KWANINI MUNGU AWEKEZE KWAKO?MUNGU ANAPATA FAIDA GANI KUWEKEZA KWAKO?
Somo: "Kwanini Mungu awekeze kwako? au Mungu anapata faida gani kuwekeza kwako?"
Bwana Yesu asifiwe sana watumishi/ makuhani wa Yesu?
JINA LA BWANA LIBARIKIWE!
*Hili somo ukilielewa tuu ume umevuka maeneo yote soma taratibu kila neno!
Kabla ya kujua kwanini au kujibu maswali hapo juu ningependa tujifunze kitu kimoja? Kwanini Mungu aliiumba Dunia na kukuumba wewe ndani yake?
Mungu alitumia mda wa siku tano kuumba dunia! na siku moja kumuumba binadamu! ushawahi jiuliza kwanini Mungu alitumia mda mwingi kuumba dunia?
Kusudi la Mungu kumuumba binadamu kumweka katika dunia ni kitu gani? kwanini asimwache tuu huko huko mbinguni? kwanini aje amtenge duniani?
Kwanini Mungu amewekeza sana kwa binadamu, mpaka akamtoa mwana wa pekee?Yesu kwanini ahangaike kukutengezea mazingira mazuri hapa duniani?
embu tuangalie uumbaji wa Mungu. > MUNGU > NCHI > ADAM > IBADA
> MUNGU- Tuangalie kuhusu Mungu kidogo
zaburi 22:3, Ufunuo 4:8-11, Zab 150:6
zaburi 150:6
6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.
zabu 22:3
3 Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.
ufunuo 4:8-11
8 Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
9 Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele,
10 ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,
11 Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.
*Mungu hukaa katika sifa! Mungu kule mbinguni ana mamillion ya malaika wanamsifu na kuabudu mchana na usiku. Mungu kuishi kwake kwategemea sifa.
Yani kusudi Mungu aishi vizuri lazima apate sifa, sifa tuseme ndio kila kitu kwa Mungu, kusudi la Mungu kuumba mbingu na viumbe vyake, kusudi Mungu kuumba malaika ni ili apate sifa.
Mungu sasa akafikiria akawaza akaona kule mbinguni ndio kuna malaika lakini hawa malaika ni watumishi wangu, ivyo akaona sasa azae watoto na kazi ya iwe kumsifu yeye.
Basi Mungu ndo akaja na masterplan ya kuumba ulimwengu! na kuweka viumbe wote ndani yake. Mwa 1:26-28, zab 8:4-8, Josh 1:3-5, kumb 8:6-18
> NCHI
Mwanzo 1:26-28
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi
* Kabla ya Mungu kumuumba binadamu Mungu aliumba kwanza mazingira alidesign ule mchoro aliumba ulimwengu kwa mda wa siku 5, Na Mungu alijalia sana mazingira sababu
alitaka kuhakikisha binadamu anakaa sehemu salama, anakaa comfortable! alitaka kuhakikisha uyu binadamu anakula anashiba, analipia ada ya watoto bila mawazo.
anaendesha gari nzuri, kama ni biashara basi ni biashara ya kimataifa, kama ni kazi basi awe Director! yani upate kila kitu the best ili ustarehe, friji limejaa vinywaji aina zote.
nyama za aina zote unafanya kuchagua, kama ni nyumba basi kila chumba kina sebule na study room full master, wafanyakazi ndani wa kutosha
hata wa kusogezea kikombe cha chai mdomoni, uwe full comfortable yani hali ya juu. alafu uwe na amani. na mali zako, na watoto wako wawe na afya ndoa yako iwe nzuri uinjoy.
Kwa iyo Mungu anajali sana mazingira yako wewe, kuliko kitu chochote na amewekeza sana ili wewe uwe comfortable ukiwa hapa duniani. ndo mana
aliumba ulimwengu kwa mda wa siku tano. lakini wewe siku moja tuu, ndani yake akaweka miti, wanyama, samaki ndege, jua , mvua, bahari mito maziwa
vyote vimekuwa design kwa
ajili ya binadamu afurahie kuwepo kwake hapa duniani. uinjoy usiishe kwa shida au masononeko! ufurahie maisha! uishi ukimtukuza Mungu pekee
> ADAM
2 Kor 9:8, Fil 4-19, Kumb 15:4, Math 8:17
2 kor 9:8
8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
Fil 4-19
19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
Mathayo 8-17
17 ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.
Kumb 15-4
4 Lakini hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa Bwana atakubarikia kweli katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;)
*Hapo tunaona ya kuwa Mungu hakumweka binadamu ili ateseke bali alimuweka kusudi binadamu a starehe, ibilisi baada ya kugundua siri hii kuwa Mungu anakaa katika sifa
kuishi kwake Mungu kunategemea sifa ibilisi akasema kwa kuwa amenifukuza mbinguni na niko dunia basi mimi nitamlipishia Mungu kisasi indirect
nitampiga Mungu indirect, nitafinya watoto wake, nitawafinya kwa kuwaletea magonjwa, nitawafinya kwa kuvuruga ndoa zao. nitawafinya kwa kuwafunga ili wasifanikiwe
wawe na maisha magumu, wasipate watoto, wasipate ndoa, wasipate kazi, nitawafukuzisha kazi, nitafunga biashara zao, nitawaondolea amani hawa watoto wa Mungu,
kule mbinguni siwezi kulipisha kisasi lakini kwa kupitia hawa watoto wake nitamfinya Mungu indirect. akijua kabisa baada ya kukuletea mateso, magumu, taabu, shida, mapito moyo
lazima utainama tuu. kwa iyo unapoumia hata Mungu anaumia! kwa iyo vita vyote unavyovipata ni ili kumuumiza Mungu haulengwi wewe. anayelengwa ni Mungu. wala
shetani hana ugomvi na binadamu bali anaugomvi na Mungu. anajua kwa kuwa hawezi kurudi mbinguni kulipisha kisasi ila anaweza lipisha kisasi kwa kuwagusa
watoto wa Mungu, kugusa ndoa zao, kugusa elimu yao, kugusa amani yao, kugusa uchumi wao lazima watoto wa Mungu watapiga kelele! kusababisha uchungu kwa binadamu Mungu
lazima ataumia tuu. maana Kumbuka Mungu amewekeza kwako.
> IBADA
Yoh 4-23-24, Kumb 28:47
Yoh 4-23-24
23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Kumb 28:47
47 kwa kuwa hukumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote
*Umeona hapo sasa Mungu alicholenga katika mzunguko ni kupata ibada katika roho na kweli. Na ibilisi naye analenga Mungu asipate ibada katika roho na Kweli ndio maana ibilisi
anamuumiza binadamu kwa kumpandikizia mateso madeni magonjwa, vifungo,vifo kutokufanikiwa , kutokupata ndoa, kivuruga ndoa yako, kufunga matumbo yasipate
watoto kuleta cancer, kuleta ukimwi, umasikini, ufukara, maisha magumu maana anajua katika hali iyo ibada yako wewe haiwezi kuwa katika roho na kweli utaabudu utakuwa
kanisa lakini moyo wako hauko pale moyo wako unawaza madeni moyo wako unawaza tatizo katika ndoa, moyo wako unawaza utakula nini? moyo wako unawaza utapata wapi
ela za kupeleka gari kwa fundi, moyo wako unawaza school fees za watoto moyo wako umekamatwa sehemu ingine kwa iyo hata sifa zinazotoka katika moyo wako kwa Mungu
si katika roho na kweli. Bwana Yesu asifiwe. Mungu kukuandali mazingira yote hayo mazuri yani school fee, huna pressure ya watoto, umeme ushalipa, maji ushalipa, friji
limejaa mboga za aina zote, nyumba nzuri ya kuishi wewe
na mwenzi wako, watoto wana afya, gari umeshaweka mafuta, na ndugu zako unawasaidia hakuna anayekusumbua, kwenye account kuna pumua yani hakuna shida ndogondogo
ushatoa fungu la 10 wala Mungu hakudai tena. yani unamaisha bora moyo wako unaamani haumwi uko fiti uko
sawasawa hapo hata ukienda
kanisa ukisifu utasifu katika
roho na kweli maana imeandikwa wanaomuabudu Mungu inawapasa kumuabudu katika roho na kweli. yani manake maombi yako yasiwe na malalamiko! yani moyo
wenye uchungu, wenye kilio, mateso, hata ukiomba na kuabudu basi hayo maombi au hizo sifa za Mungu huenda ivyo ivyo sasa inamsumbua Mungu kule mbinguni. ni kama vile upo
kwenye nyuma safi umekaa umepumzika alafu mtu anachoma takataka moshi unaingia ndani unajisikiaje? Mungu katika nyumba anahitaji avute pumzi za ibada na sifa
katika roho na kweli.
Halleluyah! kwa iyo ugomvi wa Mungu na shetani upo hapo katika ibada, na kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani ni ili umfanyie Mungu ibada that is
PRIMARY REASON, Mungu hakuketa uje unywe bia, uje uzini, au ufanye uasherati, Mungu hakukuleta uje ujifurahishe na mali za Mungu au ujisifie, yani Primary Role ni
ibada katika roho na Kweli ndio kusudi kuu la Mungu la wewe kukuleta hapa duniani. ivyo vyote anavyokupa ni ili uwe comfortable umfanyie Mungu ibada katika roho na kweli,
Mungu anathamini ibada toka kwako na sifa zako kwake sababu wewe ni mwana na malaika ni watumishi kuna tofauti kati ya sifa inayotoka kwa watumishi na sifa
inayotoka kwa mtoto. Ndio maana akukuweka Duniani.Bwana Yesu asifiwe sana.
sasa Mungu anakuangalia anapokuona unajuhudi au
umeongeza bidii kumfanyia Mungu ibada ndipo husema uyu ana manufaa kwangu, huyu anafaida nikimtolea tatizo la
uchumi, ndoa, tatizo la kutokupata kazi tatizo analopitia atafanya ibada zaidi maana atakuwa huru zaidi basi hapo malaika hutumwa nendeni mkamwagilie uyu uchumi wake,
ndoa yake kampuni yake, biashara yake, maana huyu ananifaa sana! maana nikumuondolea hili tatizo atakuwa huru zaidi! atazidisha mda wa kusifu na kuabudu.
Bwana Yesu asifiwe sana.
Katika makabila yale 12 ya Israeli kuna kabila mojawapo kazi yao ilikuwa ni kuleta uwepo wa Mungu yani kukaa madhabahuni pa Mungu, wao
walikuwa hawalimi au hawavui samaki! wanaume walikuwa wanakaa madhabahuni pa Mungu,wanawake wanawapikia na kufua nguo, wakinena kwa Lugha, wakisifu, wakiabudu, wakitafakari neno kazi yao
ilikuwa kuleta uwepo wa Mungu sasa uwepo wa Mungu unaposhuka eneo hilo ndipo yale makabila 11 yanafanikiwa wanapata maziwa, wanapata mazao bora , matunda, nyama.
Mungu akasema hawa kazi yao ni kuleta uwepo wa Mungu kwa hawa 11 wanaofanikiwa lazima wapeleke sehemu ya kumi, lazima wapeleke malimbuko nyumbani kwa Bwana maana
nyie makabila 11 mnafanikiwa sababu ya uwepo wangu, uwepo wangu ukiondoka hamuwezi kuvuna tena. sasa hili kabila lilikuwa likiishi maisha ya kifalme wao kila kitu
cha kwanza kile first ndicho wao wanapata kwanza. kama ni maziwa basi kabila la hili kwanza, kama ni sufi basi kwao kwanza kama ni nyama wao kwanza maana walikuwa
wanafanya kazi kubwa ya kuleta uwepo wa Bwana. sasa ilo kabila asili yake ni la Daudi na ndio ukoo huohuo wa Yesu. na ndio wewe sasa Bwana Yesu asifiwe sana. Kwa iyo
unaongeza mda wa kuabudu katika roho na kweli , kufanya ibada na wewe umeokoka basi Mungu huamuru mataifa kukuletea baraka. Maana wewe ni kabila lilelile na ambayo pia ni asili
yake na Yesu. Halleluyah! Halleluyah! Bwana Yesu asifiwe .kwa iyo ukijijengea kwenda kwa Mungu kwa staili hii lazima Mungu atende! mwambie Mungu ukiniondolea tatizo
langu la uchumi, ndoa, biashara , kazi nitakuwa uweponi mwako maana hili linanizuia kufanya ibada katika roho na kweli. Sasa Mungu hujua kesho yako akiona unamdanganya anakaa
kimya! au anakujaribu na kitu kidogo labla anakupa gari tuu kisha anakuangalia kama utaongeza mda wa ibada au vip? je utafanya katika roho na kweli hakuna ambaye
amemuendea Mungu katika mfumo huu na Mungu akakaa kimya maana anajua akiwekeza kwako anapata kitu. Bwana Yesu asifiwe sana. chunguza hata wanaojitoa kufanya kazi
ya Bwana mda mchache unakuta wana majibu yao tayari. mimi nimewaona wengi tuu.Bwana Yesu asifiwe sana
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment