VIFUNGO VYA MDOMO

Attachment job application letter.docx successfully uploaded and added.

Conversation opened. 1 read message











Bwana Yesu asifiwe. 

 Nawe utaijua kweli nayo kweli itakuweka huru, wapendwa natumaini una njaa ya kujua mambo ya rohoni kama mimi unahamu ya kujua neno linakuweka vipi huru kwa habari kufanikiwa kwako katika maombi. Leo kuna sehemu nataka pia tuipitie ambayo watu wengi pia huwa wanaisahau, muhimu katika kuomba uhakikishe kwamba huna kizuizi huna kifungo, ibilisi anapigana na walokole kwa vifungo, maana kwingine kote umemshinda, hawezi kukudanganya maana unauona uwongo unaona dhambi, unaona ushawishi wa dhambi, unazuia plan zake, kila mara unam'bomoa na kumuangamiza, uko kivita vita uko alert kwa ajili ya kufanya vita, na yeye anafikiria nitamshindaje mtu uyu?

 

Moja anafikiria kwa kukuvamia fikra zako ili aziharibu anakutana na duara la moto wa roho mtakatifu, anataka akuletee ajali au akurushie magonjwa anakuta malaika wako ameshika upanga mkubwa anasubiri atakaye tokea kuangamiza tuu, malaika wako yupo alert upande wako wa kulia, jinsi unavyozidi kuomba kuwa na ushirika mkuu na Mungu ndivyo jinsi anavyozidi kuwa strong kiasi cha kwamba haruusi hata wewe kujikwaa, anaweza tangulia mbele yako kuwaondosha watu wabaya wapite njia zingine ili wewe upite, anaweza muinua mtu kwenye siti ya daladala ili wewe ukae tuu, utashangaa mtu atasema moyoni ngoja nishuke tuu hapa na wewe utakaa.

 

 Unapozidi kuwa na ushirika mkuu na Mungu malaika wengine watatumwa sehemu mbalimbali duniani kujigeuza binadamu ili wewe usikwame! unaweza kupokelewa na malaika hospital au sehemu yoyote na wewe usijue, malaika anaweza jigeuza trafiki na akavuta magari upande wako ukapita. malaika wapo na wanatembea duniani. Halleluyah! mtu wa namna hii au mlokole yoyote ibilisi atakusubiri kwenye vifungo tuu, Ili akukwamishe. Sasa tuangalie vifungo ambavyo watu huwa watu hawavifikirii kabisa na vina mipaka mikubwa kwenye ulimwengu wa roho, na shetani hupita hapo. wangap wako tayari? 

 

 

 

 




tuangalie neno kwanza ili tunapokuja kuonyesha vifungo ivyo tuwe ndani ya neno!

mithali 6-2

 

  2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako,Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako

Biblia inasema umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako shetani hutega watu, pale watu wanapokata tamaa na wanapokasirika, tunajua ya kuwa hasira haitendi haki ya Mungu, unapokata tamaa na kukasirika kuna roho ya ibilisi huja juu yako na kukuforce ulaani, utukane, uongee maneno mabaya, na sababu umeongea wewe hayo maneno yana nguvu sana, ukisema tuu shetani hata sekunde haijaisha anafanya nayo kazi haraka sana, mfano hujaolewa unasema hizi ndoa ngumu siku hizi ni bora tuu nizae nikae mwenyewe, au wanaume waowaji hawapo, au mwanaume anasema wanawake wa mjini hawafai kuwa wake za watu alafu unashangaa hapo mjini hupati kweli mke wa kuoa, au hakuna wanawake wa kuoa siku hizi, unashangaa utakavyopata shida kwenye kuoa,na 

 

maneno hayo uliyasema kwa kukata tamaa au kwa kupiga stori na umeshasahau shetani maneno hayo aliyachukua kipindi cha kuolewa unashangaa kupata mme inakuwa shida, mwingine anamtamkia mtoto wakati amekasirika, "uyu mtoto bure kabisa huna akili wewe" mtoto anakuwa ndivyo ivyo anakuwa darasani mzazi anaanza kuhangaika mtoto wangu sijui ana nn jamani? kumbe ulimfunga mwenyewe, maneno mengine unamtakia mtoto wakati umekasirika yamefanyika kweli, kuna maneno ambayo huwa yanaendana na kutema mate chini hivo ni vifungo vya kipepo na ardhi, kama kuna mtu amewahi kukutemea mate chini au kumtemea mtu mate chini hivo ni vifungo vya kipepo, mwingine yupo kwenye ndoa siku wamegombana anaongea hii ndoa nimeiochoka bora nikae mwenyewe, najuta kukuowa, 

 

najuta kuolewa na wewe, shetani maneno hayo anatafanyia kazi anaanza kuwatenganisha, mwingine anasema huu wokovu basi, mwingine anasema Mungu hanisaidii tena anamuelezea mtu ambaye hajaokoka anampresent Mungu vibaya kwa watu, kilichofanya Musa asifike kaanani Musa alimpresent Mungu vibaya, Musa aliambiwa auambie mwamba utoe maji, Musa akaupiga kwa hasira na kuwaongelesha Wanawa Israeli kwa hasira Mungu alikuwa presented vibaya, wakati Mungu ni wa upendo, kuna gharama ya kupresent Mungu vibaya. kuna maneno mengi tunaongea vijiweni au katika stori, mwingine anatafuta kazi na alishawi kusema mimi sitakaa niajiriwe, na inakuwa hivyo, mwingine anasema hii kazi siipendi naichukia natamani niache, baada ya kusema hayo tuu na mambo yameanza kuwa tofauti kazini, kitu kingine unapomtamkia maneno mabaya adui yako wewe pia inageuka kwako, 

 

unapomuambia uyu mtu simpendi uyu mtu basi tuu ila kwa kweli roho yake na yangu haivani inafanyika ivyoivyo ulivyoongea sasa shida inakuja unataka msaada kwa uyo mtu shetani anakupinga sababu ya maneno yako. ndio maana biblia inasema usimguse masihi wangu usimdhuru nabii wangu. kama unamsema vibaya mtumishi wa Mungu usitegemee Mungu kumtumia kukufungua wewe, wengine kwenye biashara watasema hii biashara ngumu nitaifunga tuu duka siku siyo nyingi, tena anashuhudia kwa mteja hii biashara haina faida kabisa tunaganga njaa tupate ela ya kula tuu. na gafla maneno hayo yanageuza upepo wa biashara na inaanza kuwa kwa ajili kula tuu kama ulivyosema. Hivi ni vifungo huwa tunavisema pale tunapokuwa tumekasirika au kukata tamaa, Kama jinsi ulivyo kwako pia kuna vifungo vya laana ya nchi hivi unatakiwa uvipangue kila siku ndo mana watanzania wengi hawafanikiwi kimataifa, kama ni biashara watailetea Tanzania sio kupeleka bidhaa nje ya nchi, kuna mipaka ya watanzania kuhusu nje ya nchi, wengi hatutoki tunaishia humuhumu. Halleluyah Halleluyah

 

maombi ya kutenguwa laana ya mdomo ambayo ulitamka au kutamkiwa

 

Baba Mungu tunakushukuru tena kwa sababu umemtukuza mwanao Yesu, kwa kupitia neno asante kwa uaminifu wako Jehova, ninaomba rehema mbele zako katika jina la Yesu, Bwana Yesu naomba unisamehe maovu yangu yoote katika maisha yangu. ninatubu kwa ajili ya maneno yote niliyowahi yazungumza kwa kinywa changu yakageuka laana, natubu kwa ajili ya maneno yote niliyoyasema kwa kukata tamaa, maneno hayo juu ya uchumi wangu, maneno hayo juu yako Mungu inawezekana nilifika kiwango cha kutukana ninaomba rehema, maneno ya laana kwa habari ya ndoa yangu, kwa habari ya uchumba, kwa habari ya watoto wangu, kwa habari ya ukoo wangu, kwa habari ya familia yangu sehemu nyingine tuliropoka hii familia ina  mikosi na tuliposema tuu mikosi ilianza, kwa habari ya kazi yangu, kwa habari ya biashara yangu, kwa habari ya kutafuta kazi, Bwana Yesu wewe unajua tulivyoongea baada ya kukata tamaa, sehemu ingine tulikupresent vibaya Bwana Yesu, tulikuhoji kwa hasira, tukatukana jina lako Mungu, jina lako la wokovu, tunaomba Bwana Yesu utusamehe maneno tuliyoyaongea kwa wake zetu, kwa waume zetu, kwa wachumba wetu, kwa watoto wetu, kwa wazazi wetu, na maneno ya laana waliyoyaongea wazazi wetu hata wakati mimba zetu zilipotungwa, pale tulipokosea kama watoto, pale walipokasirika, maneno tuliyoyaongea baada ya wazazi kushindwa kufanya haki kama binadamu tunaomba toba Bwana Yesu. maneno hayo yakachukuliwa katika ulimwengu wa roho yakafanyiwa kazi haraka sana na ibilisi tunaomba utusamehe, tunaomba uturehemu, kama tumewahi kutemea watu mate chini bila kujua ni agano la kipepo, au watu waliowahi kututemea mate chini Bwana Yesu tusamehe, kwa maneno yote katika kupiga stori katika mizaha, Ambayo yamegeuka laana kwa jina la Yesu kwa damu Ya Yesu ninayafuta, ninayafuta huko yalikopelekwa katika ulimwengu wa roho, Damu ya Yesu ya Rehema ninaimimina katika milima, mabonde, mapango, kuzimu zote saba, chini ya bahari, angani, ardhini kwa jina la Yesu, Damu ya Yesu ya uwakilishi ikatembee kila mahali sasa, kila vifungo vilivyofungwa kwa mdomo wangu au midomo ya watu wengine ninaachilia damu ya Yesu ya uwakilishi, damu ya Yesu ya rufaa kwa jina la Yesu, ewe malango yangu yote, malango yangu yote popote ulipopokea maagizo ya ibilisi kuwa ufunge mlango sababu ya laana sasa kwa jina la Yesu sasa kwa damu Ya Yesu ninaamuru malango yangu inua shingo yako juu,ninakumwagia damu ya Yesu,ninakumwagia damu ya Yesu Damu ya Yesu ya rufaa, ninakuamuru ewe malango yangu fungua mlango kwa damu ya Yesu, fungua mlango kwa damu ya Yesu, makazi yoyote ya ibilisi, nguvu za ibilisi, walinzi wa kipepo wa ibilisi, watenda kazi nawakutanisha na damu ya Yesu, nawakutanisha na damu ya Yesu ya rufaa, katika malango hayo ninashusha moto sasa, kwa jina la Yesu. Mapingu ya shaba mapingu ya chumba uliopo kwenye malango shika motouungue kwa jina la Yesu, lipuka kwa moto kwa jina la Yesu, Naachilia damu ya Yesu ya rufaa juu ya Viti vya enzi kwenye malango, damu ya Yesu ya rufaa juu ya uchawi wowote kwenye malango, damu ya Yesu ya rufaa juu ya mizimu ya ukoo iliyoshikilia malango sababu ya laana ya mdomo kwa jina la Yesu, Damu ya Yesu ya rufaa juu ya makaburi, roho za mauti popote waliposhikilia kujimilikisha malango yangu sasa inatosha ninawachilia moto, ninawachilia fireee mshike moto muungue kwa jina la Yesu. naachilia damu ya Yesu ya uwakilishi na rufaa juu maeneo yoyote ya ulimwengu wa roho, juu ya ardhi, bahari, mito, sehemu yoyote yenye maji, anga, bahari sehemu kwa jina la Yesu, ninabatilisha maneno hayo hata niliyowahi kutamkiwa kwa damu ya Yesu ya rufaa kwa jina la Yesu.katika jina la Yesu naomba Amen.

kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu


josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA