MAOMBI YA KIKUHANI/MAOMBI YA KIFALME!
somo; maombi ya kikuhani/ maombi ya kifalme.
Bwana Yesu atukuzwe sana!
somo litakusaidia kuomba kikanuni na kupata matokoe yako! nataka tutafakari kwa jicho la mwalimu neno! kisha tuangalie haya maombi ya
kifalme ! maombi ya kikuhani yakoje na yanafanyaje fanyaje kazi! je wewe huwa unayaomba? kama unayaomba unaomba according to bible au
sheria ya rohoni. endelea kujikoki na maarifa ya Mungu. maana vita vyovyote vile tunashinda kwa maarifa na hekima ya Mungu. Bwana Yesu asifiwe sana?
maombi ya kikuhani ni nini?
* Kuhani ni mtu anayeunganisha madhabahu ya Mungu hapa duniani na ulimwengu wa roho. Ni mtu anayesimama katika
ulimwengu wa roho kuuleta uwepo wa Mungu. sasa tunapooenda kwa Mungu kama kuhani tunaenda kama mwanakondoo aliyechinjwa.
Tunapofanya vita na shetani tunaenda kama simba wa Yuda Halleluyah Halleluyah!
Mwanzo 1:28
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
*Kazi mojawapo ya kuhani ni kuachilia damu ya Yesu. Mbele ya Mungu Baba. Kazi nyingine ni kumkumbusha Mungu ahadi alizo ahidi. Kwa iyo kabla ya
mtu kufanya maombi ya vita au maombi ya kifalme lazima aanze maombi ya kikuhani kwanza akishapata greenlight sasa ndipo anaingia katika
ulimwengu kama mfalme!
Embu tuangalie hili kwa undani na mfano ili ulifahamu vizuri
Waebr 11:3
3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.
1 wakor 15-44
44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko.
*Upo ulimwengu huu unaonekana kwa macho ya damu na nyama tunaoishi na upo ulimwengu wa roho wa usionekana kwa macho ya
damu na nyama.Kuna jambo lazima ulielewe chochote unachokiona katika ulimwengu wa roho wa huu unaonekana na macho ya kibinadamu, basi
kipo pia ivyo ivyo katika ulimwengu pia wa huu usionekana kwa macho ya kawaida (ulimwengu wa roho)
yani ukiona stuli sehemu basi
katika ulimwengu wa roho pia ipo stuli kama iyo iyo! ukiona jiwe nje ya nyumbani kwako katika ulimwengu wa roho wa nyumba yako pia lipo jiwe hapo
hapo ulipoliona. ukiona rav gari mahali basi katika ulimwengu wa roho pia ipo rav iyo iyo ivyo ivyo. manake hakuna ambacho kipo duniani kisiwepo
ulimwengu wa roho. kila kitu vipo viwili viwili kipo katika ulimwengu wa mwili na kipo katika ulimwengu wa roho utasema mtumishi umejuaje
siyo mimi nimesema angalia neno hapo juu. sasa kitu chochote duniani original yake kimeanzia katika ulimwengu wa roho. yani vitu vyote vinakuwa
design katika ulimwengu wa roho huu usionekana kwa macho ya damu na nyama! ndipo vinakuja kuonekana katika ulimwengu huu wa duniani.
kwa iyo kwa kusema ivyo
nina maana gani! nina maana hii tatizo lolote hapa duniani huwa linaanzia katika ulimwengu wa roho ndipo
linakuja ulimwengu huu wa dunia, endelea kunifuatilia nakokupeleka ndipo unapoenda kuchomoka sasa, kitu chochote katika ulimwenguni huwa kipo
kisababisha kilichosabisha kutokea. Kama mtu ana deni basi katika ulimwengu wa roho lipo pepo lilosababisha deni, kama mtu ana matatizo ya
ndoa basi lipo pepo nyuma ya iyo ndoa, kama mtu hana kazi basi nyuma ya hiyo lipo pepo lililosabisha uyo mtu akose kazi! Kama mtu ananyama za
tumbo basi nyuma lilo pepo linalosabisha huo uvimbe.
SASA SISI TUNAKOSEA WAP?
wengi huwa tunaanza kuvunja mfano roho ya madeni bila kuvunja original! na wanashangaa hawaoni matokeo! nitakupa mfano wa
nguo na mwili! tuseme jeans nguo thamani yake ni mwili, bila mwili nguo haina kitu chochote, jinsi ikivaliwa na mwili mtu akikunja mguu nayo itajikunja!
mtu akinyoosha mguu nayo itanyooka sasa ukitaka jeans isiwe na kitu manake lazima
uitoe katika mwili. ukitoa katika mwili ukisimamisha haiwezi simama yenyewe bila mwili, wala haiwezi kujinyoosha kuruka mashimo au kujikunja
maana kuringa kote kwa jeans ni sababu ya mwili. jinsi haina lolote pasipo mwili. sasa twende kimtazamo chukulia jinsi ni tatizo. mwili ndio roho
iliyoko nyuma ya tatizo!
wengi huwa tunapambana na jeans badala ya kuanzia kwenye mwili, ukifanikiwa kuupiga mwili, jeans
inaporomoka yenyewe. nina maana gani? maana yangu ni hii wengi wanapigana na deni! wanaliamuru kwa jina la Yesu liondoke wako right
wanachosahau kuwa lile deni ipo sheria katika ulimwengu wa roho inayosimamia ilo deni. watu wengi walikuwa hawajui kwanini Yesu alikuwa haombei
watu bali anashukuru na kukoccomand na mtu anapokea, Yesu alikuwa anaomba mlimani anakesha mlimani asubuhi tayari
anakuwa anaupako anafanya miujiza, sasa watu wengi huwa hawatafuti kuwa rohoni ili wapate nguvu bali wao wanakimbia kuccomand kwa
jina la Yesu nakushangaa wanapata matokeo machache! sio swala tuu la kusema kwa jina la Yesu tokaa! hapana kuna kanuni za kufanya kabla ya
kufikia hapo! na mueshimu sana mtumishi mwenye upako wa Mungu anayeccomand mambo yanatokea kupata huo upako
kala gharama! maana uyo ni kuhani kautafuta uso wa Mungu mpaka roho Mtakatifu alivyomshuhudia ndani yake kuwa sasa uko full charged .
hapo sasa anageuka anafanya maombi ya vita kama mfalme. na ndio maana ya neno hili.
Marko 11:23-24
23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
* Umeona hapo juu lazima ufanye maombi ya kikuhani upate upako ukishapata upako na Roho Mtakatifu akikushuhudia sasa imetosha
hapo sasa unaweza kuccomand mlima huu ngoka na utangoka na utatupwa bahari. na ndiyo iyo imani ya hakika. Unafikiri Yesu
angekuwa hautafuti uso wa Mungu nakukurupuka tuu kuponywa unafikiri lingetokea jambo lolote?
Angalia hapo juu! mstari wa 23 anasema asiwe na shaka moyoni mwake, nikamuuliza roho Mtakatifu hivi kinachosababishaga mtu awe na shaka moyoni mwake
ni kitu gani? akaniambia dhambi ikaayo ndani ya mtu. Na sheria ya dhambi iliyokatika viungo vya mtu Bwana Yesu asifiwe sana ! akanipeleka mpaka hapa! macho yakafunguka
Tuangalie Warumi 7:15-24
15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
21 Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.
22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,
23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.
24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?
* Niliwahi muuliza tena Roho Mtakatifu kama hali yenyewe ndo hii? anayeelezea Paulo! je nani atakayeokoka? nani atakuwa mtakatifu? Roho wa Mungu akanionyesha kitu. Nami sasa nanyofoa sentensi humo ndani ili upate iyo maana.
"bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu, ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu"
*Bwana Yesu asifiwe kwa iyo ukitaka ishinda dhambi yoyote lazima ushughulike na dhambi ikaayo ndani yako! na kuivunja sheria ya dhambi katika
maungo yako! kuna sheria ipo
katika macho yako, masikio, mwili-hisia, akili hili ni somo lingine leo tuangalie haya maombi ya kikuhani ndo muhimu! hayo mengine ya
kifalme wengi mnayajua!
SASA UNAFANYAJE MAOMBI YA KIKUHANI KABLA YA KIFALME?
*tuchukulie mfano unadili na tatizo la nyama za tumbo
nitafupisha ingawa maelekezo ni mapana sana
i. unaomba rehema kwa ajili ya huo ugonjwa wa nyama za tumbo.
ii.unaomba rehema kwa ajili ya kisababishi (source) yani dhambi gani ilimpa pepo uhalali wa kuingia katika mwili wako na kujigeuza uvimbe. pengine ni maagano, laana, yoyote ile! unachilia damu ya Yesu katika source ya tatizo! ikatakase iyo dhambi.
iii. unaomba rehema kwa ajili ya ilo lango ambalo pepo kapita unalitakasa kwa damu ya Yesu! unaachilia damu ya Yesu katika ilo lango lililopitisha uyo pepo
iv. unaifuta iyo sheria iliyompa uhalali pepo kwa damu ya Yesu unaifuta katika ardhi, anga, bahari. hata kule kuzimu
v. unamwaga damu ya Yesu ya hukumu juu ya wasimamizi na watekelezaji wa sheria iyo.
vi. Sasa sababu za msingi hapo unamkumbusha Mungu kupitia neno kuwa kwanini uponywe! mfano Yohana 4-23-24 kuwa unataka kuabudu na kumfanyia Mungu ibada katika roho na kweli, kwa iyo nyama za tumbo ni kizuizi. izo ndo hoja za msingi kwa Mungu.
BAADA YA HAPA SASA NDIPO UNAFANYA MAOMBI YA KIFALME!
*lakini huanzi mpaka umesikia ndani yako kumewaka moto. na vitu navyokufundisha nilifundishwa kabisa na Roho Mtakatifu. Bwana Yesu asifiwe!
Maombi ya kifalme ni maombi ya vita unaongea na tatizo lenyewe hapa sasa unageuka simba. Kule ulipokuwa kuhani ulikuwa mwanakondoo! sasa
hapa ndipo unauambia mlima huu ngoka na utangoka hapa kulia ushamaliza kule unasimama kama mwanajeshi! unamuamuru adui arudishe vitu
vyako unambomoa unamuharibu na kumuangamiza. Bwana Yesu asifiwe! Na hapo ndipo hili neno linatimia
Mathayo 16:17:19
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
i. unatiisha ilo tukio au jambo
ii.unatiisha hao wasimamizi
iii.unatamkia mauti iyo sheria
iv. Tamka uzima juu ilo tukio au jambo
v. Teketeza hao wasimamizi au watekelezaji iyo sheria.( ma urgent wote wa ibilisi.
Najua Yesu muweza yote kakuvusha pa kubwa sana basi mpe Mungu utukufu kwa maarifa na hekima. Jina la Bwana libarikiwe sana!
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Asante, Barikwa sana mtumishi.
ReplyDelete