MAOMBI YA KUMUOMBA MUNGU KUKUONGOZA KWENYE FAIDA
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
17 Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
Isaya 48:17
√ leo tutakiri hili neno kisha utaona nguvu yake kupitia damu ya Yesu, neno lolote linalokuja kwako usichukulie kama faraja! shetani hupenda kuchanganya watu kuona aaah uyu anatufariji tuu! lakini nakwambia chukua
√neno kama funguo! chukua ilo neno lipeleke katika situation yako! anza kuwaza msaada wake juu ya tatizo lako! usisikilize kelele za jaribu bali sikiza, na kuwaza jinsi ilo neno linavyokukusaidia, watu wamekuwa wazito kuamini maana wanaona ni maandishi
√ lakini ungejua kinachotokea ungeheshimu na kutetemekea neno! neno ukiliamini na likaa ndani yako hilo neno haliondoki litatua changamoto iyo na ya aina iyo! unapokiri neno na kuliamini! malaika waliopewa sheria ya ilo neno huja hadi kwenye tatizo lako na kuanza kutoa msaada.
√ usipobadilisha ukiri wako wanaendelea hatua kwa hatua hadi kukutoa! tatizo saa izi tumekiri jioni tumefuta ivyo husababisha malaika wako anakuwa kazini kazi haijaisha kaacha.
Maombi:
√ Baba katika jina la Yesu, asante leo umenikumbusha na kunifundisha kuwa wewe ndiye UNIFUNDISHAYE NA KUNIONGOZA ILI NIPATE FAIDA, kama jinsi Baba unifundishavyo na kuniongoza ndivyo jinsi shetani naye hufanya kinyume cha kunifundisha na kuniongoza nipate hasara! leo
√ katika jina la Yesu nakataa kuongozwa na shetani kwa jina la Yesu, nakataa marafiki wa shetani kwa jina la Yesu, nakataa marafiki wabaya wa shetani kwa wanangu kwa jina la Yesu, nakataa ndugu wote wa kunileta hasara nawatenga nami kwa jina la Yesu,watu wowote waliopandikizwa na ibilisi katika maisha yangu ili
√ waniletee hasara na ibilisi nawasambatisha kwa jina la Yesu, nawatenga nami kwa jina la Yesu, nakataa fikra za shetani kwa jina la Yesu, nakataa mawazo ya shetani kwa jina la Yesu, nakataa vishawishi vya shetani kwa jina la Yesu, nakataa kuongozwa na shetani katika maamuzi yangu
√ kwa jina la Yesu, nawakataa roho za uchawi, roho zote za maagano zinazoniongoza katika hasara nazikataa kwa jina la Yesu, nakataa maamuzi ya shetani ya kunitumbukiza katika hasara katika jina la Yesu, nakataa mawazo ya ibilisi yatakayonipelekea kuvunja ndoa yangu, kuuwa biashara yangu, kufukuzwa kazi, kushindwa kufikia hatma yangu, kushindwa kupiga hatua kila
√mtego wa shetani kwa maneno, kwa matendo, kwa maandishi, kwa ukiri, kwa mawazo , wa matendo utakaonipelekea kunaswa katika hasara nakukataa kwa jina la Yesu, naufyeka kwa jina la Yesu, kila uvuvio wa kipepo na ufuniko wa kichawi unaonisukuma katika kutenda dhambi, utakaonipelekea kuniletea mikosi,balaaa, hasara
√ kwa jina la Yesu, shetani toa mkono wako wa hasara katika roho yangu, toa mkono wako wa hasara katika nafsi yangu, toa mkono wako wa hasara katika mwili wangu, toa mkono wako wa hasara katika uchumi wangu, toa mkono wako wa hasara katika ndoa yangu, toa mkono wako wa hasara katika nyumba yangu! toa mkono wako wa hasara katika afya yangu, ninakataa kila
√mitandao ya hasara katika maisha yangu, iyopo ardhini, angani, baharini, kwa jina la Yesu, kila wachawi wanaokaa kunipangia hasara nawasambaratisha kwa damu ya Yesu, kila hasara katika maisha yangu naitangazia imeshindwa kwa jina la Yesu,
Mungu Baba leo nakubali na kuongozwa na wewe! ninakiri na kukubali kufundishwa na wewe! ewe roho ya Mungu ya kunifundisha na kunielekeza katika faida njoo sasa kwangu kwa damu ya Yesu, njoo katika kazi yangu, mawazo yangu, biashara yangu,ndoa yangu, uchumi wangu, njia zangu, nakukaribisha roho ya faida kwa jina la Yesu, roho ya kufanikiwa nifunike sasa kwa jina la Yesu, roho ya
√ kuongezeka nifuke sasa kwa damu ya Yesu, roho kuona mafanikio nifunike sasa kwa jina la Yesu, Roho ya kusikia habari njema nifunike sasa kwa damu ya Yesu. Roho ya mafanikio ya juu nifuke sasa kwa jina la Yesu, ninakiri roho hawa wa Bwana wapo juu yangu sasa Kwa jina la Yesu! wamenifunika sasa! na watanifundisha na kuniongoza katika faida kwa jina la Yesu, katika maisha yangu, katika ulimwengu wa
√ roho! Roho Mtakatifu naomba sasa unifundishe na kuniongoza sasa katika faida katika jina la Yesu na kwa damu ya Yesu. Roho ya kunifundisha na kuniongoza njoo kila kona ya maisha yangu sasa nakukiri sasa kwa jina la Yesu Kristo. Asante Bwana Yesu maana imekuwa. Ameen
rudia mara 7*
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment