"TOFAUTI KATI YA IMANI YA UHAKIKA NA KIBURI CHA UHAKIKA"
Somo: "Tofauti Kati ya imani ya uhakika na kiburi cha uhakika"
Yakobo 4:3
3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
Bwana Yesu asifiwe!
Waebrania 11:1
1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Kuna tofuti Kati ya imani ya uhakika na kiburi cha uhakika. Imani yako inatakiwa iwe Na uhakika lakini siyo kiburi. Kiburi cha uhakika hukufanya uombe vibaya. Kiburi cha uhakika hutokea baada ya kuwa na hakika wa Mungu atafanya tuu.
Kusahau kuwa Mungu kila kitu kwako ni Neema. Kiburi cha hakika kinakufanya kujihesabia haki, kinakufanya kuomba kwa akili yako, kinakufanya kuomba kwa mazoea, kinakufanya uombe kwa akili zako. Kinakufanya usimtegemee tena Roho mtakatifu. Nikupe mfano! Mungu
aliongea Na wewe kwa habari ya sadaka ya ujenzi wa kanisa mfano ukatoa kwa kanuni za Ki Mungu, Mungu akakuinua. Kuinuliwa kwako kubakie na hakika Mungu yupo, hakika Mungu anatenda, lakini kusibakie ni lazima Mungu atatenda kwa njia iyoiyo. Baraka yoyote inakuja na maelekezo, na maelekezo hayafanani! Saa ingine sababu
ya kiburi cha uhakika unakuta unaomba against Mungu. Saa ingine ni Mungu mwenyewe anakuzuia usiende kwenye shimo sababu ya kuwa na kiburi cha hakika wewe unaanza kuvunja, kuchinja kumbe unaomba against Mungu. Na Mungu anakushangaa. Mfano uliomba kupambana na wachawi na Mungu
akakusaidia wachawi wakaanguka wakafa mtaani kwenu. Iyo isikupe kiburi cha wewe kusikia rumous mtu flani Ni mchawi na ukaingia kwenye maombi ya kuomba afe! Hapana, iyo Ni kiburi cha hakika. Kiburi cha hakika kuwa Mungu lazima atafanya bila kumtegemea roho mtakatifu kinakufanya kutosikiza maelekezo ya Mungu. Kila jambo
linamaelekezo yake, maombi yake, na mlango wake wa kutokea. Kama ulifunga Mungu akafungua njia iyo hakika iongeze imani kwa Mungu wako lakini usigeuke kiburi. Leo nitakupa siri kwanini watu wengi baada ya dalili za Baraka tuu gafla Baraka zinapotea? Ni sababu ile hakika inageuka kiburi. Kuwa lazima Mungu
atafanya kwa iyo inakutoa katika kumsikia Mungu. Inakutoa katika unyenyekevu. Ni kama vile mtu anasema moyoni afadhali nimelitua hili nipumzike sasa kumuomba Mungu. Huku anasahau kwamba kila hatua inahitaji Mungu. Kila hatua unayopiga mbele shetani hatua inayofuata atajaribu kukuzuia. Ivyo
mwanzo wa Baraka kukujengee imani ya uhakika siyo kiburi cha uhakika. Nimesema kiburi cha uhakika ni ile hali ya kujua kwa vyovyote Mungu atafanya ambayo iyo hali inakuletea kutokuwa mtii, msikivu, kujihesabia haki, kutokuwa mnyenyekevu, kuomba kwa akili zako badala ya kumtegemea roho mtakatifu sababu ya hakika.
Na wengine wanadumaa kwenye shuhuda moja hawaendelei mbele sababu ya kiburi cha hakika. Kinachowatolea unyenyekevu mbele za Mungu. Kinacholeta mazoea na Mungu. Kinaondoa ile hofu ya unyenyekevu. Kiburi cha hakika Ni mlango wa siri wa ibilisi na umebomoa vibali vya watu wengi Sana. Kumbuka shetani anachotafuta ni mashitaka juu yako ili akurudishe nyuma. Kiburi hiki kinaweza kuja kwa njia ya mawazo, matendo.
Maneno. Usipokipinga na kukikemea kinakuwa mlango wa ibilisi.Baada ya hatua ya kwanza tuu unakuta Mtu anajisahau kabisa anatumbukia kwenye mtego wa ibilisi. Wapendwa tunapaswa kuwa wanyenyekevu MDA WOTE. imani yenye uhakika ni kitu kizuri Sana, lakini muhimu Sana kuilinda imani yako isigeuke kiburi. Maanake nini ni muhimu kumtegemea Roho katika kila kitu katika maisha yako, kumuhusisha roho mtakatifu katika kila jambo. Hata jambo dogo vip.
Muhimu pia kujikabithi kwa Roho pale tuu unapoona hatua za kibali au Baraka zinaanza ukabithi iyo Baraka/kibali ili ibilisi akakupandia kiburi bila wewe kujijua. Watu wanaacha kuomba baada ya dalili za kubarikiwa, wanaacha huduma kwa dalili tuu, kama alikuwa mhudumu atapunguza, wanaacha kutoa sadaka kwa dalili za Kibali au Baraka, wanaacha kufunga kuendelea kuomba kwa dalili tuu, wanaacha kuamka usiku kuomba, wanaacha ibada walizokuwa
wanaenda kila siku, sababu tuu kapata kiburi cha hakika manake Mungu atajibu tuu. Nikifanya moja mbili lazima atajibu. Na kusahau unyenyekevu. Mungu ni wa kunyenyekewa mda wote, Si sababu ya dalili ya Baraka tuu, au kibali. Mungu ni wa kumuendea kwa adabu zote mda wote. Tena basi Muhimu kumuomba Roho akusaidie kuomba ili usije kuwa unaomba kwa kiburi cha hakika badala ya imani ya
hakika. Nachotaka kusema ukipiga hatua moja kama mfano wa ukucha wa kidole cha mwisho iwe sababu ya kunyenyekea zaidi, kumsikiza Mungu zaidi, kuomba zaidi na zaidi aendelee kukupigania, isikupe kiburi ukabadilika, iwe sababu ya kusoma neno zaidi. Isikujengee kiburi cha hakika ukabadilika. Kufumba na kufumbua kibali chako hakipo tena. Nataka uanze
kufikiria vitu vingap vilianza kuonyesha nyota nzuri na gafla vikafa? Chunguza hayo hapo juu? Kama roho wa Mungu atakukumbusha na kukuonyesha hapo ndipo pa kuanzia kazi. Mungu kukujibu kila Mara, kukupa kibali kukutengenezee unyenyekevu sio kiburi.
*Nataka nikuonyeshe kwenye Biblia jinsi kiburi cha hakika kinavyoweza kumpotezea mtu kibali chake.
HESABU 20
7 Bwana akasema na Musa, akinena,
8 Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao.
9 Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za Bwana kama alivyomwamuru.
10 Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?
11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia.
12 Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa
*Stori hii ukisoma sura yote wana wa Israeli waliona kiu, Musa ndio kiongozi Wao anaenda kwa BWANA kujiuliza Mungu nifanyaje. BWANA akamwambia Musa uambie Mwamba utoe maji, lakini Musa sababu alishajijengea kiburi cha hakika yeye anafanya kama Mara ya
kwanza. Mara ya kwanza aliupiga mwamba nao ukatoa maji, Mara ya pili kaambiwa UAMBIE MWAMBA utoe maji yeye Musa kaupiga tena Mara mbili. inawezekana kabisa Mungu hakutaka kumuaibisha Musa mbele ya wana wa Israeli. Na ndivyo wengi hatusikii maelekezo yanayofuata sababu ya kiburi cha hakika, Unafikiri kwanini alikiuka maagizo ya Mungu? Ni sababu ya kule juu niliyokuwa naelezea Musa alijua kwa vyovyote Mungu angetoa maji tuu mwenye mwamba. Angalia jinsi anavyowaita wana wa Israeli "WAASI" soma sura yote sijaweka hapo juu. Anawambia nyie waasi, je hiki siyo kiburi? Lakini angalia gharama yake hakufika kaanani Musa alifia njiani.
Ivyo ndivyo ilivyo kwangu Mimi na wewe kama tukiwa na kiburi cha hakika. Kuna gharama tutakula! Vibali vitakufa, kama Musa alivyofia njiani! na Baraka zinakufa njiani hazifiki kaanani manake hazifiki mwisho. Bwana Yesu asifiwe. Hujachelewa Sana. Hapo hapo neno hili lilipokufungua Nenda magotini omba Rehema. Mwambie Baba nisamehe maana Maombi yangu na Mimi
mwenyewe kumbe bila kujua ninaongozwa na kiburi cha hakika na sio imani ya hakika. Ivyo naomba Rehema naomba nafasi ingine kwa damu ya Yesu. Na Mungu ni mwaminifu atakuokota tena mavumbini Mungu hachoki hachoki. Hata ukianguka Mara saba atakuokota Mara saba. Endelea kunyenyekea. Jina la Bwana libarikiwe!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments
Post a Comment