NANI ANAYESTAHILI KUKIFUNGUA KITABU? NA KUZIVUNJA MIHURI YAKE!!!
ufunuo 5
1 Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.
2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake?
3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.
6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
7 Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi.
8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
*ni nani astahili kukifungua kitabu? Na kuzivunja mihuri yake? Bwana Yesu asifiwe Haya maono ya mtumishi wa Mungu Yohana. Ilikuwa ni ujumbe wa Yesu kwa yale makanisa saba, Yohana aliletewa ufunuo! Anaposema kitabu anamaanisha vifungo! Ibilisi
amewafunga watu kwa kutumia vitabu vya kuzimu. Na kuweka mihuri kutumia damu za maagano ya kishetani. Hivyo vitabu ndani yake kuna utaratibu na amri juu yako wewe. Kwa vipengele vyote vya maisha yako. Ndio maana kabla ya kuokoka wewe ni mateka wa ibilisi hii ndo
maana yake! Sasa anauliza ni nani anayestahili kukifungua kitabu? Manake ni nani anayestahili kukuweka huru wewe? Na kuvunja katika vifungo ulivyofungwa na ibilisi. Hiki ni kikao cha wale 4 na wale wazee 24,wakafilikia wakakosa jibu, mstari 4 Biblia inasema
nami nikalia sana! Yani Yohana katika maono alilia sana! Ni kama wewe vile unakifungo cha uchumi au kitu chochote miaka na miaka, hakitoki! Na umejaribu kila kitu! Umemsubiri Bwana na unajua kabisa aliyekufunga ni ibilisi! Ila wa kukufungua na Yesu. Pekee...., anasema
mmoja ya wale wazee akamwambia Yohana usilie!yani Yohana unalia nini? Embu tulia kwanza Yohana. Yani manake wewe sasa usilie haya mambo Mungu mbona anayajua? ndiyo maana hata kwenye ufunuo yapo biblia inasema maana Simba wa kabila ya yuda yeye ameshinda kukifungua hizo muuri. Mpendwa huwezi kushinda hapa duniani ni lazima Yesu akufungue vifungo. Kuna vifungo vitatoka kirahisi! Kuna vifungo bila Yesu kuifungua mihuri yake au kuingilia kati nakwambia utateseka. Naongelea
majaribu ya moto yaliyongangana na mtu miaka nenda rudi, inafika sehemu mtu anaanza fikiria hivi yupo Mungu kweli? Hivi ndo vitabu vyenye muhuri, kitabu cha ufunuo kinazungumzia! Halleluyah Halleluyah! Aya ni majibu Mungu alikuwa anayajibu makanisa yale saba. Kila tatizo lipo limeandikwa katika kitabu hiki cha ufunuo, hakuna ambalo unapitia halijaandikwa, Sasa anaelezea ukuu wa Yesu biblia inasema nikaona katikati ya wazee wanne mwanakondoo aliyechinjwa,
mwenye pembe saba, na macho saba ambazo ndizo roho ya Mungu zilizopo duniani Halleluyah Halleluyah! Hapa anaelezea authority ya Mungu. Anasema akakitwaa kile kitabu manake akachukua hiko kifungo hicho kinachotishia maisha yako. Ushawahi ona mtu anakifungo mpaka anatamani asiwepo duniani, yani
anatamani hata asingeokoka. Neno analisikia imani anayo! Ila nafsi haimpi nafasi ya amani. Wewe usifikiri unayopitia Mungu hayajui. Hapo ndio sasa Yesu anasema akatwaa! akatwaa! akatwaa! mkono wake wa kuume manake iko kitabu chenye muuri. Yesu ndivyo atakavyotwaa kwako mambo yaliyoshindikana nazungumzia impossible! Yaliyoshindikana! Yesu atayatwaa!
Yesu Atayatwaa! Yesu Atayatwaa Atayachukua mikononi mwake na huo ndio utakuwa mwisho wake, unajua matatizo au vifungo haijalishi wewe ni nani? vinaweza kukukosesha usingizi. Unaweza kukonda kabisa, unaweza usisikie njaa na huku hujala kabisa. Biblia inasema akatwaa! Akatwaa! mkono wake wa kuume. Embu angalia watu walikuwa wanaulizana ni nani atakatefungua muhuri zake? Wale wanne na wazee ishirini na nne. Yohana alikuwa analia
manake anaona hivi vifungo kama hamna wa kuvifungua sasa itakuwaje? Je hawa watoto wa Mungu watalia maisha yao yote katika maono sasa. Biblia inasema Yesu kirahisi akaenda mahali kitabu kile chenye mhuri kilipo akakitwaa! akakitwaa! Halleluyah Halleluyah! Ndivyo itakavyokuwa kwako! Ataenda sehemu kwenye tatizo atalitwaa! atalitwaa tatizo lako! Halleluyah halleluyah! sasa angalia baada ya Yesu kuchukua huo
msiba wako maandiko yanasema wale wazee wanne na wale 24, wakaanguka mbele ya mwanakondoo yani Yesu, waimba wimbo mpya wastahili wewe kukitwaa na kukifungua mihuri zake, kwa kuwa ulichinjwa ukamnunulia Mungu watu kwa damu watu wa kila kabila kila lugha! Jamaa na taifa. Ukawafanya wafalme na makuhani wakuu nao
wanamiliki juu ya nchi Halleluyah! Na wewe utamiliki juu nchi. Na ndivyo itakavyokuwa kwako hilo tatizo likiisha huo msiba! Hiko kisiki, huo ukuta chochote kile kikianguka hakitainuka tena, si wewe tuu utakayefurahia bali hata
malaika kule mbinguni watafurahia halleluyah halleluyah! Mpendwa unajua kuna mambo ambayo yanatokea katika maisha yako lakini kwenye biblia yapo wazi kabisa. Mtu pekee wa kufungua hiko kitabu na kuzivunja hizo amri zake ni Yesu pekee! Yesu pekee! Yesu pekee! Yes! Haijalishi kachelewa au kawahi yeye pekee
aliyochinjwa ndio anayestahili!kukitwaa! kufungua muhuri zake! Amri zake! zikishafunguliwa nakwambia amri kwako itabadilika! Kazi itakuwa kwao si kwako tena. Haijalishi shetani anasemaje katika moyo wako, na nafsi yako imeinama Yesu pekee ndiye anayestahili. Haijalishi hiko kitabu wameandika nini huko ndani. Na wamefunga na mhuri gani haijalishi ilikuwa ni uchawi, maagano, kafara, laana, au madhabahu zilijengwa kwenu,
haijalishi umekaaa kwenye kitanzi miaka mingap? Katika jina la Yesu lazima kitanzi muhuri ifunguliwe! Lazima huo mzigo Yesu autwae sasa maana anastahili! Lazima iko kifungo sasa kiondoke! Sababu ya mwana kondoo aliyechinjwa. Sababu ya damu ya mwana kondoo! Mwenye macho saba! Mwenye pembe saba. Na ndizo roho saba za Mungu zinazoishi duniani. Halleluyah Halleluyah! kwa neno hili sasa nenda kwa Mungu mkumbushe. Mkumbushe usichoke! Usichoke mpendwa! Mwambie Yesu pekee! Yesu pekee ndio mwenye mamlaka ya kukufungua kukuweka huru!
Sehemu moja biblia inasema habakuki 2-3 "njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake Wala haitasema uongo, ijapokawia ingojee kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia" halleluyah halleluyah! Bwana Yesu asifiwe sana. Omba sasa kwa kutumia neno hili. Jina la Bwana libarikiwe!
Maombi:
Baba katika jina la Yesu, ninaomba rehema kwa kukukatia tamaa, naomba rehema kwa kuchoka kusubiri, ninaomba rehema kwa kujaribu kutatua tatizo hili mwenyewe, naomba kwa kuwa na wasiwasi na wewe, ninaomba rehema kwa kusikiza nafsi yangu, ninaomba rehema kwa matendo yangu yote, maneno yangu yote, mawazo yangu yote, malango yote niliyoyafungulia kwa kujua au kutokujua niliyoyafungulia kwa ibilisi. Ee Mungu katika jina la Yesu ninaomba unirehemu. Rehemu kutoka kwangu na kuingia kwangu, ninaomba rehema kwa kuweka imani yangu katika binadamu ninaomba unirehemu Mungu na damu ya mwanao Bwana Yesu ipite kila mahali sasa ikanitakase na kuniweka huru! Katika jina la Yesu. Dhambi na alama za dhambi zilipo katika ardhi. Anga na mbingu zake, bahari, chini ya bahari damu ya utakaso ipite sasa kunitakasa kabisa, dhambi zangu zote zitakaswe kwa damu ya Yesu katika jina la Yesu. Mungu Baba nimetambua na kujua ya kwamba mwenye haki na anayestahili kukitwaa kitabu cha vifungo vyangu, mateso yangu, na kuvunja mihuri na amri zake ni Yesu pekee. Kwa neno hili Bwana wa majeshi ninatambua nafasi yake Yesu katika kunifungua vifungo vyangu vya mda mrefu, vifungo vinganganizi, ninaruusu damu ya mwana kondoo yenye macho saba na pembe saba, vipite katika mizizi ya tatizo langu kwa jina la Yesu. Ninaruusu malaika wa Mungu kutoka ufalme wa Mungu wapite kwa mapanga ya moto wakakate mizizi ya vifungo vyangu kwa jina la Yesu, taja vifungo ivyo ...., mapepo yoyote yaliyonyuma ya kitanzi hiki, yaliyo nyuma ya tatizo hili, yaliyonyuma ya kifungo nakupambanisha na damu ya mwana kondoo katika jina la Yesu. Ee Mungu Baba waruusu malaika zako sasa kwa damu ya Yesu kwa jina la Yesu wakafungue sasa kila kifungo kinachotesa maisha yangu, wapite kila mahali sasa kwa damu ya Yesu wapite katika ardhi, katika anga na mbingu zake, wapite baharini na chini ya bahari neno la Mungu ni shoka, ni nyundo, ni upanga, ni moto ulao nalituma kwa kambi ya adui sasa kwa jina la Yesu. Ninasambaratisha kila vikosi vya ibilisi vinavyopingana na mimi kufunguliwa, kwa moto wa roho mtakatifu, nasambaratisha kila walinzi wa kipepo na watumishi wao wanaolinda vifungo hivyo katika jina la Yesu! Kwa damu ya Yesu. Na moto wa roho mtakatifu. Mungu Baba biblia imeandika vita ni vya Bwana. Ivyo naungana na roho mtakatifu kwa damu ya Yesu katika vita hivi katika jina la Yesu. Ninaruusu majeshi yako ya kumi na mawili tokea mbinguni yaje kunisaidia vita hivi kwa jina la Yesu. Kwa damu ya Yesu. Ninaruusu mvua ya damu ya Yesu inyishe kwenye kila kifungo sasa, ninaruusu mvua ya acid ya Mungu iyeyushe kila kifungo sasa kwa jina la Yesu. Ninaruusu mvua ya moto ishuke katika kila kifungo hadi kuweka huru bila kuacha katika jina la Yesu. Asante Yesu kwa kukitwaa kitabu na kufungua muhuri zake ninaomba na kushukuru. Amen
kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments
Post a Comment