MAOMBI YA KUNGOA MAPINGO YA CHUMA NA MILANGO YA SHABA KATIKA VIBALI

*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.

ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.

Isaya 45-2

"nitakwenda mbele yako, na kupawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukatakata mapingo ya chuma"

√ Bwana Yesu tukaangalie hilo neno kwa undani wake alafu tukaombe kupitia hilo neno! unajua biblia inakila kitu wapendwa! ni sheria ya kuishi hapa duniani. ndo njia pekee ya kufanikiwa.

√Rudia hayo maneno nitakwenda mbele yako kupasawazisha mahali palipo paruza! alafu akaelezea jinsi atakavyo pasawasisha kwa

√kukatakata  mapingo ya chuma na kuvunja vunja vipande milango ya shaba. kumbe tunachokipata hapa au kwanini Mungu kasema hivi ni

√sababu adui akitaka kukuparuza katika njia yako basi huwafunga watu na milango ya shaba na mapingo ya chuma. milango ya

√shaba manake ni milango migumu iliyofunga kwa ajili yako, mapingo ya chuma ni pingu anazopigwa mtu ili asisogee! ni kama vile mfungwa

√anapigwa pingu mkononi na miguuni kisha bado mlango wenyewe ni wa shaba

√ uliomfungia maana huu ni mzito mgumu zaidi ya wa chuma umefungwa ili usitoke

√kabisa.sasa hali hii ipo katika ulimwengu wa Roho! ndo mana wengi wanahangaika hawasogei

√hapo alipo ni hapohapo! havuki, akitaka kuvuka anarudi nyuma, yani yupo kifungoni! mtu wa namna hii atafanya

√maombi ya vita ya kila
namna lakini usipojua siri hii nakuambia utabaki umefungwa maana hatushindi kwa

√kuomba tuu no tunashinda maarifa na hekima za Mungu. kwa iyo ni aina ya vifungo ambavyo ni superior

√ kabisa. na Mungu amejua watu wangu watakwamia hapa! amejua kabisa hawawezi kusogea

√hapa! ndo mana kaahidi kuwa nitayaondoa hayo mafungo ili uweze kuwa huru! ili uweze kuvuka. mapingo haya ya

√shaba na ya chuma yapo kabisa katika ulimwengu wa roho nakuambia inaweza kukufunga sehemu moja tuu na ukakwama

√hapo. haikufungi kila mahali mara nyingi inashikilia labla kipengele cha uchumi huvuki, inashikilia kipengele cha ndoa huvuki, au kipengele cha

√ajira, au uponyaji kitangangana na wewe hasa alafu unashangaa kila unalolifanya juhudi zote bado! unajiuliza nimemkosea wapi

√Mungu? kumbe hujawahi kufunguliwa kuna mapingo ya shaba na mapingo ya chuma Bwana Yesu Asifiwe sana! iyo ndo

√anayozungumzia mahali palipoparuza yeye atapasawazisha, kuna mambo kwa kweli bila Mungu kuingilia kati basi huwezi vuka!

√lazima Mungu vifungo kama hivi avingoe mbele yako ili wewe uweze kupita unakimbia! Bwana Yesu asifiwe! kinachofanyaga kazi ni

√maombi ya namna hii ya ukiri wa neno la Mungu nakuambia ukiomba maombi haya shetani atakukimbia, hakuna ambaye atakiri neno kwa

√kuomba na abaki alivyokuwa. weka akilini kila unavyoomba basi kuna tofali unaliweka juu katika maisha yako! na vizuizi vinasukumwa

√nyuma! na ushindi upo karibu sana. ila unapooacha kuomba shetani anabomoa ukuta wako anajenga wa kwake na hali yako inakuwa mbaya

√zaidi ya kwanza. ivyo mtafute Mungu usichoke! wala usisikize nafsi yako inakuambia nini wala izo kelele ndani yako za

√shetani. Bwana Yesu asifiwe kiri hili neno kwa kuomba na utajisikia kuishi tena. tukakiri kwa kuomba sasa!

Tukaombe Sasa;

ISAYA 45-2
"nitakwenda mbele yako, na kupawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukatakata mapingo ya chuma"

Baba katika jina la Yesu asante kwa maarifa ya rohoni na mwilini, kupitia neno lako umenijulisha kuwa yapo

mapingo ya chuma na milango ya shaba, na hivi vinafungwa katika vibali vya mtu ili asifanikiwe, ili asipite, ndicho

ulichokiita mahali pakipoparuza. kwa neema yako kuu ya ajabu Mungu wangu umeahidi kututoa hapo

kutuvusha hapo asante Yesu. Maana maisha yetu yameparuzika! na bila wewe hatuwezi enda, bila wewe

hatufiki! nami eee Mungu sina tofauti kama hao wengine mimi sina akili kuliko hao wengine, si mwaminifu kuliko hao wengine,

sina  haki kuliko hao wengine, bali mimi ni matope yako tuu, mimi ni kazi yako tuu, wewe ni mfinyanzi wangu, mimi ni

udongo wako, katika kiganja chako sienei wala sitoshi wala sitakaa nitoshe, nina madhaifu yote kama binadamu, nina

mapungufu kama binadamu, mbele zako Mungu wangu si kitu zaidi ya udongo uliotengeneza katika viganja

vyako ninashuka chini kabisa mbele zako, Bwana ninaomba rehema katika kunena kwangu, katika kutenda kwangu katika

katika kuwaza kwangu nimekukosea mbele zako mimi ni mwenye dhambi wewe ni mwenye haki ninaomba

unisamehe Mungu, ninaomba unitakase kwa damu ya Yesu, ninaomba unitakase kwa damu ya Yesu, Baba nimekosa mbele

zako, naoomba rehema, naoomba unisamehe! ninatubu Baba! nirehemu Baba nitakase kwa damu ya Yesu, nioshe

Baba nisafishe Baba kwa damu ya Yesu, Ee Mungu wa neema na Rehemu Mungu wa haki, naomba unihesabie tena haki

kwa damu ya Yesu, kwa damu Yesu, katika laana yoyote iliyonipata sababu kutenda dhambi, ikatoa mlango wa

mapingo ya chuma na malango ya Shaba kukakwaza katika vibali vyangu leo hii naomba rehema Bwana katika jina la

Yesu, Baba wa milele popote penye mapingo ya chuma na milango ya shaba katika ndoa palipo paruzika ninamwaga

damu ya Yesu ya kupasawazisha kwa jina la Yesu ya kufungua mafungo hayo sasa katika jina la Yesu,

popote penye mapingo ya chuma na milango ya shaba katika vibali vyangu palipo paruzika ninamwaga damu ya

Yesu ya kupasawazisha kwa jina la Yesu, juu ya ardhi na chini ya mbingu katika jina la Yesu Popote penye mapingo ya

chuma na milango ya shaba katika uchumi wangu ninamwaga damu ya Yesu ya
kupasawazisha kwa jina la

Yesu, juu ya ardhi na chini ya mbingu kwa jina la Yesu, Baba popote penye mapingo ya chuma na milango ya shaba

katika kazi, huduma, biashara palipo paruzika ninamwaga damu ya Yesu ya kupasawazisha juu ya ardhi na

chini ya mbingu kwa jina la Yesu, Baba popote penye mapingo ya chuma na milango ya Shaba katika hatua zangu

kufanikiwa kwangu ninamwaga damu ya Yesu ya kupasawazisha sasa juu ya ardhi na chini ya mbingu kwa

jina la Yesu, Baba popote penye mapingo ya chuma na milango ya shaba juu ya kupata nafasi za kazi, juu ya kupata mtaji,

kupata tenda kupata fursa, nafasi ya kusoma, school fee, scholarship ninamwaga damu ya Yesu, ya kupasawazisha

juu ya ardhi na chini ya mbingu kwa jina la Yesu, Baba popote pale penye mapingo ya chuma na milango ya shaba katika

uponyaji wangu ninamwaga damu ya Yesu ya kupasawazisha juu ardhi na chini ya mbingu kwa jina la

Yesu, Baba popote pale penye mapingo ya chuma na mlango wa shaba katika kufikia hatma yangu, katika kufikia mda

wangu wa kufanikiwa, katika mda wangu kupata kile Mungu anachotaka nikipate, katika kumaliza elimu yangu, katika

mda wa kupata watoto, katika mda wa kuwa na ndoa, katika mda wa kuwa na familia, katika mda wa kujifungua kwangu

nina imwaga damu ya Yesu ya kupasawazisha majira na nyakati za Bwana ambazo zimeliwa na nzige kufungua

mapingo hayo juu ya ardhi na chini ya mbingu kwa jina la Yesu. Baba popote pale penye mapingo ya chuma na milango

ya shaba katika kununua kiwanja katika kujenga katika kumalizia kujenga, katika kuanza jambo lolote katika

kumalizia jambo lolote ninamwaga damu ya Yesu ya kupasawazisha juu ya ardhi na chini ya mbingu kwa kwa jina la

Yesu, Baba popote pale penye mapingo ya chuma na milango ya shaba katika kupiga hatua, katika kuendelea katika

kutanua hema, katika kuongezeka ninamwaga damu ya Yesu ya kupasawazisha juu ya ardhi na chini ya mbingu

katika jina la Yesu. Baba mahali popote penye mapingo ya chuma na milango ya shaba kipengele cha Elimu

ninamwaga damu ya Yesu ya kupasawazisha juu ya ardhi na chini ya mbingu katika jina la Yesu.Baba popote pale penye

mapingo ya chuma na milango ya shaba katika kufunguliwa kwangu katika nguvu za giza ninamwaga damu ya Yesu ya

kupasawazisha juu ardhi na chini ya mbingu kwa jina la Yesu. Baba asante kwa sababu
umeahidi kufanya zaidi

tuombavyo na zaidi tufikiriavyo! ivyo popote ambako sikupakumbuka au kupataja
ninamwaga damu ya Yesu

Kristo ika locate juu ardhi katika anga na baharini, mahali
hapo palipoparuzika penye mapingo ya chuma na malango

ya shaba ninamwaga damu ya Yesu ya kupasawazisha sasa kwa  jina la Yesu juu ya ardhi na chini ya mbingu katika jina la
Yesu Ameen.

rudia mara 7*

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA