UWEZO WA DAMU YA YESU


Bwana Yesu asifiwe!

somo; uwezo wa damu ya Yesu

ufunuo 5:5:6
5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.

6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.

Bwana Yesu asifiwe! kwa wale ambao hawajapitia ufunuo 5 sura yote basi nashauri upitie,tena na tena na tena.kitu cha kukumbuka katika kitabu hiki kitabu na mihuri saba inamaanisha kifungo kikubwa

kilichoshindikana sehemu tatu mbinguni, duniani hata kuzimu. mwanakondoo pekee ndiye aliwepewa uwezo wa kufungua vifungo hivyo vilivyoshindikana point nayotaka uchukue hapa, Zile muhuri saba na kile kitabu kilichofungwa kilifunguliwa kwa damu ya mwanakondoo. soma mstari wa 9.

hakikufunguliwa na malaika Gabriel, Hakikufunguliwa na moto wa roho mtakatifu! bali damu ya mwanakondoo! nataka uchukue hii na uitumie. Yesu anapoenda kupigana kwa ajili ya kukutetea anaenda kama Simba wa Yuda.

Yesu anapoenda kukufungua kifungo chako anaenda kama mwanakondoo aliyechinjwa, kwa iyo si vifungo vyote! vinafunguka kwa kukemea, vifungo vingine vinafunguka kwa kunyunyiza damu ya Yesu.

 unajua vifungo vyote na shida yote hapa duniani huletwa na wachawi na waganga wa kienyeji, vifungo hufungwa na wachawi, shida yoyote iliyokungangania jua tuu huletwa na wachawi

 wanapokutana katika mikutano yao usiku wanapeleka jina lako au yenu. wanapeleka mashitaka kwa ibilisi, wanafanya vikao jinsi ya kukufunga, kisha ili pepo lije

kusudi sasa lije likufunge lazima wamwage damu. aidha ya njiwa, paka, kondoo, mbuzi, ngombe, hata binadamu, au chochote! damu inauhai, wanapouwa kile kiumbe katika ulimwengu wa roho wamekuuwa wewe, lakini si kwa wana wa Mungu.

 wanajifunika kwa damu ya Yesu, ivyo usiogope unaulinzi mkubwa sana wa Mungu.sasa kifungo ukubwa wake hutegemea kafara iliyotolewa. nakufundisha maarifa ya Mungu si uchawi. kifungo cha damu ya kuku au mbuzi ni tofauti na mtu aliyemwaga

 damu ya ngombe saba (7) wanapomwaga damu za kafara ndipo sasa pepo linapata uhalali wa kukufunga wewe, ukubwa wa kafara au udogo wa kafara ndio itatoa picha uzito wa kifungo chako, ndio maana mwingine atafunguliwa haraka mwingine kidogokidogo, sasa hii damu ya Yesu inanguvu kuliko damu

 zooote kabisa na hii habari njema. damu ya Yesu si ya kujitakasa tuu, au kujifunika tuu. damu ya Yesu kazi yake pia ni pamoja na kufungua mapingo ya shaba na ya chuma, au uchawi wa mafundo, kwenye biblia wameelezea hiyo ni aina ya vifungo vikubwa sana

 , sasa wachawi hawawezi fanya lolote bila damu za kafara hata ajali unazosikia ni kafara za kuongezea majini uwezo au mapepo uwezo wa kufanya kazi. Ndo mana ajali za kutisha utazisikia katika mifungo ya ndugu zetu mwezi huu. kwa sababu ndugu zetu wanaabudu

 mapepo wakijua ni Mungu Jehova. naongea hii ili kweli ikuweke huru"

kuna maombi ya kufunga ni yale tunayofanya kila siku usiku vita ukiangamiza, ukiteketeza, ukiharibu manake unafunga mapepo yasiweze kufanya kazi, ukiyaharibu yanateketea kweli lakini sasa vipi kuhusu vifungo walivyofunga je umevifungua?

kuna maombi ya kufungua ambayo wengi huwa hatufanyi wengi tukishafanya maombi ya vita tunajua automatic mambo yatajifungua yenyewe, kumbe ulitakiwa umalizie kwa kufungua kilichofungwa kwa damu ya Yesu. yenyewe ni agano kubwa, na kuchukua mbe le ya damu ya Yesu.

 ni kafara kubwa kuliko zote, ukimwaga hii damu ya Yesu kwa imani ujue ya kwamba damu hii inauwezo zaidi mara mil 1 zaidi ya damu zozote wanazotumia kukufunga.

kwa iyo usifurahie adui yako kupigwa au mchawi kafa sababu umeomba, au usifurahie adui yako kuumbuka, au kula msoto au kupigwa bali furahia wewe kuwekwa huru. kwa iyo lazima lazima ufungue vilivyofungwa kwa damu ya Yesu yenye password zooote. yenyewe inafungua kila tatizo kila tatizo.

 nitakupa mfano kilichowatoa wana wa Israeli wakawa huru, si yale mapigo 10, si mapigo ya vyura, chawa, maji kuwa damu, mvua ya mawe, hapana kilichotoa wana wa Israeli ile damu waliyoipaka katika miimo ya milango yao!

kwa iyo wana wa Israeli walifurahia zile ishara na miujiz a ya Mungu lakini hakuwa huru, walifurahi kuwaona watesi wao wakipigwa na Mungu huku giza kwetu mwanga lakini hawakuwa huru. kumbuka hawa watu walikaa kifungoni miaka 400, ni kama wewe tatizo

 lako jinsi lina miaka wewe mwenyewe unajua, wengi tukianza kuona adui anapigwa, au ishara au miujiza inaanza huwa tunaacha kuomba, kupigwa kwa mapigo 10 wamisri hakukuwaweka huru wana wa Israeli ni mpaka walipochinja mwanakondoo

 asiye na hila. na wataalamu wa biblia wanasema tukio lile lilikuwa linamwandalia Yesu njia, yani agano la kale ni kivuli cha agano jipya. agano la kale walichinja mwanakondoo, huku agano jipya alichinjwa Yesu mwenyewe. ndo maana Mungu alimleta mwanae duniani kwa ajili gani ni kwa.sababu ya

 damu imwagige, kwa hii damu ya Yesu kila vifungo au utumwa vifunguke, nakuambia ukiamini utashangaa jinsi tatizo lako litakavyofunguka kirahisi, wana wa Israeli hawakutoka misri kwa ahadi za Mungu tuu, au ishara na miujiza aliyoifanya Musa, au kwa mapigo kumi!

 walitoka baada ya kuamini, na kufanya kama neno la Musa. baada ya kupigwa wana wa misri walienda kuteka nyara kuchukua walivyozulumiwa vya miaka yote 400, ivyo na wewe lazima udai na uchukue mbele ya hii ya damu ya Yesu Kristo.

 Na nimepata jibu zuri kwanini Mungu aliwachinja wazaliwa wa kwanza wa misri, unajua upinzani ule walikuwa wanauona ulikuwa unatoka rohoni, yani ile miungu ya akina farao ndio ilikuwa inawasukuma wa misri kuwatesa wana wa Israeli, kwa Mungu kuwauwa wazaliwa wa kwanza ile miungu ikafa, yani

 wachawi wanaweka nguvu zao kwa wazaliwa wa kwanza, kuwachinja katika mwili kulimaanisha kuchinjwa kwa mapepo katika ulinwengu wa roho, ndio maana walikuwa hawana nguvu tena au nguvu ya kuwakandamiza wana wa

 Israeli. na Farao mwenyewe aliwaruusu! embu tuangalie ilo neno. ila yote haya yalifanyika kwa kivuli tuu cha damu ya Yesu. kwa iyo damu ya Yesu ndiyo itakayokufungua! halleluyah halleluyah!

kutoka 12
1 Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia,

2 Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.

3 Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;

4 na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo.

5 Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.

* Tunaona wana wa Israeli wakipewa maagizo au maelekezo kwa maneno mengine wakipewa neno
wakukubali na kuamini.

kutoka 12
29 Hata ikawa, usiku wa manane Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.

30 Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu.

31 Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, kamtumikieni Bwana kama mlivyosema.

32 Twaeni kondoo zenu na ng'ombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu, mkanibariki mimi pia.

33 Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote.

34 Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani.

35 Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi.

36 Bwana akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara.

kesho tutaingia ndani zaidi! ili unapoomba nataka ujue damu ya Yesu manake ni nini ili usichukulie unavyoichukulia! ni ufunguo mkubwa sana kwa wanaojua kutumia! kitu kikubwa sana tena mno! mission ya Mungu kwa Yesu kuja duniani ni ili damu imwagike! damu imwagige baada ya damu kumwagiga akasema imekwisha. kesho tutaingia ndani zaidi.

JINA LA BWANA LIBARIKIWE!

somo: uwezo wa damu ya Yesu.(B)

kutoka 12-21-23
1Wakor 5-7

Bwana Yesu asifiwe jana tuliangalia jinsi wana wa Israeli walivyopata ruusa na kuwa huru baada ya damu ya mwana kondoo kuchinjwa. Leo tutaenda kuangalia katika ulimwengu wa roho damu iliwaleteaje ushindi! ukijua hizo sababu hutaiacha damu ya Yesu.

najua wote ni wasomaji wa biblia kwa iyo kama umesahau hii stori ipo katika kutoka 12 sura yote- tunaona jinsi malaika wa Mungu Michaeli alivyoshuka baada ya kuchinjwa mwana kondoo! manake baada ya damu kumwagiga.

*Damu ile ya mwanakondoo ilivyochinjwa manake iliangusha miungu ya wa misri, jana nilisema ile nguvu ya kuwakalia wana wa israeli, haikuwa jinsi ya mwilini ilitoka rohoni ile miungu ya misri iliweza kuwatia hofu wana wa israeli ndio maana walitawalika kirahisi. ile
damu sasa baada kumwagiga ile miungu ya misri ilikuwa haina nguvu tena. ndivyo inavyofanyika unapomwaga damu ya Yesu ile miungu ya adui yako inakuwa haina nguvu tena. ulimwengu wa roho unafanya kazi kaa damu. inategemea ni damu ipi yenye nguvu rohoni.

*Damu ya Yesu iliwapa nguvu ya maneno wana wa Israeli, iliwafanya majasiri, kama jinsi wamisri kabla ya kupigwa walivyokuwa majasiri ukitaka kujua stori hii angalia baada ya kugundua wako huru walienda kwa wamisri na kuwateka na

 kuwaamrisha wawape mali zote. walichukua kila kitu soma mwenyewe kutoka 12-35, na ndivyo inavyokuwa ukimwaga damu ya Yesu chochote utakachokitaka adui atakupa hata ambavyo hujamwomba. sababu ya uwezo ulio katika damu ya Yesu. anahisi utamdhuru zaidi. ile nguvu ya damu ya Yesu inamkandamiza.

*Damu ya Yesu iliwafidia walichoibiwa miaka 400 yote angalia baada ya lile tukio la mauaji farao mwenyewe aliamka usiku wa manane akamfuata Musa na Joshua kuwamsha usiku uleule! kuwaambia kachukueni kila kitu muondoke muondoke! mkamtumikie Mungu wenu

 unapomwaga hii damu ya Yesu adui huwa anachanganyikiwa na anaona akiendelea kushikilia cha kwako au wewe Mungu atampiga zaidi ndiyo maana anarudisha vyote. hapa tunaona damu ya Yesu ikimwagwa inamlazimisha adui kurudisha kila kitu sababu hofu kuu inakuwa inawaingia.

*Damu ya Yesu iliwatia hofu kuu wa misri, baada ya kugundua kila nyumba kuna msiba, hakuna wa kumpa pole mwingine ni kila nyumba kila mahali kuna msiba, kile ambacho kilichokuwa kinawapa nguvu kimeangushwa, kitu ulichokuwa unategemea, ni kama usikie

 majeshi yote ya Tanzania hayapo yameuwawa alafu unasikia alishabibi wameeingia wapo mtaani kwako sidhani kama utalala kwa iyo hawana ulinzi tena. niliwaambia miungu wa misri ilikuwa inakaa kwa wazaliwa wa kwanza, kwa sasa ikawa zamu ya Misri kuwa na hofu kuu na wana wa Israeli kuwa na ujasiri mkuu.Damu ya Yesu inakusukuma uwe jasiri.

*Damu ya Yesu ilitia nguvu maneno ya Musa kwa farao kutoka 12-30, mpendwa Musa kila alipokuwa akienda kwa Farao kumpa ujumbe wa Mungu anawadharau akiona pigo likiondoka anawadharau hawapi ruusa, ilipomwagiga damu ya mwanakondoo, nakuambia yale maneno ya

 Musa yote farao aliyakumbuka yote ndio maana akasema enendeni kamtumikieni Bwana kama mlivyosema, unafanya mchezo aliwaasha usiku wa manane,angalia tena kutoka 12:35, biblia inasema wana wa Israeli wakafanya kama neno la Musa, kisha ikaendelea huko mbele ikasema nao wakawateka nyara wa misri,

 kuna maombi utaomba lakini yanapata nguvu tuu yanapounganishwa na damu ya Yesu, Bwana Yesu asifiwe sana, maana anaona tusije tukafa na sisi, maombi yoyote yanatamkwa nyuma ya damu ya Yesu yana nguvu kuliko maneno tupu.

*Damu ya mwanakondoo iliwateka nyara na ufahamu wana wa misri, angalia wakati wana wa israeli wanachukua mali, wa misri biblia inasema walikuwa wakiwasaidia kuwatolea vitu nje, kwa hofu, walipata bumbuwazi la moyo

 ndio maana baada ya kuondoka tuu wale wazee wa misri wakagundua nchi yote uchumi wote umeenda na waisraeli ndipo wakaanza kuwafuatilia nyuma. manake wakati walikuwa wakichukuliwa vitu vyao, walikuwa wametekwa nyara akili

zao na ufahamu ndio
 inavyokuwa ukipigana vita vyovyote kwa damu ya Yesu, unachukua kirahisi maana adui atapigwa bumbuwazi atatekwa ufahamu, baada ya wewe kumaliza tuu ndipo yeye ufahamu wake utamrudia. Na damu ya mwanakondoo haikuishia hapo tuu.

 walipojaribu kuwafuatilia wakapigwa bumbuwazi tena kisha waliishilia wote baharini.iyo ni damu ya mwanakondoo agano jipya damu ya Yesu. halleluyah Halleluyah! halleluyah! damu ya Yesu ni msaaada mkubwa wa

 vita, Damu ya Yesu inafanya vita vinakuwa rahisi. unajua ukisema misri kwa maneno mengine ni kifungo chako cha sasa, wewe unakijua na Israeli ni wewe. kwa iyo kifungo chako kiko utumwani, kifungo cha ndoa, kazi, biashara, mahusiano, kifungo chochote wewe unakijua...

unaona mapigo kumi (10) wana wa Israeli hawakuwa huru ila ilipomwagwa (mwanakondoo) damu ya Yesu, Damu ya Yesu haifungui tuu bali itakutetea hata kama wewe ndo uliofungulia hiyo miungu au

 upande wa kwenu, ukiomba rehema utafutiwa hatia zako.na mashitaka, damu ya Yesu itanena mema juu yako! kwa iyo bila damu ya Yesu wewe kama mkristo huwezi fanya jambo lolote lile. au huwezi kupigana ukashinda vifungo vikubwa bila damu ya Yesu.

*Kitu kilichochukuliwa kwako kwa damu ya giza utakirudisha kwa damu ya Yesu pekee iyo ndo kanuni.

*Jinsi ya kuomba kwanza lazima utambue uwezo wa damu ya Yesu, kisha vikusanye vitu vyako vyote vilivyokuwa kifungoni ndani ya damu ya Yesu, baada ya kuvikusanya sasa vitake ivyo vitu kwa damu ya Yesu ya pasaka.

* Muhimu sana kusikiliza maelekezo ya roho mtakatifu, maana 100% tunafaili katika maelekezo ya Mungu baada ya kuomba! tunaomba vizuri lakini katika maelekezo tunafaili. Biblia inasema wana wa Israeli walifanya kama neno la Musa kutoka 12:35 , kama wangekosea maelekezo wana wa Israeli usiku ule wangekufa.

unatamka kabisa kwa sauti ninaitambua damu ya Yesu, ninajua uwezo wake, ninaiamini damu ya Yesu,na moyoni uwe unaiamini kweli Mungu huangalia moyo si mdomo, soma ili somo utafakari sana ndipo utaielewa na kuamini

kutakuwa rahisi, unasema naachilia damu ya Yesubya pasaka katika kifungo changu....... unakitaja. unaanza kukusanya vitu vyako vilivyopotea kwa damu ya Yesu ya pasaka, sema uchumi wangu ninakukusanya popote ulipo kwa damu ya Yesu ya pasaka,

 ndoa yangu ninakukusanya kwa damu ya Yesu ya pasaka. kisha sasa ninafungua vifungo vya uchumi wangu kwa damu ya Yesu ya pasaka. ninafungua biashara kwa damu ya Yesu ya pasaka... na kuendelea na kuendelea. omba haya maombi kwa juhudi, kwa hasira ya roho

 mtakatifu vitake kwa kumaanisha, omba maombi haya usiache mpaka mzigo umeisha, mpaka maombi yamekukaukia. baada ya hapo uwe makini kusikiza maelekezo ya Mungu. maombi haya ni ya siku moja. bila kusahau kufungua ilo lango juu ya ardhi na chini ya mbingu zako,

 vifungo vyote vikubwa hufungwa juu ardhi na chini ya mbingu, sema naachilia damu ya Yesu ya kufungua kifungo hiki... juu ya ardhi na chini ya mbingu zangu, nakuweka huru kwa damu ya Yesu.ni muhimu sana wakati huu kutokukengeuka au kujichanganya, watu wengi tunajisahau tunaongea sana,

 tunajiiingiza sehemu ambazo sizo,tunamitandao mingi inayoondoa uwepo wa Mungu, tunakengeuka, matokeo yake unafungua laana, malaika anapoaanza kukufungua mara umeingiza laana. linda wokovu wako, weka mambo yote pembeni dili kwanza na tatizo lako. pia vizuizi vikubwa vya maombi ni vifungo vya nafsi, roho, na mwili hakikisha uko safi hujambeba

 mtu moyoni, huna uchungu ndani yako, huna hasira ndani yako, uko huru wala huna kizuizi cha maombi. na usipoe unapoanza hadi umemaliza. ila hakikisha sana sana unasikiza kwa makini maelekezo ya Mungu. na kuyafuata wengi tumeanguka hapo. nikutakie mafanikio mema kwa jina la Yesu.

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA