MADHARA YA KUTUMIA BARAKA ZA MUNGU KWA BAALI

Somo: "Madhara ya kutumia Baraka za Mungu kwa Baali"

HOSEA 2

1 Waambieni ndugu zenu wanaume, Ami na ndugu zenu wanawake , Ruhama.

2  Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na ayawekee mbali mambo ya uasherati wake yasiwe mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi wake yasiwe kati ya maziwa yake;

3  nisije nikamvua nguo zake akawa uchi, nikamweka katika hali aliyokuwa nayo siku ya kuzaliwa kwake, na kumfanya kama jangwa, na kumweka kama nchi kame, na kumfisha kwa kiu;

4  naam, sitawaonea rehema watoto wake; kwa maana ni watoto wa uzinzi.

5  Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, Nitafuatana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu na vileo vyangu.

6  Basi kwa ajili ya hayo, angalia, nitaiziba njia yako kwa miiba, nami nitafanya kitalu juu yake, asipate kuyaona mapito yake.

7  Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa.

8  Maana hakujua ya kuwa mimi ndiye aliyempa ngano, na divai, na mafuta, na kumwongezea fedha na dhahabu, walivyovitumia kwa ajili ya Baali.

 9  Basi kwa ajili ya hayo, nitaitwaa tena ngano yangu kwa wakati wake, na divai yangu kwa wakati wake, nami nitamnyang'anya sufu yangu na kitani yangu, vya kumfunika uchi wake.

 10  Na sasa nitaifunua aibu yake mbele ya macho ya wapenzi wake, wala hapana mtu atakayemwokoa katika mkono wangu.

 11  Tena nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na makusanyiko yake yote yaliyoamriwa.

 12  Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, Hii ndiyo ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa msitu, na wanyama wa mashamba wataila.

 13  Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake

*Kuna baathi ya mambo yanatukuta sababu ya kumtumika Baali. Baali kwa wasomaji wa Biblia Ni mungu anayekaa kwenye maji. Yeye anapenda kujifananisha Na Mungu aliyehai.

 anapenda kuchukua nafasi ya Mungu. mungu baali uyu ndo anayewasukuma watu wanatumikia miungu miwili. Yeye ndo anayefanya au kukusukuma kukushawishi Unachanganya mambo! Ndio anayefanya Baraka ya Mungu unaitumia katika njia zisizo!

Ile hali ya Kuchanganya mambo huku uko na huku unatamani Ni hali inayoletwa na mungu baali, isipokuwa controlled na Roho mtakatifu. Inakupelekea Mungu kukunyanganya kile alichokupa.

Mpaka utambue yeye hataki kuchanganywa. Wivu, tamaa ya mwili, hasira, kiburi, kujikweza, unafiki, uongo, husuda, kijicho, usijichanganye kwa wenye mizaha,

 ni baathi ya mambo ya mungu baali anayoyafanya! Hapo juu uzinzi na uasherati imetajwa kama dhambi ambazo sisi binadamu tunamchanganya Mungu aliyehai Na mambo ya dunia hii. Ile hali ya

kuchukua cha Mungu na kukitumia kwa shetani.mfano Kuchukua mshahara kazi uliyopewa na Mungu kutumia ndivyo sivyo kwa ibilisi, kutafuta ushauri kutegemea watu badala ya Mungu aliyehai.

 Ile hali ya kuwa upande wa Mungu na kupenda na kutamani ya shetani.kumpenda Mungu na kutamani ya shetani. Iyo ndo kazi ya mungu baali! Anakusukuma utumie cha

Mungu kwa ibilisi. Au uchanganye cha Mungu na shetani. Roho yako inakuwa huku kwa Mungu huku kwa shetani. Huku unapenda na huku unatamani. Bwana Yesu asifiwe!

Ndio anasema Mstari wa pili msihini mama yenu anarudia tena msihini kwa maana yeye Si mke wangu, wala Mimi sio Mme wake. Kwa maana nyingine Mungu anakuambia

Mimi sio Babu yako. Mimi ni Mungu. Anasema hatakuwa na rehema kwa uyo mzinzi na muasherati wala watoto wake.

Watoto wake ni maanake ni  matokeo ya iyo dhambi aliyoitengeneza. Unaona anaelezea sasa madhara ya hao watoto yani izo dhambi yani uyo muasherati na mzinzi uyo kuwa hutaacha

utaendelea kufuata waume zake, na wapenzi wake (miungu baali)biblia inasema maana akasema (muasherati) ndio wanaompa chakula, maji, na divai.

 Hii Ni ile Hali ya wewe mpendwa kutafuta amani kwa njia ya ibilisi, Baraka ya Mungu lakini unatafuta kicheko amani furaha kwa njia ya ibilisi. Unajichanganya na kusahau wewe ni wa Mungu. Angalia

mwenyewe mstari wa 5. Mstari wa 8 Mungu analalamika anasema Mimi nikupaye ngano, divai. Mafuta na fedha na dhahabu alafu wewe unaenda kuvitumia kwa mungu baali.

Ndo baada hapo sasa mstari wa 9 Mungu anaongea sasa kila ambacho atakifanya anasema nitafunua aibu yake, nitamnyanganya sufu na kitani changu. Anasema nitaikomesha furaha yake, nitaharibu mzabibu

wake, nitawafanya wanyama kula mazao yake. Bwana Yesu asifiwe Kuna baadhi ya mambo hutokea sababu ya sisi wenyewe. Kuchanganya mambo. Huku upo huku unatamani angalia Mungu alikuwa anaongea na Hosea.

 Juu ya kila atakachokifanya. Hii message inatukumbusha kutunza utakatifu wetu. Usimchanganye Mungu na matendo, mawazo au maneno yako. Usiwe vuguvugu. Kwa upande mmoja. Usiwe mguu mmoja huku na mwingine kule. Kuna madhara makubwa.

 Unaweza msingizia shetani lakini kumbe wewe ndio uliofungua mlango. Neno linakuja mchana huu kukumbusha tuu. Pengine ndio kizuizi cha hatma yako.ushindi wako, Roho mtakatifu atusaidie jina la Bwana libarikiwe Sana.

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA