KILICHOMEZA MAISHA YAKO

Somo fupi; "kilichomeza maisha yako"

Bwana Yesu asifiwe!

"SABABU KUU MBILI YA MAISHA YAKO KUMEZWA"

i)kutoka nje ya njia ya Mungu,kutoka kwenye ramani ya Mungu/ au kwenye kalenda ya Mungu (MUNGU KUMEZA)

ii)maonevu ya ibilisi sababu ya wewe kutokuwa na nguvu za kiroho. (IBILISI KUMEZA)

Mungu wetu atukuzwe!

KUTOKA NJE YA RAMANI  YA MUNGU

Watu hawapendi kusikia kuwa Mungu ndo amewazuia wasifanikiwe! na watu wengi hawapendi kusikia wao ndio wamehusika kuzuia kufanikiwa, yani unapoongea hayo wanata mani wakurukie wakurarue! ndo mana saa ingine hata hapa baada ya kuandika somo flani

Neno likampiga mtu hujawa na hasira na jaziba anajikuta akinipinga kwa njia ambazo sitaziandika hapa! lakini kwa kuwa si mimi nimesema ni Mungu basi najua wanashinda na na Mungu hawashindani na mimi! Mungu wetu wa rehema! amesamehe na kusahau! Wengi hupenda kusikia Ibilisi ndo

Kasababisha! vita kati yetu sisi na ibilisi ni vita rahisi sana, vita kati yetu sisi na Mungu ni ngumu, maana Mungu ana njia zake za kukurejesha katika mstari na lazima uzipitie na hazikwepeki! Tunasema haya ili upone ukishapona sasa Mungu ataachilia kile kilichomezwa.

Katika maisha Mungu saa ingine akiona unaenda njia isiyofaa, au nje ya mpango wake na amekuonya husikii, basi Mungu humeza kitu chako kimoja tuu, ili umrudie yeye! usipomrudia hakiachii mpaka
aone sasa uko tayari

Kumsikiza ndipo sasa anaanza kusema, saa ingine Mungu ana draw attention kwa lazima,anajua uyu nikimbana katika uchumi, au asipate mtoto, au asiolewe kwa muda kwanza, au niondoe maelewano katika ndoa yake atanikimbilia kunitafuta kwa gharama, au

Hicho kinachomfanya anikatae nakiondoa kwanza kisha baadae nitamrudishia! kwenye kitabu cha ufunuo Mungu akasema nawe utubu usipotubu naja kwako upesi nakuondoa kinara chako! kinara maana yake ni kitu  kinachokuheshi misha au umekifanya cha thamani kabla yaMungu anajua huyu nikimnyima hiki au nikikio ndoa basi kiburi kimeisha! ataanza kunisikiza. Bwana Yesu asifiwe!

Tuangali neno!
Yona 1:3 - 4
3 Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa Bwana.
4 Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika.

wengi wanafahamu hii stori Yoha alipewa ujumbe wa Mungu apeleke ninawi yeye akaamua kutokwenda kwa iyo akawa anakimbia uso wa Mungu! akaenda zake Tarshishi! Yona alikuwa nje ya mpango wa Mungu! nje ya ramani ya Mungu! kila mtu hapa duniani anaenda au kuishi kutokana na ratiba ya Mungu,

Hivyo kama hujui muelekeo wako maisha ni muhimu kumuuliza Mungu kitu ambacho Mungu amekupangia ufanye au kibali chako kipo wapi! Bwana Yesu asifiwe! kwa Yona alimkimbia Mungu! ni kama vile Mungu anavyokuonya kisha wewe unaamua kumkimbia Mungu, unaamua kumsusa Mungu na unasema lolote na

liwalo na liwe nishaomba sana Mungu amekaa kimya! ivyo nitaishi kama navyotaka mimi sitamfuata Mungu tena.na huyu Yona ukifuatilia maandiko ni yule ambaye alikufa nabii Eliya alimlalia juu yake akafufuka tena! Kama utakumbuka stori hii katika biblia! Kwa iyo Mungu aliwekeza kwake na utaweza kuona au kujifunza kitu cha Mungu

vina upinzani mkali sana, shetani alishamuua Yona akiwa mtoto lakini Mungu akam rudisha kupitia nabii Eliya! ivyo ukiwa unakibali chochote cha ki Mungu jua utapigwa vita usione ajabu vita unavyopitia jua unaki tu cha Ki Mungu si lazima uhubi ri kama hivi watumishi kibali kinaweza kikawa katika ndoa kuna watu ndoa zao Mungu

Kazipa vibali kufyatua watoto wa maana,watumishi wakubwa ,viongozi katika nchi wenye hofu ya Mungu ivyo ibilisi ataku pinga usikutane na mtu sahihi, Yona akajikuta ametupwa bahari tumboni mwa samaki ili apate mda wa kumsikiza Mungu! ni kama wewe sasa jinsi ulivyo pengine umemezwa, kiuchumi, kindoa, biashara, hatua, afya ili kwanza upate mda wa kuomba rehema na

uanze kumsikiza Mungu. kuna watu hawamsikii Mungu mpaka wapate mapigo ya Mungu, viboko vya Mungu ndipo sasa anakuwa tayari akiambiwa sasa geuka kushota atageuka kwa nguvu zote! Halleluyah!

Paulo pia alijikuta matatizoni, Yesu alimuambia wewe nimekupangia uhubiri injili kwa mataifa, na Petro nimempangia ahubiri injili Jerusalem, Paulo akawa anabishana na Yesu, akaenda kuhubiri Jerusalem siku moja wakamkamata Bana walimtandika viboko 40 kasoro 1 , wakamtupia kwenye mtaro,

Walimchapa na kumfunga kumbeba na kumpeleka mji mwingine wakamwacha huko, huko alipopelekwa kumbe ndipo Yesu alimuambia akahubiri! akashangaa kule akihubiri anapata matokeo makubwa! mpendwa ni vizuri kumtii Mungu tusiende kwa viboko kama Paulo,au Yona baada ya kutapikwa na samaki pale ufukweni

Alipokuwa mpaka ninawi ilikuwa ni mwendo wa siku 3, lakini Yona alitembea mwendo wa siku moja, si mchezo kukaa tumboni mwa samaki siku 3, yani manake Yona alifungishwa tatu kavu tumboni mwasamaki, ukisoma hiko kitabu inaonekana Yona hakujua hata yuko wapi maana yeye akasema Mungu alimwingiza shimo la kuzimu kumbe ni tumboni mwa samaki Bwana Yesu asifiwe sana!

Sasa uyo ni Yona kwako wewe leo hii Mungu atameza kitu chako kimoja ili urudi katika mstari na unapoomba sana na unaona bado unapata vita jifunze kumuuliza Mungu kwani ni upinzani unaendelea? utasiki a sauti inakuambia Omba rehema. usije ukasema aaah mimi ni mtakatifu sijamkosea Mungu au hainuusu. usijihesa bie haki maana hujui Mungu ndo anayejua. Halleluyah!

"MAONEVU YA IBILISI SABABU YA KUKOSA NGUVU ZA KIROHO"

Kama jinsi vile  Yona alimezwa na samaki, ibilisi pia humeza vitu vya watu! tuangalie maandiko!

zaburi 56:1-2
1 Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza, Mchana kutwa ananionea akileta vita.
2 Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa, Maana waletao vita juu yangu kwa kiburi ni wengi.

1Petro 5-8
8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

Ayubu 20 - 15
15 Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake.

Shetani humeza vitu vya wengi sana, na Mungu akimeza kitu chako ni kwa mda kwa nia ya kukurudisha katika mstari wa kwake au kukuleta kwenye ramani yake! lakini ibilisi anameza ili kuyaharibu maisha yako, na anaweza meza toka

Ukiwa mtoto, amemeza vitu vyako, unajua tunashinda vita kwa maarifa na hekima ya kumshinda ibilisi! ivyo baada ya maombi !shetani ataachilia kila kitu alichokimeza, shetani anaweza meza kizazi na usipate watoto, anaweza kumeza kazi yako, usipate kazi, anaweza meza ndoa yako ndoa

ikawa inasumbua yenye misukosuko mingi, anaweza meza hatua zako, ukawa hupigi hatua, anaweza meza cheo chako na hupati promotion kazini, anaweza meza nyota yako na hii ndo imeathiri watu wengi sana. sasa kitu kilichomezwa huwa hakitafutwi bali kinaamriwa kitoke tumboni mwa adui, ndio maana kitabu

Cha Ayubu anasema naye amemeza mali atayatapika tena atayatoa tumboni mwake! baada ya kusoma nakuelewa hapa tutaweka maombi nakuhakikishia Mungu mwenyewe atamtapisha shetani apende asipende lazima atapike na vitu vyako vitaachiliwa kwa jina la Yesu,

wengine nyota zao za biashara shetani kazimeza, gafla biashara ya mtu inaaanza kuyumba!swala si hali ya uchumi no unapotembea na kibali cha Mungu nakuambia ardhi na Mbingu zako hulazimishwa kukutii ivyo mafanikio ni lazima. Embu nikuulize mfano ungepewa kazi

Ya kazi ya kumtafuta Yona ungempata wap? ukiienda juu ardhini usingempata! angani usingempata, hata baharini kwenyewe ungempata wapi na mtu yupo tumboni mwa samaki, hata wale waliomtumbukiza Yona baharini walijua amekufa! hawakujua kama amemezwa na samaki! hata ukijua amemezwa na samaki ungejua

ni samaki yupi? je kuna samaki wangapi baharini? ivyo ndivyo shetani humeza vitu vya watu na wao wanavitafuta kwa maombi kumbe haviko. kwa iyo kitu kilichomezwa kinaamriwa kitapikwe maana ukikitafuta huwezi kukipata. Halleluyah! Halleluyah!

JINA LA BWANA LIBARIKIWE!

tunaenda kuomba sasa!

15 Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake.
Ayubu 20:15

Baba katika jina la Yesu asante kwa ufunuo huu! nami nimejua leo ya kuwa kwa kusudi Yona kurudi katika mstari katika ramani yako kufanya kile ulimchomtuma ilibidi Yona aingizwe ndani ya tumbo  la samaki! yawezekana Pia maisha yangu yako tumboni mwa samaki! ndoa yangu!

Elimu yangu! kazi! biashara! vibali! hatua zangu, na hatima ya maisha yangu pia ipo tumboni mwa samaki sababu ya kutokufuata maagizo yako! sababu ya kutozishika sheria yako! Baba wa utukufu Mungu wa utukufu! Mungu Mtakatifu wa Israeli Mungu uyashikayo maagano ya watu wako! Eee Bwana!

Ninaomba unirehemu katika jambo lolote nilililolifanya na leo hii umemuamuru samaki ayameze maisha yangu mpaka nitakapo kuwa tayari kukusikiza njia zangu mbaya njia zangu ovu zenye dhambi unirehemu unisamehe katika jina la Yesu, mashitaka yoyote mbele zangu Mungu naomba unirehemu unitakase kwa damu ya Yesu, 

Unitakase kwa damu ya Yesu! unitakase kwa damu ya Yesu ninakiri ya kwamba siyajui maisha yangu lakini najitoa mbele zako Mungu Baba wa mbinguni kwa ajili ya utakaso kamili, wala sijui ni lini au saa ngapi nilikutenda dhambi lakini nachojua kwako Mungu wangu wa kweli kuna utakaso kamili! naja mbele zako Baba naomba rehema juu dhambi zangu zote naomba unirehemu naomba

Unitakase kwa damu ya mwanao Yesu,takasa maisha yangu yote kwa damu ya Yesu, naomba unihesabia haki tena kwa damu ya Yesu, Ee Mungu Baba Yona alipotoka tumboni mwa samaki alikuwa tayari kukusikiza alikuwa tayari kukufuata na alikuwa tayari kukutii nami katika jina la Yesu kwa uweza wa Roho Mtakatifu niko tayari sasa kukufuata niko

Tayari kukutii, Ee Mungu Baba Yona alikaa siku tatu tumboni mwa samaki, lakini mimi Mungu Baba wewe ndo unayejua nimekaa mda gani! Ee Mungu nakuomba uwe na rehema nami sasa katika jina la Yesu, naomba umuamuru samaki sasa anitapike kwa jina la Yesu atapike kazi yangu, atapike ndoa yangu, atapike uchumi wangu, atapike elimu yangu, atapike mafanikio yangu, atapike yule mtu

Aliyemwandaa katika ndoa, atapike kitu chochote ambacho alikimeza katika jina la Yesu, atapike hatua  zangu sasa, atapike ufahamu wangu, atapike kisu cha kukatia kamba za mauti, atapike panga na shoka la kukata minyororo yote katika maisha yangu, katika miguu yangu, katika mikono yangu, atapike majibu yangu, atapike nyumba yangu, viwanja vyangu, atapike huduma yangu

Katika jina la Yesu! Ee Mungu Baba ninaomba sasa maisha yangu yaliyomezwa na samaki yatapikwe sasa! yatapikwe sasa! yatapikwe sasa katika jina la Yesu Kristo! vyote ambavyo nimevitaja ambavyo sijavitaja ee Mungu Baba ninaomba sasa vitapikwe katika jina la Yesu. Baba asante kwa neno lako katika kitabu cha Ayubu kwa kutujulisha ya kuwa Ibilisi ndio aliyomeza maisha yetu, asante kwa ahadi yako

Mungu ya kumtapisha ibilisi chochote alichokimeza umesema lazima avitapike! Neno lako hili katika kitabu cha ayubu 20:15 neni hili ni Roho nami nawakiri hao roho wa Mungu wako juu yangu sasa, neno lako ni makaa ya moto, uweza huo uko juu ya ulimi wangu sasa, neno lako ni silaha hatari ni shoka, nyundo, ni upanga, ni moto ulao, neno lako ni mamlaka ya kumtapisha ibilisi ee Mungu Baba nami

Sasa katika jina la Yesu nakutangazia adui yoyote uliyemeza maisha yangu lazima utapike, neno la Mungu linasema utatapika ulichomeza ibilisi, Mungu atakutapisha! enyi mawakala wa ibilisi, majoka ya baharini, mliomeza kizazi changu, wafalme wa giza , wakuu wa giza, mizimu ya ukoo, wachawi , waganga wa kienyeji, mapepo, majini, jeshi la pepo wabaya, malkia wa kuzimu, mfalme wa kuzimu,

Malkia wa anga, na woote pamoja na roho chafu  za ibilisi wote waliomeza vitu vyangu kwa damu ya Yesu, katika jina la Yesu,naongea na wewe kwa damu Ya Yesu, wewe uliyemeza ajira yangu, wewe uliyemeza, biashara yangu, wewe uliyemeza hatua zangu, wewe

uliyemeza kibali changu, wewe uliyemeza elimu yangu, wewe uliyemeza mwezi wa ndoa, wewe uliyemeza ndoa yangu, wewe uliyemeza mafanikio yangu, wewe uliyemeza huduma yangu, wewe uliyemeza hatma yangu nzuri ya kimungu ndani yangu, wewe uliyemeza familia yangu, wewe uliyemeza afya yangu, wewe yoyote katika ulimwengu wa roho ninatuma damu ya Yesu

Msako ndani ya tumbo la adui aliyemeza mambo yangu, aliyemeza vitu vyangu katika jina la Yesu, kwa mamlaka ya jina la Yesu nakuapisha adui! nakuapisha adui! kwa damu ya Yesu kwa jina la Yesu! kwa neno Ayubu 20:15 utapike sasa vitu vyangu utoe vitu vyangu katika ilo shimo kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu, wote waliomeza vitu vyangu watapike sasa

Ninaingiza damu ya Yesu ya kichefuchefu katika matumbo yao katika jina la Yesu, nageuza vitu vyangu tumboni mwa adui kuwa makaa ya moto kwa jina la Yesu, nawaletea kichefuchefu maaadui  zangu naaamuru watapike sasa kwa jina la Yesu, nawashambulia kwa moto, nawaponda kwa nyundo, nawapiga mishale ya moto! nawafyeka sasa kwa upanga na shoka la Mungu kwa jina la

Yesu, ninakamata wachawi wote kwa damu ya Yesu, nawasambaratisha kwa damu ya Yesu! ninaamuru vitu vyangu vitapikwe sasa! vitapikwe sasa!  vitapikwe sasa! katika jina la Yesu kwa damu ya Yesu, ninawafunga kwa moto ! ninawatesa kwa moto mpaka watapike vitu vyangu, ninawaangamiza kwa moto katika jina la Yesu Kristo! kwa

Damu ya Yesu. hayo matumbo ya ibilisi yenye vitu vyangu nayanywesha damu ya Yesu! nayanywesha damu ya Yesu! ya kichefu chefu katika jina la Yesu, kwa jina la Yesu! kwa damu ya Yesu! nimekutuma malaika wa Bwana ukawatapishe! ukawatapishe! kwa sheria ya mbinguni Ayubu 20:15 katika jina la Yesu asante Bwana Yesu

*rudia maombi x 7

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA