NGUZO ZA MIKONO-ULIMWENGU WA ROHO
SOMO: Nguzo za mikono-ulimwengu wa Roho
Bwana Yesu asifiwe!
Nguzo katika ulimwengu wa roho inamaanisha direction. Yaani muelekeo. Wapendwa wengi tuliokoka changamoto tunayopata Si Yale yanayokuja tuu. Bali hasa Yale yaliyopita Na hatujui chanzo chake. Sasa inategemea asili yako ni ipi kabla ya wewe kuamua kuokoka, kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wako, inategemea pia umetokea falme ipi ulipozaliwa, asili yako ni nini? Wengi eneo hili huwa hawalitilii maanani sababu ibilisi adui amewafunika watu na Giza.katika fikra zao ili wasiyaelewe maandiko.
Nguzo za kifamilia au ukoo kabla ya wewe kuokoka au kuzishugulikia ndizo zinazosema kufanikiwa kwako au kutokufanikiwa kwako katika maisha haya. Mfano Kama asili yako kufanikiwa kwako lazima kupitie ibilisi shetani yani maagano, au matambiko basi utakapookoka utapata upinzani mkubwa Sana. Wengi wanasema ukishaokoka umekuwa kiumbe kipya ni kweli, lakini yapo maagano ya mababu zetu bado hayajatenguliwa, Lakini ndani ya Yesu tunashinda zaidi ya kushinda, Inaweza kuwa asili yako walitamka kuwa lazima mtumikie pombe, msidumu katika ndoa, lazima mmwage damu. Au walitamka mtu yoyote atakaye vunja miko ya ukoo kwa kuacha kuabudu miungu basi afuatiliwe asifanikiwe. Aidha unaiabudu kwa kujua au kutokujua. Wengi wanajua mikono ndo inayoshika kufanikiwa kwako katika ulimwengu wa roho. Na wanajua mkono katika ulimwengu wa roho Una nguvu ya kuongezeka.
Sasa Leo nataka nikuonyeshe aina za nguzo za mikono katika ulimwengu wa roho kisha ujitafakari. Kabla ya kuwaletea mtiririko huo, fahamu ili kitu chochote katika ulimwengu wa roho kimeshikiliwa na mikono, sasa inategemea ni mikono ipi iliyokushikilia katika ulimwengu wa roho, ipo mikono inayoshikilia kibali, ndoa, uchumi, afya, nikupe mfano huu ili uelewe, mtoto katika tumbo la mama amezungukwa na sehemu yake maalumu yakumzunguka ili asije anaenda kila mahali, au anaenda kujibanza sehemu yoyote katika tumbo la mama, anakuta zile zilizomzunguka. Sasa zile kuta katika ulimwengu wa roho ndio mikono. Kila kitu kimeshikiliwa na mikono, sasa inategemea mikono iyo iliyoshika inaasili gani, makubaliano gani, au mapatano aidha na Mungu aliyehai au ibilisi. Na hapa ndipo wengi tulipobanwa. Sasa wengi tunapofanya maombi ya vita huwa tunadili na ule uharibifu uliofanywa na mikono, kumbe kazi Si nyepesi Kama inavyooneka, inatakiwa uende kwenye huo mkono uachilie Toba, kisha umuombe Mungu aingilie Kati, abatilishe ili wewe sasa uwezo kutoka. Sasa tuangalie aina ya mikono katika ulimwengu wa roho ili Leo roho mtakatifu akufungue....
I) mkono wenye uwezo
Kumbu 28:32
Sababu ya maagano yaliyofanywa na asili yako aidha kwa mama yako, baba yako adui anauwezo wa kukuondolea uwezo katika mikono yako, inawezekana walitoa laana mababu zako kwa uchungu au kimagano, mf. Labla baba yako alitolewa laana kwa hasira na wakubwa kuwa usifanikiwe wewe na ukoo wako wote au vizazi vyako vyote. Au sababu ya kuzulumu mtu, au kupishana katika maamuzi, au biashara au chochote, basi mambo haya yanaenda katika mikono yako iliyoshikilia ndoa yako, hata Kama haukuwepo, mikono yako iliyoshikilia uchumi, iliyoshikilia vibali, unashangaa kila unalolifanya halifanikiwi. Inawezekana asili yako waliuza haki yako kwa miungu Kama Esau au Gidion. Kwa iyo sababu iyo katika ulimwengu wa roho huna mikono ya kushikilia uchumi wako, ndoa yako, pia Kama mikono ya ukoo wako katika ulimwengu wa roho iliunganisha na ibilisi basi utapata upinzani katika kila kitu. Na mikono yako itavuliwa uwezo wa kuzalisha.
ii) mikono ya utumwa
Yoshua 6:2
Yoshua 9:27
Yoshua 10: 2
Yoshua aliambiwa na Mungu nimeiweka Yerico mikononi mwako, na ufalme wake na utawala wake, hii inatuonyesha kuwa kabla ya kupewa Yoshua Yerico ilikuwa chini ya mikono mingine. Manake ilikuwa katika utumwa. Sasa inawezekana asili yako mikono yenu imeunganishwa na utumwa, ile hali ya kufanya kazi kwa bidii Sana na kutokufanikiwa au kufanikiwa kidogo Sana, ujue unamkono ya kitumwa, mikono ndiyo inayodetermine iko kitu kizae au kisizae. Ile hali ya kutaabika Sana mda mrefu huna matokeo basi ujue. Iyo ni mikono ya kitumwa. Niliwasikia mtu akiaambiwa wewe utaishia kutumwa mafaili tuu, wewe utaishia kutumwa tuu. Na kweli hata mtu asome vip? Apewe mtaji mkubwa mwisho wa siku ataishia kuwa mtumwa tuu.
iii) mkono wa uovu
Mwanzo 4:8
Kaini aliulizwa na Mungu Yuko wapi ndugu yako Habili? Mungu akalaani mikono ya kaini, unakumbuka stori iyo? Sasa inawezekana asili yako wewe Kuna mtu alifanya uovu aidha alimwaga damu, aidha alizulumu sasa ile laana inatembea inafuatilia mikono yako inaweka mbegu ya uovu, kwa iyo unashutukia kila unachokifanya kinatumbukia uovu, unazulumiwa, unaibiwa, unatapeliwa, matukio ya kiovu yanafuatilia uchumi wako kumbe hujui asili yako inamikataba hata na wewe. Kwa iyo mikono yako katika ulimwengu wa roho Ina uovu, hata Kama wewe uko okey, unashangaa kila unaloanzisha uovu unatokea upande wa pili unapata hasara, unaanza hiki unaacha unaanza kingine unaacha, hata kazini unapata kesi ya kusingiziwa, unakumbwa na bahati mbaya za kiovu hata uhusiki.
iv) mikono yenye nguvu
Ezira 1:6
Musa aliulizwa Una nini mkononi?akajibu ninafimbo
Yule mama mjane aliulizwa Una nini nyumbani? Anasema nimebakiwa na unga wa ngano kidogo, na tone la mafuta. Sasa mikono yenye nguvu huwa inaudhubutu wa kuanzisha jambo, Kuna watu hawana uwezo wa kuanzisha jambo, akifail Mara moja harudii tena, anamipango mingi katika mdomo lakini Hana udhubutu wa kuanza sasa Si makosa Yao, ni sababu Katika ulimwengu wa roho hawana nguvu, huku nje anaonekana Yuko vizuri tuu, katika ulimwengu wa roho Hana nguvu. Yuko weak, ni mdhaifu ndivyo anavyoonekana katika ulimwengu wa roho.
v) mkono wa kumiliki
Mwanzo 9:2
Mkono wa kumiliki ni huu ni ule ambao unazalisha na vitu vinakaa, sio vitu vinapita tuu maisha yako yote, Yana unabaki na historia tuu. Kuwa nilikuwa na ela, nilikuwa na hiki, sasa asili yako inaweza kuwa na maagano ya yeyote asipofanya jambo la kimzimu, au akivunja masharti ya miungu basi kitu chako kisikae, kitu chako kinapigwa, kwa iyo mkono wako unaondolewa kumiliki. Hii ni ile hali ambayo unahangaika Sana lakini hufanikiwi lakini akija mtu akigusa tuu tayari, akijaribu tuu tayari, kitu ambacho wewe umejaribu miaka yote umeshindwa, basi ukiona ivyo jua ya kuwa katika ulimwengu wa roho mikono yako imezuiliwa au imeondolewa umiliki, ivyo vitu mikononi kwako havikai vinapita tuu.
vi) mikono ya kumilikiwa
Mwanzo 16:6
Hii manake mikono yako katika ulimwengu wa roho haiko huru inamilikiwa, hii pia inajumuisha na watu kuchukua nyote yako ya mafanikio, wapo watu wakikusalimia tuu kwa kukushika mkono basi Kama hukuachilia damu tayari amechukua nyota yako, kwa iyo utafanya kazi kwa bidii Sana lakini unashangaa matokea uyaoni. Hapo ndipo utasikia anatembelea nyota ya mtu, kwa iyo mikono yako katika ulimwengu wa roho inamilikiwa na mtu mwingine. Sasa inawezekana asili yako ilingia mikataba, au maagano, au kwa kafara au kwa damu za wanyama. Na wakakabithi mikono yako kwa miungu. Kwa iyo miungu wanakufuatilia kwa madeni, kwa chuma ulete unapopata pesa tuu wanafungua madeni kwako, kisha mwisho wa siku pesa zinawarudia wao.
vii) mikono dhaifu
Ezakiel 4:4
Ushawahi kuona mtu ni mzima kabisa Hana matatizo anaomba ela? Ukimuona mtu wa aina iyo tokea leo ujue ya kuwa mtu wa aina iyo katika ulimwengu wa roho anamikono dhaifu, anazaa mapoooza, inawezakana katika asili yako, walienda kukata mti wakimaanisha katika ulimwengu wa roho, kukukata wewe mikono, kwa iyo mtu wa aina iyo hawezi kufanya kazi sio makosa yake, ndio maana ni mvivu, ndio maana anaomba, na kila anachokifanya kinazaliwa dhaifu, au kinazaa mapooza. Unakuta hawezi kabisa kuzalisha kitu kikaonekana. Na wengine uwezo Wao wa kuzalisha umepungua na siku hizi wanazaa mapooza na hawajui kwa nini?
viii) mkono wa vita
Zaburi 144:1
Lipo neno linalosema Bwana anafundisha mikono yangu vita, kikubwa cha kuelewa, kila kitu katika ulimwengu wa roho, vitu havihang tuu, vimeshikiwa na mikono, uchumi wako, ndoa yako, ile hali ya kibali, ile nguvu ya kuzalisha, nguvu ya kuendelea mbele, mikono yenye nguvu hushikiliwa na mikono ya ulimwengu wa roho,ibilisi anaweza kuondoa kitu katika ulimwengu wa roho huku duniani ukashindwa kabisa kufanya lolote, mfano wakizika kichwa cha mbuzi wakiunganisha na kichwa chako au jina lako, manake wameathiri akili yako,jitahada yako,ile hali ya kutaka kufanya, ile hali ya kuendelea mbele. mikono ina siri kubwa ya ajabu sana, ndo mana nguvu za Mungu zinapitia mikononi, lakini umiliki na na hatua zako zozote zipo katika miguu- nyayo zako. wapendwa imefikia sasa lazima tukue kiroho, lazima tuwe na ufahamu mkubwa, ibilisi kila siku anatumia mbinu mpya, kukufunga kupambana na wewe, alimradi upo hapa duniani haijalishi umeokoka miaka mingap vita ni kila siku, kufungwa ni kila siku,mitego ya ibilisi ni kila siku, vita hivi haviishi mpaka tunaingia mbinguni kwenda mji mpya kustareheshwa, ivyo usiseme umechoka, usiseme huwezi.
ibilisi anatumia nature iliyokuzunguka kupambana na wewe, hutumia anga, hutumia ardhi, hutumia maji-bahari hutumia nyota yako(kibali kwenye malango) hutumia malango yako ya kuzalisha vitu, hutumia mazingira yako sehemu uliopo, hutumia vitu unavyoshika hata simu yako, ibilisi anaweza kuitumia kukufunga,unaweza kupewa zawadi, hutumia vitu unavyokula, vitu unavyopokea, vitu unavyokunywa, vitu unavyonunua, vitu unavyopaka, kitu chochote (nature) ambacho kitakuwa na contact na wewe direct au indirect,katika ulimwengu wa roho hakuna non living things vyote ni living things,katika biology Kuna living things na non living things katika ulimwengu wa roho vyote ni living things ndo mana mtu anaweza kukuharibia maisha kwa kukushika tuu mkono, au kukupa zawadi au fedha ambayo imeunganishwa kimikataba unashangaa mambo hayaendi, mambo yanaanza kuyumba. ufahamu huu muhimu kujua Ili unapoona unapata upinzani sehemu flani ujue jinsi ya kushughulikia. Lango la uchumi lazima lipitie mikono, mikono ya ulimwengu wa roho. Tukienda katika mkono wa vita, ni ule uwezo wa wewe kufanya vita katika ulimwengu wa roho, uwezo wa kuona mambo hayaendi na ukasimama ukaomba , ngoja nikuambie kitu kimoja, unaweza unapata matatizo ya uchumi alafu kuomba unashindwa, unabaki kuchanganyikiwa, unabaki kulalamika, mfano biashara yako haiendi, au kazini mambo hayaendi badala ya kuomba kupigana katika ulimwengu wa roho, wewe unabaki kulaumu, unabaki kupiga hesabu jinsi ulivyopata hasara, jinsi ilivyokuathiri, unaanza kujutia, ukiona ivyo ujue ya kwamba mkono wako katika ulimwengu wa roho umeondolewa uwezo wa vita. Mungu mkono wako kaupa uwezo wa kuzalisha, uwezo wa kuongeza na uwezo wa kulinda. Ni pamoja na kile Mungu alichokupa kukilinda kwa maombi, mwingine Mungu akishampa hata kukilinda kwa maombi hawezi tena ataomba siku moja ya pili kaacha. Iyo ni dalili mikono yako kuondolewa uweza wake wa vita. Unashangaa mtu anamatatizo analia badala ya kuomba, anatamani hata asiwepo! Iyo ni dalili mikono yako imeondolewa uwezo wa kufanya vita. Mpendwa roho mtakatifu akusaidie haya ni mambo ya ndani Sana, ya rohoni Sana. Zipo koo asili Yao hawana uwezo wa vita katika mikono yao, wao ni watu wa kuonewa tuu, nazungumzia kiroho na si kimwili.
ix) mikono iliyokatika/kilema
Waamuzi 1:6
1samweli 2:27
Wapendwa wapo watu katika asili Yao mikono Yao imekatwa, imekatwa Katika ulimwengu wa roho, ingawa huku nje wanaonekana wako sawasawa ndio maana wanashindwa, kufanya lolote maana mikono yako ni kilema katika ulimwengu wa roho, mikono kilema uwezo wake ni mdogo, mkono kilema haiwezi kushikilia vizuri ndo mana kila unalolishika linakuponyoka, mikono kilema haina spidi, haina nguvu, hivyo hivyo ndivyo inavyokuwa katika uchumi wako, Hizi nguzo zinawezekana zimewekwa na mababu, walikabithi mikono yenu kwa mizimu, sehemu ingine wanakabithi moyo, wanakabithi vifua, sasa maagano yanapovunjwa ndipo ile mizimu inaleta uharibu ikiwemo kukata uwezo wa mikono ili watu wabaki masikini, wabaki fukara, maisha duni, hata akipewa msaada mtu wa aina hii atapoteza alichopewa maana katika ulimwengu wa roho mikono yake inaukilema. Roho mtakatifu akusaidie kujua, kutambua siri hizi. Ni mpaka ujue tatizo lako na roho akusaidie maarifa jinsi ya kushughulikia. Ndipo utakapo okoka, ivyo usije ona mtu ni fukara Hana uwezo, ila hata akisaidiwa akiwezeshwa hawezi alafu mnamkasirikia ukajua ni tatizo lake. Hapana! kuna kitu katika ulimwengu wa roho kilifanyika. Bwana Yesu asifiwe, roho mtakatifu akusaidie uelewe siri hizi. Si kila anayeonekana nje ndivyo jinsi alivyo, bali ni vifungo vya vizazi hata vizazi pamoja na kuokoka lakini kama bado hujashughulia bado utabaki kwenye umateka huo.
x) mkono wa uharibifu
Danieli 11-6
Nitatoa mfano ambao unaujua hajawahi kuona housegirl anakuja nyumbani kwako anavunja vyombo vyote, kila anachoshika kinavunjika unanunua vyombo vingine anavunja. Ila wewe mwenyewe ukitumia au ukiosha havivunjiki? Ushawahi jiuliza what happened? Kuna koo zinalaana za kutokufanikiwa, na hizo laana zimeleta uharibifu katika mikono, kwa iyo mikono iyo kila itakachokifanya lazima kiharibike, mikono hii ipo hata kwenye ndoa, alafu watu wanapambana kwa maombi ya vita wanashughulikia matokeo ya ile mikono ya uharibifu vita hii inaisha inainuka nyingine, hii inaisha inainuka nyingine, unakuta kama ni gari kanunua leo ataenda kuligonga tuu, kama anafuga kuku watakufa, chochote anachoshika lazima kipate uharibifu tuu, sasa hii haishii hapa, ni kwake yeye au watu watakaowazunguka, kama mtu aliingia kwenye ndoa ambao huo ukoo kuna mikono ya uharibifu atapata shida sana, chochote mikono hii itakachoshika lazima ilete uharibu. Na wewe unasema ni vita vya ibilisi labla ni uchawi, kumbe vifungo vipo katika mikono yako. Bwana Yesu asifiwe. Hii pia ndo inayosababisha vitu hazikai, akinunua leo kesho kimekufa, kila anachoanzisha kimekufa, kila biashara atakayofanya inakufa. Sasa ukiona watu wa namna hii ujue na utambue ya kwamba ipo mikono ya uharibifu katika ulimwengu wa roho.
xi) Mkono wenye hila
Daniel 8:25
Hii ni mikono ya utapeli, ni ile hali kuongozwa na hila katika kila unalolifanya yani hupati mtiririko mzuri, unapitia magumu isivyo kawaida katika utafutaji wako, mara umesingiziwa, mara umeibiwa, mara umetapeliwa. Yani mabaya yanakukumba wewe, mara unapata kesi ya polisi haikuusu wewe, mara umenyanganywa kiwanja na wenye fedha, mtu wa aina hii sawasawa na Daniel 8:25 , mikono yake katika ulimwengu wa roho.yawezekana imeunganishwa na mikono ya hila. Hila za adui, mizimu, au roho wanazoabudu sasa wanafuatilia vizazi hadi vizazi na inakuletea wewe shida. Inakuletea wewe taabu, unakuta wewe ni mtu wa bahati mbaya tuu, mara wakuvunjie duka, mara nyumba ishike moto, au biashara iungue kwa moto, kama ni gari la biashara utakuta linapata ajali kila leo. Wengine ile kununua biashara ya bodaboda siku iyoiyo inapata ajali, yeye anafikiri ni vita vya kichawi kumbe hajui mikono yake asili Kuna hila katika mikono. Roho wa Mungu akusaidie Sana. Kwa iyo kila anachofanya kiuchumi kinaishia kupata hila.
xii)mikono ya udanganyifu
Hosea 12:7
Udanganyifu ni ile hali ya kudhania iko ndicho kumbe siko, wako watu huwa always wanaangukia kwenye kitu kibaya, mtu wa aina hii huwa anauchaguzi mbovu wa biashara au kazi, utakuta kapata mtaji mzuri tuu, mikono ya udanganyifu inamfunga kwenda kufanya vitu ambavyo haviwezi kumtoa wala kumsaidia na vitaishia kumpa hasara, mfano ameenda kununua kiwanja kumbe cha udanganyifu, kinamletea matatizo, kakurupuka kufanya biashara ambayo haina faida. Ila mikono ya udanganyifu ndiyo iliyomsukuma, anaenda kununua kitu kwa nia ya kupata fedha lakini kilichomsukuma ni ile mikono ya udanganyifu. Sasa hii inapelekea kufanya maamuzi mabaya. Kuingia katika mitego ya matatizo, kujikuta katika madeni, kujikuta kupata hasara na kila siku kuanza mwanzo. Kinachomfanya afanye kitu ambacho ni hatari kwake au kitamuingizia hasara ni ule mkono wa udanganyifu unamfanya afanye vitu kwa kurupuka na mwisho wake ni hasara, sasa zipo koo au familia wana mikono ya udanganyifu au kukurupuka ni kila Mara inaishia kuwaletea hasara. BWANA Yesu asifiwe kwa iyo ukimuona mtu wa aina hii jua siyo yeye Bali lipo tanzi katika mikono yako linalomfanya ashindwe kufanya maamuzi sahihi, mikono iyo ya udanganyifu ndiyo iliyoshikilia ufahamu wako, akili yako, maamuzi, na kuamini kuwa upo sawa angali umekosea. Na mikono hii imeshikilia mpaka upande wa ndoa, kazi, biashara na imani pia. Roho wa Mungu akusaidie uweze kuelewa, ujue tunaposema mikono katika ulimwengu wako wa roho tunamaanisha nini? Jina la BWANA libarikiwe Sana. Endelea kusoma maneno yote katika biblia yaliyowekwa hapa, usiishie tuu katika maelezo. Omba rehema kwa ajili ya mikono yako kwa kipenge chochote ulichokiona fanya ukombozi wa mikono yako kwa damu ya Yesu. Kwa kudeal na sehemu husika.
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Amen! Amen! Amen! YESU wangu akukumbuke akubariki sana
ReplyDelete