MAOMBI YA KUFUTA MAAGANO YA IBILISI
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
*ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
*Maombi haya ni maombi hatari ivyo lazima ujiwekee ulinzi wa Ki Mungu pia kama hujaokoka kiri Kwanza sala ya toba ili uwe upande
*wa Yesu ambao ni salama. sala ya toba ipo chini kabisa! ni hatari kumpinga ibilisi na huku upo upande wake.
MAOMBI YA ULINZI
Baba katika jina la Yesu. ninakuja mbele zako kwa ajili ya ulinzi nikitambua ya kwamba umesema Bwana asipoulinda
mji basi wakeshao wafanya kazi ya bure! Neno lako linasema Ufunuo 12:11 Nao wakamshida ibilisi kwa damu
ya mwanakondoo na kwa neno la ushuhuda! Ee Mungu Baba kila malipizi na visasi vya ibilisi navitamkia kushindwa ndani
yangu, kushindwa nje yangu kwa jina la Yesu kwa jina la Yesu! kushindwa katika familia yangu, kushindwa kwa mzazi
wangu, kushindwa kwa mme
wangu kwa jina la Yesu, kishindwa kwa watoto wangu kwa jina la Yesu, Natamka kila
mpango wa ibilisi juu ya ardhi,
juu ya anga, katika bahari chini ya bahari natamkia kushindwa kwa jina la Yesu!
Neno lako linasema katika Isaya 54:17 kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa, kila ulimi utakao
inuka juu kwa kuhumu utahukumu kuwa mkosa nami kwa jina la Yesu kwa damu Yesu. nawatamkia Wachawi,
watu wabaya wote, natamkia madhabahu zote za ibilisi zinazonifuatilia, natangaza mipango yote ya ibilisi juu
yangu kutofanikiwa kwa jina la Yesu, kila mishale wanayorusha kwangu natamka kutokufanikiwa kwa jina la
Yesu, ninaangusha mipango yote ya siri iliyopangwa dhidi yangu kwa damu ya Yesu, kila baya wanalolifanya kila majini
wanayoyatuma kwa kwangu ninatamka yarudi kwao na kuwaangamiza waliowatuma kwa jina la Yesu. kwa kuwa
imeandikwa achimbaye shimo litamfukia yeye mwenyewe na abingirishaye jiwe litamrudia yeye mwenyewe nina amuru
kila ubaya ambayo adui zangu wanaufanya juu yangu na kwa familia yangu, katika maisha yangu mashumbulizi yoyote ya
giza naamuru kuwarudia wao wenyewe, na kuwasambar atisha wao wenyewe kwa jina la Yesu. imeandikwa Mungu
hadhihakiwi apandacho mtu ndicho atakachokivuna. ninaamuru ubaya wote wa ibilisi washirika wa ibilisi
watenda kazi wa ibilisi kuvuna uovu wanaofanya juu yangu kwa jina la Yesu. Bwana neno lako linasema zakaria 2:5 nami
nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake. Baba kuwa ukuta wa moto sasa
katika maisha yangu, katika ulimwengu wangu wa roho, kuwa ukuta wa moto kunizunguka sasa, kuwa ukuta
wa moto kwa mme wangu,
kuwa ukuta wa moto kwa watoto wangu. katika jina la Yesu. nami sasa najifunika kwa
kuta saba za moto kwa jina la
Yesu. najifunika kwa kuta saba za moto wa roho mtakatifu kwa jina la Yesu. najifunika kwa
kuta saba za damu ya Yesu
katika jina la Yesu. mimi na mali zangu, mimi na mzazi wangu, mimi na familia yangu
katika jina la Yesu. Na nyumba
yangu, na kila kitu kinacho
nihusu kwa jina la Yesu. zaburi 34:17 inasema malaika wa
Bwana hufanya vituo
akiwazungukia wao wamchao Bwana. Nami kwa mamlaka ya jina la Yesu ninakuamuru
malaika wa Mungu kwa sheria
hii uje hapa kunilinda sasa kwa jina la Yesu. Ameen.
rudia mara 3!
*Maagano hufutwa kwa damu ya Yesu ivyo tutatumia ufunuo 12:11
*kila unapopata mpenyo shetani ana tabia ya kutafuta maagano ya siri ambayo wewe hutagundua, akishapata anachofanya anakutega, ukiingia mtego anakubomoa taratibu wakati wewe hapo umetulia unajua vita vimeisha akifikia mahali pa zuri ana kuattack kwa gafla! tayari kakuharibu na kukuharibia unaanza tena upya! lazima tuvunje maagano yote kwa jina la Yesu kisha tutaweka ulinzi!
*Shetani anajua kwa wewe kuomba yeye yupo hatarini na atafanya juu chini usiombe ndo mana ukichunguza 80% ya waliokoka hawaombi wanasubiri waombewe na wachungaji wawekewe mikono! wapakwe mafuta! ni hatari sana nakwambia hata ukiwa na mafuta toka south Africa, na maji toka Nigeria kama Mungu hajakupa maarifa na hekima ya kupigana shetani atakushinda maana yeye anakuona wewe humuoni! anajua unasubiri ishara za nje ndipo uanze kuomba, na anajua kabisa wewe unaomba vipi na kikomo chako ni wap? ivyo anasubiri ile umemaliza tuu au umechoka na yeye ndo anaanza vita, na anajua huwa unadili na matunda au matawi lakini mti utauacha ivyo baada ya mda mti unachipua tena.
Maombi ya Vunja maagano:
Baba katika jina la Yesu Kristo! niko mbele zako Mungu uliyehai wewe mwingi wa rehema na neema! Roho mtakatifu naingia makubaliano na wewe katika maombi haya na wewe naomba uombe kutumia kinywa changu katika jina la Yesu! Bwana Yesu naomba umtukuze Baba ndani yako wakati maombi haya
yanaendelea katika jina la Yesu! Mungu Baba maombi haya tayari tuko zaidi ya wawili ivyo tunaomba uwe pamoja nasi utusikie tunapokuomba tunaomba umtukuze mwanao tunapoomba maombi haya! katika jina la Yesu!
Baba kwa imani naishika ardhi ya mkono wangu wa kuume, ardhi ya kwetu, ardhi ya asili yetu, Baba ninaomba rehema kwa kila maagano yote Mungu yaliyofanyika pasipo mimi kujua ama kujua na asili yangu upande wa Baba yangu, upande wa mama yangu, hata ikawa ya kwamba kwetu hatufanikiwi,
hatupati kazi, hatuwezi biashara, tunaumwa magonjwa,hatuolewi,mimba zinaharibika, hatusomi, tunakufa na ukimwi,tunapukutika, tumekaliwa na wachawi, tunaabudu mizimu, hakuna aliyefanikiwa, tunaumwa Pressure, kisukari, cancer, watu
wanakufa kila mara katika ukoo wetu, tunazaa kabla ya wakati,tunazaa nje ya ndoa, ndoa hazikai zinavunjika, ni walevi wa kutupwa, tunaomba rehema Mungu Baba kwa maagano yote ya kichawi, kupitia ardhi ya asili yangu,
kupitia madhabahu za shetani za asili yangu, kupitia vyakula, kupitia vinywaji, kupitia mavazi tuliyovalishwa rohoni, kupitia maneno ya kukiri, kupitia kusikia, kupitia kuona, kupitia ndoto. Mungu Baba tunajua ya
kuwa Maneno yako yamesema katika biblia "ufunuo 12:11 nao wakamshinda ibilisi kwa damu ya mwanakondoo na kwa neno la ushuhuda wao" Baba wa mbinguni tunajua ya kuwa ili pepo la ibilisi au malaika waasi waje kutuasi lazima kuwe na agano la damu, ambalo hutolew a kwa kafara! nami pia ninakiri damu ya mwanakondoo ya ufunuo 12:11 iliyoachiliwa ili
kumshinda ibilisi! na leo hii maagano yote yanayompa ibilisi shetani uhalali ninaenda kuyashinda kwa damu ya mwanakondoo! ninaenda kuyavunja kwa nyundo ya Mungu ufunuo 12:11, ninaenda kuyachoma moto wa roho mtakatifu wa ufunuo 12:11,
waliotumwa na wachawi ninaenda kuwafyeka kwa upanga wa Mungu wa ufunuo 12:11, naenda kuharibu falme zote madhabahu zote zenye maagano kwa nyundo ya ufunuo 12:11 katika jina la Yesu Kristo! Baba Mungu wa mbinguni katika jambo lolote!
lile lililotoa malango kwa ibilisi hata akapata nafasi ya pepo ninaomba rehema Bwana Yesu, naomba unitakase kwa damu ya Yesu, unitakase kwa damu ya Yesu, Baba naomba utakase roho yangu, utakase mwili wangu,utakase nafsi yangu, utakase ardhi na mbingu zangu, utakase ulimwengu wangu wa roho,
utakase malango yangu yote, utakase macho yangu, utakase masikio yangu, utakase vyakula nilivyokula, utakase vinywaji nilivyokunywa, kwa damu ya Yesu kwa damu ya Yesu kwa damu ya Yesu, ninaomba utakase nguo zangu ninazo vaa, utakase mafuta vipodozi vyangu, utakase vitu vyangu
vyote navyovitumia vya nje ya mwili na ndani ya mwili kwa damu ya Yesu, kwa damu ya Yesu, kwa damu ya Yesu, katika jina la Yesu Kristo! Dhambi yoyote Mungu nayokumbuka na nisiyoikumbuka, niliyoshiriki au nisiyoshiriki ama kushirikishwa dhambi ambazo sijui hata ni dhambi! dhambi zilizojificha leo hii Mungu ninaomba damu yako
Bwana ya Yesu ya ufunuo 12:11 initakase leo! initakase leo! inatakase leo katika jina la Yesu! kila mahali niliposhikiliwa nachilia damu ya Yesu ya rehema, katika jina la Yesu, kila mashitaka ya dhambi, kila alama ya dhambi, viambaza vya dhambi katika ardhi, anga, bahari hadi chini ya bahari ninaachilia damu ya Yesu ya rehema kwa jina la Yesu, kwa damu ya Yesu,
Baba nirehemu mimi na familia yangu, mimi na ukoo wangu, mimi na mtaa wangu, mimi na watu wangu wa karibu, mambo yoyote ambayo Mungu nimekuasi sijafuata sheria zako ninaomba rehema unisamehe Mungu, kwa damu ya Yesu, kwa damu ya Yesu, katika jina la Yesu! asante Bwana Yesu kwa kuniweka huru kwa damu ya ufunuo 12:11, asante kwa kunisamehe dhambi, asante kwa kuwa sasa nahesabiwa haki mbele ya Mungu Baba katika jina la Yesu,
Ufunuo 12:11 Neno hili la Mungu ni nyundo na mimi ni nyundo ya Mungu, neno la Mungu ni moto ulao nami navaa moto sasa katika kinywa changu, neno la Mungu Ni upanga nami natwaa upanga mkono wangu wa kuume sasa, neno la Mungu ni shoka nami nashika shoka mkono wangu wa kushoto, neno la Mungu la ufunuo 12: 11 ni silaha hatari
kwa ibilisi nami sasa navaa silaha hii ya ufunuo 12:11 , kuharibu maagano yote, ninatwaa damu ya Yesu ya ufunuo 12:11 ya kumshinda ibilisi, ibilisi nakujia sasa nikiwa nimevaa silaha kamili,Kwa jina la Yesu Kristo kila agano la
kutokufanikiwa nalivunja kwa damu
ya Yesu, waliotumwa nawasamba ratisha na moto wa Mungu katika jina la Yesu, agano la kutokusoma nalivunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa nawafyeka kwa upanga kwa jina la Yesu,
agano la kutokupata kazi nalivunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa nawalipua kwa moto wa Mungu,kwa jina la Yesu, agano la kutokuolewa nalifyeka kwa damu ya Yesu, waliotumwa nawayeyusha kwa moto kwa jina la Yesu, agano la magonjwa nalivunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa nawakamata kwa damu ya
Yesu nawafyeka kwa shoka kwa jina la Yesu, agano la kupata hasara ya biashara la wachawi nalivunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa nawasambatisha kwa nyundo nawapiga nawavunjavunja kwa jina la Yesu, agano la kupiga marktime, utasa, mapooza, mwendo wa konokono, mwendo wa kobe nalivunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa ninawashika
kwa damu ya Yesu, nawatupa katika moto wa kuzimu kwa jina la Yesu, agano la hofu, wasiwasi,mashaka, kutokujiamini, bumbuwazi, kutokujua cha kufanya nalivunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa nawakamata kwa damu ya Yesu nawafyeka kwa upanga, katika jina la Yesu, agano la kutikisa ndoa yangu nalivunja kwa damu ya Yesu,
waliotumwa ninawadaka kwa damu ya Yesu ninawachinja kwa upanga, agano la madeni nalivunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa ninawakamata kwa damu ya Yesu, nawateketeza kwa moto hadi majivu kwa jina la Yesu, agano la kutokushika mimba na kupata watoto nalivunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa nawakamata kwa damu ya Yesu, nawalipua kwa moto kwa jina la Yesu, agano la kulishwa ndotoni, kufanya
mapenzi ndotoni nalifuta kwa damu ya Yesu, majini yaliyotumwa nayakamata kaa damu ya Yesu, ninawafyeka kwa upanga wa roho mtakatifu, agano la kichawi wakati nimelala nalivunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa ninawakamata kwa moto wa roho mtakatifu, nawapasua kwa moto kwa jina la Yesu, agano la ulevi, tabia mbaya, zote za roho chafu nalifuta kwa damu
ya Yesu waliotumwa nawapasua kwa moto wa roho mtakatifu kwa jina la Yesu, agano la umasikini, ufakara na uchumi mbaya nalivunja kaa damu ya Yesu, waliotumwa ninawakamata kwa damu ya Yesu, nawayeyusha kwa moto kwa jina la Yesu, agano la uonevu kazini nalivunja kwa
damu ya Yesu waliotumwa nawakamata na pingu za moto , nawapasua kwa moto kwa jina la Yesu, maagano yote ya siri nayavunja kwa damu ya Yesu ya kunaswa katika dhambi, nayavunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa nawadaka kwa nyavu za Mungu, ninapasua kwa moto kwa jina la Yesu, maagano yote ya kuniingiza
katika laana ninayavunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa ninawakamata kwa moto, kwa damu ya Yesu, nawapasua kwa moto kwa jina la Yesu, maagano yote ya siri ya wachawi juu yangu ninayavunja kwa damu ya Yesu, waliotumwa na wachawi na wachawi wenyewe ninawadaka kwa moto, kwa damu ya Yesu, ninakamata upanga wa roho ninaweka shingoni mwao ninawachinja kwa jina la Yesu,
agano lolote nilisolijua ambalo sijalitaja mahali hapa! ninatuma damu ya Yesu Yenye macho saba, pembe saba, na roho saba likasakwe kwa jina la Yesu, nayavunja yote kwa damu ya Yesu, waliotumwa wote nawatia nguvuni mwa mkononi mwa JEHOVA kwa damu ya Yesu, ninawafyeka kwa shoka shingo zao, nawayeyusha kwa moto Mungu, nawanyeshea
mvua ya acid ya Mungu, nawapondaponda vichwa vyao kwa nyundo ya Mungu, nawaseta kuzimu kwa jina la Yesu. Natangaza kuanzia leo hii hakuna agano lolote litakalo simama mbele yangu na kumpa ibilisi mlango maana nimemshinda kwa damu ya mwanakondoo Amen.
* rudia mara 7
√Haya ni maombi ya kumkaribisha Yesu na Roho Mtakatifu
√Maombi ya kufagia njia
√ Maombi haya jifungie ndani uombe kwa sauti kama yalivyo.
√Baba katika jina la Yesu Kristo! niko mbele zako mfalme ninakuja mbele zako leo kwa ajili ya upatano na wewe! nimetambua na kufahamu ya kwamba bila wewe siwezi enda mbele wala kufanikiwa. Bwana Yesu niko mbele zako ninaomba unisamehe katika
√jambo lolote katika maisha yangu ambalo halikupendezi wewe nitakase unioshe kwa damu ya Yesu Kristo! ninakiri na nimetambua makosa yangu yote leo hii Bwana Yesu ninakiri makosa hayo naomba unisamehe. nataka kuanza na wewe leo. sitachoka kukukiri
√nitakukiri kila siku ya maisha yangu. Bwana Yesu leo nakupokea tena kwa mara ingine kwa upya uingie ndani ya moyo wangu, uishi ndani ya moyo wangu! ndani ya vilindi vya moyo wangu! nifanye mimi niwe mtoto wako! na wewe uwe
√Baba yangu, niingize katika ufalme wako Bwana Yesu nami niitwe mtoto wa kifalme, Shetani leo na siku zote nimekukataa siku zote za maisha yangu! tokeo leo laana zote juu yangu zimefutwa kwa damu ya Yesu, dhambi zote juu yangu zimefutwa kwa damu ya Yesu, maagano yote na shetani
√yamefutwa kwa damu ya Yesu! nimekukataa ibilisi na kazi zako zote! tokea leo hii mimi siko upande wako. Bwana Yesu chukua maisha yangu kwa uwezo wa roho Mtakatifu, ishi ndani yangu kwa uweza wa roho Mtakatifu, mruusu Roho wako sasa aje juu yangu! aje kwa nguvu na mamlaka
√aniatamie mimi katika jina la Yesu Kristo! Roho Mtakatifu sasa yachukue mawazo yangu, yachukue maneno yangu, yachukue matendo ufanye ya kwako katika jina la Yesu, kila hamu ya kumtumikia shetani imekatwa kwa damu ya Yesu! Bwana Yesu mfungue mtu wangu wa ndani sasa aliyekuwa amefungwa aanze kuishi sasa sawasawa na neno lako katika jina la Yesu Kristo. Ameen
rudia mara 3*
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Amen.barikiwa
ReplyDeleteAmen mtumishi
ReplyDeleteAmen. Glory be unto God, this has been a true revelation unto my life
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteAmeeeen ameeeen
ReplyDeleteBarikiwaaaa mnooo mtumish was Mungu
ReplyDeleteMungu akubariki kwa kukuongezea mafunuo
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteAmen Mtumishi
ReplyDeleteAmeen
ReplyDeleteAmen🙏
ReplyDeleteAmeen
DeleteAmeeeeen
ReplyDeleteAsante Yesu...
Asante Yesu
Amen
ReplyDeleteNimekuwa huru nimepata ukombozi
ReplyDeleteThanks very much & be blessed by our creator known as God
ReplyDelete