MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA MATESO

*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.

ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.

✋Katika biblia kuna sehemu Mungu kaongea kuhusu "mateso" yanaweza yakawa kazini, biashara, afya, uchumi,

✋kupiga hatua, mafanikio, amani ya nafasi, inawezekana kabisa mtu anateseka na yupo ndani amejifungia ndani hajui afanye nini! mateso yapo kwenye ndoa! mateso yapo kupitia

✋masengenyo! mateso yapo kupitia watu wanaokuzunguka, watu waliojuu yako, au wasaidizi wako. lakini mateso ni nini hasa? mateso ni roho ya

✋ibilisi kabisa ni wakala wa uchungu ni roho ya kukusababishia maumivu kwa makusudi ili moyo wako uiname, kuna mwingine anataka aache utumwa wa dhambi flani, ila

✋hawezi hayo pia ni mateso kabisa, hakuna mateso mabaya kama ya nafsi, vikao vya ibilisi kupitia nafsi unasikia vitu vibaya tuu ndani yako, unasikia kukata

✋tamaa, unasikia kuchoka! uyo si Mungu uyo ni ibilisi! uyo ni ibilisi lakini leo tutaingoa iyo roho ya mateso kwa maombi ya kukiri kwa jina la Yesu Kristo. Ameen

Tuangalie!
Nahumu 1:9
Zaburi 34:19

9 Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.

19 Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.

√ Tuangalie tafakari kidogo
mateso haya tunayoshughulikia hapa ni ya shetani! Kama ni Mungu ameruusu unaomba neema ya kufupishwa mda wa jaribu. Bwana Yesu asifiwe.

√ Kama nilivyosema awali Mateso ni roho ya ibilisi aidha Mungu aliruusu kwako au imepata mlango kwako wewe kwa maagano ya dhambi, au laana iliyokupa sababu kutokushika sheria ya Mungu

√Na amri zake, Ibilisi husababisha njia za kuleta mateso kwa watoto wa Mungu. nia yake si wewe nia yake ni kuumiza moyo wa Mungu. Maana anajua akikutesa wewe basi Mungu huzunika na kuumia Mungu hapendi hata kidogo viumbe vyake viteseke!

√Ambacho kinaniudhi shetani hufanya vitu alafu anamsingizia Mungu. utasikia kwenye moyo wako hayo ni majaribu ya Mungu kumbe Mungu saa ingine hata Mungu hausiki! shetani hutumia mazingira uliyopo na yanayokuzunguka kukuletea mateso! Atatumia watu waliokuzunguka! kama

√unaishi nyumbani ataleta mateso kupitia watu wa nyumbani kwako, ushaona mtu katika familia anakuwa mzigo wa ndugu wengine? hayo ni mateso ya ibilisi. Mateso yapo ya mwili, yapo ya mazingira, yapo ya watu wanaokuzunguka
yapo ya nafsi nia ni kukuachia uchungu. lakini katika jina la Yesu Kristo. hii roho leo itaondoka na kukuacha kuwa uhuru. ukiomba kwa imani na juhudi kubwa.

Tukaombee sasa kusambaratisha roho ya ibilisi ya mateso✋

9 Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.
Nahumu 1:9

19 Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote. zaburi 34:19

√Baba katika jina la Yesu! neno lako linasema Nahumu 1:9 Manawaza nini juu ya Bwana: Yeye atakomesha kabisa, mateso hayatainuka mara ya pili. Pia Zaburi 34:19

√imeandikwa mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana humponya nayo yote. Asante Baba kwa kunijulisha kuwa wewe hutaki niteseke, ndomana umeapa ya kinywa

√chako kuwa wewe Mungu utayakomesha mateso yangu hayatainuka mara ya pili. Mungu asante kwa kuwa hukuishia hapo ukaende

√lea kusema kuwa utakomesha mateso yangu. Pia nakushukuru kwa kuwa leo nimejua roho ya mateso ni ya ibilisi na wewe ndio unaohusika kukomesha hizi roho asante Mungu katika jina la Yesu. ewe

√roho ya mateso nakutangazia uko hatarini sasa katika jina la Yesu. Asante Mungu maana neno lako linanipa ujasiri ya kuwa wewe Mungu unayajua mateso yangu yote, Ndo mana ukasema nitamponya nayo

√yote. Asante Baba yangu uliye mbinguni.Nami Bwana Mungu kwa neno hili ninakuja mbele zako Mungu kwa ajili ya utakaso kamili, Ee Mungu ninaomba unirehemu katika jina la Yesu, katika

√dhambi yoyote mbele zako, ninaomba unirehemu rehema zako Mungu kwa ajili ya mashtaka yote ya dhambi mbele yangu Bwana. Naomba unirehemu dhambi zangu zote!

√unisamehe makosa yangu yote!ninaungama dhambi zangu zote kwa jina la Yesu Kristo!  ninaomba damu yako Bwana Yesu ipite katika nafsi yangu initakase, ipite katika roho yangu initakase, ipite katika mwili initakase jambo

√lolote Mungu litakalokuzuia Mungu wewe kunisikia au kunihudumia ninaomba Mungu unisamehe! unitakase kwa damu ya Yesu, unitakase kwa damu ya Yesu! unitakase kwa damu ya Yesu katika jina la Yesu Kristo wa nazareth. Ee

√Mungu kwa kujua kwangu ama kwa kutojua nimeruusu mateso ndani yangu! aidha Kwa mimi mwenyewe au kuingizwa katika maagano hayo! Baba wa

√Mbinguni leo ninaomba rehema kwa ajili ya lango lolote la maagano ya roho ya uchungu na mateso lililo pata mlango ndani ya maisha yangu au laana yoyote iliyonipata ya

√mateso aidha kwa kumtesa mtu au kutenda isivyo haki! Baba laana yoyote au maagano yaliyosababisha mlango wa mateso ninaomba unisamehe unirehemu katika jina la Yesu, kwa damu ya Yesu Kristo!

√Ninavunja maagano ya mateso kwa damu ya Yesu, ninavunja laana za mateso kwa damu ya Yesu. Popote laana ya mateso ilipotoka, au maagano ya mateso yalipotoka

√nayavunja kwa damu ya Yesu, nayavunja kwa damu ya Yesu! iwe imetoka katika madhabahu za ukoo wangu, iwe imetoka juu ya ardhi, iwe imetoka chini ya

√mbingu, iwe imetoka angani, iwe imetoka baharini! iwe imetoka chini ya bahari kule kuzimu wewe sheria ya mateso

√popote ulipotengenezwa, nakufuta kwa damu ya Yesu, nakufuta kwa damu ya Yesu, iko kitabu kilichopo kuzimu kilichoandika jina langu katika

√kitabu cha mateso ninafuta jina  langu kuzimu kwa damu Ya Yesu. Ee Mungu Baba wasimamizi wa maagano ya mateso, katika madhabahu ya

√aina yoyote, uyo mkuu wa kipepo aliyepewa sheria ya kunitesa, uyo mkuu wa madhabahu, hao watenda kazi wa madhabahu! hao washirika
wa madhabahu, hao miungu wa

√madhabahu na ukuta kipepo ulionizunguka wa kipepo ninamwaga damu ya Yesu juu yao! ninamwaga damu ya Yesu juu yao! katika jina la Yesu Kristro. Ee Mungu Baba

√ninaomba hukumu sasa juu ya hao wote, ninaomba hukumu ya haki, hukumu ya haki katika jina la Yesu Kristo! hukumu ya haki , hukumu ya haki eee Baba yangu ninaomba sasa kwa

√damu ya Yesu. juu ya wote wanaonitesa, mapepo mnaonitesa damu ya Yesu iko juu yenu sasa, majini mnaonikalia damu ya Yesu iko juu yenu sasa, leo

√mmekamatwa kwa jina la Yesu, roho chafu wa ibilisi mnaonitesa damu ya Yesu ipo juu yenu sasa, mizimu ya ukoo, falme za giza, wakuu wa giza, jeshi la pepo wabaya, wakuu

√wa anga, nyie wachawi, nyie waganga wa kienyeji, Biblia inasema yeye Mungu atakomesha mateso hayatainuka mara ya pili hayatainuka tena. nami nawakomesha sasa kwa moto! ewe mateso katika ndoa yangu nakukomesha kwa moto

√wewe ni roho nakukamata kwa damu ya Yesu, nakulipua kwa moto toka katika ndoa yangu, nakuseta kuzimu, ewe roho ya mateso katika hatua zangu, roho ya mateso katika biashara yangu, kazi yangu ya

√mikono, huduma yangu, katika uchumi wangu, kupitia wasaidizi wangu, ewe roho wa mateso kupitia nafsi wewe unayeniletea uwongo wa kuniumiza, wewe unayeniambia

√maneno ya kukata tamaa, ewe roho ya mateso kupitia wivu, roho ya mateso ya magonjwa, roho ya mateso kupitia mme wangu, roho ya mateso kupitia mke wangu, roho ya mateso

√kupitia watoto wangu, roho ya mateso kupitia ndugu zangu umekaa nyuma ya mtu au watu unafikiri jicho la Mungu halita kuona roho mateso kupitia Boss wangu. Wewe roho

√ya kuzimu wewe, wewe unayekaa ndani yangu wewe, wewe pepo la mateso wewe jini la mateso neno la Mungu linasema Bwana ataikomesha

√mateso, ambayo ni wewe nami sasa nakukomesha kwa damu ya Yesu, nawahukumu kwa damu ya Yesu ya hukumu, ninawazungushia moto nawayeyusha wote kwa jina la Yesu . najidisconnect kila aina ya mateso kwa damu ya Yesu.kila aina ya

√mateso maishani mwangu kamata moto unateketezwa sasa! unaharibiwa sasa na moto! moto! moto! katika jina la Yesu! ninakamata shoka la Mungu nawafyeka sasa kwa jina la Yesu!

√nawafyeka kwa jina la Yesu! popote ulipo achia mali yangu! achia ndoa yangu, achia elimu yangu, achia mafanikio yangu, achia hatua zangu, achia mme

√wangu, achia watoto wangu, achia mke wangu wewe mateso, achia vibali vyangu, achia furaha yangu, achia nafsi yangu kila mahali uliposhikilia nakumwagia damu ya Yesu ya .

√hukumu katika jina la Yesu. kila ulikoshikilia wewe ibilisi nakuzungushia moto wa Yesu, ukuyeyushe sasa! ukuyeyushe sasa! ukuyeyushe sasa! katika jina la Yesu.  Baba wa mbinguni kulingana na

√sheria hii ya mbinguni ya kukomesha mateso nahumu 1:9 namtuma malaika wa iyo sheria kwa mamlaka ya jina la Yesu na damu ya Yesu ewe malaika wa Mungu wa kukomeshe mateso

√sasa! nakuamuru kaharibu kila juu ya maisha yangu,  mateso yote kila mahali katika ardhi, katika anga katika bahari katika jina la Yesu. Leo hiii mateso yoyote katika maisha yangu nakutamkia umauti. mauti! mauti! mauti!

√katika jina la Yesu. na hiyo sheria ya mateso iliyokuwa katika ulimwengu wa roho nimeitamkia umauti katika jina la Yesu. Asante Bwana Yesu kwa kuwa mateso hayatainuka mara ya pili. AMEEEN

*rudia mara  7

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA