini Ni ya mda tuu, kila mara tunaishi kwa hofu,na tuna Mungu, kutembea katika utakatifu ni kwa mda tuu, tena inawezekana ni wakati wa ibada tuu, ukitoka nje ya mlango wa ibada ushavaa ubinadamu wako wa asili, kama ni imani ni kwa mda tuu, sio wakati wa majaribu.


*Kama ni huruma ni ya mda tuu, na kama ni upole ni wa mda tuu. Upendo ni kwa mda tuu.Zile tabia 9 za roho wa BWANA Ni za mda tuu na mpendwa huyu amejazwa roho mtakatifu. Nikawa Nina maswali Mengi Sana, Mungu kanifunulia Na Mimi nimeona ni share na wewe mkate huu utakusaidia katika safari yako ya wokovu. Wokovu si rahisi Sana. Ila kwa Neema ya Mungu jaribu ili linakuja linapita, masaa yanaenda, siku zinaenda, miezi, mwaka hadi miaka, Na bado tunangangana na Yesu. Bwana Yesu
asifiwe Sana!


*Kibali ni nini? Kibali ni mpenyo wa Ki Mungu. Ni uwezo wa Mungu utakao juu unaokuja kukusaidia mahali flani, ili uwe na rahisi, inakusaidia kumsukuma adui nyuma, ili wewe upite. Kibali hushikilia mazingira, nafasi, watu, ulimwengu wako wa roho ili yakupendelee na kukutii wewe. Tuko pamoja? Kwa iyo kibali hiki kinapokuja ndipo unapoona kila mtu anakukubali, anakufurahia, mazingira Yana suite na wewe, yani yanakubaliana na wewe yani hakuna upinzani.


 Nikupe mfano wa mtu aliyepata kibali cha kufungua kampuni. Kwanza kabisa atapata kibali cha idea nzuri, iyo idea itakubalika atakapoipeleka, watu wa kibali hicho watakapoipata wataikubali na kumfurahia, na watakuwa tayari kumpa ushauri na kumuonyesha njia za kupita ili apate mtaji na aweze kuanza, kibali hiko hakitaishia hapo upatikanaji wa ofisi wa


iyo kampuni kibali kitafanya kazi automatic, usajili wa iyo kampuni utaenda kikibali hatapata usumbufu Brella, procedure zoote, mpaka wafanyakazi, wataalamu, management atakayoiunda, board of directors! Zoote kibali kitachagua mpaka watu. Hata iyo product mpaka kwenda kwa wateja Ni kibali kitupu kitacontrol.

Mambo matatu ambayo yanaondoa kibali;

Mathayo 6:14,15

Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.


*Usipowasamehe watu makosa Yao. Baba yenu hatawasamehe ninyi, hili neno ni zito Sana, kama huwasamehi maana yake wewe mbele za Mungu hata uombe vip? Hata uombe msamaha kwa Mungu hatakusamehe! Kwa iyo kama Mungu hajakusemehe manake wewe na Mungu ni adui. Maana yake Una dhambi, kwa iyo kila kitu kinaharibika kuanzia hapo, kwa iyo yule mshitaki wetu anaenda kwa Mungu anakushitaki kuwa wewe hujasamehe,


 kwa iyo sababu unadhambi mbele za Mungu kwa maana hauko upande wa Mungu kwa habari ya kuhesabiwa haki. Kwa iyo huo ni mlango kwa ibilisi kwa sababu kapata mlango anapata uhalali wa kuharibu kibali chako, unashangaa mambo yanaanza kubadilika tena. Shetani  huinua makwazo ili ukasirike ukisha kasirika anakuwekea chuki moyoni kwako na unashindwa kusamehe! Watu wengi katika nyumba moja wanaoishi  na wanakwazana lakini wengi


 msamaha ni wa mdomoni sio wa ndani? Unauliza umejuaje? Kama umemsamehe kwanini bado unahasira naye? Kwanini bado unamlaamu, kwanini bado unaelezea watu ubaya aliokufanyia? Kwanini hakutoki kwenye akili yako? Kwanini bado Una uchungu? Kwanini hujamwachilia? By the way usipomsamehe mtu umejifunga hiko ni kifungo cha kukuondolea amani, kila Mara ibilisi akitaka akurudishe nyuma


 atakukumbusha utakasirika utaingia jazba tayari umeingia katika dhambi. Ili ibilisi asipate mlango lazima usamehe kiukweli utangaze kusamehe ili mlango huo ufungwe na Yesu, Uondoke, watu hawajui wanabeba uchungu, wanaumwa moyo, Bp sababu ya kutokusamehe, hawana amani, furaha sababu ya kutokusamehe.wanabeba vitu vingi kwenye moyo Wao kunasababisha magonjwa. Shetani anakuangalia tuu ukianza ku catch fire, anakukumbusha unaingia hasira.


Na ibilisi neno hili huwa anadanganya watu aaah Hilo neno lipo ili kukurudisha kwa Mungu tuu. Ni technique ya wachungaji ili turudi kwenye mstari, mpendwa Mungu hatanii, wala Hana utani, akisema utakuta unakufa kweli muulize mfalme Hezekiah alipoambiwa atakufa alilia alimjua Mungu hatanii yule ni Mungu na Si binadamu.


Leo hii nakuambia kwa ukweli na uwazi wala sikutishi, umeokoka na unampenda Yesu ndio, lakini kama hujasamehe yoyote aliyokukosea bahati mbaya ukafa hujamtoa uyo mtu moyoni. Moja kwa moja bonde la uvuli wa mauti linakusubiri. Hutaiona mbingu. Hii ni Mimi na wewe. Bwana Yesu asifiwe. Lakini neno hili limekuja ili kukuponya. Halleluyah!kutokusamehe ni kusitisha kibali chako. Bwana Yesu asifiwe Sana!

Ufunuo 12:10-11

10  Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. 11  Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.

*usiku na mchana ibilisi hutushitaki kwanini anatushitaki ni ili kuondoa uhalali wa kibali chako, mashitaka yanaweza kuwa ya aina nyingi, na pia watenda kazi wa ibilisi wanafanya kazi kupitia mashataka haya. Hata ya nyuma ambayo wewe hakuwepo mashitaja haya ibilisi anayafuatilia ili tuu kibali chako akiuwe, mfano kama huko nyuma Kuna watu aliingiza familia katika maagano, mikataba hayo ni mashitaka, unaweza kuwa ngazi ya familia, ukoo, au mtu amekuingiza bila wewe kujua yote hayo ni mashitaka.  Maneno mabaya wanayoyatamka watu bila wewe kuwepo au ukawepo alafu hukuyatangua Ayo ni mashitaka, maneno mabaya unayoyakiri wewe hayo Ni mashitaka, umessuport dhambi, umekubaliana na dhambi, kukaa kimya manake ni kukubaliana hayo Ni mashitaka.

Hapo mashitaka ya wewe kubakia masikini, kutokufanya biashara, kutokufanikiwa, kuingia katika madeni, kutokupona ugonjwa unaokusumbua, kutokuendelea katika lolote, kuwa fukara, kutokujenga nyumba, kutokuolewa, kutokuoa, mashitaka ya wewe kuwa tasa katika lolote unalolifanya, mashitaka ya wewe kupiga marktime, and so on! And so on! Mashitaka yanakutoa kwenye nafasi yako, yanakuondolea uhalali! Mashitaka hata ya watu wananaokuzunguka, unaofanya nao kazi, unaofanya nao biashara wanaweza kuwa kinyume na wewe, mashitaka ya ndugu, majirani. Hata wachawi wanaotaka wewe usiinuke wala usifanikiwe . Yako meengi roho Mtakatifu atakukumbusha na kukusaidia. Simama kwa damu ya Yesu ufute hayo mashitaka. Ndo maana ya huo mstari wa 11, anasema nao wakamshinda ibilisi kwa damu ya mwana kondoo na kwa neno la ushuhuda Wao, anamalizia hawakupenda hata kufa, kufa nini unafikiri? Alikuwa anazungumzia kibali. Bwana Yesu asifiwe Sana? Tumia Damu Ya Yesu ya kufuta mashitaka kila mahali kwenye ardhi, kwenye bahari, katika anga. Mashitaka ya wachawi, wanga, wakuu wa Giza, falme za Giza , wakuu wa anga, ma argent wote wa baharini, wa kuzimu, futa mashitaka katika vitabu vyao kwa damu ya Yesu. Bwana Yesu asifiwe Sana.

Waefeso 2-14-15
14  Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.
 15  Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani.

*Baada ya kufuta mashitaka lazima sasa ubomoe kiambaza, kiambaza ni kizuizi baina yako wewe na Mungu. Baina yako wewe na mafanikio yako. Wewe na imani, wewe na Baraka yako. Nikupe mfano umeomba vizuri kwa ushindi mkubwa ila Ibilisi anakujua kabisa wewe Una udhaifu wa hasira. Baada ya kupokea tuu na kutoka ushindi mkubwa kwa maombi ibilisi anakuleta kiambaza mazingira ya tukio au anainua watu au chochote ili ukasirike hiko ni kiambaza ndicho Yesu anasema alikivunja pale msabalani, alikibomoa. Kiambaza kinaweza kuwa akili yako mwenyewe, kinaweza kuwa wewe mwenyewe na udhaifu wa tabia yako, inaweza kuwa mtu. Inaweza kuwa mazingira, inaweza kuwa vitu, inaweza kuwa hasira kwa mfano unamuona mtu anakasirika eti sababu anatafuta kitu ndani kwake hakioni. Kiambaza Ni ibilisi mwenyewe Katika maumbo ya vitu,watu,mazingira ambapo wewe huwezi kugundua. Mfano Mme wako, au mke wako anaweza kutumika kama kiambaza cha wewe kutokuomba au kwenda ibadani, kiambaza kinaweza kuwa mtu aliyekukalia ofisini, kiambaza inaweza kuwa mtu aliyekaa katikati yako ili kukuzuia usipite. Mfano unataka mkopo bosi hataki ku sign iko ni kiambaza. Kiambaza kipo kwa ajili ya kudhoofisha kibali kisifanye kazi sawasawa. Kiende kwa kusuasua. Kwa iyo lazima ukivunje ndipo njia ionekane vizuri. Kuna mwingine ataomba Sana kisha anabakia kuona dalili tuu za kuvuka. Ila havuki ujue hapo Kuna kiambaza. Mwingine anaanza ila haendelei hapo Kuna kiambaza. Mwingine hafiki mwisho always mwishoni ndipo panaharibika ujue Kuna kiambaza. Kiambaza hiko lazima ukibomoe. Mpendwa neno lipo na jina la Yesu lipo. Lazima ulitumie ndipo lifanye kazi, kama hulitumii Ni sawa kwenda hospital ukalipia kumuona Dr. Ukafanya vipimo, ukapatiwa dawa, ukarudi nyumbani alafu hutumii dawa kabisa.Na bado Una lalamika maumivu, Achana na jinsi ya kutumia dawa labla ulikosea hapo pia ipo Neema Ya Yesu lakini wewe hutumii kabisa kisa umeokoka kwa iyo unajua mambo yatakuwa automatic. No! Haiendi ivyo, au umeshiriki Mara moja, ibada, au umeomba Mara moja basi unajua maombi yatakubeba kila mahali hapana haiendi ivyo.lazima utumie dawa. Sawasawa na maelekezo ya Yesu. Ivyo lazima kila siku uombe at least haya mambo matatu. naenda ku summarize. Sasa;

1. Usameheme waliokukosea .Mathayo 6-14-14

2.Ufute mashitaka .Ufunuo 12: 10:11

3.Ubomoe viambaza .Waefeso 2-14-15

Jina la Bwana Libarikiwe. Halleluyah! Mshukuru MUNGU Na Roho mtakatifu. Na Yesu maana alifanya kazi kubwa Sana pale msalabani. kama amekuvusha mahali. Bwana Yesu asifiwe Sana!

*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu


josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA