SI UWEZO WAKO WA KUOMBA UNAKUFANIKISHA BALI NI NEEMA!
Tuangalie neno la kusimamia kuusu Neema.tulitafakari
Bwana Yesu asifiwe Sana.
Pamoja na biblia kukupa haki ya kudai! Kumkumbusha Mungu. Kukanyaga nyoka na nge! Na
maagano ya Ibrahimu Isaka na Yakobo. Maagano ya Msalaba Yesu aliyoyafanya pale kalvari na Mungu
kwa ajili ya sisi tunaokolewa, na tuliokolewa. Usije kusahau kila kitu kinapatikana kwa Neema. Na
Mungu ameweka ivyo ili usije ingia kiburi. Kuwa ninaomba nikapata. Jua ni Neema! Mungu atabaki kuwa
Mungu aidha umemsusa kwa sababu hajajibu haja ya moyo wako yeye atabaki kuwa Mungu. Aidha
amechelewa kukujibu yeye atabaki kuwa Mungu tuu. Wewe ukikataa kumwabudu, kumsifu, kumtumikia atafungua hata vinywa vya
wanyama wataongea, atafungua vinywa vya mawe vitasema. Halleluyah. Nilitaka kukukumbusha kila kitu kinapatikana kwa Neema.
Ivyo tunapoenda kuanza wiki hiii usisahau kuomba Neema ya Mungu Katika shida yaako. Kuomba Neema
haimaanishi Mungu kashindwa no! Manake ni kwamba unamuambia wewe Ni Mungu Mimi Ni binadamu.
Unamwambia Mungu wewe utabaki kuwa Mungu aidha umenipa au hujanipa. Bado wewe Ni Mungu.
Na ndivyo itakavyokuwa Na haitabadilika. Bwana Yesu asifiwe. Mungu anapenda kutambulika. Bwana Yesu asifiwe Sana!
WAEFESO 4
7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.
8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.
9 Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?
10 Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote.
Neno linajielezea Na kueleweka haliitaji stori nyingi Sana ili uelewe, Bwana Yesu asifiwe Sana! Kikubwa
nataka tukumbushane kitu chochote ambacho unacho wengine hawana(kwa utukufu wa Mungu) iyo ni Neema.
Kitendo cha wewe kujua umetenda dhambi na huwezi kulala mpaka utubu iyo ni Neema. Kitendo cha kujua hapa Kuna vita napigwa vya
kiroho iyo Neema. Kuomba maombi! Katika roho na kweli iyo ni Neema. Kulitafakari neno la Mungu kulielewa, kuwa na kiu nalo iyo Neema.
Kutamani kutembea Katika utakatifu kuwa shahidi wa Yesu bila aibu au kificho iyo ni Neema. Neema
ya mtu manake ni upendeleo maalumu wa Kimungu wa kupata jambo flani. Katika maombi haya
mtambue Mungu ndio mwenye Neema. Na yeye ndio mgawaji wa Neema. Na jinsi ulivyo Ni Neema
zake wala si kitu kingine. Kwanini uu mwanaume au mwanamke ni neema ya Mungu. Kila Neema Ina kusudi la Mungu.
Unauliza kivip? Angalia kusudi la Yesu kushuka chini duniani na kupaa juu kuliko vitu vyote manake katika ulimwengu wa roho alikuwa
anaachilia Neema za kila kitu. Angalia mstari wa 10, ili avijaze vitu vyote kwa kutambua Yesu alikuwa anajaza Neema kuliko vitu vyote chini ya dunia.
Sasa Nenda magotini pake kwa Maombi ya dua(kumsihi Mungu) Neema yake ile aliyoiachilia alipokuwa anapaa kwa kupitia roho mtakatifu na kwa damu ya Yesu.
Ifunike iyo shida yako sasa. Wewe omba Neema tuu.usiombe kingine. Usi mwelekeze Mungu jinsi ya kufanya. Au jinsi ulivyoshindwa au jinsi ulivyoumia, usilalamike Bali omba.
Wengi wanamlalamikia Mungu badala ya kuomba kwa jina la Yesu. Omba Neema iyo kwa damu ya Yesu. Neema inameet qualification zote hata kama huna qualification
Neema ya Yesu itakufunika. Alimradi unaomba katika mapenzi
ya Mungu. And it's not for personal issue kama kuonyesha kwa watu kuringishia waru kulipisha kisasi. Halleluyah!
Haya ni Maombi ya kuatamia pia ivyo usiondoke mpaka umetotoa vifaranga. Jina la Bwana libarikiwe. Tumia damu ya Yesu kuomba iyo
Neema. Chochote na iyo damu ya Yesu ya Neema ni funguo ya kila mahali. Itafungua kwa kadri ya jinsi ulivyolielewa neno hili na kuliamini. Sifa na utukufu kwake Yesu.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment