MSITENDE NENO LOLOTE KWA KUSHINDANA
Somo:
Msitende neno lolote kwa kushindana
3 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa
majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko
nafsi yake.
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali
kila mtu aangalie mambo ya wengine.
5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo
ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya
Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa
namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu,
alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa
hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili
kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na
vya chini ya nchi;
11 na
kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
12
Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi
nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu
wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
13 Kwa
maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa
kulitimiza kusudi lake jema.
14
Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala mashindano,
Wafilipi 2.
*Bwana Yesu
asifiwe, Leo asubuhi tuangalie roho ya mshindano jinsi inavyozuia Baraka za
wapendwa. Roho ya mshindano ni roho wa ibilisi. Mashindano yanaleta chuki,
mashindano yanaleta kijicho, mashindano yanaleta wivu, mashindano yanaleta
kutaka kuonekana(roho ya yebesi), roho ya kujionyesha, roho ya kutaka
kutambulika.
Roho ya
kutaka kuabudiwa, roho ya kutaka kusifiwa, roho ya kutowadhamini watu wengine,
roho ya kujikweza, roho wa kuwashusha wengine, inasikitisha kanisa siku hizi
limeingia kwenye
mashindano, baathi ya wazazi wetu wa kiroho kidogo baathi
yao wamepungukiwa na utukufu wa Mungu na
kutaka kuonekana Wao badala ya kuonekana Yesu.
Kiasi cha kuanza kuponda makanisa mengine,
kuponda watumishi wengine,bila kujua huyu ni mtumishi aliyeitwa na Mungu au
siyo! kitu kibaya Sana kumnyooshea kidole mtumishi ambaye kala gharama, ambaye
Mungu
kampaka mafuta sababu ya mashindano ya kimwili. Yesu atusaidie! Tabia hii
imehamia mpaka kwa waumini kiasi cha kutoa sadaka kwa mashindano ya kuonekana
sio kwa kusikia sauti ya Roho wa Mungu, mashindano yameingia
mpaka kwenye
mavazi kanisani, mashindano yameingia mpaka mtu anapopata nafasi ya kusimama
mbele ya kanisa kutaka kutambulikana. Kufahamika. Yesu atusaidie!
Tumefikia
sehemu ya kujitanguliza sisi kisha Yesu nyuma, Bwana Yesu asifiwe, kumekuwa Na
mashindano hata kwenye utoaji wa neno, ufundishaji wa neno, kusifu na kuabudu,
kuhubiri neno nia ya kwanza ni mtu binafsi apate sifa badala
Yesu apate sifa.
Hii huwa inaenda mpaka kwa waimbaji wa nyimbo za injili, utakuta akishapata
nafasi tuu ya kuimba akimaliza kuimba anaondoka katika ibada au anaenda kukaa
nje. Kana kwamba ile ibada haimuhusu tena. Bwana Yesu atusaidie.
Sehemu
ambayo mtu anakuwa juu ya Yesu au juu ya Mungu, utukufu wa Mungu hupungua mahali hapo, Neema ya Mungu haikai,
maana nia ya Neema
ya Mungu, utukufu wa Mungu, nuru ya Mungu kwa watumishi, au
wapendwa ni ili utukufu umrudie Yesu. Yesu utusaidie!
Mahali ambako Kuna
mashindano katika kazi ya Yesu utukufu wa Mungu hupungua huondoka, mahali penye
kufunga kwa mashindano, kutoa sadaka
kwa mashindano, kuomba kwa mashindano,
kuhubiri kwa mashindano,
kufundisha kwa mashindano, kuabudu&kusifu kwa
mashindano, kufanya ya Mungu kwa mashindano utukufu wa Mungu huondoka. Utukufu
wa Mungu hukimbia.
Mungu
hawezi toa matokeo makubwa kwenye mashindano, maana tokea mwanzo nia
imebadilishwa imekuwa Na kusudi sio la kumtukuza Mungu. Kwa iyo
utukufu
haumrudii Mungu. Mungu sehemu iyo hatendi, hafanyi, anakaa kimya, sababu iyo
Baraka, Neema, Nuru, utukufu wa Mungu utatumika vibaya
upande wa ibilisi. Ni
mpaka ujitambue, urudi kwa Mungu ndipo sasa atakuvusha. Swali la kujiuliza
ndani mwako Kuna mashindano? Zipo
chembechembe za kutaka
sifa?,kutambulika?,kuoneka umefanya?, kabla ya Yesu? Huo ni ukuta mpendwa. Je
unaposhauri mambo ya Mungu je
unashauri kwa mashindano?unarekebisha kwa
mashindano? Sehemu unapoabudu Kuna
mashindano? Mungu anaona kila kitu huwezi mficha chochote kila mahali yupo,
hata ukienda kuzimu utamkuta.
Lakufanya usiingie kwenye dhambi ingine usiinue
mdomo wako kuanza kuongea kuhusu hayo mashindano, wala usijaribu kuhukumu.
Omba
rehema, tubu kwa ajili yako, tubu kwa ajili ya kanisa, tubu kwa ajili ya
waimbaji usiwahukumu, tubu kwa ajili ya mzazi wako wa kiroho usimnyooshee mtu
yoyote kidole, iyo ndio kama
iliyokufunga kusababisha usipokee mda wote huu. Leo kweli imekuweka huru omba
rehema mbele ya Mungu Baba kwa mashindano ndani yako, omba
rehema kwa kufanya
kusukumwa na mashindano, iyo ni kamba ya mauti, omba rehema kiri udhaifu wako
kwa Yesu, Mwombe Yesu akusaidie ukivuka hapo. Yesu atakupa alichokuzuia sababu
ya mashindano. Jina la Bwana libarikiwe. Amen
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment