NAMNA YA KUFUTA HUKUMU
Somo fupi: NAMNA YA KUFUTA HUKUMU
Bwana Yesu asifiwe sana!
Yeremia 18:18
18 Hapo ndipo waliposema, Njoni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njoni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yo yote.
19 Niangalie, Ee Bwana, ukasikilize sauti ya wanaoshindana nami.
*Wapendwa mlango wa ibilisi wa kwanza kabisa ni hukumu. Neno hukumu za ibilisi juu ya wana wa Mungu limekanushwa mara nyingi sana.Biblia imetoa hati ya kupinga / kufuta .Vitabu vingi sana vimetoa. Hukumu zipo za aina nyingi sana. Hukumu za maneno ya binadamu. Hukumu za moyo/nafsi. Leo nitaongea kifupi sana, nia ni kukujulisha ili upinge hukumu za ibilisi.
Kwanini tujifunze kuhusu hukumu?
1.Hubomoa imani
2.ni ukuta kabla ya kupokea kiimani
3.Ni ukuta wakati unasubiri kupokea katika mwili.
Wakolosai 2-13-14
13 Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote;
14 akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
* Hati ya mashitaka ni hati ya kukuhukumu moyo wako, ushawahi fanya kitu ukajisiki vibaya siku mbili tatu, unasikia katika moyo wako hujafanya haki, "ulichofanya ni kitu kibaya sana. Wewe una dhambi hata Mungu hawezi kukusamehe. ushawahi jiuliza kwanini watu wanatumia pombe au sigara au vilevi vya aina yoyote ili kutuliza mawazo? Sababu ni hii katika mioyo yao au nafsi zao kuna hukumu. Ushawahi jiuliza kwanini waizi, au muaji, au mbakaji au mtenda dhambi za kutisha au kawaida kwanini hawawezi fanya wanayoyafanya ni mpaka wabadili akili zao? Au ushawahi kuona mtu anavaa miwani nyeusi mda wote hata anapoongea na watu?Ni dalili ya kutokujiamini. Je unajua ni kwanini? Ni sababu moyoni mwake anasikia sauti wewe huwezi! Wewe ni mwoga! Wewe si jasiri! Wewe huna sauti nzuri mbele ya watu! Wewe utakosea ukianza kuongea! Manake hizo zinaitwa hukumu.
Ufunuo 12:10
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
* Biblia inasema ametupwa mshataka chini duniani, mshitaka uyu ana kazi hizi kukuhumu wewe katika mioyo ya watu wengine, hii inasababisha watu wasikuamini, unakosa uaminifu, hukubaliki katika mioyo ya watu, watu wanakuchukia bila sababu, hawakupendi bila sababu, yani huna kibali mbele za watu. Mioyoni mwao wanachosikia uyu anaringa, uyu mchoyo, uyu anajidahi, uyu hajapendeza, huyu anajionyesha, uyu anakuchukia. Watu wengi hizi sauti wanazisikia na huwa hata hawajiulizi ni sauti zao au zinatoka wapi? Mpendwa ukisikia sauti kama hizo ujue ni ibilisi uyo mshitaka. Ibilisi anakufanya wewe uhukumu watu wengine, ndivyo sivyo, hapo juu nimeelezea watu wanaweza kukuhukumu! Sasa pia wewe unaweza kuhukumu watu. Aidha kwa kujiinua kuwa huyu hana fedha, hana lolote, hajasoma, hajui kuvaa, hawezi kufanikiwa, hata kama hujatamka lakini ndani mwako ipo sauti unasikia inahukumu kabisa.
Hii ndio inafanya kazi mpaka kuwadharau watumishi wa Mungu, utasikia uyu njaa inamsumbua tuu. Au uyu anataka sadaka tuu. Au huyu hana upako, sasa hizi hukumu unaweza zitoa kwa kinywa chako au kwa moyo wako. Hukumu ni hukumu tuu. Unaweza muhukumu mtu ni mwizi, au tapeli, au kitu chochote kumbe masikini ya Mungu hayo maneno ni ibilisi ameyaweka ndani ya moyo wako,kumbuka ibilisi ni roho. Roho mtakatifu akusaidie kukuelewesha hapa uelewe! Hukumu hizi za maneno au mioyo huwa zinafungua laana, laana manake kutokufanikiwa. Kabla hujaanza kuomba zitakuja hukumu za kukuzuia usiombe. Utasikia ndani mwako mbona lile uliloliomba hukufanikiwa? Kwani hili litakuwa na tofauti gani na lililopita? Au mbona umetoa sadaka hamna kitu? Au unasikia wewe hujaokoka vizuri Mungu hawezi kukujibu, au wewe una dhambi hata ukitubu Mungu hawezi kukusikia,
au wewe hujui kuomba ivyo Mungu hawezi kukusikia inakuja kama mawazo na wewe unafikiri ni wewe kumbe ni hukumu za ibilisi ya Pili ni hii! Baada ya kupokea katika roho kama ushaombewa au umeomba na unaamini imekuwa kabisa, ibilisi anaweza kukutega katika dhambi au hasira, au jazba, au kitu chochote alafu baada ya dhambi tuu ile kuisha atakuambia umeharibu ule mlango uliofungua kwa kuwa umetenda dhambi. Sasa kama huna neno kwa wingi ndani yako, utaamini tayari hukumu imekuchukua. Baada ya hapo anakushitaki mbele za Mungu kuwa wewe huna imani.
Warumi 8:1
Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
* Shetani hutumia hukumu za watu juu yako aidha kwa maneno ya mdomo. Au kwenye mioyo yao.
*Shetani hutumia hukumu za mdomo wako, na hukumu za moyo wako kukuharibia mlango ambao tayari umeshafunguka
*Kumbuka Mafarisayo waliwekewa hukumu ya uongo katika mioyo Yao, wakamuonea hasira Yesu wakamuuwa. Baada ya dhambi ya kuuwa ndipo sasa akili zikajirudia.
*Kumbuka pia Stephano aliuwawa na kanisa kwa kupigwa mawe, wale mafarisayo kilichofanya wampige wamuuwe ni hukumu juu ya Stephano katika mioyo Yao.
*Hivi hivi ndivyo shetani hutumia hukumu kuharibu kibali chako. Aidha kwa kutumia watu, wewe mwenyewe, au ma urgent wake alimradi apate kitu cha kukushitaki. Ili hati iyo iweze kutumika kukunyanganga haki.
Hizi hukumu bila kuzifuta katika ulimwengu wa roho zina adhari kubwa.zinaweka alama ya wewe kushindwa. Watu wanaweza kukulaani na midomo yao usipotengua ukalaanika, mfano "hawezi fanikiwa yule" hawezi pata mtoto" hawezi fanya biashara" sidhani kama atafanikiwa" hata wachawi wanatoa hukumu juu yako juu ya ndoa yako, kazi yako, biashara yako, afya yako, mali zako ili uanguke, wanatoa hati ya wewe kuhukumiwa ili uanguke usifanikiwe katika hata moja. BWANA Yesu asifiwe sana. Ndo mana ikatoka hati ya kufuta mashitaka kupitia maneno ya Biblia. Unapohukumiwa mahakamani wanatoa haki ya mashitaka. Pia unapotaka kuachiwa huru pia wanatoa hati ya kufuta mashitaka.Kuwa mahakama hii imemkuta flani Hana hatia ya kujibu. Basi ndivyo ilivyo ilivyo usipotengua mashitaka utabaki gereza la shetani. Utasota huko Ni mpaka aje wakili Yesu afute hayo mashitaka. Akifuta tuu wale waliokuwa wanakuzuia watakimbia Na utakuwa huru.
Shetani kila siku hukutega katika maneno ya kinywa chako, hukutega katika matendo yako, hukutega katika mawazo ili tuu apate mashitaka ya kukufungulia hati. Ya wewe Mungu kutokukubariki. Nia ya neno hili ni kukumbushana tuu. Maana unaweza ukawa unapata Breakthrough ile inaanza tuu unashangaa imesimama. Kumbe mshitaki ameshakushitaki. Shetani ni mshitaki wetu kwa Mungu. Ashukuriwe Yesu! ni kweli sisi ni watenda dhambi lakini damu ya Yesu ipo kwa ajili ya kutengua kila shitaka. Maana inawezekana kweli kila dakika tunafanya dhambi. Na dhambi manake umeshakuwa adui wa Mungu lakini ipo damu ya Yesu ya kufuta mashitaka. Ni muhimu kufuta mashitaka haya. Au hukumu hizi ili mlango wako uendelee kuwa wazi. Ili mpenyo wako usije ukawa wa mda tuu, yani kila mara unarudi nyuma. Kumbe kuna mtu alikutamkia maneno mabaya aidha umesikia au hukusikia sheria ya ulimwengu wa roho inafanya kazi.
Saa ingine tunaongea sana, si wasiri hata kidogo ile umeanza kuona mwanga wa Mungu- kufanikiwa tunatangaza kwa kila mtu, bila kujua uyo mtu kakutamkia nini? Jifunze kukaa kimya kwa habari ya plan zako, kwa habari ya breakthrough, kwa habari ya mpenyo wako. Uongee pale roho anapotaka ushuhudie tuu. Au roho anapokupa go ahead. Si kila kitu cha kumuambia mtu au kusema mbele za watu. Bwana Yesu asifiwe, mwingine ile imeanza tuu tayari kila mtu anajua wengine hawapendi wanalaani uyu asifanikiwe sababu hujui sheria za rohoni na hujui kutangua kuleta hati ya kufuta mshitaka ndo inakuwa wewe unapiga mark time. Kama Mungu kaanza kukufunilia kitu au kakupa maono tujifunze kuwa magotini kwa Mungu ni mpaka ushuhuda umekamilika. Bwana Yesu asifiwe. Nilitaka twende vitani tukafute kila hati ya mashitaka juu yetu, ya kutokufanikiwa, kupiga maritime, kushindwa. Futa kwa damu ya Yesu. Omba rehema kwa wewe kuwa lango, au watu kuwa lango lako la hukumu. Futa mashitaka yote ya binadamu na Ibilisi kwa damu Ya Yesu. Tumia haya maneno hapo juu kupangua mashitaka. Kama wewe unachangamoto katika ndoa, biashara, kazi, uchumi, kufanikiwa chochote kile ujue kuna hati ya mashitaka ya ibilisi kwa Mungu. Sasa omba rehema futa hati hizo kwa damu ya Yesu ya wewe kutokufanikiwa according to tatizo lako.
Nawe utaijua kweli. Na iyo kweli itakuweka huru.
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments
Post a Comment