"NAMNA YA KUFANYA ENEO AMBALO KUNA USHIRIKINA, WASHIRIKINA, WACHAWI! AIDHA NI MTAA, SHAMBA,, NYUMBA YA KUPANGA,SHAMBA, KAZI N.K....
Somo: "Namna ya kufanya eneo ambalo kuna ushirikina, washirikina , wachawi! Aidha ni mtaa, shamba, nyumba ya kupanga, biashara , kazi . N.k.....
Bwana Yesu asifiwe!
Kabla ya kuanza kukuelezea namna ya kufanya kwanza nataka nikuonye kitu! Maombi haya ni ya waliokoka! Kama hujaokoka usifanye haya maombi! Ili usije ukapata mabaya au madhara.
Huwezi mpinga adui na bado uko upande wa adui. Okoka kwanza haichukui hata dk. 2 ukiamua kuokoka. Ivyo tafadhali okoka kwanza ndipo ufanye maombi haya. Bwana Yesu asifiwe!
Pili wale waliosoma somo la ardhi la kwanza utagundua ya kwamba katika nyumba tatu za watanzania atleast katika mtaa nyumba moja kati ya tatu itakuwa na washirikina, au wachawi! Kuna tofauti ya mshirikina na
mchawi.
Wote ni waabudu shetani. Tatizo linakuja hapa sababu mpo katika ardhi moja au jengo moja basi laana itokanayo na ardhi na madhara ya uchawi basi yatakukumba hata wewe hata kama si mshirikina utaona neno chini limesema.
Na pia kama hujui la kufanya. Ndo mana watu mambo hayaendi, wanafunga biashara, na ameokoka haelewi kwanini mambo yanakuwa magumu siku hadi siku.
Toka enzi za akina Musa. Musa alipoenda kuwaokoa wana wa Israeli kikwazo cha kwanza kukutana nacho ni uchawi. Nataka nikuambie kwamba uchawi upo na usipowashughulikia wachawi watakushughulikia wewe.
Ayubu alipigwa uchawi.Danieli wakina Meshack, Shedrack Abednego kilichopata ilikuwa ni sababu kupinga kushiriki ushirikina. Adui wa kwanza kwa ibilisi ni wewe ambaye mwenye uwezo wa kuzuia uchawi. Yani uliyeokoka na ukasimama katika nafasi yako. Uchawi si lazima ukudhuru katika mwili.
Hata mambo yako tuu yanaweza kuchezewa ukakwama. Kwa iyo katika dunia hii hakuna katikati ni aidha upo upande wa Mungu au shetani. Hakuna kukaa katikati. Kama upo katikati manake umemruusu mchawi kukuloga.
Akili yako inaweza kulogwa, uchumi wako, ndoa yako, biashara yako, kazi yako. Au unaweza kukaliwa ukatumiwa kama daraja la kuwaletea wenzio fedha. Nyota yako (kibali chako) kinaweza kutumia na wachawi na wewe ukawa fukara masikini
Kwa iyo get into your mind uchawi upo na kama hujilindi kwa damu ya Yesu watakuloga. Tuu. Kuokoka ni kibali kwenda mbinguni! Haina maana kuwa haulogeki, kama umeokoka na hujui la kufanya
watakuloga tuu aidha unapenda au hupendi. Ivyo lazima uwe on ukae upande wa Mungu kila wakati. Bwana Yesu asifiwe!
*Sasa leo nitashear nanyi hatua 2! As times goes on tutashear ingine ziko kama saba. But muhimu kuelewa kibiblia unajua unapoelewa kitu inakutengenezea uhakika hata unapoomba unakuwa na uhakika. Na ukipita hapa mtu atakayeshindana na wewe atahamishwa, ushawi ona mtu kalogwa kazini badala yake yule aliyemloga ndio anafukuzwa kazi au kuhamishwa?
*Pia muhimu kuliko yote maombi haya hulengi mtu bali unalenga roho ya ibilisi, ukienda na picha ya kulipiza kisasi au jina la mtu katika maombi Mungu atakaa kimya alafu utakuja kulalamika sikufanikiwa. Ni sababu umelipiza kisasi na iyo si kazi yako. Utaona jinsi inavyokuwa.Kwa iyo maarifa haya ya Mungu yatumie vizuri.
1. Omba rehema kwa ajili ya ushirikina unaofanyika hilo eneo unalokaa ambayo hayo mambo yamenajisi iyo ardhi. Aidha ni nyumba ya kupanga, aidha ni ofisini kwako, aidha ni fremu ya biashara uliyopanga, aidha ni mtaa unaokaa, aidha ni shambani kwako. Omba rehema kwa ardhi kuishika kama kawaida.
ISAYA 58:12
12 Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia
*Always Mungu anatafuta mtu wa kujenga mahali palipo bomoka, kazini kama kuna ushirikina au kuna watu wanafanya ushirikina ni mahali palipo
bomoka, kwenye fremu za biashara pasipo kuwa na Mungu, shamba, nyumba uliyopanga kama hujapajenga basi ni mahali palipo bomoka! Mungu anakutegemea wewe uliyookoka usimame upajenge maana ardhi
EZEKIEL 22: 30:31
30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.
31 Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.
* umeona hapo juu ardhi isiyoponywa Mungu huachia gadhabu yake, labla nikufafanulie ili uelewe kwa undani, anasema nitawateketeza kwa moto wa hasira yangu, anasema nami nimeileta
njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao. Yani huo ushirikina unaofanyika katika ilo eneo la biashara au kazi . Mungu yeye mwenyewe madhara yake atayaweka juu ya vichwa vyao. Kama asipopatikana mtu
wa kujenga palipo bomoka.Madhara yake yatakuwa juu ya wote waliojuu ya iyo ardhi, Bwana Yesu asifiwe mpaka hapo ushajua madhara yanayopatikana kimaandiko haijalishi wewe si mshirikina.
Sasa jinsi ya kuomba rehema
Daniel 9:1-7
1 Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo;
2 katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.
3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.
4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;
5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako;
6 wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.
* tunaona jinsi Danieli alivyokuwa anaomba baada ya yeye pia kusoma maandiko, kuelewa mambo haya! Kitu nachotaka uone unapoenda kuomba rehema kwa iyo ardhi kutumika katika
ushirikina unaomba sisi. Not wao... Manake usijitoe! Angalia mstari wa 5- tumefanya dhambi! Sio wamefanya dhambi! Mtu anayesimama mahali palipo bomoka huwa hajitengi, hajiaachi nyuma maana nawe upo katika ile ardhi! Sema
sisi na sio wao. Kwa iyo unaweza shika ardhi ya ofisini, au biashara yako omba rehema na wewe ukiwepo. Unapofanya hivyo manake damu ya Yesu yenyewe itakutenga but usijitenge maana kwa kufanya hivyo utakuwa umejihesabia haki,
sema sisi tumefanya ushirikina, tumetoa kafara, tumemwaga damu hata kama wewe haukuwepo,manake unasimama mahali palipo bomoka,hata unaposimama kuwaombea rehema watu wowote sehemu yoyote si maombi haya tuu kama kuhani always jiweke
ndani.usijitenge. Bwana Yesu asifiwe!
ombea rehema iyo ardhi ya ilo jengo omba rehema kwa wote mliopo katika iyo ardhi bila kujali ni wakristo au ni waislamu. Kwa kusema sisi manake umejumuisha wote.Wanamjua Yesu au hawamjui Yesu. Bwana Yesu asifiwe.
2. Weka mipaka kwa damu ya Yesu baina ya ulimwengu wako wa roho na ulimwengu wao wa roho.
Unapofanya hivi unawazuia wasiingie, yale madhara yasikupate. Mtumishi mmoja alihamia mtaa mpya akaenda kulipia chumba kodi lakini usiku huohuo akaoteshwa kuwa iyo
nyumba anayoenda kunawashirikina
katika eneo hilo hilo upande wa pili mpangaji mwenzake, alichofanya akamuuliza Mungu nina fanyaje akaambiwa tenga ulimwengu wako wa roho na ulimwengu wao wa roho. Kwa iyo akatenga kwa damu ya Yesu.
Unajua mnaweza kuwa
nyumba moja na vyumba tofauti tofauti na pia ulimwengu wa roho ukawa tofauti. Kwa iyo alijetenga na akaamuru yale mapepo na zile roho za uchawi zisikatize ulimwengu wake wa roho.
Sababu mtu kama ni mchawi wa kuridhi na alikubali
kuwa mchawi kutoa huo uchawi ni mpaka akubali. Unaweza kutoa mapepo lakini baadae ukiondoka yatamrudia tuu. Ila uchawi wa kutupiwa, ule ambao mtu hakukubali unaweza utoa kwa iyo
tunachofanya tunaweka mpaka katika ulimwengu wako wa roho kwa damu ya Yesu. Kwa iyo chochote watakachofanya damu ya Yesu itawazuia madhara yasije kwako au yasikupate. Bwana Yesu asifiwe!
KUTOKA 8-20-23
20 Bwana akamwambia Musa, Inuka asubuhi na mapema usimame mbele ya Farao; angalia! Atoka aende majini; kamwambie, Bwana asema, Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie mimi.
21 Au kwamba huwapi ruhusa watu wangu, tazama, nitaleta wingi wa mainzi juu yako wewe, na juu ya watumishi wako, na juu ya watu wako, nao wataingia ndani ya nyumba zako; na nyumba za Wamisri zitajawa na wingi wa mainzi, na nchi nayo ambayo wa juu yake.
22 Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao mainzi wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi Bwana kati ya dunia.
23 Nami nitatia mpaka kati ya watu wangu na watu wako; ishara hiyo italetwa kesho.
*angalia ilo neno nami nitatia mipaka.kati ya watu wangu na wako.
KUTOKA 23:31-32
31 Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hata bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako.
32 Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao.
33 Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni tanzi kwako.
*Mungu anasema nitakuwekea mipaka lakini usije ukafanya maagano kwa ajili yao. Mfano wanafanya mambo yao ya asili tamaduni sijui kumbukumbu wanapika chakula wanakupa uwe na akili
usikimbilie kula kula tuu sababu umepewa iyo lazima ujue wewe uliyeokoka hatuli kila chakula au kinywaji vingine vinamaagano, unauliza umejuaje? Kwani wanafunzi wa Yesu walipokula divai na mkate
katika ulimwengu wa roho
inamaanisha nini? Si damu na mwili je si agano lile la wanafunzi na Yesu? Je shetani haigagi vya Mungu? Jibu umelipata kwa iyo angalia chakula unachopewa, sijasema usishirikiane na watu katika shughuli but utumie akili? Kwanini nasema ivyo sababu Mungu hapo juu kasema kabisa waziwazi. Ukitumikia miungu yao Tanzi litakuwa kwako.
Tanzi ni kizuizi. Bwana Yesu asifiwe. Hizi ni siri za ndani sana! Za Bwana Yesu ivyo uelewe kwa makini ufanyie kazi.
Kesho tutaendelea hatua zingine jina la Bwana libarikiwe!
kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu.Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Asante Sana mtumishi wa Mungu
ReplyDeleteMungu akubariki sana umenibariki sana ucku wa Leo
ReplyDeleteTAFADHALI MWAMINI YESU
ReplyDelete