MAOMBI YA KUMNGOA IBILISI KWA MOTO

*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.

ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.

Zakaria 2:5 Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.

√Halleluyah Halleluyah! hili neno ninapolifikia huwa najisikia mkubwa zaidi

√ya malaika wa Mungu kwa umbo. ukisoma ufunuo utakuta na stori hii

√yupo malaika mmoja aliweka mguu mmoja baharini mwingie nchi kavu alafu mikono yake akaielekeza kwa Mungu akiapa mbele

√za Mungu kabla ya kushusha kipigo. you can imagine alikuwa mkubwa kiasi gani! malaika mmoja wa Mungu anaweza kuwa na umbo la ukubwa wa

√viwanja vitatu vya mpira urefu na upana. sasa embu fikiria malaika hao ndio unaowatuma katika uchumi, sijui ndoa, kazi, nakwambia

√shetani atafanywa kuni, alafu unajisikia more power more energy ni kama BULLDOZER yani hakuna cha kusimama mbele yangu! sasa utamu wa hili neno ni kwamba

√ unalikiri hawa Roho wa Mungu ambao wanawaka moto mda wote wanaenda sehemu husika na kuteketeza kila kitu kwa moto. Halleluyah! Halleluyah!

Tulitafakari kidogo:
anasema nami nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, Biblia kuna

Sehemu inasema kama jinsi watu walivyozungukwa na milima mimi nami nitaizunguka Yerusalemu kwa moto

Huu moto unapokuzunguka nakwambia hakuna wa kukushika! shida ni kwamba huu moto una

uachia kwa shetani tuu, inakupasa kuachilia kila mahali adui anapatafuta apafungue, mfano malango yako, nyayo zako za miguu, mikono

mipango yako, akili yako, fahamu yako, mawazo yako, ulimi wako, sauti yako, macho yako! uchumi wako kila mahali! unapofanya hivi

kwa kukiri hata kama kuna wageni ndani yako watakimbia hawawezi kaa. Achana kabisa na moto wa Mungu. Halleluyah Halleluyah!

Anza kwa kuomba rehema kwanza!

Baba katika jina la Yesu asante kwa neno lako linalosema " Kwa maana mimi asema BWANA nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake"

Neno lako ni kweli neno lako Roho nami sasa nakiri iyo pumzi iliyopo katika neno ambayo ipo ndani yangu ambayo pia ndio neno lako! nami nakiri huo ukuta wa moto kwa neno sasa huo ukuta wa moto

umezunguka  hata kazi yangu ewe kazi yangu wewe ni ukuta wa moto .wa Mungu ninaamuru kila kisicho na utukufu wa Mungu ndani ya kazi kumezwa sasa na moto wa Mungu kwa jina la Yesu.

Ewe ndoa yangu wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, ninaamuru kila kisicho utukufu wa Mungu ndani ya ndoa yangu kumezwa sasa na moto wa Mungu kwa jina  la Yesu.

Ewe Kibali changu wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, ninaamuru kila kisicho na utukufu wa Mungu ndani ya kibali changu kumezwa sasa na moto wa Mungu kwa jina la Yesu.

Ewe Huduma yangu, biashara, kazi za mikono wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, ninaamuru kila kisichokuwa na utukufu wa Mungu ndani yake kumezwa sasa na moto wa Mungu kwa jina la Yesu.

Ewe mafanikio yangu wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, ninaamuru kila kisichokuwa na utukufu wa Mungu ndani ya mafanikio yangu kumezwa sasa na moto wa Mungu kwa jina la Yesu.

Ewe elimu ya yangu wewe ni ukuta wa moto wa Mungu,ninaamuru kila kisicho na utukufu wa Mungu ndani ya Elimu yangu kumezwa sasa na moto wa Mungu kwa jina la Yesu.

Ewe afya yangu wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, ninaamuru kila kisicho na utukufu wa Mungu ndani ya afya yangu kumezwa sasa na moto wa Mungu kwa jina la Yesu.

Ewe uchumi wangu wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, ninaamuru sasa kila kisicho na utukufu wa Mungu ndani ya uchumi wangu kumezwa sasa na moto wa Mungu kwa jina la Yesu.

Ewe  Hatua zangu wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, naamuru chochote kisicho na utukufu wa Mungu ndani ya Hatua zangu kumezwa sasa na moto wa Mungu kwa jina la Yesu.

Ewe nafsi roho na mwili wangu wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, ninaamuru chochote kisicho na utukufu wa Mungu ndani ya roho nafsi na mwili wangu kumezwa sasa na moto wa Mungu kwa jina la Yesu.

Ewe ulimwengu wangu wa roho wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, ninaamuru sasa chochote kisicho na utukufu wa Mungu ndani ya ulimwengu wangu wa roho kumezwa sasa kwa jina la Yesu.

Ewe malango yangu mimi, wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, ninaamuru chochote kisicho na utukufu wa Mungu ndani ya malango yangu kumezwa sasa na moto wa Mungu. kwa jina la Yesu.

Ewe kibali juu ya nchi na chini ya mbingu yangu mimi wewe ni ukuta wa moto wa Mungu, ninaamuru chochote kisicho na utukufu wa Mungu juu ya vibali vyangu juu ya nchi na chini ya mbingu kumezwa sasa na moto wa Mungu. Kwa jina la Yesu.
AMEEN!

Rudia mara 7 maombi haya

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA