VIGEZO VYA MUNGU KUKUSIKIZA
Somo: "Vigezo
vya Mungu kukusikiza"
Ufunuo 5
1 Kisha nikaona katika mkono wa
kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu
kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.
2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake?
3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.
6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
7 Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi.
8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,
12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.
13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.
14 Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.
Halleluyah! Halleluyah! Halleluyah!
2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake?
3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.
6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
7 Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi.
8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,
12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.
13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.
14 Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.
Halleluyah! Halleluyah! Halleluyah!
Bwana Yesu
asifiwe! ni muhimu kujua kwanini Mungu akusikize wewe? hasa wewe mtoto wake? unapojua hili basi itapandisha kiwango cha imani yako unapomuomba Mungu na utapata matokeo makubwa!
"Wastahili wewe kukitwaa hiko kitabu na kuzifungua muhuri wake" MSTARI WA 9. Hiki ni
kitabu gani? Hiki ni kitabu cha kuzimu ambacho yoyote hajaokoka kuna kumbukumbu
zake kuna jina lake huko. Vitabu vyenye kukumiliki wewe kama haujaokoka,Yesu
alipokufa na kufufuka kafufuka na ufunguo wa hivyo vitabu ndio maana anasema
kuzifungua muhuri zake, halleluyah halleluyah, vitabu ivyo vina mpango wako
kila kitu na jinsi watakavyokutumia na kukuangamiza Ndo mana biblia inasema
kufungua mihuri zake. Manake baada jina lako kuwekwa kwenye vitabu vya kuzimu
wanapiga mihuri ya kipepo.
Mihuri kwa maagano ya kipepo ya kukutesa wewe na
kukushughulikia wewe.
Anasema kwa
kuwa ulichinjwa na ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila, kila
lugha, jamaa na taifa. Bwana Yesu asifiwe sana! Twende taratibu nataka uipate
point ya Mungu alafu uifanyie kazi. Yesu kwa kumwaga damu yake manake
amekununua wewe kutoka kwenye mauti ya vile vitabu vya kuzimu, na kukutoa
katika mihuri ya kipepo na kukuweka huru. Alinunua kila kabila, kila lugha,
kila jamaa na kila taifa. Manake yoyote anayetaka kumfuata Yesu haijalishi ni
kabila gani, haijalishi anaongea lugha gani, haijalishi ni jamii gani au taifa
gani. Tayari Yesu alimwaga damu ya Yesu ili kukunua wewe uingie katika ufalme
wa Mungu.
Niweke katika
mfano ili uelewe vizuri ni kigezo gani Mungu hutumia kukusikiza wewe? Mtu
anapoenda au anapotaka ku adopt mtoto huwa kuna sheria anafuata na kanuni na
vigezo vya kufuata ili kumpata mtoto, na anapoenda ku adopt mtoto huwa anaenda
mfano kituo cha watoto yatima kuchagua mtoto anayemwitaji au anayependezwa naye
kati ya watoto wengi. Ila akisha adopt mtoto yule mtoto anakuwa wake kabisa,
kwa iyo yule mtoto anaridhi kila kitu cha uyo mzazi wake wa kisheria kuanzia
jina, haki ya kusomeshwa anakua nayo, haki ya kutibiwa anakuwa nayo, haki ya
kulishwa anakuwa nayo na haki zoote kama biological further
au mother atafanya
kwa mtoto wake! Kama mtoto wako anaumwa njaa hautaji agalegale chini wewe ndio
umpikie uji au chakula, ile inakuja automatic,mtoto wake akiumwa haitaji apige
kelele sana automatical utampeleka hospital, uyo mtoto uliyemwa adopt anakuwa
na haki zote, yuko huru kucheza ndani, yuko huru na wewe saa ingine ni vigumu
kujua huyu mtoto ni wake au alimuadopt! Maana amekuwa wa familia ile! Amekuwa
mmoja wa familia. Kwa kuwa amekuwa mmoja wa familia hana haja ya kuomba ruhusa
kila saa au kila wakati juu ya vitu vilivyopo ndani ya nyumba.yupo huru. Jinsi
mzazi alivyo ndivyo jinsi mtoto atakavyokuwa. Kama anauchumi mzuri basi mtoto
naye ataenda soma shule nzuri. International skul ikibidi.
Mungu
anakujibu sababu tuu Yesu alikununua wewe kwa damu yake, amemnunulia watu Mungu
kila kabila kuna mtu kaokoka, kila lugha kuna mtu kaokoka, kila taifa kuna mtu
kaokoka,kila jamii kuna mtu kaokoka. Amemnunulia watu kwa damu yake na kuwa
umbu moja la Yesu. Kwa iyo sababu wewe umekuwa adopted na damu ya Yesu manake
wewe ni mdogo wake Yesu. Wewe una haki sawa na Yesu. Wewe ni umbu la Yesu,
Kumbuka ule mfano kule juu. Mungu anakujibu si sababu umepitia majaribu
mazito,au unayajua majaribu, au unafunga tatu kavu sana, au umetoa sadaka kubwa
sana, au unajua neno sana, umesoma vitabu vingi sana vya rohoni, au unajua
kuomba sana ingekuwa ni ivyo kila mlokole angejibiwa kwa wakati anaotaka yeye.
Mungu anakujibu tuu sababu ni haki yako wewe kama mwana wa mfalme. Ukiendelea
kusoma kitabu cha ufunuo mlango huo huo amezungumzia mambo ya ufalme, utajiri
na kila kilichopo ambacho anamiliki Yesu na wewe pia unamiliki. Nataka nikupe
siri hii Mungu angekuwa anajibu sababu tuu
ya sadaka kubwa mabillionea wote
wangefanikiwa sana. Mungu angejibu sababu ulipitia magumu au majaribu au sababu
unajua sana neno, au unajua kuomba sana, au unaufahamu sana wa Mungu lazima
ungeinuka na kiburi. Kusudi ujue kila kitu kinapatikana kwa neema ndo mana anajibu
kwa wakati wake, ili usije anza kuhukumu watu "mimi nilisota nilifunga na
kuomba Mungu akanifungua" "unatakiwa uvumilie ufunge na kuomba"
"wewe unamtania Mungu mimi nilisota nikafunga tatu kavu" "mimi nilivunja maagano ya kwetu ndio
nikawekwa huru" wewe kama hujavunja huwezi kuwa huru, hutafanikiwa"
ndio maneno ya wapendwa. Mungu anakutendea sababu tuu wewe ni Mwana na yeye ni
Baba. Iyo ikae kichwani. Manake unaspecial place kama wewe mtoto wa ufalme wa
Mungu. Sehemu zingine Mungu hatendi au hafanyi ili usije kuona ni juhudi zako
ndo zimekutoa hapo kumbe ni neema ya
damu ya Yesu. MUNGU ANAKUJIBU NA KUKUTENDEA SABABU YA MAHUSIANO ULIYO NAYO NA
MUNGU NA WENGINE HAWANA. MAHUSIANO YA WEWE KUWA MWANA WA MUNGU NA YEYE KUWA
BABA YAKO.
Tuangalie
neno;
Mathayo 6
9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye
mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Anasema
ninyi sio kila mtu ni wale waliokoka tuu. Anasema Baba yetu uliye mbinguni.
Mungu si kila Baba wa kila mtu. Ndio maana anasema "ninyi" wale walionunuliwa na damu ya Yesu.
Wakaingizwa kwenye ufalme wa Mungu (waliokoka) ndio wanayo haki ya kuita Baba.
Ndo Biblia inasema Yeremia 32:27 "Mimi ni Mungu wa wote wenye mwili"
sio Baba wa kila mwenye mwili. Mungu anakujibu tuu sababu ni haki yako kwa kuwa
umeingizwa kwenye ufalme wa Mungu kwa kuwa Yesu alikununua kwa damu yake. Hii
ndo mana Mungu alikuwa na mwana wa pekee mmoja Yesu maana alijua baada ya Yesu
kuwa adopt wengine basi Mungu atakuwa na wana wengi. Bwana Yesu asifiwe sana.
Wagalatia
3-13-14
13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati,
kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu
aangikwaye juu ya mti;
14 ili
kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea
ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
Bwana Yesu
asifiwe, kuna vitu vingine Mungu haviachiliwi ni mpaka ujue kwanini Mungu
anakupa au kwanini kakutendea ukishajua anakiachilia katika maisha yako. Lazima
utambue nafasi yako kama mwana wa Mungu. Ya kuwa unapewa si sababu yoyote bali
nafasi uliyonayo katika ufalme wa Mungu. Na unaposimama kama mwana ujiamini
usiseme mimi ni mtoto wa mfalme huku hujiamini. Lazima ujiamini. Kujiamini
kwako ndiko mbingu inaona wewe umetambua nafasi yako. Hakuna kitu shetani
hakipendi kama watu kutambua nafasi zao. Bwana Yesu asifiwe.
Lakufanya;
Kama
hujaokoka! Okoka kwanza ili upate ile nafasi ya kuwa mwana. Upate special
treatment ya ki Mungu. Pili,Nenda mbele
za Mungu Baba tambua ya kwamba wewe ni mwana wa Mungu katika ufalme wa Mungu
kwa kupitia kuwa adopted na damu ya Yesu. Na kununuliwa kutoka mautini(
kuokoka). Kwa iyo kama mtoto wa mfalme una haki juu ya yote yaliyochini ya
Yesu. Yote yaliyowekwa chini ya miguu ya Yesu ni ya kwako pia maana ni familia
moja. Maana biblia imesema yote yako chini ya miguu yake na ambalo kanisa ndilo
jina lake. Ambaye ni mimi na wewe haya ni maombi simple lakini utashangaa
matokeo!
Kwa kutambua ivo Mungu atafanya kitu kwa mwana. Halleluyah halleluyah!
Ulizia kwa habari ya uchumi wako
uliokwama kama mwana, ndoa yako yenye misukosuko kama mwana, habari ya kazi
unayotafuta kama mwana, habari ya kibali cha biashara chochote unaulizia kama
mwana wa Mungu na unamuulizia Baba. Na unatambua nafasi yako ya kuwa wewe mwana
hivyo ni haki yako.Maana ulinunuliwa kwa
damu ya Yesu na kuingizwa katika familia ya Mungu. Simple as that. Nakutakia
mafanikio na uje na ushuhuda hapa in Jesus name. Just kutambua hilo Mungu
ataenda kufanya kitu. Jina la Bwana libarikiwe.
Tuangalie neno kwa ufupi;
8
Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho
langu likikutazama.
Zaburi 32:8
Anasema nitakufundisha na kukuonyesha njia
utakayoiendea; nitakushauri, jicho langu likutazama. Halleluyah! Halleluyah! MUNGU wetu ni Mungu mkuu Sana,
mkuu mno! Mungu hufundisha watu njia za kutoka katika majaribu, majangwa, katika
hila, katika vitanzi, katika vifungo! Na Si tuu hivyo anakufundisha na
kukuonyesha kwa macho kabisa njia utakayoiendea kama umekwama sehemu yoyote
atakuonyesha chanzo cha tatizo, na jinsi ya kutoka hapo na nini unachotakiwa
ukifanye yani manake, njia unayotakiwa uifuate au ufanye nini kujinasua hapo,
pia kwenye iyo njia atakushauri, na jicho lake likiendelea kukutazama usije
tena ukaanguka. Tuchukue mfano wa mfanyabiashara aliyefungua alianza vizuri
katikati akafunga biashara. Mungu atamuonyesha chanzo cha tatizo, ndio
kumfundisha. Atampa maelekezo jinsi ya kufanya!
Ndio njia iyo, pia atamshauri
pia katika iyo njia anayoiendea ili afike salama, kana kwamba haitoshi Mungu
jicho lake litakutazama, yani tokea hapo atakulinda usianguke tena. Halleluyah.
Halleluyah Mungu wetu ni Mungu mkuu Sana. Mkuu mno! Anakupenda zaidi
unavyomchukulia au kujichukulia. Unajua mfalme Daudi Mungu alimpenda Sana Si
kwamba alikuwa hakosei au kutenda dhambi ila kila Mara alijua kurudi kwa Mungu
kuomba rehema. Alijua jinsi ya kujirudi kwa Mungu. Na hakujihesabia haki mbele
ya Mungu au mbele ya mtu. Hii ndo sababu Mungu alimpenda Sana Daudi. Leo wewe
uliyeokoka kama roho wa Mungu hafanyi hizi kazi hapo juu mpendwa unakazi ya
kutengeneza mahusiank yako tena na Mungu. Si Mara moja Bali kila wakati uwe
Safi mbele za Mungu. Mwambie Mungu akusaidie. Ili uufikie au uuone ukuu wa
Mungu. Jina la Bwana libarikiwe.
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka
nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako
biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni
kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige
hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande
wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi
ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment