MAOMBI YA KUJIFUNGUA VIFUNGO VINAVYOTOKANA NA ARDHI(MADHABAHU)
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
*ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
*Maombi haya ni hatari kwa ibilisi ivyo wakati unaomba unaweza ukawa unataka kushambuliwa, ivyo vaa silaha zote za kiroho pamoja na
*kutubu dhambi zako zote, kuokoka, kujifunika kwa damu ya Yesu na moto wa roho Mtakatifu. iwapo wakati unaomba ukahitaji msaada
*basi piga simu hapo chini. omba kwa ujasiri wala usiogope Yesu yuko nyuma yako. Na malaika wa Mungu wanakulinda.
Baba katika jina la Yesu ninakuja mbele zako mimi (taja jina lako) naja Kwako ndiko kuna msaada wa pekee! maana imeandikwa luka 1:37
kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Nami sawasawa na Marko 9:23 imeandikwe yote yawezekana kwake aaminiye! ni imani yangu
ni kwamba hata case yangu hii Bwana kwako inawezekana na ishawezekana. Mungu Baba wa mbinguni ninakushukuru kwa kunifanya mimi mwanao,
ninakushukuru pia uniponilinda tokea nimezaliwa kwa jina lako JEHOVA, asante kwa utetezi wako toka nilipozaliwa hadi hapa nilipofikia ewe Mungu wa
Mbinguni wewe ndio unayejua mapito yangu, misukosuko yangu, wewe ndo unayejua kutoka kwangu na kuingia kwangu na wewe ndo unayejua
nini kinaendelea katika maisha yangu, ninakurudishia utukufu Mungu mtakatifu wa Israeli maana umesema mwenyewe kuwa hakuna jambo lililofichwa
ambalo halitafichuliwa wala hakuna jambo lililositirika ambalo halitajulikana nami naamini sasa eee Baba wangu wa mbinguni ninapoanza safari
hii ya maombi utaanza kuongea na kuzungumza kuhusu maisha yangu. Roho Mtakatifu nakukaribisha katika maombi haya! Bwana Yesu naungana
na wewe katika maombi! haya! pia natangaza katika ulimwengu wa Roho kuungana vita katika ulimwengu wa Roho na Roho Mtakatifu na Bwana Yesu
ninakubali kuongozwa na Roho atakayombesha katika ulimwengu wangu wa roho kupitia kinywa changu mimi katika jina la Yesu! Baba kabla ya kuanza maombi
haya naomba kutengeneza na wewe katika jina la Yesu, Baba wa mbinguni mtu yoyote aliyeniumiza katika maisha yangu NINATANGAZA KUMSAMEHE, ninasahau uovu
aliyonifanyia katika jina la Yesu! ninasamehe na kusahau watu wote walionitia katika matatizo niliyonayo. ninatangaza na kumsamehe
mama yangu mzazi, ninatangaza na kumsamehe Baba yangu mzazi! ninatangaza kumsamehe na kumwachilia mme wangu,
ninatangaza na kusamehe watu wote walionijeruhi na kuniumiza katika maisha yangu, maana imeandikwa hasira haitendi haki ya Bwana,
pia imeandikwa mtu asiweke hasira ndani yake hata jua kukuchwa, ivyo ee Bwana kwa kutambua hukumu zako ni za kweli na ziko kwako Bwana pekee, na kwa
kutambua ya kwamba kuweka uchungu wa hasira ndani yangu ni kukuzuia wewe kunisaidia, ni kukuwekea wewe ukuta wewe wa kunisaidia maana kwa
kufanya hivyo tayari ninakuwa nimetenda kazi yako ya hukumu ivyo leo kwa neema ya Yesu, na kwa uwezo wa damu ya Yesu, leo ninawafuta watu wote
katika moyo wangu walionijeruhi moyo kisha hukumu zote za hasira au uchungu ndani yangu nakuachia wewe. Neno la Mungu linasema msipowasamehe watu makosa
yao, Baba yenu wa mbinguni pia hatawasamehe, Ee Mungu Baba mtakatifu wa Israeli, ninaomba neema ya kuwasamehe wote Bwana wako walioniudhi! na nimewabeba
katika moyo wangu na nimewashikilia katika moyo wangu na ikanisababishia uchungu ndani yangu na ndiyo ikawa njia ya mapepo kupita,
kwa kutambua uchungu na hasira ni njia ya mapepo kupita, kwa kutambua kwamba nisipo wasamehe watu walionikosea Pia Baba yangu wa mbinguni
hatanisamehe! kwa iyo hata maombi haya hayatafika leo ninaomba unirehemu Mungu. leo ninatangaza kuwaachia kabisa leo ninatangaza kuwasamehe, ninawafuta wote
katika moyo wangu kwa damu ya Yesu! Roho wa uchungu na hasira mmenisikia hana kibali tena cha kushika moyo wangu maana watu wote
nimewasamehe ivyo ondoka kwangu sasa kwa jina la Yesu.
Mungu Baba wa mbinguni leo ninakuja kwako kwa ajili utakaso kamili maana nishawasamehe walionikosea basi nimezingatia sheria ya kusamehewa ninaomba
unirehemu katika jambo lolote Mungu nililotenda aidha likageuka laana au maagano katika maisha yangu, ninaomba rehema ninatubu mbele zako Mungu mtakatifu wa Israeli
Mungu usiyeshindwa! umesema "naam mimi ndimi mimi niyafutaye makosa yako yote kwa ajili yangu mwenyewe wala siyakumbuki tena" Baba sasa
ninaomba unirehemu ninaomba unisamehe! ninaomba unitakase, ninatubu mbele zako kia uovu mbele zako niliyoutenda, kila sheria zako
nilizozivunja, na kutokufuata maagizo yako ninaomba unisamehe unirehemu katika jina la Yesu! unisamehe
katika jina la Yesu. mimi mjoli wako Bwana leo ninashuka chini, leo niko jalalani, katika matope sifai hata kutizamwa na wewe, unaponiangilia maisha
yangu unaona niko uchi unaona uovu wangu eee Mungu mwenye wingi wa rehema na neema ninaomba unisamehe, ninaomba unitakase, naomba
ufute makosa yangu yote! ninaomba unirehemu Mungu. uovu wangu umegeuka mateso yangu mwenyewe, laana zimenipata kwa ajili ya kukutenda dhambi ninaomba
unisamehe naomba unirehemu katika jina la Yesu Kristo! unisamehe Baba katika jina la Yesu Kristo na kwa damu ya Yesu Kristo. Baba leo nasimama kama kuhani
nehemia 12:30 ninaishika kwa imani ardhi ya asili yangu ardhi ya asili ya Mama yangu ardhi ya asili ya Baba yangu ninaomba uirehemu hii ardhi
Bwana! Ee Mungu Baba kwa imani mkononi mwangu nimeshika ardhi ya asili ya Mama yangu,Baba yangu ambako mimi ni asili yangu, pale
(pataje) kwenye asili yangu mimi penye asili ya mama yangu,Ya Baba yangu penye muunganiko wangu mimi,tokea kwa mama,tokea kwa Baba Ee Mungu uliyehai hii
case wewe pekee ndio wa kuimaliza! Baba hii ni ardhi ambayo tumefanya kila aina ya dhambi, hii ndo ardhi ambayo tumefanya ushirikina,
tumetambika,tumeweka mazindiko,tumefanya maagano na ibilisi, hii ndo ile ardhi ambayo mizimu ilikabithiwa kwangu kwa maagano ya kuzaliwa kwangu,
hii ndo ardhi ambayo tumejiwekea ulinzi wa kipepo
mafanikio ya kipepo, hii ndo ardhi ambayo kuna dhambi zote chafu tunazitenda tumefanya uasherati, tumezini, tumeuwa kwa kuchukua nyota
za watu, tunatembea ndugu kwa ndugu, tunawanga, tunauchawi, tunafuga majini, tunaabudu sanamu, tunaabudu miungu mingine, tunampinga
Kristo katika ardhi hii tuna laana za kila aina, tunavita katika ndoa, ee Mungu Baba tumeishi kwa ushirikina, tumetengeneza madhabahu za
ibilisi katika ardhi hii, tumefungua malango ya ibilisi katika ardhi hii, hii ndo ardhi Bwana Yesu iliyokabithiwa maisha yangu, ikakabithiwa
elimu yangu, ikakabithiwa kazi yangu, ikakabithiwa ndoa yangu, hii ndo ardhi iliyofunga ndugu zangu, ndo ardhi iliyo mfunga mama yangu, Baba tangu hii ndo ardhi iliyomfunga maisha yetu,
hii ndo ardhi ambayo majini mahaba wamekabithiwa kwetu kupitia madhabahu! hii ndo ile ardhi ambayo miungu inatufuatulia kutulazimisha
kuutumikia, Ee Mungu hii ardhi imefunga maisha yetu, Hii ndo ardhi iliyofunga ndugu zangu, hii ndo ardhi iliyofunga mikono yote, hii ndo ardhi ambayo
imefunga miguu yetu, hii ndo ardhi ambayo roho za mauti zinatufuatilia, roho chafu kupitia mapepo zinatufuatilia kupitia hii
ardhi hii niliyoishika, hii ndo ardhi yenye madhabahu wanayonifuatilia ndotoni, wanatulisha ndotoni, hii ndo ardhi ambayo ibilisi kupitia hii
ardhi kupitia madhabahu anatuzonga na roho za uchungu, mateso, kutokusamehe, kukataliwa, Eee Mungu Baba ninaomba unisamehe, tunaomba
utusamehe! tunahitaji Bwana uiponye hii ardhi yetu ili tuwe huru, ninaomba Mungu utusamehe! ninaomba Bwana ututakase kwa damu yako! ewe ardhi ya
asili yangu pale (pataje) asili ya mama yangu,Asili ya Baba yangu nakunywesha damu ya Yesu, nakunywesha damu ya Yesu, nakunywesha damu ya Yesu!
katika jina la Yesu. Ee Mungu naomba uiponye hiii ardhi kwa damu ya Yesu, Kwa damu ya Yesu! ninatubu kila dhambi juu ya hii ardhi ya asili yangu mimi kwa damu ya Yesu! kwa damu ya Yesu.
Eee Baba wa mbinguni hii ndo ardhi ambayo vitovu vyetu vimeunganishwa kupitia hii madhabahu, nywele zetu zimeunganishwa kupitia madhabahu, hii ndo ardhi
ambayo kucha na meno yetu ya kwanza, nguo za ndani au sehemu yoyote ya miili yetu tumeungamanishwa kupitia madhabahu, hiii ndo ile ardhi
ambayo tumeunganisha kupitia
chale za wachawi! Ee Mungu Baba ninaomba toba siku ya leo! hii ndo ardhi ambayo tumefungiwa katika miti
mikubwa! hiii ndo ardhi ambayo tumezikwa kupitia makaburi,
tumekabithiwa kwa mizimu, na sasa Baba wanatusumbua! Baba naomba toba kwa ajili ya hii ardhi naomba uirehemu sasa! naomba uitakase kwa damu ya
Yesu, uitakase kwa damu ya Yesu! ewe ardhi
wa asili yangu leo nakunyesha damu ya Yesu! damu ya Yesu! nakutakasa kwa damu ya Yesu!
Bwana Yesu hii case sasa naileta kwako kwa damu ya
Yesu, Bwana Yesu nahitaji kuwa huru! naitaji nikutumikie kwa uhuru katika jina la Yesu, Case hii ya ardhi ya kwetu
Bwana Yesu haya mashitaka nayaleta kwako, katika mahakama ya mwanakondoo, nayaleta kwako, nayaleta kwako! naomba hukumu yako Bwana Yesu kwa damu ya Yesu.
Ninanyunyizia damu ya Yesu katika ardhi ya kwetu (pataje) ardhi ya asili yangu kule kwa Baba yangu ninaomba hukumu yako sasa Bwana Yesu katika jina la Yesu! Kwa damu ya Yesu.
Bwana Mungu wa majeshi ninanyunyizia damu ya Yesu katika malango yote adui aliyoyamiliki kwa maagano mbalimbali kwa sheria za
mikataba, kwa laana, kwa kafara, kwa damu za wanyama, kwa damu za watu, kwa maagano aina yote ninamwaga damu ya Yesu katika malango
hayo katika ardhi ya asili yangu pale (pataje) kule kwa Baba yangu, ninamwaga damu ya Yesu katika ya asili yangu, Damu ya Yesu iende katika kiini cha asili yangu,
iende katika kuta za asili yangu ninaomba hukumu yako Bwana Yesu, ninaomba hukumu yako Bwana Yesu. Nimemwaga damu ya Yesu ya hukumu sasa! juu ya wote waliotushikilia
waganga wa kienyeji, wachawi, mizimu ya ukooo damu ya Yesu ya hukumu ya haki ipo juu yenu sasa! damu ya Yesu ya hukumu ya haki ipo juu yenu sasa wote mnaonijia nikiwa kazini, nikiwa
nyumbani! usingizini Bwana Yesu nimemwaga damu ya Yesu ya hukumu ya haki sasa! Bwana Yesu ninaomba hukumu yako ya haki juu ya miungu, mizimu, waganga wa kienyeji!
wachawi wote wanaonikalia katika jina la Yesu, Bwana Yesu hata kama sikuwataja hapa ila wanatumia nguvu za giza kunidhuru ee Bwana Yesu
ninaomba damu ya Yesu ya hukumu ya haki sasa. Damu ya Yesu ya hukumu iwe juu yao sasa katika jina la Yesu. Kwa damu ya Yesu.
Asante Bwana Yesu kwa huu ushindi mkuu kwa kuwa utafanya zaidi nilivyoomba na zaidi ninavyofikiria. Sifa na Heshima zirudi kwako Bwana Yesu kwako pekee. Ameen
Rudia mara 7*
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete