MAOMBI YA KUFICHUA YALIYOSITIRIKA NA YALIYOFICHWA
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
⭐Neno la leo litaenda kufichua mambo yote yamefichwa, ambayo yamesitirika, baada ya kukiri neno hili mambo mengi yatawekwa wazi mbele yako kwa uwezo wa roho Mtakatifu! Halleluyah!
Mathayo 10:26
Basi msiwaogope, Kwa maana hakuna neno lilisitirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana.
⭐ Mungu ataenda ongea baada ya maombi haya lakini ataangalia moyo wako! kuna watu hawezi kutunza siri za Mungu akizipata anazimwaga nje! au anatoka rohoni anaenda mwilini kumattack. Mtu! Roho wa Mungu akusaidie!
Maombi:
√Baba Mtakatifu wa Israeli, ninakusifu ninakuinua JEHOVA, kwa jina la Yesu Kristo wa nazareth, nimekuja mbele zako kwa ajili ya utakaso kamili, sina haki na ni mchafu mbele zako, naomba unirehemu katika jambo lolote mbele zako unitakase kwa damu ya Yesu, sababu yoyote itakayofanya usisikie maombi yangu, au mashitaka yoyote ya dhambi mbele zangu, na viambaza vya kuzuia maombi yangu ninatubu mbele zako Mtakatifu wa Israeli ninaomba rehema mbele zako, ninatubu mbele zako, ninaomba unisamehe Baba yangu nimetambua ninakiri na kujutia njia zangu zote za dhambi, naomba unirehemu na unisafishe kwa damu ya mwanao ya agano jipya la msamaha wa dhambi, katika jina la Yesu.
√Ee Mungu Baba wa utukufu Baba wa utukufu, katika jina la Yesu nasogelea mbele zako kwa maombi kwa jina la Yesu na kwa damu ya Yesu, ninakiri lile neno lako ya kuwa atakuja uyo Roho na kazi mojawapo kwetu ni kutuweka katika kweli yote, na kutujulisha katika mambo yanayokuja, pia nakiri neno lako katika Mathayo 10:26 kuwa hakuna neno lilisitirika, ambalo halitafunuliwa wala lililofichwa ambalo halitajulikana, Baba wa Mbinguni neno lako ni Roho, na uyo Roho yuko juu yangu sasa katika jina la Yesu, neno lako ni pumzi, pumzi ya uhai iko ndani yangu sasa kwa jina la Yesu, Neno lako ni moto ulao, huo moto uko ndani yangu sasa kwa jina la Yesu, neno lako ni nyudo nami naichukua iyo nyudo sasa kwa damu ya Yesu, neno lako ni shoka, neno lako ni upanga nami nachukua izo silaha sasa za kumharibu ibilisi na mapepo yake yote katika jina la Yesu!
√Baba kwa neno lako hili nafichua kila wachawi wanaokuja kuniloga usiku wafichuliwe sasa kwa damu Yesu, katika jina la Yesu, Baba Kwa neno hili nafichua kila siri shetani aliyopanga juu ya maisha yangu ili mabaya yanipate nafichua hizo siri kwa jina la Yesu, kwa neno hili Baba nafichua kila wachawi wanaokuja kunilisha ndotoni wafichuke kwa jina la Yesu. Baba kwa neno lako nafichua wachawi wanaokuja ndotoni au kuwaona ndotoni kwa jina la Yesu, Kwa neno hili kila lililositirika ambalo limejificha katika biashara
√yangu la ibilisi nalifichua sasa kwa damu ya Yesu, Kwa neno hili kila lililositirika katika kazi yangu, huduma yangu, kazi za mikono la ibilisi nalifichua kwa jina la Yesu, Kwa neno hili kila lililositirika la ibilisi katika ndoa yangu nalifichua sasa kwa jina la Yesu, kwa neno hili kila lililositirika katika familia yangu na ukoo wangu la ibilisi nalifichua kwa jina la Yesu, Kwa neno hili kila lililositirika la kwa wabaya zangu, maadui zangu wenye nia mbaya nawafichua sasa kwa jina la Yesu, Kwa neno hili
√kila linalomaliza uchumi wangu pesa zangu ambalo la ibilisi na limesitirika, nalifichua kwa jina la Yesu, kwa neno hili kila linalonirudisha nyuma kiroho la ibilisi na limesitirika nalifichua kwa jina la Yesu, kwa neno hili kila rafiki mbaya au mtu yoyote aliyepandwa na ibilisi katika maisha yangu na amesitirika namfichua sasa kwa jina la Yesu, Kwa neno hili kila nguvu ya ibilisi inayokuja kunizuia nisikumbuke ndoto
√baada ya kuota ndoto, naifichua iyo nguvu sasa ya kuzuia ndoto kwa jina la Yesu, Kwa neno hili kila nisilolijua ambalo ibilisi kapanga, kila fumbo katika maisha yangu, nalifichua sasa kwa jina la Yesu, Bwana Yesu asante ninakiri sasa neno lako na Roho wako wakufichua siri hizi wako juu yangu sasa kwa jina la Yesu, Na Roho wako wakunisaidia kuzihifadhi izo siri zitakazowekwa kwangu wazi, baada ya kufichuka yuko juu yangu sasa kwa jina la Yesu, Na moto wa Roho
√Mtakatifu uko pamoja na Roho wako kupitia neno lako, ili kuharibu ukuta, ulinzi, ngome za ibilisi za kuficha siri zinaharibiwa sasa kazi zote za ibilisi kwa jina la Yesu. Roho ya uweza yuko juu yangu sasa kwa jina la Yesu, Roho wa kumcha Bwana yuko juu yangu sasa kwa jina la Yesu, Roho wa maarifa yuko juu yangu sasa kwa jina la Yesu, Roho wa hekima wa Bwana yuko juu yangu sasa kwa jina la Yesu, Roho Mtakatifu yupo pia juu yangu sasa kwa jina la Yesu. Asante Baba maana imekuwa katika jina la Yesu Amen.
rudia mara 7* kukiri haya maombi.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment