PART B, "NAMNA YA KUFANYA ENEO AMBALO KUNA USHIRIKINA, WASHIRIKINA, WACHAWI! AIDHA NI MTAA, SHAMBA,, NYUMBA YA KUPANGA,SHAMBA, KAZI N.K....
PART B
Bwana Yesu asifiwe!!!
3. Tuma utiisho kwa wale wanaofanya ushirikina
Kutoka 23-27-28,30
27 Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao.
28 Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako.
29 Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua.
30 Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi.
*Kama hujafanya hatua za nyuma usikimbilie hatua za mbele haya ni maombi ya kikanuni! Bwana Yesu asifiwe ukiwa unaomba kikanuni adui hawezi kukuepuka! Pia ni maombi hatari kwa ibilisi ivyo hakikisha umevaa silaha zote za Mungu kabla ya vita. Hakikisha huna kikwazo kwa upande wako wala kizuizi.
Tuendelee
Baada ya kuweka mipaka hatua inayofuata kutuma utiisho wa kimungu. Wapendwa hakuna kitu kinachotisha kama utiisho wa Kimungu.
Mtumishi mmoja alienda kupanga sehemu kumbe mwenye nyumba mshirikina! Alipofikia step ya kutuma utiisho baada ya kutuma utiisho yule mwenye nyumba alikuwa
anamkwepa yule mchungaji hatoki nje mpaka yule mchungaji katoka. Mpendwa wewe ni mtu mkubwa sana katika ulimwengu wa roho!
Hatushindi vita sababu ya maombi tunashinda vita kwa sababu ya kuomba kikanuni, na kwa maarifa ya Yesu,unajua umepewa mamlaka kubwa Sana mpendwa? Ukimtumia mtu utiisho wa Mungu. Mungu ndiye anaenda kuwatisha wanakosa amani mtu kama uyo hawezi simama na
wewe sehemu moja akiona umetokea mahali anaondoka Bwana Yesu
asifiwe!
kama ilikuwa ni ofisi moja na mshirikina unaweza sikia mtu kaacha kazi, au kama ni fremu za biashara unaweza sikia kafungaduka, usicheze na utiisho wa Mungu Ila hakikisha, narudia tena wewe uwe Safi mbele ya Mungu! Yani umeokoka, umesamehe wote waliokukosea moyoni siyo
mdomoni,unajua kipimo cha kumsamehe mtu moyoni. Ni hiki tangaza kuwa umemsamehe, kisha muombee rehema mbele za Mungu. Muombee ulinzi mbele
za Mungu.
Kisha mbariki afanikiwe!Muombee baraka Ukiona umeshindwa basi jua hujamsamehe! Hii ni ukuta mkubwa Sana wa maombi, na watu wengi wanafikiri wamesamehe watu kumbe wamewaweka moyoni.
Bwana Yesu asifiwe sana sababu hayo ni Maombi ya mamlaka, ivyo lazima uwe Safi maana Mungu ni msafi. Turudi hapo juu anasema nami nitatuma utiisho wangu utangulie mbele yako! Unaona mpendwa kwenye Maombi haya kama utaenda hujasamehe waliokukosea manake utakuwa na hasira ndani yako isiyoisha na unaweza katika sehemu hii kwa hasira ukatuma utiisho wako badala ya wa Mungu. Na unapotuma utiisho huu usimpangie Mungu jinsi ya kufanya omba tuu Mungu atume utiisho wake the rest mwachie Mungu. Kuna wakati mwingine
tunachukua nafasi ya Mungu. Ndo mana Mungu anakaa kimya!
Anasema nitafanya maadui zako wakuonyeshe maungo Yao si Katika lugha ya kwanza no! But lugha ya pili manake wataaibika mbele yako. Kivipi
kama walikusudia ufunge duka Wao ndo watafunga duka, Kama walitaka uache kazi au ufukuzwe kwa uchawi Wao ndio waacha au kuachishwa kwa kuogopa, kwa kukosa amani kama walikusudia mabaya hayo mabaya yanageukia kwao na wewe unazidi kupata kibali. Hii ndo siri ya utiisho wa Mungu. Lakini narudia tena
ili ifanye kazi kwako. Maombi ya namna hii yasisukumwe na wivu, hasira, chuki, kijicho, kutokusamehe, kisirani, uchungu na yanayofanana na hayo. Ni wewe na Mungu si wewe na Mtu.
najua nimeeleweka naongea hivi ili uone mkono wa Mungu sawasawa na maandiko. Bwana Yesu asifiwe Sana. Anaendelea kusema nami nitapeleka
mbele Yao mavu Ni nyavu. juu ya mhiti, mkaanani, mhivi hayo makabila walikuwa washirikina wakubwa, Bwana Yesu asifiwe Sana. Soma mwenyewe iyo stori hapo juu. Very interesting.
4. Tuma malaika wa Mungu kuwatubulia mipango Yao juu Yao wanayofanya ya ushirikina
Waebrania 1:14
14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
*anasema je hao si roho? Watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? Bwana Yesu asifiwe mtu yoyote anapookoka malaika wake anakuwa on!Halleluyah! Kuna watu hawajui jinsi ya kuwatumia malaika zao. Unajua niliwaji jiuliza swali moja na Mungu akanipa jibu!
Nilijiuliza Mungu anawezaje
kuwahudumia watu wote hawa kwa wakati mmoja? Dunia mzima, tuko wengi zaidi ya bil 7! Kila mmoja anaomba au nusu ya hao wanamuomba Mungu mahitaji mbalimbali Mungu anawezaje? Kuwahudumia at same time? Anajigawa vip?
Kumbe kila mtu anayeokoka malaika wake anakuwa on! Kila mtu anamalaika Ivyo ni muhimu Sana kuokoka kwa kinywa chako! Kuongozwa sala ya Toba kwa kumkiri Yesu Katika moyo wako na kumpa nafasi.
Naongea ivi sababu kama hujaokoka sikufichi kipengele hiki hakita fanya kazi kwako, kabisa kabisa ninaweka wazi kabisa. Kuna kumtambua Yesu! Na Kuna kumkiri Yesu kwa mdomo wako. Sasa dini nyingi zina
mtambua lakini hawajamkiri Yesu. Kwa iyo malaika ndio hufanya kazi kwa niaba ya Mungu hapa duniani ukiwa on nao watakuwa on.
Mtumishi mmoja wa kimataifa aliwahi muuliza Mungu kuhusu malaika na akaoteshwa akaletewa katika ndoto, vyumba vitatu. Chumba cha kwanza alimuona malaika amelala anakoroma, chumba cha pili alimuona malaika anatoka baada ya masaa matatu ndo anarudi au baada ya masaa sita. Chumba cha tatu alimuona malaika anatoka anaingia kila baada ya sekunde sasa Mungu akamwambia hao malaika wanafanya kazi kutokana na Maombi ya
watu huko duniani?
Sasa jiulize wewe Leo malaika wako atakuwa chumba gani? Mwingine haombi kila siku anakazi ya
kujifunika na damu ya Yesu analala! Anabariki chakula anakupa. Mwingine dk 5 kisha baada ya siku mbili tena, mwingine anangurumisha masaa matatu usiku halali sasa uyu ndo yule wa chuma cha mwisho. Uyu lazima malaika wake awe bize vibaya Sana.
Zaburi 91:11
11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.
*malaika hufanya kwa damu ya Yesu na kwa jina la Yesu pekee! Mwaga damu ya Yesu unakotaka waende, command kwa jina La Yesu, hakikisha unachowaccomand kipo katika mpango wa Mungu. Sio mpango wako, Mungu amekataa uchawi. Ivyo unawatuma malaika kwa damu ya Yesu na jina la Yesu wakavuruge mipango yao.
SOMA HII STORI CHINI NZURI SANA YA BIBLIA KUHUSU MALAIKA.
Hesabu 22-5-6
5 Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi.
6 Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa
9 Mungu akamjia Balaamu, akasema, Ni watu gani hawa ulio nao pamoja nawe?
10 Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, amewatuma kwangu, akisema,
11 Tazama, kuna watu waliotoka Misri, wanaufunika uso wa nchi; basi njoo unilaanie watu hawa; labda nitaweza kupigana nao, na kuwafukuza.
12 Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa.
15 Basi Balaki akatuma wakuu mara ya pili, wengi zaidi, wenye cheo wakubwa kuliko wale wa kwanza.
16 Wakamfikilia Balaamu, wakamwambia, Balaki mwana wa Sipori asema hivi, Nakusihi, neno lo lote lisikuzuie usinijie;
17 maana nitakufanyizia heshima nyingi sana, na neno lo lote utakaloniomba nitalitenda; basi njoo, nakusihi, unilaanie watu hawa.
22 Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa Bwana akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye.
23 Na yule punda akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, na upanga wake mkononi mwake amekwisha kuufuta; punda akageuka upande ili kuiacha njia, akaingia shambani. Balaamu akampiga punda ili kumrejeza njiani.
24 Kisha malaika wa Bwana akasimama mahali penye bonde, katikati ya mashamba ya mizabibu, tena penye kitalu upande huu na kitalu upande huu.
25 Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajisonga ukutani, akamseta Balaamu mguu wake, basi akampiga mara ya pili.
26 Malaika wa Bwana akaendelea mbele akasimama mahali pembamba sana, hapakuwa na nafasi ya kugeukia mkono wa kuume, wala mkono wa kushoto.
27 Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake.
28 Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?
29 Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi.
30 Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La!
31 Ndipo Bwana akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi.
32 Malaika wa Bwana akamwambia, Mbona umempiga punda wako mara tatu hizi? Tazama mimi nimekuja ili kukupinga, kwa sababu njia yako imepotoka mbele zangu,
33 punda akaniona, akageuka upande mbele zangu mara tatu hizi; kama asingejiepusha nami, bila shaka ningalikuua wewe, nikamwacha yeye hai.
34 Balaamu akamwambia malaika wa Bwana, Nimefanya dhambi; maana sikujua ya kuwa wewe umesimama njiani ili kunipinga; basi sasa, ikiwa umechukizwa, nitarudi tena.
*umeona malaika wa Mungu anavyotumwa kuwazuia maadui zako! Sitaielezea nataka uisome? Iyo stori.
5. Agiza malaika wa Mungu wa kukuhudumia.
*Kama. Ni nyumbani, kazini au kwenye biashara yako waagize kwa damu ya Yesu chochote kama unataka wateja, kama unataka kibali Wao wanafanya kazi kwa damu ya Yesu na jina la Yesu.
6. Mshukuru Mungu kwa sadaka na matoleo
*Hapa ndipo Kuna siri kubwa Sana na wengine huwa wanasahau kidogo Mungu hata akikutoa hatua ndogo kama kidole cha mguu wa mwisho lazima umshukuru na utoe sadaka ya shukrani.
Nitakuonyesha kimaandiko huko mbele, kama umeomba kazi mfano ile kuitwa kwenye interview tuu, unatoa shukrani, pia umefanikiwa ukaitwa kazini unatoa shukrani.Baada ya kupokea mshahara unaendelea kutoa shukrani. Umeomba mkopo jina lako limepita. ile jina lako tuu limepita unatoa shukrani, baada ya kupokea Huo mkopo unatoa zaka na shukrani, biashara imeanza na kufanikiwa unaendelea na kutoa shukrani Mimi hii kitu nimejifunza personal, na hata baada ya
kufanikiwa unaendelea unatoa shukrani.
USISUBIRI UFANIKIWE MWISHINI NDO UTOE SHUKRANI, kila hatua Mungu anayokusaidia lazima utoe shukrani, Mimi miaka ya nyuma nilikuwa napitia magumu. Nikawa katika mtandao nikapitia mtandao mmoja wa maishaushindi! Yule Mtumishi Mabula Kuna somo alikuwa ameweka la siku nyingi Bwana akaongea nami Sana kupitia lile somo Ni kama nilipata ufumbuzi jinsi
ya kutoka kwa jinsi nilivyofunguliwa na lile somo nilitoa sadaka ya shukrani. Nilivyomtumia huwezi amini akaniambia huu kwangu Ni muujiza maana nilikuwa napitia sehemu ngumu Sana.
Basi akaniombea na kunibariki kwa jina la Yesu wiki ile ile nilipata bonge la breakthrough! Katika kila hatua Mungu anayokupitisha Toa shukrani,usidharau hatua za Mungu hata kama ni ndogo vip! ndio maana wengi tunapoteza breakthrough hatua za
mwanzo tuu. Mapema asubuhi shuhuda ibilisi anavuruga. Ibilisi anayajua maandiko yeye anayatumia kukushitaki na kukuvuruga. Umepata wazo la biashara iyo ni hatua. Mshukuru Mungu.
Unapomshukuru Mungu unaijengea msingi! Mimi Nina kanuni mahali ninapolishwa ndipo natoa shukrani! Naangalia source ya jibu langu ni wapi ndipo ninapotoa. Sasa na wewe angalia roho Mtakatifu anaongea na wewe vipi. Ila muhimu Sana Katika kila hatua unayopiga Toa shukrani. Shukrani si lazima iwe kubwa kama unavyofikiri Bali kama inadhamani kwako basi inadhamani mbele ya Mungu.
Zaburi 50-14-15
14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.
15 Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.
Zaburi 50:23
23 Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
Zaburi 56:12-13
*Toa shukrani baada ya Maombi haya! Manake ni tendo la imani la kuvuka. JINA LA BWANA LIBARIKIWE!
kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066

12 Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru.
13 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili nienende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.*Toa shukrani baada ya Maombi haya! Manake ni tendo la imani la kuvuka. JINA LA BWANA LIBARIKIWE!
kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment