UKUTA UNAOZUIA BARAKA
Somo: "Ukuta unaozuia Baraka"
Bwana Yesu
asifiwe Sana!
Yohana
8-31-32
31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi
waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli
kweli;
32 tena
mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Ninyi
MKIKAA ndani YANGU na maneno yangu YAKIKAA ndani YENU. mmekuwa WANAFUNZI wangu KWELI
KWELI mmekuwa wanafunzi. Tena MTAIFAHAMU KWELI, nayo hiyo KWELI itawaweka HURU
Leo
tunazungumzia ukuta wa Baraka, Kuna njia ya Baraka na ukuta wa Baraka, wengi
hatumalizii homework, njia ya Baraka tunaijua na tunaifuata, kupanda mbegu
tunapanda, tunakesha tukiomba, tunafunga, tunatoa sadaka kwa yatima,
tunasupport kazi ya Mungu, matendo mema kwa wengine, tunafanya huduma ya Mungu.
Well done! Na mambo yoote kabisa. Izo ni njia za Baraka, tunatoa fungu la kumi
(10) kuongezeka. Tunatoa malimbuko kupata ulinzi Bwana Yesu asifiwe Sana.
Tunakumbushana tuu! Biblia ni kukumbushana alafu roho mtakatifu katika
kukumbusha anasema kitu kingine, njia ingine anaongeza kitu kwenye ufahamu
wako. Bwana Yesu asifiwe Sana.
Kwanini
Baraka zinachelewa? Au zinakawia?
Kutoka
13:17-18
17 Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu
hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa
ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo
watakapokutana na vita, na kurudi Misri;
18
lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya
Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha.
*Baada ya
Mungu kukubariki kwa kawaida ndiyo mwanzo ya vita mpya! Just imagine mtu kasota
kwenye magoti miaka minne (4) baada tuu ya kupata kazi miezi 6 mtu uyouyo,
unasikia anataka kuacha kazi?unasikia hii kazi basi! Bora nitafute kitu
kingine, Unajiuliza why? Mtu kasota anatafuta angalau aolewe au aowe! Baada ya
mwaka mmoja tuu anataka kutengana unajiuliza amekuwa akimuomba Mungu miaka 5,
Mungu kufanya vile anavyotaka hataki tena why?
Mtu naomba
biashara (mtaji) kwa Muda mrefu Sana baada tuu ya kupata iyo biashara unasikia
hii biashara naifunga! Unajiuliza why? Mwingine analia na watoto Hana mtoto.
Baada ya kupata tuu mtoto akishaanza kukua Tuu anamlaani yule mtoto. Afadhali
Mungu nisingekuwa na uyu mtoto, maana amegeuka mwiba,ananitesa, ananipandisha
Bp, ananiletea uchungu kwenye moyo. unajiuliza why anatamka maneno kama haya
kwa tatizo la kawaida kabisa? Dogo kabisa? Kwani watu baada ya Baraka tuu,
wanakimbilia ku quit, hawataki tena why? Ndipo hapo ilo neno linakuja
"wasije wakaghairi hawa watu watakapokutana na vita" kutoka 17.Mungu
hukuzungusha njia ya kufika ili kukuandaa! Anajua moyo wako mdogo, imani yako
ndogo, anajua hujakomaa kiroho kitu kidogo
unataka kumuacha Mungu.
Mungu
anajua bado unakunywa maziwa hujaanza kula vyakula vya watu wazima katika
wokovu. Mungu anajua nafsi yako ikiinamishwa na wachawi huwa unakata tamaa,
unatamani kufa, huwa huwezi Ata kuomba. Mungu anajua moyo wako mdogo hauwezi
kuhimili vita maana utakimbia.Mungu anakujua madhaifu yako. Anakujua wewe Ni
mwoga si jasiri,anajua wewe Una aibu, aibu ni ukuta wa kufanikiwa, huwezi hata
kuongea mbele za watu,anajua wewe ni mwoga, wewe huwezi kusema ukweli mbele
unapotakiwa. Huwezi kutete haki maana Una huruma Sana. Mungu anakujua.Mungu
anakujua wewe ni mtu wa kupanic ovyo. Na ukishapanic huna control tena ya akili
yako. Mungu anakujua kabisa.
anajua wewe
huwezi simamia watu katika kazi,maana huwezi kutoa Order unawaogopa watu,macho
ya watu wewe unaogopa, ajua wewe huwa
unasusa ovyo, unazira ovyo, anajua wewe unachowaza ni kukimbia tatizo na sio
kudeal na tatizo, anajua wewe huwezi kucontrol hasira, huna uvumilivu, Si
msiri,mwingine Ni mwoga hata wa kuendesha gari tuu hajiamini alafu unatajka
Mungu akupe hotel inayoingiza mil 10, kwa mwezi utaicontrol vip sasa? ivyo anakurekebisha hatua kwa hatua ili
ufikie kiwango kinachokibalika ili ufanye vita. Yes hapa duniani Ni vita mda wote.
Mungu hakuandai ili ukalale ustarehe anakuandaa ili ufanye vita.
Ushinde
wachawi, wanga, wapiga ramli, wasoma nyota, wachukua nyota, ushinde falme za
Giza, ushinde wakuu wa Giza, ushinde mizimu ya ukoo inayokufuatilia Bwana Yesu
asifiwe. Bwana anakutaka uwe chombo cha kupuria, uwe upanga wa kukatia,
usitishwe usifadhaike. Uwe jasiri kuharibu kazi za ibilisi maana ndicho
alichosema katika Yeremia 1:10. Akikupa unachotaka na bado hujavuka katika
mifano huko juu utaharibu tuu. Misukosuko kidogo ikija utakimbia! Ndoa
utaharibu! Mke utamkimbia! Mme utamkimbia! Kazi utaacha! Biashara utafunga!
Huduma utaaicha! MUNGU anajua kila kitu bana. Ivyo unapochelewa wewe mshukuru
Mungu tena mwombe Mungu akupe ukaribu na yeye! Yani jinsi ambacho hupati
unachokiomba uwe sababu ya wewe kumsogelea Mungu umbali wa zero distance! Sio
kukaa mbali Na Mungu au kuchukua shortcut unapofanya hivyo ndio unazidi
kujichelewesha Bwana Yesu asifiwe!
Hakuna njia nyingine shetani nia yake Ni kukuingiza kwenye shimo Hana
urafiki na wewe! Wewe utaona ni fahari ya mda ila mwisho wa siku lazima
akutumbukize kwenye shimo alafu atakucheka.
Nini ni
ukuta wa Baraka?
Mwanzo 4-
2-12
6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una
ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali?
Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe,
walakini yapasa uishinde.
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende
uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.
9 Bwana
akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi
wa ndugu yangu?
10
Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka
katika ardhi.
11 Basi
sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya
ndugu yako kwa mkono wako;
12
utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na
kikao duniani.
*WIVU
Watu wengi
wanajidanganya Sana na matendo mema ya nje! Mungu huangalia nia ya moyo, Mungu
huijua Ni ya moyo! Ukuta mkubwa mmoja wapo ni roho wa wivu, kumuonea wivu
mwenzako Ni laana ya kutokufanikiwa, soma hapo juu Kaini alilaaniwa, kijicho
pia kinakuleta laana ya kutokufanikiwa, mwingine anamwonea wivu mpaka Mchungaji
wake anavyovaa, au mama Mchungaji anavyovaa, mtu akipendeza anamuonea
wivu-kijicho anakasirika kama kaini soma hapo juu. Ukitaka kujua Kaini
alikasirika Na kughadhibika angalia anavyomjibu Mungu alipoulizwa ndugu yako
yupo wapi? Anamwambia Mungu Mimi ni mlinzi wa Habili? Je kweli unaweza mjibu
Mungu kama binadamu kama siyo aliongozwa na hasira?
Watu wengi wanamuonea Mungu wivu kwanini
umembariki yule kwanini sio Mimi? Kwanini umempa biashara yule? Kwanini Mungu
yule umempa gari? Kwanini umemfanya mkurugenzi, kwanini kampuni inamuamini
anacontrol fedha zote, Je Mungu Mimi Na yeye kunatofauti gani? Watu wengi
wanamuonea Mungu wivu na kumkasirikia kwa nini kabariki wengine na sio Wao?
Kwanini uyu anamaisha mazuri na Sio Wao! Sasa hii ni mtego na wengi wanaona Ni
kitu cha kawaida soma pale mstari wa 7 " usipotenda vyema dhambi iko
inakuotea malangoni kwako nayo inakutamani wewe, yakupasa uishinde" Bwana
Yesu asifiwe unapotenda wivu dhambi ii malangoni pako, inakutamani wewe, umeona
laana inapotoka wapendwa. Juhudi zako zote zinafutwa na wivu.maana wivu huja na
ghadhabu, hasira na chuki. Angalia pia situation mzima Mungu anaongea baada ya
watu hawa kutoa sadaka kama wewe unavyotoa ili kufungua mlango wa Baraka, haina
tofauti. Mwombe roho mtakatifu akujaze nguvu zake ili wivu huo kwa watu na kwa
Mungu usiwe ukuta wa Baraka zako.
Mwanzo
25:29-34
29 Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja
kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana.
30 Esau
akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa
ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.
31
Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza.
32 Esau
akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi?
33
Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki
yake ya mzaliwa wa kwanza.
34
Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa,
kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa
kwanza.
*KUUZA BARAKA
Watu wengi
tunauza Baraka, kwa kujua au bila kujijua, Yohana 10:10 inasema shetani haji
ila aibe, auwe, aharibu, achinje. Sasa kuibiwa huku usifikiri ni fedha kuibiwa
huku ni pamoja na Baraka zako. Shetani hukutamanisha dhambi, na wewe
ukishaitamani unamuuzia kwa kubadilishana naye! Anakupa hasira na wewe unampa
Baraka, anakupa kutokusamehe na wewe unampa Baraka. Anakupa hongo na wewe
unampa Baraka, anakupa kulipisha kisasi na wewe unampa Baraka, anakupa kiburi
na wewe unampa Baraka, anakupa pombe, uasherati, uzinzi, Mali ya uwizi,
utapeli, na wewe unampa Baraka, anakupa uongo na wewe unampa Baraka, anakupa
chakula cha mda, na wewe unampa Baraka, Kuna tofauti ya Baraka na vitu. Isaka,
yakobo, Mungu aliwapa Baraka yani Lango hawakupa vitu. Vitu huwa vinaisha
lakini Baraka huwa haishi, vitu ni magari, nyumba, fedha iliyoko bank. Vikiondoka
huwa vimeondoka. Wakristo wengi huwa wanaomba vitu kwa Mungu huwa hawaombi
Baraka. Baraka haishi. Baraka linafanya lango kila linapokuwa halina ukomo,
haliishi. Wengi Leo shetani anakupa vitu alafu anaondoka Na Baraka zako. Ulijua
njia ya Baraka lakini Leo umejua ukuta wa Baraka. Na ili uache kumpa shetani
Baraka na wewe ukabaki na vitu. Ndicho alichokifanya Esau alimpa Baraka Yakobo
yeye akachukua kitu. Embu tuangalie Biblia
MWANZO
27:27
27 Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya
mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya
shamba alilolibariki Bwana.
28
Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa
nafaka na mvinyo.
29
Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako,
Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na
atakayekubariki abarikiwe.
*Angalia
hizo Baraka na kile chakula alichokula Esau je vinalingana? Vina dhamani? Tokea
Leo acha kuuuza Baraka zako.
Nawe
utaijua kweli. Na iyo kweli itakuweka huru.
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment