MADARASA YA MUNGU
Somo: "Madarasa ya Mungu"
Bwana Yesu asifiwe sana!
Ezekiel 36:26-27
26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.
27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
√ Mtu kubadilishwa Roho ya jiwe kwenda Roho ya nyama si kitu cha siku moja, si kitu chepesi wala hili
neno usikichukulie rahisi kiasi hiko! kusudi hili somo uelewe vizuri na likusaidie unapoendelea kukua kiroho basi, fuatilia lile
√somo la "maisha ya mtu yaliyomezwa" . Its process ya mda mrefu! sasa inategemea na mtu mwenyewe! kuna wale
wanaobadilishwa alafu hawataki kubadilishwa na Mungu hawa ndio hukaa kwenye majaribu mda mrefu, kuna ile hali ya kujua hili ni
√darasa la Mungu ni kitu kimoja na kuna ile hali ya kutokujua nayopitia ni darasa la Mungu. na ivyo mtu wa aina hii ataendelea kupambana na
ibilisi na asijue, matokeo yake hukata tamaa. kwa iyo kutokujua au kutokuwa na ufahamu wa aina hii basi hupelekea mtu akakaa kwenye jaribu mda mrefu.
√Mungu kama amekuandikia kitu kikubwa huko mbele Mungu hawezi kukupa bila kushughulika na moyo wako! chochote kile ambacho
Mungu atataka kukupa lazima ashughulike na moyo wako kwanza! sasa si kazi nyepesi na sio rahisi! ila kama utakuwa umepata neema ya kumuuliza
√liza Mungu kuhusu wewe na nini kinaendelea kuhusu maisha yako basi. Mungu huongea! ukiwa na ukaribu na Mungu atajifunua kwako na mambo mengi utayajua. Bwana
Yesu asifiwe sana. Kwa iyo moyo wa mtu hugeuzwa kwa madarasa ya Mungu. Ndio maana ya kuweka lile neno pale juu. Mungu hawezi kukupa roho yake ndani yako ikiwa
wewe hauko tayari.ndo mana Mungu akiona mtu hamsikii huwa anaachia mapigo kwanza yampige yamtandike mtu kisawasawa akija
tulia sasa Mungu ndipo huanza kuongea. Tuangalie mifano ya madarasa ya Mungu sasa.
√i. Darasa la unyenyekevu
Mungu akigundua huna moyo wa unyenyekevu.Mungu huwez a kukuletea ile hali ya kutamani kuwa na kitu flani! alafu huo uw ezo
Mungu hukuondolea,mfano kuna ile ya kutamani kuwa na mme bora mfano kuwa na mais ha mazuri, kuwa na vitu vizuri kiasi cha kwamba ukiviona moy o hukulipuka
na huo uwezo hun a! unabaki kimya tuu! Mungu hu weza ruusu hali iendelee ndani yako kwa mda mrefu, inapoend elea kwa mda mrefu yale mau mivu ya kutokuwa nacho unaa
nza kuyazoea taratibu unaanza kujipa moyo, hata nisipo kipata nina Mungu wangu! kwa iyo hali itakuforce ujifunze kushukuru na icho ulichonacho! iyo hali
itakusababisha u appreiciate unacho kipata, na itafikia sehe mu itakupelekea kutambua Mungu ndo hugawa kila kitu kwa kila mtu.ile hali kukubali sina na niendeleee
kusubiri au yale maumivu Mungu huyatumia na automatic unyenyekevu utazaliwa ndani yako. Hapo sasa Roho wa unyenyekevu huja kukaa juu yako.
√ ii. Darasa la kuvunja tamaa ya juu iliyoko ndani yako
Kuna ile hali ya kutamani kila kitu, kutokudhamini ulichona cho, kutaka more and more, kama una moyo wa namna hii huu ni moyo wa jiwe. Mungu anajua kabisa mtu wa
namna hii kama nikimpa mke au mme atamsumbua! kwa iyo anaanza kudeal na moyo wako, formula ile ile ya kwanza Mungu huwe za itumia katika mazingira tofauti, Mungu huweza kukuta
manisha vitu vizuri moyo wako unavyovitaka vingii alafu uwezo wa kuvipata anakuondolea, ile tamaa moyoni mwako anaiacha ikue ikue
mpaka igeuke maum ivu, ikishageuka maumivu sasa wewe mwenyewe utatafuta jinsi ya kujiganga, na utaanza kuona hata nisingekuwa navyo lakini si ninaishi,
ile tamaa ya juu huo ndoka kwa sauti ya Mungu nda ni akikuonyesha kuwa umekiko sa hiki kwani umekufa? mbona haumwi? una afya,
vip kama ni kikupa ugonjwa na kile ambac ho unakililia? umekikosa hiki lakini una mimi Mungu, taratibu moyo huanza
kubadilika na ile hali ya kukiko sa inakuwa covered na nafasi ya Mungu. hii pia Inamsaidia Mungu atakapo kupa iko kitu unachokitaka
basi usije abudu iko kitu ukamuacha Mungu, yani Mungu hutofautisha nafasi yake na iko kitu unachokipenda. kwanza unakikosa
alafu iyo na fasi inajazwa na Mungu. kisha baadae sasa Mungu ndo anakupatia na moyo wa tamaa wa juu hapa umeondoka.
√iii. Darasa la Mungu la uvumilivu.
Hapa ndipo pagumu kuna mioyo ya watu haina uvumilivu, na inamaombi mengi sana kwa Mungu kabla ya Mungu kukujibu! Mungu
anaweza kukuletea yale wewe usiyotaka, yale unayoyataka ndio hayaji, mfano hupendi kugombana na mtu wa karibu yako! Mungu ndo
anamuinua juu yako alafu anakukasirisha unakasirika kwelikweli ukitaka kuanza kuomba anakukumbusha hujamsamehe
ndugu yako! au ile hali ya kutaka jambo lifanyike sasa ivi alafu Mungu ndo analichelewesha, lile ambalo unataka lifanyike baadae hilo ndo Mungu analileta. ile hali ya kutaka
jambo lisogee liende kwa spidi alafu ndo haliendi! ukiomba mengine yanaenda ilo muhimu kuliko lote haliendi alafu iyo hali
anaicha na wewe kwa mda! anapoicha kwa mda basi ile wewe huanza kuizoea taratibu inakuwa maumivu baadae inauwa hali ya
kawaida! sasa inakuwa si jambo hili tuu mambo mengi! ukitaka kukimbia anakuwekea mazingira ya kukurudisha. kidogo kidogo
unajenga uvumilivu ndani yako! Mungu hutumia situation iyo iyo unapiga nayo kelele kuondoa moyo wa jiwe.
√iv. Darasa la usikivu na utii
Hili Mungu wengi huwapitisha kile unachokiomba anakaa kimya mda mrefu! Utazunguka kila mahali utakuta Mungu yupo kimya! kama ni
uchumi mbaya utakuwa palepale, ni hali mbaya ya ndoa itakuwa palepale, kama unaumwa unashangaa unaombea mpaka na watumishi ambao wewe unaamini
wana upako alafu hali ndio iko palepale. hapa Mungu anakuforce uzame ndani yake uachane na mambo yote kwa mda mrefu kisha ataanza kuongea kidogo dogo na
kuacha kwa iyo itakupa hamu ya kuzama zaidi na kusikia na kutii tayari kupitia yale maumivu ya kunyamiziwa na Mungu mda mrefu yatakujengea msingi wa kuwa
msikivu na kutii. Hasa Mungu akakusemesha kwenye iyo ishu yako akakupa maelezo na ukatii na ukafanikiwa nakuambia ukitoka hapo utakuwa mtii maisha yako yote.
√ v. Darasa la kuondoa jiwe la kiburi na dharau
Mungu hapa mara nyingi humshusha na mtu au humfungia vibali vyake vyote! humshusha chini kabisa kama alikuwa juu. Na Mungu huwainua wale waliokuwa chini na
kuwafanya kumsaidia uyo aliyokuwa juu. Maumivu ya ilo tukio yatakufanya uwe mtii mnyenyekevu na mwenye heshima na kumueshimu kila mtu, kiburi chote na dharau yote hapa husuguliwa na
maumivu ya kushuka chini kuwa mavumbini kabisa unakuta unaenda zero kabisa alafu Mungu anakuacha kama miaka 2, alafu anapandisha maadui zako wote, na waliokuwa chini yako wote.
√vi. Lipo darasa la kuwa msiri/ Mungu anapokupa siri zake.
atakuwa anakujaribu kukufunulia mambo kisha ukiyasema anaondoa
amani yako au anakuondolea ujasiri, unakuwa una hofu kuu! kisha iyo hali anaweza iacha kwa mda mrefu. baadae katika kuombea
iyo hali iondoke ndipo atakuambia nilikuambia siri zangu wewe ukasema mbele za watu bila ruhusa zangu. Na jiwe huondoka.
√vii. Darasa la kuondoa hasira katika moyo wa Mtu.
Mungu aliongea nami akaniambia ukiaachana na mlango wa pombe na uzinzi, uasherati mlango mwingine ambao unaingiza mapepo
mengi kwa mara moja ni mlango wa hasira. maana hasira haitendi haki ya Mungu. Mtu mwenye hasira automatical ana uchungu, mtu mwenye uchungu hawezi kusamehe
dhambi, na asiye samehe dhambi Mungu hasikii maombi yake! tayari ilibilisi kapata mlango wa kupita. kwa iyo Mungu hudili na situation yako akitaka akomeshe iyo tabia
katika moyo wako ataleta situation zile zile ambazo wewe huwa huzipendi alafu wewe utakasirika, kisha sasa baada ya hapo izo situation atakuweka ufanye kitu cha
kujilaumu maisha yako yote! mfano umekasirika ukaamua kuacha kazi, baada ya kuacha kazi Mungu anafunga milango mingine ya
kupata kazi kisha anaachia maisha magumu hasa anakuacha kama mwaka mzima nyumbani, kisha sasa anakuja
baadae anakuonyesha haya yote ni matokeo ya hasira zako. au anakuacha uvunje uhusiano wa ndoa au uchumba kisha anakuacha
u deal na matokeo kwanza ingawa baadaye atakurudishia kila kitu kitakuwa sawa. Hapo jiwe litaondoka akijaweka roho wake sasa atakaa na utabadilika.
√ Hata wana wa Israeli walienda misri ili kutolewa mioyo ya jiwe kwanza Sisemi kila majaribu ni darasa la Mungu. Isipokuwa Mungu
bila kukuandaa hawezi kukupa chochote. Hata Yesu aliandaliwa, Mungu hawezi kukupa kitu chake kama
√unamoyo wa jiwe. unaweza kukuta unapambana na uchumu mbaya, ndoa yenye misukosuko, biashara ina madeni, misukosuko kazini,
hupigi hatua, au unaumwa hupati afya n.k na Mungu katika situation hizo hizo ndipo Mungu hutoa majiwe mioyoni mwa watu, wewe
huko utaita balaa, Mungu anaita darasa! Kumbe si
√tatizo kama linavyoonekana kumbe ni darasa la unyenyekevu, darasa la kuondoa kiburi, dharau,
kuondoa ukatili, darasa la kusikia Mungu akisema na kutii, ndo mana watu wakishavushwa katika majaribu huwa hawana majuto. mtafute mtu aliyepitia darasa la
Mungu na sasa amefanikiwa utakuta hana majuto kabisa sababu mwisho wa siku Mungu
√uongea kwanini aliruusu iyo hali na ilikuwa inamaana gani jina la Bwana
libarikiwe! kukueleza haya ni ili upate mda wa kijifanyia review! haina maana usiombe no! darasa la Mungu ni halisi ukikaa kimya
utaendelea kula kibano! ivyo lazima uombe mapepo yasikukalie na jinsi unavyoomba unamuonyesha Mungu hali hii siitaki! yani
√manake niko tayari kufanya vile unavyotaka nitoe katika hali hii. Na ndo maana ya maandiko kule juu "nitaondoa moyo wa jiwe, alafu
ataweka moyo wa nyama, baada ya hayo yote ndipo ataweka sasa Roho wake. Bwana Yesu asifiwe sana.
Mungu hawezi weka roho wake unayemuomba juu yako huku wewe unamoyo wa jiwe hapana haiendi ivyo. kipindi
√cha kutolewa moyo wa jiwe hutegemea na mtu mwenyewe kama ni msikivu na mtiifu. kwa iyo ukisema mimi na Mungu basi
sitamtafuta Mungu. Mungu anajua aaaha huyu pia ana jiwe la kiburi anazidi kuachia mapigo mpaka unyooshe mikono juu na kurudi
kwake. vitu vingi tunavyopitia ni madarasa ya kutolewa mawe ndani yetu. Nakwambia ukivuka na Mungu akikuelewesha na
√wewe mwenyewe ukayaona matokea utasema kama wengine waliovushwa Mungu yu mwema! Mungu yu mwema! Halleluyah!
Halleluyah! nami nitatoa moyo wa jiwe, nami nitaweka moyo wangu, nami nitatia roho wangu. jina la Bwana libarikiwe.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment