MUNGU KASEMA USIOGOPE! KWANINI UNAOGOPA?
BWANA YESU ASIFIWE!!!
10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
ISAYA 41:10
katika mambo yanayokondesha watu ni hofu, katika mambo yanayofanya mtu ashibe hata kama
anasikia njaa ni hofu. Watu wengi kwa nje wana amani lakini ndani wanahofu kubwa hata kama hawasemi.
Wanahofu ya vitu vingi kiasi cha kwamba hawataki hata kufikiria. Mwingine anaogopa kwa kuwa tayari ameambiwa ana pressure,
kisukari, hiv ivyo anaishi kwa hofu na wasiwasi mkubwa,kinachomkondesha ni hofu wala sio uo ugonjwa, maana hajui mwili
utaamkaje kesho, mwingine ana hofu benki wanamdai kila akikukumbuka ilo deni anapata hofu kubwa! Mwingine anamkopo saccos!
Anamkopo kazini wanamkata pesa nyingi na bado matatizo ndo kwanza yanaongeza na yote yanataka pesa.Mwingine anahofu na
ndoa yake maana anaona Ina dalili zote za kuvunjika,Na ameomba na kuomba but no changes! mwingine anahofu anajiuliza what if kama
nikifukuzwa kazi itakuwaje?wengine wana hofu ya kutokupata kazi maana Katika chuo na Hana uzoefu Wengine wana hofu kuusu uchumi maana biashara zimekuwa ngumu akiangalia hali ya
uchumi wa sasa! Anajiuliza nitajenga kweli? Nitanunua kiwanja kweli? Mwingine ana hofu ya kufeli mtihani vip kama nisipofaulu? Vip
kama Niki disco? Je maisha yangu ndo yameishia hapa? Watu wanahofu wanaishi Na hofu. Wenye huduma nao wanahofu wanaona
idadi ya waumini inazidi kupungua anajiuliza nitaishi vip? Na mimi ndo kazi yangu hii?anahuburi neno lakini yeye mwenyewe ana hofu kuu ingawa hasemi!Mwingine Leo ni
tarehe 15 tayari mshahara umeisha na zimebaki ela ambayo haimalizi hata siku 3, na anafamilia kubwa,anafikiria itakuwaje? Nani atanikopa? mwingine anahofu vip
kama kodi ikiiisha na sina pesa ya kulipa, mwingine anahofu ya mazingira yanayomzunguka kila analolijaribu halifanikiwi,akianza biashara unakuta, kila
anachokishika kinaharibika. Mwingine anahofu kuusu maisha yake maana akijiangalia miaka
inaenda hajaona hata mtu kaleta posa kwao. Na anahitaji awe mke wa mtu.
Anahitaji awe na watoto aitwe Mama flank au aitwe Baba flani. Na akiangalia hii ni June, anajiuliza je vikao vya harusi vitaanza kweli?
Mwingine anafanya kazi lakini kila akikumbuka kustaafu hofu kubwa inampata moyoni. Anashika shavu anainama chini! Ana hofu ataishi
vip? Anahofu je vip kama hii ela itaisha je nitaomba omba au itakuwaje? Hofu! Hofu!
Hofu! Yesu alijua haya mambo ndo mana anakuambia usiogope! Usiogoge! Watu wengine wanaogopa mpaka wanakuwa
wapole wakimya. Mungu anasema usiogope! Usiogope! Usiogope mpendwa! Shetani mbaya huyu
anawanyanyasa watu na kuwatishia! Kwa hofu. Ndo mana Mungu akasema mkatae shetani naye
atakukimbia! Inawezekana mashitaka anayoongea shetani moyoni mwako Kati nafsi yako ni ya kweli. Lakini mjibu nayaweza yote
Katika yeye anitiaye nguvu Wafilip 4:13, mwambie ibilisi Yesu alisema hataniacha wala sitakuwa yatima atakuwa pamoja nami hata mwisho wa dunia,
Mwambie Yesu alisema ananijua toka tumboni mwa mama yangu, kabla ya misingi hii ya dunia Mungu anakujua Yeremia 1, Mwambie
Mungu alisema atanipigania nami nitakaa kimya kutoka 14:14! Naelewa ndani yako kunaweza
kuwa kunakelele ya hofu zaidi ya haya unayoyasoma. Maana ukiangalia unaona kama Kuna ukweli wa hizo kelele
Mungu alijua haya ndo mana akasema neno langu halitapita, hadi limetimiza mapenzi yangu yote. Ndo mana akasema usiogope
nitakushika mkono! Najua unaweza kupita sehemu hata ukashindwa kuomba kusoma neno. Hata ukawa mpole na ukabaki kusubiri litakalo tokea
mpendwa mchana wa Leo neno la Bwana linakuja kama Moto kuunguza izo kelele za ibilisi moyoni mwako, nafsi yako. Neno la Mungu
ni Moto, ni upanga wa Moto. Linakuja kukurudishia tumaini. Mungu kasema Mimi ni Mungu wako,
nitakusaidia nitakushika mkono,nitakutia nguvu Mungu anajua huna nguvu za kuomba, anajua kila kitu Mungu. Mpendwa usiogope hata
kama unaona umefika mwisho, hata kama umeomba umechoka, umefunga umechoka, umetoa
sadaka umechoka hakuna mabadiliko, mwaka Jana Ni bora kuliko mwaka huu.
Mungu ndiye aliyeruusu upite haya majaribu yanayokufanya hata ushindwe kuomba! Ili ajitukuze, ili wewe mwenyewe ukiri si kwa
kusoma uje kusema Mungu ni mwaminifu vizazi hata vizazi. Mimi kanifanyia ivi, kanitoa hapa na sasa niko hapa. Halleluyah halleluyah! Mpendwa usiogope Mungu.
Usiogope Kaka, usiogope Dada! Usiogope Mama, usiogope Baba. Usiogope kijana. Majaribu ni maji ya moto tuu na yatapoa.Hautakufa bali utaishi. Wala hautaaibika mtu wa
Mungu! Mungu atakutia nguvu, ndoa yako ataitia nguvu, kazi yako ataitia nguvu biashara yako ataitia nguvu, huduma yako ataitia nguvu, najua moyoni mwako, najua kwenye nafsi yako Kuna pinga hichi
unachokisoma lakini neno la Mungu ni Moto, Neno la Mungu ni nyundo, Neno la Mungu ni upanga ukatao kuwili. Naona malaika sasa
wameshuka kuteketeza izo Roho za ibilisi zinazokuhukumu, wameshuka kukata izo kamba, kukata iyo minyororo,wameshuka kuvunja ivo viambaza, kubomoa huo ukuta wa
hofu. Halleluyah naona Moto umeshuka toka mbinguni kwenye ulimwengu wako wa roho, na maurgent wa ibilisi wanakimbia maana mkono wa mwenye nguvu
sasa umeshuka kukusaidia. Kukuponya. Mkono wa simba wa Yuda, mkono wa mwenye nguvu uwakao moto umeshuka hata
kuzimu. Na malaika wenye mapanga yawakao moto wameshuka kukusaidia.Na
amani yako Roho mtakatifu anairejesha sasa.halleluyah halleluyah. Bwana Yesu asifiwe. Sana. Na mwisho anamalizia
nitakupatia haki yako. Mungu si kwamba hajui unahaki unadai. Haki ya uchumi mzuri, ndoa yenye amani, kupata watoto, kupona, biashara yenye faida nzuri, kazi nzuri,
nyumba nzuri, gari nzuri. Wokovu endelevu unakuwa utukufu mpaka utukufu. Usiogope mpendwa. Jina la Bwana libarikiwe!
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment