PART B ARDHI IMEBEBA ROBO TATU YA MAISHA YA BINADAMU
Part B
Somo: Ardhi imebeba roho tatu ya maisha ya binadamu.
*Baada ya kujifunza kuhusu madhabahu jinsi ambavyo
inavyocontrol ulimwengu wa roho,kuhusu ardhi hasa sehemu tunazokaa au kuishi na
jinsi Mungu anavyoweza kuwa establish madhabahu sehemu tunazoishi and what is
happening baada
ya kuistablish katika
ardhi unayoishi! Na jinsi shetani ivyo ivyo anavyoweza iga na kujitambulisha
kwa madhabahu kupitia ardhi. Na nini kinatokea, na umuhimu wa ardhi na maisha
yako.
*sasa ni muhimu. Kuona Mungu mwenyewe alivyobomoa madhabahu
za ibilisi. Same alivyofanya ndo jinsi wewe utaenda kufanya kwa msaada wa roho
mtakatifu.
*Pls maneno yote yaliyowekwa hapa ufuatilie kwenye biblia
yako na kufuatilia.contents na msisitizo wa maelezo kwenye somo hili utalipata
utakapokuwa unasoma mistari ile ya biblia kwa kuirudia na kuirudia!
Maelekezo yangu ni
kukusaidia uelewe! Kama nilivyosema Ni somo sensitive, ivyo soma Mara ya kwanza
ya pili utaanza kuelewa taratibu kupitia hayo maandiko,
jinsi unavyosoma na
kusoma ndivyo unazidi kufunguliwa na maelezo yangu kidogo. Ukielewa hapa jua
kabisa umevuka kipande kikubwa Sana.
Waamuzi 6-11-16
11 Malaika wa Bwana
akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake
Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya
shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
12 Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana
yu pamoja nawe, Ee shujaa.
13 Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa
Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake
ya ajabu,
waliyotuhadithia baba
zetu, wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa
ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.
14 Bwana akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo
wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?
15 Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa
jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi
ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.
16 Bwana akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja
nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja.
* wote tunaifahamu habari ya Gedion na ninajua wote
mnaipenda kama Mimi jinsi ninavyoipenda;
*Baba yake Gedion alikuwa mshirikina na watu walikuwa
wanakuja nyumbani kwa Baba yake Gedion kufanya mambo Yao.
*Mungu akaamua kumtumia Gedion ambaye ndo alikuwa mdogo
kabisa Katika familia hii. Na akaamua kwenda kwenye ingini ya tatizo. Yani Ni
sawa na sasa hivi awepo mshirikina mtaani kwenu alafu Mungu amtumie mtoto wa
mshirikina kukomboa mtaa mzima. Bwana Yesu asifiwe!
*angalia pia hapo juu Gedion anamwambia BWANA kuwa Mimi ni
mdogo na pia ni masikini nitawaokoaje wana wa Israeli? Kitu kimoja ambacho
nataka nikumegee
angalia Baba yake Gedion anamtumikia shetani na nyumbani kwake Kuna madhabahu
ya ibilisi, lakini pamoja na hayo bado wakina Gedion ni masikini wakutupwa.
Angalia hapo juu anavyomjibu Bwana. Labla ulitegemea
wakina Gedion wawe na
maisha mazuri sababu lango la kuzimu lipo kwao kwa iyo watu wanapokuja kuleta
kafara zile au sadaka kwenye iyo madhabahu labla
wangenufaika lakini
ndo kwanza maisha yakina Gedion yanakuwa magumu zaidi. Ndo mana hata wachawi na
waganga
angalia maisha
Yao.angalia maisha ya watoto Wao, angalia ndugu zao wa karibu utakuta wanakufa
tuu. Au wanauana Si kitu mtu unaweza tamani hata kidogo.
*Sasa angalia Mungu anampa assignment Gedion ya kuvunja
Madhabahu ya Baba yake mwenyewe,Na Baba yake hajui. maana ndio inayowaletea
umasikini na taabu zote.
Angalia mstari wa
13,mlango wa 6 kule juu. Gedion anamlalamikia Mungu kuwa yule Mungu
tuliyemsikia kwa Baba zetu
yako wapi matendo
yake? Bila kujua sasa Mungu kaleta majibu. Yani kwa maana ingine anamwambia
Gedion tatizo lipo
nyumbani kwa Baba
yako hapo unapoishi.maana ndiyo inayofanya Yale matendo makuu ya Bwana
msiyaone. Ndio inayowalete umasikini wenu. Angalia mwenyewe hapo juu maandiko.
Mlango wa 6
22 Gideoni akaona ya
kuwa ni malaika wa Bwana; Gideoni akasema, Ole wangu, Ee Bwana MUNGU! Kwa kuwa
nimemwona Bwana uso kwa uso.
23 Bwana akamwambia Amani iwe pamoja nawe;
usiogope; hutakufa.
24 Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu
hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya
Waabiezeri.
25 Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae
ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe
madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu
nayo;
26 ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu
ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe
sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.
27 Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa
watumishi wake, akafanya kama Bwana alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu
aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo
wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku.
28 Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na
mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu
nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu
iliyojengwa.
29
Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo hili? Hata walipotafuta habari na
kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi, ndiye aliyetenda jambo hili.
30
Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao, afe; kwa sababu
ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera iliyokuwa karibu
nayo.
31
Yoashi akawaambia watu wote waliokuwa wakishindana naye, Je! Mtamtetea
Baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye atakayemtetea na auawe hivi asubuhi; kama yeye
ni Mungu, na ajitetee nafsi yake, kwa sababu mtu mmoja ameibomoa madhabahu
yake.
*Sasa hapa
tunakuja jinsi kubomoa tatizo, nikupe kitu kimoja unapo okoka Ni tiketi ya
kwenda mbinguni. Ila kufanikiwa hapa duniani ni vita ingine lazima upigane bila
kuchoka. Katika kupigana ndipo Bwana
atakuja kukusaidia kukutoa. Jiulize kama Bwana
asingelimtokea Gedion hivi angejuaje kama matatizo yote kumbe yapo nyumbani
kwako. Tena kwa Baba yake? Can you imagine? Unaenda kanisani huko mnakesha kuomba, unamtafuta
Mungu kwa gharama
kubwa mno kumbe tatizo lipo nyumbani kwako. Kumbe tatizo lipo kwenye Shamba la
Babu yako huko kwenu. Kumbe nyie mlikabithiwa kwa mizimu. Mwingine atasema
lakini si nimeokoka ni sawa. Kumbuka Yesu
ilimbidi Angie
ardhini afe afufuke ushawahi jiuliza kwanini Yesu alizikwa ardhini? Leo ngoja
nikujibu Yesu alizikwa ardhini ili kuharibu madhabahu zote ziliwekwa na ibilisi
katika ardhi. Ushawahi sikia wakisema nchi ya Israeli ukienda kule
ukikanyaga unasikia
uwepo wa Mungu? Ushawahi jiuliza kwanini? Ni sababu ile ardhi imetengenezewa
madhabahu. Kitendo cha Yesu kutoka Katika ukoo wa Ibrahimu na Daudi
kimemuunganisha na ardhi ya Israeli. Kwa iyo yeye kufa na kuzikwa katika ardhi
manake Ni
kukamilisha madhabahu
katika Israeli ndo mana kuna uwepo wa Mungu. Yesu alikuwa anajenga madhabahu
pale kaivari. Bwana Yesu asifiwe.By the way Shetani anaiga kila kitu. Angalia
jinsi Yesu alivyosulubiwa na kufa na kuzikwa. Haina tofauti
wanavyochukua mnyama
kumchinja na kumfukia katika ardhi.sema kinachotofautisha ni lango lipi?
Shetani anaiga tuu. Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu. Ninaongea haya ili macho
yako yafunguke. Na ukifunguka wewe utawafundisha wengine.
*Sasa angalia maelekezo ya Mungu Gedion aliyopewa ili
kuangusha madhabahu za baali. Ooh Jesus i love your bible! Ni nzuri! Mungu
akamwambia achukue ngombe wawili, ngombe wa kwanza ni wa kuangusha madhabahu ya
Baba yake.
Ngombe wa pili ni kumjengea Mungu madhabahu. Soma
kwa makini mstari wa 25,26,27,28! Niliposema
neno hili ni sensitive angalia jinsi kiti cha enzi cha
shetani Mungu alivyokingoa. Kwa
utaratibu! Gedion pengine angekosea maelekezo pengine angekufa. Sababu usifanye
mchezo na madhabahu.
*Sasa Gedion kwa kuona ile hatari alivunja ile madhabahu
usiku na walipoaamka wakakuta madhabahu hakuna tena. Angevunja mchana
ingemletea shida.
*Sasa hapa ndipo patamu baada ya ile madhabahu kuvunjwa mstari wa 29, wale wachawi, waganga, wapiga
ramli, ma urgent wa ibilisi wakajiuliza ni nani aliyebomoa madhabahu hii?
Walipotafuta
wakaja gundua Ni
Gedion mwana wa Yoashi, sasa angalia mstari 30! Yoashi ndo alikuwa mkubwa wa
Ile madhabahu ya ibilisi na sasa wale waabudu baali wanamfuata Yoashi
wanamuambia mtoe
mwanao auawe! Sasa
hapo ndipo lile neno somo la Kwanza
ufunuo 11-7 utaliona, kuhusu yule mnyama aliyepewa nguvu na ibilisi na kiti cha
enzi, na nguvu nyingi. uyu ndo anasukuma watu sasa wakamuue Gedion. Lakini
Sababu sasa ile madhabahu haipo haina nguvu ndo mana Baba yake
mwenyewe Gedion,
mstari wa 31 anawajibu "Mtamtetea baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye
atakayemtetea auawe hii asubuhi!anasema kama yeye ni Mungu ajitetee nafsi
yake" halleluyah halleluyah! God is Good. Angalia baada ya
kuvunjwa madhabahu
yule mkubwa wa wachawi ndio anawageuka wenzake anawaambia uyu mungu baali
tuliyokuwa tunamwabudu kama yeye ni Mungu ajitetee mwenyewe, manake alikuwa
anasema hivi ni Mungu gani uyu ambaye binadamu mpaka washike marungu na
mapanga wamteteee!
Mungu gani asiyeweza jitetea. Kwa maana ingine Mungu akanionyesha kitu angalia
jinsi mungu wa ndugu zetu waislamu kwanini wanafikia sehemu wanatumia upanga au
kujilipua na mabomu kulazimisha sheria zao je maombi Yao hayatoshi?
Inamaana ni mungu
ambaye hawezi kujitetea ndo mana wanamtetea kwa nguvu zao. Ni Mungu wa aina
gani anayetetewa na watu? Mungu anatakiwa atetee watu. Sio watu wamtetee kwa
kumpigania vita. Vita vinafanywa na mungu na sio na watu Bwana Yesu asifiwe
ndio maana sisi Mungu
wetu anajitetea mwenyewe. Bwana Yesu asifiwe Sana. Inamaana kama ile madhabahu ingalikuwa
haijavunjwa pengine Baba yake angemnyonga mwenyewe mwanae. Maana lile joka la
ibilisi lingemwekea
hasira ndani ya Baba yake. Bwana Yesu asifiwe
Sana.na ivyo ndivyo jinsi Gedion alivyowaokoa wana wa Israeli kutoka Katika
mateso ya mungu baali.
*mpendwa nachotaka kukuambia ni hiki kila tatizo
linaufumbuzi wake. Kama ulifungua kipengele cha uchumi kwa kutumia upako mafuta
wa mafuta ya Mtumishi flani haina maana pia
unapotaka kupata
watoto lazima Mungu atumie hayohayo mafuta. Bwana Yesu asifiwe Sana.
Inawezekana kabisa shida unayopitia inatokea kwenye ardhi.vita vya miungu. Sisi
hatuchinji ila isipokuwa tunatumia damu
ya Yesu ambayo
ilishaandaliwa kwa ajili ya wewe kutumia. Kuiombea ardhi tunaiombea kwa
kuishika tuu.ardhi asili yake inalaana rejea stori ya kaini kitabu cha mwanzo. Lakini laana ile vunjwa na Yesu.
Halleluyah. Ila hata baada ya ukombozi wa ardhi bado binadamu wameendelea
kumjenge ibilisi madhabahu kupitia ardhi hapo ndipo tatizo linapokuja sasa. Na
kujua unachokifanya. Baada ya kuelewa sasa.
Sasa twende jinsi ya kuiombea ardhi. Hapa nazungumzia ardhi
ya maisha yako. Unapoishi, ulipowahi kukaa, ardhi ya kwenu, kabila la mama
yako, kabila la baba yako, ardhi hii ikifunguka na vitu vingi Sana vitafunguka.
Na unapoanza
maombi haya usiache!
Ila tuu nikujulishe vita lazima vitakuwepo ila Ni bora kupambana kwa Maombi ili
ufanikiwe kuliko kubaki kwenye vifungo unaenda mbinguni na umasikini wako na
vifungo
vyako. MUNGU
ATAKUSAUDIA UTASHINDA.Ardhi hii unachukua kidogo tuu mkononi unaomba. iyo iyo
hapo unapoishi unaishika kwa kutumia ardhi ya kwenu kwa imani. Yani ardhi
mkoani kwenu unaishika kwa imani. Kumbuka ulimwengu wa roho hakuna umbali.
Kumbuka yule akida akamwambia Yesu sema neno moja tuu. Ili ujue kuwa katika
ulimwengu wa roho hakuna umbali. Na dunia hii hata kiganjani kwa Mungu
haitoshi. katika Yale mambo yako magumu embu yafungue kupitia ardhi.
Mtumishi mmoja anasema alipoanza kuiombea ardhi ya kwao kule
machame moshi akaanza kuota wanyama wa kutisha anapambana nao. Kumbe kwao Kuna
makaburi si unajua wachagga makaburi yanakuwa nyumbani kwa mtu. Akawa anaamshwa
usiku Sana anaomba. Baada ya kuomba
mda si mrefu akaja
akaota limetokea dubu na Chui wanamua attack lakini katika vita ivyo Mara
wakageuka watu wenye upanga mrefu Sana, wakataka kumkata, akashika ule upanga
akausukumia shingoni mwake akamchinja wakafa. Na baada ya hapo alipata ushindi
mkubwa
Sana anasema Kuna
mahali alikwama kabisa akavuka kiurahisi. Mama mwingine arusha alikuwa akilala
anatambaliwa na wadudu sisimizi hawaoni lakini wakamuombea miaka na miaka
hajawahi
pata nafuu lakini
watumishi walipoenda kuiombea ardhi wale sisimizi Mtumishi anasema aliwaona
kwenye ndoto wanaanguka wanakufa ndio uponyaji wa uyo mama.
*kwa iyo Roho mtakatifu akikusukuma Leo au baadae ufanye
maombi haya yafanye. Ila akikuambia subiri basi subiri.
Sasa twende kwenye hatua ya mwisho
kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka
nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako
biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni
kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige
hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande
wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi
ndugu yako Joseph Ntandu
Hatua 10 za kuiombea ardhi
(according to Roho Mtakatifu alivyonifunulia)
*Maombi yawe ya siku 7, na muendelezo mpaka umevuka na
kupata ushindi. Muhimu kufunga masaa 12, kufunga manake kuruusu ulimwengu wa
roho uwe active zaidi ya mwili. Uwe katika mood ya kuomba mda wote.
1.Jitakase kwanza wewe mwenyewe kwa damu ya Yesu. Omba
uongozi wa roho mtakatifu katika maombi haya. Omba ulinzi wa Mungu kwako kwa
damu ya Yesu juu ya Maombi haya. Isaya 54:17
2. Watakase watu wote waliohusika kujenga madhabahu kwa damu
ya Yesu. Hata kama huwajui achilia damu ya Yesu juu Yao watatakasika na kuwekwa
huru. Isaya 1:18. Damu ya Yesu inamacho Saba (7) na roho Saba (7) damu
itawafuata na kuwatakasa. Hata kama hawapo ila madhara yake yaliyobaki kwa watu
yatatakaswa kwa damu ya Yesu. Usicheze na hii damu kabisa.
3. Shika ardhi mkono wa kuume omba rehema kwa ajili ya ardhi
iyo. Itakase iyo ardhi kwa damu ya Yesu, futa laana zote zilizotokana na
kafara, madhabahu za ibilisi omba rehema kwa iyo ardhi kwa kutumia kama malango
ya kuzimu. Achilia damu ya Yesu juu ya iyo ardhi. Utakaso na uponyaji.
4. Sifu na kuabudu huku umeshika iyo ardhi ili isikie nyimbo
za Mungu. Ardhi huwa inasikia. Abudu na kusifu mpaka mzigo huo umeisha ndani
yako. Kwa kufanya ivyo unakaribisha uwepo wa Mungu Katika iyo ardhi.
5. Anza kubomoa sasa na kuharibu kwa damu ya Yesu madhabahu
zote zilizojengwa na ibilisi, na kungoa viti vya enzi kwa mamlaka ya jina la
Yesu, na kwa damu ya Yesu huku umeishikilia ardhi.
6. Kwa damu ya Yesu sasa na mamlaka ya Yesu shusha kiti cha
enzi cha Yesu Katika iyo ardhi, ruusu sasa makao ya kiti cha Yesu Katika iyo
ardhi. Huku umeishika iyo ardhi.
7.Jenga sasa madhabahu ya Yesu. Unganisha iyo ardhi na
madhabahu ya msalaba wa Yesu. Unganisha iyo ardhi kwa damu ya Yesu na madhabahu
ya Yesu aliyoijenga pale msalabani. Amuru uhai tokea ardhini wa Yesu ule
ulioshinda mauti uje katika ardhi uingie katika iyo ardhi kwa jina la Yesu.
8.Mshukuru Yesu kwa yote mpaka sasa. Utakuwa umefanya jambo
kubwa Sana katika ulimwengu wa roho. Ingawa kwa macho huoni ila amini
inatendeka kwa 100%. Shetani asije kukudanganya eti hakuna kitu. Inafanyika.
9. Sasa ni mda mzuri wa kutamkia mema iyo ardhi, kupitia iyo
madhabahu uliyoishusha sasa jenga upya vitu vyote vilivyoharibika, fungua
malango ya kifamilia na ukoo yaliyofungwa katika iyo madhabahu ya Yesu. Fungua
mambo yako binafsi pia yaliyofungwa au ambayo hayaendi kupitia iyo madhabahu ya
Yesu. Tumia damu ya Yesu kutamka.
10. Toa sadaka ya shukrani ya maneno, katika iyo madhabahu
ya Yesu. Toa sadaka ya shukrani dhabihu ya kumshukuru Yesu kwa kujenga
madhabahu mpya katika iyo ardhi. Hakuna madhabahu ambayo haitolewi sadaka. Sasa kwa sadaka iyo Eneenee kwa damu ya Yesu
kupitia iyo madhabahu uombe Yesu akupiganie endapo Kuna vita vyoyote vitainuka
kwa sababu ya kungoa viti vya enzi vya ibilisi. Na kwa sadaka iyo uliyoiunga
kwa damu ya Yesu. Omba Yesu afungue mipango yote iliyokuwa imefungwa.
*mpaka hapo unaushindi mkubwa Sana. Jina la Bwana
libarikiwe.
*kumbuka tunaombea ardhi ili kufungua mambo yaliyokuwa
yametufunga. Na kuleta ufalme wa Mungu mahali unapokaa. Ivyo baada ya Maombi
haya utaendelea na Maombi yako ya kila siku. Bwana Yesu asifiwe Sana.
*Pia hata siku Saba zikiisha tokea Leo weka utaratibu wa
kuendelea kufungua ardhi. Jinsi inavyofunguka ndivyo jinsi Kuna mambo ilikuwa
huyaoni utaanza kuyaona. Na utaanza sikia Mungu kwa clear akiongoe.
*Ibilisi asikudanganye eti hakuna kitu no kipo kitu. Ni janja ya kukufanya uache kuomba.
Nikutakie ushindi
mkubwa katika maombi haya Katika jina la Yesu.
Comments
Post a Comment