MAOMBI YA KUMWOMBA MUNGU MAELEKEZO YA NJIA YA KUKUFANIKISHA
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
√ tafakari fupi kuhusu neno la leo, watu baada ya kuomba sana hufikiri pengine Mungu hawasikii, au maombi hayajafika, Au maombi yao hayawezi kusukuma ilo tatizo, Au wanadhambi sana, au hawana upako wa kusukuma tatizo, wengine huamisha imani zao katika maji, mafuta, sabuni, sticker, au chochote kile! badala imani yake aiweke katika neno! by the way ivyo vitu havifanyi kazi bila imani ya neno! ukitumia bila neno la Mungu inakuwa haina tofauti
√na kitu umepewa kwa mganga! lazima ivyo viwe attached na neno la Mungu, na haitafanya kazi bila neno la Mungu! ikifanya kazi bila neno la Mungu basi jua si cha Mungu. kutokana na hali iyo wengine imani zao wameziamishia kwenye jina la Mtumishi badala ya neno la Mungu linalotokana na mtumishi. usiweke imani yako kwenye jina la mtumishi weka imani yako kwenye neno la Mungu linalotoka kwa mtumishi
√ Mungu hujibu kila siku Mungu huendelea kujibu! Mungu huongea tatizo sisi hatusikii! Mungu ana lugha zake! ivyo ukitaka kusikia Mungu anakujibu nini lazima baada ya kuomba uwe attentive kujua Mungu anasema nini! muhimu kujua lugha za Mungu, aidha kasema kwa kinywa cha mtumishi, au kasema kwa matukio, au kwa ndoto, au kwa maono, au kwa picha, au kwa sauti kabisa ndani yako. kwa ishara, kwa kutumia body language Mungu huongea kwa njia nyingi, tatizo sisi tunajua njia
√moja tuu ya maongezi ndio maana tunasema Mungu yupo kimya.Mungu huongea! kama umeomba hujasikia chochote basi tatizo liko kwako! shetani anatabia ya kuwadanganya watu Mungu anakupitisha kwenye majaribu ndio maana yupo kimya! si kweli, hata ukipita kwenye majaribu ataongea tuu Mungu. Halleluyah! Halleluyah!
maombi yanayokuja hayatakuwa mapya kwa Mungu! tutamkumbusha ili Mungu aseme tena. ni kitu ambacho nimekipractice katika maswali 12
√niliyomuuliza Nikaja jikuta maswali 11 kumbe Mungu alishanijibu tena hata kabla ya kuuliza! sasa akaniambia wafundishe watu iko kitu. jina la Bwana libarikiwe sana.
15 Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. ISAYA 49:15
Maombi:
√Baba katika jina la Yesu asante kwa kuwa leo kwa neno lako utaenda kunifungua mahali nilipokwama! umesema ya kuwa kamwe huwezi kunisahau mimi mfinyanzi wako! Nami nakushukuru kwa ahadi iyo nzuri kwangu, maana
√najua upo pamoja nami no matter what! Nami Bwana nimekuwa nikikusibiri unijibu maombi yangu kwa ishara kumbe wewe Baba hujibu watu wako kwa maelekezo! na maelekezo hayo huwa katika
√sauti yako, na huongei kama binadamu, huongea kwa kutumia kila kitu, Baba nami ninasubiri unijibu kwa njia za kibinadamu, asante Bwana Yesu kwa ufunuo huu!
√Mungu mtakatifu wa Israeli ninaomba rehema leo Baba najua wewe ni Mungu unayeongea God who speak, nirehemu katika jambo lolote ambalo haikupendezi katika jina la Yesu, kila mashataka mbele yangu ninaungama
√naomba unisamehe Bwana katika jina la Yesu, Ninaomba unitakase kwa damu ya mwanao Yesu Krisro! katika jina la Yesu! Ee Mungu Baba katika jina la Yesu ninaomba unisamehe pale ulipoongea sikukuelewa Bwana, pia Bwana
√yako mambo yaliyosababisha mimi kutokusikia! nirehemu kwa kutokutulia uweponi mwako, nirehemu kwa kiburi cha uzima ndani yangu, nirehemu kwa kuweka uchungu na hasira ndani yangu,
√nirehemu kwa kutokusamehe walionikosea, nisaidie Bwana Yesu na unibadilishe tabia zangu, na unipe tabia zako katika jina la Yesu, ili nianze kusikia sauti yako Mungu.kila dhambi ambayo ipo ndani yangu na ipo nje yangu kwa kujua ama kutokukujua iliyosababisha
√ukuta katika maisha yangu, nirehemu Bwana katika jina la Yesu! nirehemu kwa kujiungamanisha na mitandao ya ibilisi ambayo imeniwekea ukuta wa kutokusikia katika jina la Yesu, nami leo huo ukuta naubomoa sasa kwa damu ya Yesu! Baba neno lako ni kweli
√Baba huwezi nisahau mimi mjoli wako Bwana, kama ulimtoa mwana wako wa pekee kwa ajili ya kunikomboa iweje ujeunisahau leo, na umenitoa misri kwa gharama kubwa Bwana Mungu wa Majeshi Ee Mungu Baba ninaomba unisamehe katika
√jina la Yesu, tatizo lipo kwangu ndio maana leo nakugeukia wewe Mungu wa kweli kwa ajili ya utakaso kamili, nisamehe Bwana katika jina la Yesu.nitakase kwa damu ya Yesu, nitakase kwa damu ya Yesu! nioshe Bwana! nisamehe Bwana! katika jina la Yesu.
√Ee Mungu Baba umesema katika neno lako isaya 49:15 lakini mimi sitakusahau wewe, nami najua Mungu hujasahau maombi yangu niliyokuletea mbele zako katika jina la Yesu, na ninajua ushayajibu ee Mungu wa milele naomba leo unipe tena maelekezo Nami nitakusikiza katika jina la Yesu, Roho Mtakatifu nisaidie niitambue! nitafakari, nielewe sauti ya Mungu.
√Mungu naomba maelekezo juu ya maombi yangu ya kupata kazi katika jina la Yesu, Mungu Baba naomba leo unipe maelekezo juu ya maombi yangu ya tatizo la ndoa yangu katika jina la Yesu, Mungu Baba naomba leo unipe maelekezo juu ya maombi yangu ya tatizo la uchumi wangu katika jina la Yesu, Mungu Baba naomba leo unipe maelekezo juu ya maombi ya yangu ya changamoto ya biashara
katika jina la Yesu, Mungu Baba naomba leo unipe maelekezo juu ya maombi yangu ya changamoto juu ya kazi, kazi za mikono, huduma yangu jina la Yesu, Mungu Baba leo naomba unipe maelekezo juu ya maombi yangu ya changamoto juu ya nguvu za giza zinazonifuatilia katika jina la Yesu, Mungu Baba naomba leo unipe maelekezo juu ya maombi
√yangu juu ya changamoto ya mahusiano kwa jina la Yesu, Mungu Baba leo ninaomba unipe maelekezo ya maombi yangu dhidi ya watoto wangu katika jina la Yesu! Baba asante kwa kuwa nitaanza kupokea maelekezo hayo sasa maana hutanisahau, wala hujawahi nisahau Mungu mtakatifu wa Israeli! Mungu Baba leo
√naomba unipe maelekezo juu ya maombi yangu dhidi ya hofu, wasiwasi, mashaka, sintofahamu katika jina la Yesu, Mungu Baba leo ninaomba unipe maelekezo juu ya maombi yangu ya muelekeo wa maisha yangu, na njia nitakayoifuata katika jina la Yesu, Mungu Baba ninaomba leo
√unipe maelekezo juu maombi yangu ya changamoto katika uchumba katika jina la Yesu, Mungu Baba leo naomba unipe maelekezo juu maombi yangu changamoto dhidi ya vifungo katika jina la Yesu. Asante Bwana Yesu kwa roho wako wa kunikumbusha haya maelekezo ninakiri wako juu yangu sasa, nitasikia sauti yako sasa, maana masikio yangu ya rohoni, na macho yangu ya rohoni yamefunguka sasa
√katika jina la Yesu, maana Bwana Yesu umesema lakini Mimi Mungu wako sintakusahau. Asante Bwana Yesu kwa kutonisahau! na maelekezo ninayangoja sasa! sema nami Bwana, teta nami Bwana sauti yako ndio faraja yangu, maelekezo yako ndio njia yangu, neno lako ndio ushindi wangu. Sema nami Mungu katika jina la Yesu!Asante kwa Roho wa hekima yuko juu yangu sasa! Roho wa maarifa yuko juu yangu sasa!Asante kwa Roho wa uweza!Asante kwa Roho wa kumcha Bwana! Na asante kwa Roho wako Mtakatifu wako juu yangu sasa katika jina la Yesu. Ameen
rudia mara 7*
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment