MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA UCHACHE
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
√BWANA YESU ASIFIWE!
√ Kwa kawaida sheria ya kupata lazima utoe hii ni ya Mungu. watu wengi wanapogusiwa swala la sadaka wanakasirika! lakini kwanini
√wanakasirika au kwanini nimeanza hivi? wakati nilisema tunaomba kuondoa roho ya uchache? Kabla ya kuondoa
roho ya uchache lazima uondoe
√mlango iyo roho ilipoingia.Biblia inasema Mungu hadhihakiwi akipandacho mtu ndicho atakachokachokivuna. Na haya maombi kila
√unapoyaomba yanakufungua kila unapoyaomba yanabomoa tofali la shetani yanajenga tofali ya Mungu.Halleluyah! kila
√siku kwa neema ya Mungu soma neno kiri neno! kuna wengine wamefunguliwa kiuchumi lakini wamefungwa kiafya! mwingine ana kila kitu
√ila ndoa yake imefungwa! kila siku ni kujifungua! kila siku ni kuwekwa huru. kitabu Yohana 17 wakati Yesu anaclose chapter akiongea na Mungu akisema ile kazi uliyonituma
√hapa duniani nimeimaliza na kusudi lako limelimaliza nalo ni watu "wakujue wewe Mungu wa ukweli pekee" niliwahi kusoma ili neno nikashangaa sana sasa
√ndo imekuja very clear kusudi la binadamu hapa duniani ni wewe kumjua Mungu wa kweli pekee! sio lingine kumbe Mungu bado hatuja mjua.
√Utapata amani kwa kumjua Mungu. na Roho akazidi kunieleza Mungu anasiri nyingi sana mno za wewe kufanikiwa kwa iyo kwa wewe kumjua
√manake anakufunulia siri. anakufunulia siri. anaanza kuongea mambo ya ndani sana wengine hawajui.
√ Kama umefuata sheria ya kubarikiwa na Mungu ni lazima upokee baraka za Mungu kwa wingi wake Mungu aliokusudia, Mungu aliumba na kutengeneza
√kwa ajili yako! vitu vya hapa duniani mbinguni havitumiki wala havina kazi, vina maana kwako tuu. ushawahi fikiria ni kwanini Mungu akunyime hasa?
√wakati kakutengenezea wewe? Mungu ni Mungu lazima uwe chini ya sheria yake na ukubali kutawaliwa na Mungu kwa sheria zake. una uhuru wa
√kuzifuata au kutozifuata kwa iyo wengi hapa mnapajua.
sasa nataka nikukumbushe jinsi ya kuchota baraka sadaka! ndo njia Mungu humbariki mtu
√kwa utoaji. sadaka haiwakilishi fedha inawakilisha thamani ya moyo wa mtu kwa Mungu. manake ule uwezo wa foregone kitu akipendacho na
√kumpa moyo wake Mungu. sadaka husema hivi bila wewe mimi siwezi, sadaka husema hivi wewe ni Mungu ni zaidi ya vitu ninavyovipenda. sadaka
√husema ivi nakubaliana na icho ulichosema. thamani ya sadaka ipo katika moyo wako. mfano una elfu 10 katika elfu 10 ukatoa 500/= ukatoa sadaka
√swali la kujiuliza iyo uliyotoa inadhamani kwako wakati huo? kama haina dhamani basi haina dhamani kwa Mungu. mfano mke na mme. mme anataka
√ampelelee mkewe zawadi kabla ya kununua zawadi ataipima katika moyo wake. moyo wake ukiona haina dhamani basi ujue ndivyo jinsi mke wake ataipokea kwa
√kutoidhamani maana biblia inasema ajionavyo mtu nafsini kwake ndivyo alivyo. Bwana Yesu asifiwe sana! ila akivalue kwa furaha basi automatic mke
√wake ataivalue kwa furaha. sadaka ndivyo ilivyo haingalii thamani bali value katika moyo kwenye somo letu lilelile la roho ya uchache. sadaka zenyewe ni zipi?
i)Pale maji yanapotibuliwa unapanda mbegu. kwenye biblia utakumbuka lile birika watu walikuwa wakisubiri maji yatibuliwe na atakayewahi ingia ndio anaponywa. Haijafa
√maji kutibuliwa manaka pale roho mtakatifu anaposhuka kwa maombi, kwa neno, kwa sifa, Hapo hapo ndipo pazuri pakupanda mbegu yako. Na
√watu wamekremu vibaya ukipanda mbegu mara nyingi Mungu hukutengenezea mazingira siyo kukurudishia fedha.
ii) Dhabihu/shukrani
hapa watu wengi huwa husahau katika kila hatua Mungu anayokuvusha lazima ushukuru! iwe ni ufunuo
√umepata, neno umepata, maombi umepata moyoni mwako ukabarikiwa ukavushwa basi muhimu kushukuru. manake unamwambia Mungu
√asante fanya tena. unamwambia Mungu naweka msingi kwa hicho ulichokisema naweka kwa sadaka yangu.kila hatua usisubiri mafanikio ya
√mwisho yakupasa umshukuru Mungu. hapo unaweka msingi wa Kimungu katika muujiza wako. nakupa siri hapa! uamuzi uko.moyoni mwako kuchukua
au kuacha. Halleluyah!
iii)Zaka Malaki 3:10
hii fungu la 10 kama ni mwaminifu kutoa fungu
√kila pesa unayopata au kila kitu unachokipata dhamani yake unatoa fungu la 10, mfano mtu kakupa mikate 10 tafuta thamani yake ni 20000/= fungu
√la 10 lake ni 2000/= nia ya kutoa fungu la ni kuungana na moyo wa Mungu kupitia mtumishi wake! kumbuka watumishi wengi wa Mungu
√wanategemea sadaka ndipo waendeshe maisha yao.Mungu kawapa kibali kwenye huduma pekee,ivyo wakienda sehemu ingine hawezi fanikiwa. kila mtu
√anakibali sehemu Mungu aliyompa watumushi wamepewa baraka za watu ziko mikononi mwao! ila baraka za watumishi zipo
√mikononi mwa watu hii ndo system ya kimungu. nakupa siri hizi.ili ukitoa usitoe kwa daught jua unampa Mungu, ivyo ukiwa mwaminifu na Mungu naye
√atakuwa mwaminifu hataruusu uaibike. na unapanda katika udongo wewe unaokuletea matokeo.
iv) Malimbuko.
hii kila mtu anaijua siyo! malimbuko ya kitu chochote ambacho ni source ya mapato unatoa mara moja tuu na basi. ile faida ya kwanza yote pia unatoa katika udongo ule uliokuoteshea mbegu yako ikaanza kuchipua Bwana Yesu asifiwe.
√ Baada ya kujua hayo na umetimiza hayo ni haki yako Mungu kukujaza baraka! sasa hapo ndipo maombi yetu yanapoanzia kwa iyo
√ kama huko nyuma umewahi jikanyanga kanyaga basi utaomba rehema. sadaka ya lazima na sheria kwa Mungu ni fungu la 10, izo nyingine huwa
√tunatoa kuchota baraka za Mungu na kupanua hema, nakupata ulinzi wa Mungu, kupata kibali, kufungua kibali.Bwana Yesu asifiwe!
√Twende kwenye neno sasa kisha tukaombe!!!
Hagai 1:6
Yoeli 2:26
Isaya 49:4
√neno la maombi haya ni Isaya 49:4 hayo utayasoma pia ili kujenga imani yako juu ya kile tunachoenda kuomba! Halleluyah!
ISAYA 49:4
4 Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina Bwana, na thawabu yangu ina Mungu wangu.
4 Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina Bwana, na thawabu yangu ina Mungu wangu.
ISAYA 49:4
√Bwana Yesu nakushukuru sababu neno lako ni nguvu kwangu! maelekezo yako ni njia yangu! ahadi yako ni ushindi
√kwangu! Mungu Mtakatifu wa Israeli sitachoka kuyakiri maneno yako usiku na mchana maana neno lako kwangu ni
√taa, maneno yako kwako ni nuru kwangu, neno lako kwangu ni silaha ya vita kwa ibilisi. Asante Mungu kwa kuwa
√hukumu yako ndio haki yangu. Asante kwa kutokupendezwa na mimi kupata kidogo kidogo! Nami leo ninaomba hukumu
√yako leo kwa damu ya Yesu ya hukumu ya haki juu ya mimi kutokupata faida, sababu ya maonevu ya kazi ibilisi
√mapando ya ibilisi juu yangu. Kwa kuwa Bwana yapo matobo yavujishayo baraka zangu, ziko hila za ibilisi zikwamishazo
√baraka zangu, iko mipango ya ibilisi ya utasa, iko mipango ya ibilisi kuleta ukame katika uchumi wangu, yako maonevu
√Mungu ya kupoteza jasho
langu, vipo vifungo vya kunifanya mtumwa wa watu wengine, daraja la watu
√wengine kufanikiwa, Wako ambao Bwana wanafanikiwa kupitia vibali vyangu(nyota) na kusababisha kupata matokeo
√matone! matone! leo hii Bwana naomba hukumu yako juu ya roho za uharibifu wa mali, roho za upotevu wa pesa,
√roho za chuma ulete, roho za kutapanya fedha. Nami sasa kwa damu ya Yesu ninakemea kwa jina la Yesu nikiamuru roho za chuma ulete zitoke katika
√mikono yangu kwa damu ya Yesu, roho zote kinyonga, kutokupiga hatua, zitoke katika hatua zangu kupitia miguu kwa
√jina la Yesu, najifungua kwa damu ya Yesu uchawi wowote uliotumwa kufunga mikono yangu, kufunga miguu yangu
√najifungua kwa damu ya Yesu, uchawi wowote uliotumwa kumeza kibali changu, uliotu mwa kumeza pesa zangu,
√uliotumwa kunitia hasara, uliotumwa kupoteza pesa zangu kwa kupitia kufungwa akili Naachilia damu ya Yesu ya
√kuvunja uchawi, uchawi wote nauteketeza kwa moto roho Mtakatifu. imeandika Hesabu 23:23 hakuna uchawi juu ya
√Yakobo wala uganga juu ya Israeli. toka uchawi kwenye uchumi kwa jina la Yesu, imeandikwa kila silaha
√itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa kwa jina la Yesu, silaha yoyote ya nguvu za giza ya kunisababishia kupata
√matone! matone! ya faida naharibu nguvu zako kwa damu ya Yesu, nakuyeyusha kwa damu Yesu, nakupasaua kwa
√moto wa roho mtakatifu. mapepo yote ya kutapanya pesa, mapepo yote ya kutoboa fuko la baraka zangu kwa njia
√ya madeni, kwa njia ya uwizi, mapepo ya kunifunga akili, mapepo yote ya kunikandamiza kupitia matukio ya kupoteza
√pesa! mapepo yote yanayonyonya uchumi wangu kwa siri, mapepo ya kunikatisha tamaa, mapepo yote ya
√kinyonga, mapepo yote ya kobe, ya chura, ya utasa, ya mapooza, mapepo yote yanayosababisha uchache
katika juhudi zangu, mafanikio yangu leo kwa mamlaka ya jina la Yesu agano lenu nimelifuta kwa damu ya Yesu, nimelifuta
√kila mahali lilipoandikwa kwa kafara, kwa matambiko, kwa ukiri, kwa damu za wanyama na watu, kwa sadaka za miungu,
√iyo sheria jinsi ilivyoingia katika ulimwengu wa roho, iyo sheria popote ilipo naifuta kwa damu ya Yesu, naifuta kwa
√damu ya Yesu, kwenye vitabu vya kuzimu napitisha damu ya Yesu ninafuta jina langu huko. ewe sheria popote ulipo
√wasimamizi wa sheria hii, leo ninawamwagia damu ya Yesu ya hukumu ya haki, damu ya Yesu ya hukumu ya haki,
√ninaagiza moto wa roho mtakatifu juu ya mapepo yote juu ya mapepo yanayo sababisha uchache, popote
√pale moto wa roho Mtakatifu uwayaharibu! katika nchi kavu anga, katika bahari na chini ya bahari katika jina la Yesu Kristo. Ameen
rudia mara 7*
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment