MSIHI MUNGU AKUJILISHE MAWAZO YAKE JUU YAKO
Chukua hii situation umesikia habari njema may be akiba commercial bank, wanatoa mkopo vigezo uwe
raia tuu wa Tanzania. Wanatoa mpaka mil 100 hii si itakuwa habari njema? Kwenda kuulizia ukaambiwa
reception unatakiwa uwe tuu kitambulisho cha raia. Ukajaza form na picha na barua zote na kila kitu
ukapeleka pale reception wakapokea. Sasa unasubiri upigiwe simu kuwa mkopo wako tayari
tumeingiza pesa kwenye account, hakuna kitu , mwezi miezi miaka inapita hakuna kitu na ushaweka
mipango yako vizuri. Yani matumizi unakuja kugundua sababu ya wewe kutokupa mkopo ni meneja mikopo
hajasaini faili lako! Jinsi ya kuripoti tatizo hili hawakuruusu pale bank. Ukitaka kuonana na meneja umuelezee hawakuruusu umfikie.
Unabaki kulalamika tuu na kulaumu. Siku ambayo atatokea mtu wa kukupa maarifa jinsi ya kusolve
tatizo lako. Na jina lako likapita na unaambiwa ela yako itaingia baada ya siku tatu. Je utakuwa na furaha kiasi gani?
Hivi ndivyo inavyokuwa mtu aliyeokoka akipata maarifa ya kutoka katika kifungo alichonacho!
Akipata the way out. Na akijua kabisa maneno haya Mungu kayatamka na kwamba pia
anarusiwa kumkumbusha Mungu. Na kudai mbele za Mungu. Kwa Mkristo hii inakuwaga siku njema sana kupita yote. Na furaha ya
mkristo ni pale kajua solution ya tatizo lake la siku nyingi. Kapata jawabu. Yani ile aaaaah! Kumbe!
Kujua kumbe nahangaika miaka yote hii kumbe hata ndipo palikuwa na tatizo. Kumbe ningefanya hivi siku nyingi sana. Ningeshavuka
hapa. Bwana Yesu asifiwe. Ni siku ambayo kwako utacheka mpaka kicheko cha mwisho utasalimia
mpaka mtoto mdogo. Utatamani umwambie kila mtu. Ni siku ambayo hutataka kusikia habari ingine yoyote. Ni siku ambayo utakuwa
unawaza na kucheka tuu bila kuchekeshwa. Na siku iyo ni leo. Bwana Yesu asifiwe. Fuatana na
mimi huu ufunuo Bwana amenipa hata mwenyewe baada ya hapa ndo naenda kuufanyia kazi. Jina la Bwana libarikiwe. Heshima na utukufu ni kwa Yesu.
ISAYA 55
8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.
9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
Hili Neno watu wanalijua wanaliimba, wamelitungia mwimbo na pengine nikikushutua usiku utaniambia aaah iyo ni Isaya
55-8-9, nachotaka ukione Mungu alichonionyesha ni jinsi ya kulitumia katika ulimwengu wa roho hapo ndipo
uwezo ndani yake na nguvu ndani yako utakapoijua. Utakapo ifahamu. Bwana Yesu asifiwe! Anasema mawazo yangu mimi sio mawazo yenu ninyi. Njia zangu mimi sio njia
zenu ninyi. Tuanzie kwenye mawazo mawazo ni maarifa, kwani kinachokufanya mpaka hujatoka katika ilo tatizo ni nini ni sababu huna maarifa.
Na ndivyo ulimwengu ulivyoumbwa. Utafanya vyote lakini maarifa na hekima lazima unyenyekee kwa Yesu ili aweze kukupa. Ndio maana
biblia ikasema sasa imefunuliwa ile hazina kuu iliyositirika mbinguni Hazina yenyewe ni Yesu. Maana palipo Yesu ndipo kuna maarifa na hekima.
Mpendwa maarifa ni njia ya kutoka kwenye tatizo. Hapo ndipo inakuwa gap kati ya binadamu na Mungu. Mungu atabaki kuwa Mungu. Mungu
anasolution ya tatizo lako. Iyo solution inaitwa maarifa. Jinsi ya ku excute iyo maarifa ya Mungu inaitwa hekima. Mfano kama
shida yako ni uchumi Mungu anajua mtu wa kukusaidia wewe ili utoke kabisa kwenye umasikini.anajua
ukutane naye wapi,na jinsi ya kuongea naye akuelewe. Mungu
Akikupa maarifa hayo jina lako tayari limebadilika tokea umasikini kwenda utajiri. Mungu anasolution
yako ya ugonjwa wako.Mungu anamaarifa ya kila tatizo. Akikupa iyo maarifa utaitwa mwenye afya
njema si "yule mgonjwa" halleluyah watu wa Mungu. Sasa maarifa yetu sisi ni ya kushindwa. Kukata tamaa,
kutokuona njia, baada ya kushindwa tunamlaumu Mungu. Tunaona hasira, tunakasirika, tunaona wivu
kwa wengine,tunaona kijicho, tunasema ovyo, halleluyah! Sasa maarifa ya Mungu ni tofauti na hayo hapo juu. Ndo mana akasema mawazo yangu mimi si ya kwenu
ninyi. Kwa iyo unachohitaji ni maarifa ya Mungu. Si ya degree zako ulizozipanga si ya ujuzi wako,
si ya uzoefu wako!si maarifa ya kutokana na kawaida ya vitu.utasikia mtu akisema aah iyo
kawaida inakuwaga hivi na hivi. Si maarifa ya proffessor! Au mtu sababu ana hela, au uwezo.Au yuko kwenye postion nzuri Hapana
unachohitaji ni maarifa ya Mungu. Sasa nachotaka ufanye jioni ta leo list mambo yote ambayo unahitaji Mungu
ayasogeze ambayo yanahitaji maarifa ya Mungu. Omba rehema kwa ajili ya kutatua na akili zako
mwenyewe. Kisha futa mashataka yoyote ya ibilisi katika ivo vitu.Mungu anataka umwamini 100%
kuwa maarifa yako ndiyo alpha na Omega. Hata kama mazingira yanatukana imani yako na hakuna
hata mfano wa njia. Baada ya hapo kimoja kimoja mwambie Mungu
maarifa yangu mfano juu ya kufanya hii ndoa isonge mbele, kufanya biashara, kusoma, kutafuta kazi
nimeshindwa/yameshindwa Ee Mungu mawazo yako maarifa yako ndiyo
yatakayotoa majibu hapa. Maarifa Yako Mungu hata pia jinsi ya kuliombea hili unalitaja... Ndio yatakayo nivusha hapa. Ninaomba
sasa maarifa yako katika jina la Yesu. Maarifa jinsi ya kukaa na
mwenzangu katika ndoa, jinsi ya kulea watoto. Maarifa ya kutoka katika umasikini.Maarifa yako katika hili na hili. Maarifa jinsi ya
kufanya hii biashara. Maarifa ya kupata kazi. Maarifa jinsi ya kupata kibali kwa bosi wangu, mme,mke
wangu. Jinsi ya kutoka hapa. Mwambie Mungu hata jinsi ya kuomba mbele zako ninaomba
maaerifa. Maana ya ayo maombi manake unamwambia Mungu i surrender all to you. Maana umesema Mungu katika mstari wa 10,
maarifa yako ni kama mvua inyeshayo juu ya ardhi ikimwagilia mbegu. Mbegu ambayo ni mimi. Na
maarifa yako uliyoyafananisha na mvua yakininyeshea nitachipua. EE Mungu katika jina la Yesu. Naomba
sasa mvua ya maarifa katika uchumi. Ndoa. Kazi. Biashara. Katika lolote ambalo unalo sasa utaanza kuomba. Huku ndiko
kuomba katika mapenzi ya Mungu. Kuomba ipasavyo. Halleluyah! Usiumize kichwa, usilie, usione
hasira, usimlaumu mtu, usibebe uchungu bali omba maarifa ya Mungu. Omba mvua ya Mungu ya maarifa inyeshee iyo mbegu yako.
Oooh my God neno la Mungu lina nguvu a word of God is power. Linanguvu kuliko hata jina lake! Limetukuzwa kuliko hata jina lake. Halleluyah halleluyah.
Manake umemkumbusha Mungu ahadi yake according to situation yako. Sasa ukimaliza maombi haya
usiwe na haraka yakutoka kuwa na subira Mungu anaweza kuongea na wewe. Akakupa maarifa kwa maono
au ndoto. Na kama akikupa kama hujaeelewa usijali msihi roho mtakatifu akueleweshe yeye ndio kazi yake.usiwe na haraka wengi
majibu wanapewa ila wanaharaka ivyo hayawasaidii maana wameyacha nyuma. Maombi ya namna hii yanataka
unyenyekevu na subira. Usimlazimishe Mungu. Usiwe na haraka endelea kuomba kwa
kuatamia Mungu ataongea na wewe. Pia ukianza kuyaomba haya maombi kaa katika utakatifu
usijichanganye. Omba mpaka Mungu ameanza kuongea na wewe mipango mingine ataweza ikataa au
kuibadilisha. Chochote atakachokuambia tii. Akikuambia acha ukiache iko kitu hata kama
unakipenda. Kuwa mtiifi wa maarifa ya Mungu. Bwana Yesu asifiwe sana.Nakutakia mafanikio na uje na shuhuda katika jina la Yesu.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment