MAOMBI YA KUJIWEKA HURU MAENEO MBALIMBALI
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
leo tutumie Warumi 8:31
"Basi tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu?"
Baba Katika jina la Yesu, ni kweli wewe ukiwa upande wangu ni nani aliye juu yangu? Eee Mungu neno lako ni moto ulao, na mimi moto.ulao, Mungu
neno lako ni nyundo na mimi ni nyudo yako, neno lako Mungu ni shoka na mimi ni shoka lako la kukatia nguvu za giza, neno lako Mungu ni panga na mimi
napanga lako, neno lako Mungu ni nyundo na mimi ni nyundo yako, neno lako Mungu ni rungu na mimi ni rungu lako! katika jina la Yesu! naongea na wewe ibilisi wewe ni nani wa
kunijia mimi na Mungu yuko upande wangu, umepata wapi maagano ya ibilisi ya kunigusa na mimi ni
mwana wa Mungu, wewe uchawi wa mfundo wewe, wewe mizimu ya ukoo, naongea na nyie kwa damu ya Yesu,
wewe hofu, wasiwasi, wewe mashaka, wewe jini wewe, wewe roho chafu ya ibilisi wewe
ninakakutuma kwangu kwangu unitese? nani kakuambia uje kwangu hivi
unajua Mungu yuko upande wangu? nyie wa wachawi hivi mnajua Mungu yuko upande wangu, wewe
kifungo hivi unajua Mungu yuko upande wangu? Mungu akiwa upande
wangu unajua nini Mungu kile atakufanya?sikiza ibilisi majini yako, mapepo yako, mizimu yako, roho
zako chafu, walinzi wako wa kipepo, makuhani wa madhabahu, wachawi, waganga wa kienyeji, wafalme wa giza, wakuu wa giza,
mamlaka za giza, jeshi la pepo wabaya, majoka ya baharini yote, na wote wanaotumika chini ya shetani
ninakuangalia kupitia jicho la Mungu, nani kawatuma mnipinge? nani kawatuma mfunge njia zangu,
nani kawatuma mpindishe njia zangu, nani kawatuma mfunge biashara yangu, nani kawatuma mtumie nyota yangu! hivi mnajua
Mungu yuko upande wangu, nani kawatuma nyie roho chafu? mnajua nimebeba mamlaka ya Mungu, mnajua kitu Mungu atawafanya? nami
sasa kwa hasira ya roho mtakatifu katika jina la Yesu ninamwaga damu ya Yesu, katika ardhi, katika anga, katika bahari hata chini ya
bahari! ya kuwakamata! ibilisi nakujia kwa damu ya Yesu, nakujia kwa moto ulao, nakujia kwa shoka la Mungu, nguvu ya hofu nakuteketeza kwa moto, nguvu
ya mikosi balaa nakufyeka kwa upanga huu wa warumi 8:31 kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu, adui
yoyote mbele yangu nakamata shingo nakufyeka kwa jina la Yesu, nawalipua kwa moto! falme za giza nazisambaratisha kwa moto,
malkia wa anga nakusambaratisha kwa moto, malkia wa bahari nakusambaratisha kwa moto,
mapepo wachafu, mapepo wabaya nawasambaratishwa kwa moto kwa jina la Yesu,
ninaamuru mlipuliwe mtoke majivu kabisa kwa jina la Yesu, uchawi wowote uliotumwa kwangu naudaka
kwa moto kwa jina la Yesu, naudaka kwa damu ya Yesu, ewe uchawi nakualipua kwa moto,
nakusambaratisha kwa jina la Yesu, Bwana Yesu! vita vyovyote tokea baharini, ardhini, angani, chini ya
bahari vilivyoelekezwa kwangu kwa damu ya Yesu, kwa jina la Yesu, navilipua kwa moto, nawalipua
kwa moto, nawateketeza kwa jina la Yesu, nawafyeka wachawi kwa upanga, nawafyeka majini yote kwa
shoka, nafyeka mapepo kwa upanga, nafyeka roho chafu zote kwa upanga, nafyeka majoka yote kwa upanga, hao
wanaotumia nyota yangu nawafyeka kwa upanga, hao walionikalia wanafyeka kwa upanga, nawaaangamiza kwa moto,
nawalipua kabisa kwa jina la Yesu, mkononi mwangu nimeshika silaha hatari ya warumi 8:31, maadui wote wa siri nawafyeka kwa upanga
nawangamiza kabisa , nawalipua kwa moto maadui wote wa maisha yangu, nawapinga kwa damu ya Yesu, yoyote aliye juu yangu naamuru kuangusha chini kuteketezwa kwa upanga,
kuteketezwa kwa upanga kwa jina la Yesu, kwa damu ya Yesu! leo ninakiri Mungu yuko upande wangu hivyo hakuna aliye juu yangu. wote watakao jiinua watafyekwa kwa jina la Yesu. Ameen.
rudia mara 7*
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment