SWALI LA KIBIBLIA: KWANINI MUNGU ALIAMUA KUMWAMBIA IBRAHIM AMTOE MWANAWE SADAKA ISAKA? JE ILIKUWA NINI TAFSIRI YAKE?


Bwana Yesu asifiwe sana!

 Mwanzo 22-1-2
 1 Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
2  Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.

 1.Isaka alikuwa sadaka ya Mbegu. Kupitia Isaka alibarikiwa Ibrahimu, alibarikiwa Isaka, alibarikiwa watoto wa Isaka, lilibarikiwa taifa la Israeli, lilibarikiwa mataifa yote na vizazi vyote vya Ibrahimu. Isaka alikuwa sadaka ya Mbegu. Mungu akitaka kukuchipua atakupa au kukuonyesha Mbegu. Isaya 43:19

2. Mungu alitaka kuutoa moyo ya Ibrahimu katika sadaka ya mbegu, yani Isaka. Biblia inasema Ibrahim alimpenda Sana Isaka. Mungu alipogundua ilo akaamua kumuua Isaka katika ulimwengu wa roho katika moyo wa Ibrahimu ili mahusiano yake yasije kuwa ruled na Isaka. Kwani mbegu ikipandwa katika ardhi Si lazima ife ndipo ifufuke?

Kitendo kile cha Isaka Kuchinjwa kwa mfano wa kondoo katika ulimwengu wa roho Ile nafasi ya Mungu Katika moyo wa Ibrahim ambayo ilianza kuchukuliwa na Isaka, iliuwawa na kurudishwa kwa Mungu. Ni kawaida kabisa ukisubiri kitu kwa mda mrefu Sana kwa Mungu utakapo kipata kinaweza chukua mpaka nafasi ya Mungu. Maana kama umekipata unapataje msukumo tena! Wa kumtafuta Mungu. Kama ni kazi

 umepata msukumo wa kumtafuta Mungu labla utoke sehemu ingine Si wa kazi tena. Bwana Yesu asifiwe.kama umepata kazi mtu akikuambia ufunge kwa ajili ya kuomba kupata kazi utamwelewa? Ndio maana ukifanikiwa jambo moja Mungu ataruusu jaribu la pili ili uendelee kumtafuta ili isije iyo kazi ikachukua nafasi ya Mungu.Hii unahitaji Neema kuyaona aya nayoyaandika, ama sivyo utabakia kumlaumu Mungu. Maana yake Asije mme akachukua nafasi ya Mungu asije mke akachukua nafasi ya Mungu. Lisije ilo gari likachukua nafasi ya Mungu. Isije huo mshahara au iko cheo

 kikachukua nafasi ya Mungu. Hii inajibu lile swali mbona majaribu hayaishi Mungu? Hili likiisha hili linakuja why? Kama unataka nyumba au ndoa au biashara kubwa nzuri ukivipata hivyo vitu bila jaribu la pili hutakuwa na msukumo wa Mungu ndivyo. Ilivyo. Ndivyo binadamu alivyo. Bwana Yesu asifiwe. Nikutakie mafanikio mema, mpe Mungu nafasi ya kwanza.

*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu


josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA