WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA

 Tuangali indeep neno ambalo unalijua tulitafakari in light of Holly spirit. Halleluyah!

 Tuangali indeep neno ambalo unalijua tulitafakari in light of Holly spirit. Halleluyah!

 Actual maneno mawili kwa kifupi sana. Alafu tutaona jinsi yanavyohusiana. Haya ni maneno ya maarifa.

: 6  Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. HOSEA 4:6

 :17  Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. WARUMI 10:17

: Anasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa! Neno la pili imani chanzo chake ni kusikia hapo sina tatizo ninapopataka nako kusikia huja kwa neno la Kristro. Haya maneno mawili.

 nilipoyapata Roho akafungua ufahamu wangu la kwanza maarifa ya Mungu huja kwa kusikia. Pili huko kusikia lazima kuje kwa neno la Kristo. Tatu imani huzaliwa baada ya kusikia kwa neno la Kristo. Kwa iyo inaanza kusikia

 kwa neno la Kristo. Sio NA no! KWA neno la Kristo. Kisha inafuata maarifa ya Mungu! Ukitaka kuwa na maarifa au kuyatambua maarifa ya Mungu lazima neno likusaidie kuyajua maarifa ya Mungu. Twende taratibu!

 Nimesema hivi maarifa ya Mungu huyawezi kuyajua au kuyasikia isipokuwa umesikia kwa neno la Kristo. Kitakachokusaidia kupata maarifa ya Mungu au kuyasikia maarifa ya Mungu ni kwa kusikia kwa neno la Kristo. Maarifa ya Mungu yanakusaidia usiangamie.

 Sasa angalia. Kwanini anasema kusikia kwa neno la Kristo na siyo na neno la Kristo? Neno la Mungu ndilo linalotafakari sauti ya Mungu. Bila hilo neno huwezi huwezi kusikia. Neno la Mungu linaroho ndani yake ambayo inayokusaidia kutafsiri lugha za Mungu. Au mawazo ya Mungu

 kuja katika nyama na damu. Mungu ni Mungu anamfumo wake na utaratibu yake. Ni sawa na gari nzuri umepewe iko full tank, lakini haina sehemu ya kuingizia mafuta yatakapoisha. Ule mlango wa

 mafuta wenye gari(kiwandani) hawakuweka! Lakini option ya kuweka ipo kwa fundi, iyo option ndio umeachiwa wewe uamue uweke mlango wa disel au petrol. Kwa sababu hakuna mlango lakini lipo tank. Ilo gari litatembea kwa

mda tuu litakapoishiwa mafuta kutakuwa hakuna jinsi ya kuingiza mafuta kwenye tank.isipokuwa umeweka mlango.  upitishe petrol au disel huo ni uamuzi wako. Pia Mlango unategemea engine yako imejengwaje. Tupo pamoja!

 Maana mlango au mdomo wa kuingiza mafuta haupo. Sasa ilete sasa katika wewe na Mungu. Mungu ili uweze kusikia toka kwake lazima kuwe na Mlango wa kuingizia mafuta.ila sasa tukumbuke

uchaguzi wa mafuta unao wewe,kiwango cha mafuta kuingia inategemea mlango unafungukaje kiwango gani? kwa iyo Mlango wa kutafakari ili wewe uweze kumuelewa Mungu. Mungu

 akizungumza na wewe mojakwamoja bila huo mlango hutamwelewa wala hutajua kama ameongea.sababu kila mlango unanjia yake ya kuingiza mafuta. Ukitaka uingize mafuta kwenye gari yako benzi hutumii mlango wa landcruiser,lazima kuwe na mlango

husika. Ndivyo Mungu anavyofanya kwa watu wake.sio kila mtu atasikia sauti yake isipokuwa wewe uliyefungua mlango. Ndo mana neno sasa la Mungu ni mlango wa wewe kusikia si mwingine wewe. Yani wewe na Mungu. Lazima kuwepo mlango wa kupitisha sauti, mawazo, vitu vya Mungu. Sababu vitu vya Mungu havipiti kila mahali.

 Vinapita kwenye mlango wa Mungu tuu. Na huo mlango ni neno la Mungu. Sasa jinsi vitu ivyo vitakavyopita inategemea umefungua mlango kiasi. Gani. Kiasi cha jicho moja kuchungulia, macho mawili kuona, uso kupita, kichwa na bega moja kuonekana. Halleluyah watu wa Mungu.

 Kusikia kwa neno la Kristo ni huku. Kile kitendo cha kusoma neno na lile neno kuzungumza na wewe iyo ndo kusikia kwa neno la Kristo. Unaposoma neno maana ya kwanza utaipata unaposoma maana ya pili ipo sauti itakuelewesha ilo neno kulinganisha na situation yako.

 Itakutafsiria kiasi cha kuona amani katika moyo wako. Huko ndiko kusikia kwa neno.  Sasa haishii hapo Mungu anaweza kuzungumza na wewe kwa picha, ndoto kwa shuhuda ya mtu mwingine, kama maono, kusudi kusikia lazima uwepo mlango wa kuingizia iyo sauti ya Mungu na kukutafsiria ili uelewe

 katika level yako hii ya kibinadamu. Kwa kusema hayo point nilitaka uipate hapa Mungu hutupa maarifa kila siku! Hutujibu kila siku isipokuwa mlango wa kusikia kwenye moyo wako hakuna. Mungu huonya, hufundisha, hukuelekeza, hukuongoza katika mambo yote sema

 mlango huwa umefunguliwa kidogo au haupo kabisa. Nilisema juzi matatizo yako yote yanahitaji tuu maarifa ya Mungu.Na ibilisi anaufunga kwa vitu vingi ikiwemo hasira, chuki, jazba, kutokusamehe, hukumu, wivu, kijicho! Na mambo yafananayo na hayo. Bwana Yesu asifiwe! Vitu na mfano wa ivyo huziba lile tundu la kuingiza maarifa ya Mungu.

 Nilikuambia kwanini sisi ni  binadamu na Mungu ni Mungu sababu mojawapo maarifa na hekima vinatoka kwa Mungu. Sisi hatuna lazima tumuombe yeye. BWANA YESU ASIFIWE SANA! kwa iyo fungua mlango wako wa kusikia kwa neno kwa kusoma biblia kila siku si

 upatapo nafasi! Pili funga nafasi ya ibilisi ya kufunga mlango wako kwa kuomba rehema na kusamehe wengine. Na hii ndo formula ya kuyapata maarifa ya Mungu.

 Kwa iyo utaamuwa wewe mwenyewe uangamizwe kwa kukosa maarifa au utafute maarifa ya Mungu kwa kufungua mlango. Bwana Yesu asifiwe. Uchaguzi upo mikononi mwako jina la Bwana libarikiwe.

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA