TEKETEZA ROHO ZINAZOPOFUSHA NENO LA MUNGU

Tuangalie neno kwa kifupi

 Somo: "Teketeza roho zinazopofusha neno la Mungu"

 Matendo 13-6.....

 Mpendwa neno la Mungu limehakikishwa Mara saba, ni taa pale kwenye Giza, ni upanga ukatao kuwili, kazi yake kukata kufyeka ya ibilisi. Ndani ya neno Kuna nguvu kubwa Sana ya kujenga, kubomoa, kila kitu hapa duniani kilitokana na neno la Mungu, neno ni silaa, neno Lina nguvu kuliko kitu chochote hasa neno 

litakalo na Mungu. Neno la Mungu katika biblia linachunguza moyo wako, linahuisha, linatafsiri, linaongea Yale ya Mungu kwako, linaleta maono, neno la Mungu Lina maelekezo ya Mungu. Kila kitu kimefichwa kwenye neno, kila shida na taabu hapa duniani jibu lake limefichwa katika neno, ndio maana ibilisi hufanya

 mbinu zote ili kupofusha akili za watu, kupigana nao wasije wakasoma biblia hata wakisoma wasielewe, wakielewa wasiamini, neno linapisomwa linapokaa moyoni humzuia ibilisi kufanya kazi, 

katika maisha yako, roho mtakatifu hawezi ongea mambo ya kimungu au mafumbo ya Kimungu katika maisha yako maana huwezi lielewa ni mpaka uwe na neno katika moyo wako. Mungu watu wengi haongei nao jumbe nzito direct

 na Wao maana hawana neno la kutosha, vifua vyao ni vidogo, bado hawako tayari, mtu wa ndani kusudi afanye kazi kiwango kinachotakiwa lazima umlishe neno, umpe chakula cha kutosha, muhimu kupata mda binafsi wa kusoma biblia, watu wengi Sana huwa wanalalamika wamechoka kiroho, wamechoka majaribu, 

maombi yamekauka, lakini ukichunguza neno aliloweka katika moyo wake ndilo lililotumika kumpigania. Lakini ukiwa na neno la kutosha hutasinyaa, wala kuchoka kiroho, mambo ya hapa duniani hayatakuchosha moyo wako, neno 

linapojaa kwa wingi vitu vya nje au vya duniani haviwi tena ishu, tena neno linaondoa hofu, wasiwasi mashaka, linaleta amani na furaha ya kweli. Lakini ipo vita katika kufikia uhuru wa kusoma neno, 

ivyo nilitaka kukuonyesha hata biblia imezungumza kwa habari ya uchawi wa kuzuia wewe usilipende neno, usiliamini neno, ndo mana ni muhimu kujikabithi kabla ya kusoma biblia yako, kabla ya kuanza ibada au seminar mwambie Mungu nataka nitoke na kitu changu. Kukemea roho za kupofusha akili, roho za kuzuia 

wewe kuamini. Maana utakapolisikia neno na kuliamini na kuliweka katika matendo hata wakati wa majaribu hakika utaokolewa, biblia inasema walitialo jina la Bwana wataokoka.

  6  Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; 

7  mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 

8  Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. 

 9  Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 

 10  akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? 

 11  Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. 

 12  Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.

  Ibilisi akitaka akucheleweshe katika miujiza yako, atapigana na wewe katika neno katika kusoma neno, ni vizuri kwenda katika maombi kufunguliwa for delivarence, au maombi ya ukombozi. Ni vizuri kutumia mafuta yaliyoombewa, ni 

vizuri kutumia maji yenye upako yaliyoombewa, ni vizuri kuwekewa mikono lakini amini usiamini kupokea kwako kunategemea kiwango cha neno na imani iliyojengenga ndani yako, bila neno hutaweza pita kwenye maandalizi ya wewe kupokea ya Mungu, bila neno utaanguka katika dhambi kila 

Mara, bila neno utazunguka makanisa yoote kwenda kuombewa lakini amini usiamini bila neno hata iko unachopokea kitadumu kwa Mda tuu. Maana ni jukumu lako kukitunza kwa imani, Si akili zako za duniani. 

Halleluyah! BWANA Yesu asifiwe, matatizo yote unayaona katika akili ya ufahamu wako, ni uongo ulijengwa na ibilisi, ivyo bila neno hakuna lolote utakalofanikiwa. Hatuna ujanja. Tenga mda wako wa kusoma neno, 

jijengee imani yako, Si kila Mara imani ya mtumishi itakusaidia wewe, Tenga mda wako kwa ajili ya kusoma biblia. Hii injili ya pokea! Pokea! Ni nzuri lakini pasipo neno la imani ni kujifirahisha tuu nafsi yako. Halleluyah! Jiongeze! 

Ufahamu wako, sikiza watumishi mbalimbali, kupata vyakula tofauti tofauti, ongeza kiwango, komaa kiroho. Kitu chochote mtu anacholalamika analalamika ni sababu neno halijakaa vizuri ndani kwake.

 Tokea Leo hii jua ya kwamba Kama huwezi soma biblia inasoma vipande vipande vya mstari basi unapambana na nguvu za Giza za kupofusha akili za watu, Kama hulielewi neno jua ni ibilisi, Kama huna mda wa kusoma neno jua ni ibilisi, Kama hamu ya kusoma inakatika 

au huna kabisa jua ni ibilisi, wakati wewe ukivunja na kuangamiza kwa jina la Yesu, ni kweli inatendeka lakini yeye atakubania kwenye neno ili matokeo yako yawe madogomadogo tuu, atakuzuia kiwango chako cha neno, atapigana na wewe kipengele 

cha neno, maana ukifunguka hapo wewe ni mshindi. Usikubali kupigwa eneo la neno, ni sehemu ambayo unatakiwa umwombe Mungu kila siku kipengele 

cha neno, mpaka pale utakapokuwa huru kabisa. Kusoma neno kwa kulipenda. Kulimiss unapokosa biblia uone kiu. Silaha ya kwanza kabisa ni neno kukaa kwa wingi

 ndani yako. Si kweli huna mda, iyo pia ni vita ya ibilisi, utalia na Baraka kwa Mda mrefu baada ya mda inatoweka, kwani hujawahi ona au expirience? Kama ni ela inakatika, ukichunguza shetani alianza 

vita ndani ya moyo wako, sababu kulikuwa wazi ndo mana kakushinda. Message hizi ni ngumu na Si kila mtu hufuraia, lakini lazima tuseme ili mtu wa ndani apone. Jina lake Mungu libarikiwe



JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu


josephntandu@gmail.com,0713297066
.




Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA