MAOMBI YA KUONDOA WATU WABAYA KATIKA MAISHA YAKO
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa
lipo neno zuri sana hapa tuangalie tukalikiri!
Yeremia 15:21
21 Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha.
√Nami nitakukomboa na mkono wa watu wabaya! Halleluyah! Halleluyah! Halleluyah! mkono wa watu wabaya ni huu! ni wale
√wanaokuendea kwa waganga kufunga maisha yako, ni wale wanaokutolea sadaka kwa shetani ili wafunge ndoa yako,
√ili ufukizwe kazi, ni wale wanaokufunga kizazi, ni wale wale wanazika makaburini kazi yako, biashara yako, ni wale
√wanaofunga mikono yako ili ushindwe kumiliki, ni wale wanaofunga miguu yako ili ushindwe kupigwa hatua, ni
√wale wanaenda kutoa kafara kwa waganga ili pepo likuingie katika moyo lijigeuze ugonjwa, ni wale wanaokuja usiku
√kukulisha chakula na wewe unaota unakula nyama chapati, au uko kwenye sherehe kisha hujui kuwa umelishwa. uchawi.
√na kuna watu hawaamini uchawi upo! hapo duniani ibilisi hana njia ingine isipokuwa uchawi. Ndo mana bila neno
√haupo salama! bila neno haupo salama. maana malango yako wanaingia wanavyotaka! matatizo yote hapa duniani
√yamesababishwa na uchawi. mkono wa wenye kutisha ni watu wenye hila wanaokuchekea machoni lakini
√ndani yao wamejaa hila za kukuangamiza. ukiwaambia mipango wao wanafikiri jinsi ya kukurudisha nyuma. Biblia
√imeandika adui wa mtu yu nyumbani kwake wengine hawaamini! kuwa mtu unayeishi naye anaweza kuwa
√anakuwazia mabaya. lakini Neno la Mungu linauweza wa kutambua mawazo mabaya hila mbaya. Kama huna neno
√moyoni mwako wewe ni kondoo katikati ya mbwa mwitu wakali. na huwezi amini hicho nachokuambia sababu ibilisi
√kawekeza ili usifunguliwe, kawekeza katika akili yako fikra zako ili nuru isije kukuzukia ukaifahamu kweli. Bwana Yesu
√asifiwe! leo tutaenda kuondoa mikono ya watu wabaya. tutaenda kujitenga na mikono yenye watu wa kutisha. lazima
√umwambie roho Mtakatifu akuchagulie marafiki usiambatane na kila mtu! mwingine atasema mtumishi
√mshamba anataka kutupangia hata marafiki, lakini nataka kukuambia Mungu anakujua kuliko unavyojijua, anajua
√chanzo cha tatizo lako. shetani hupandia watu wabaya katika maisha ya watu. ili kuharibu miujiza, au baraka. chunguza
√rafiki uliyenaye au mtu unayeambatana naye anakupeleka rohoni kwa Mungu au anakurudisha nyuma,
utajikuta si msengenyaji baada ya mda unaanza kusengenya na kukaa katika vikao vya usengenyaji, utakuta ulikuwa
√hunywi pombe unaanza gafla kunywa pombe, ulikuwa huna mchepuko na wewe unaanza tafuta mchepuko, na wewe
√umeokoka, angalia anakokupeleka uwe mwangalifu, sehemu zingine zina maagano ya kuzimu. mtoto
√wa Mungu kabla ya kufanya chochote anamuuliza Mungu kwanza. sio ushamba bali ni kwa usalama wako. Leo
√tutaenda kumuambia Mungu aondoe magugu yote! na Mungu akikutenga na watu wabaya uwe tayari, kutii,
√usinganganie! huwezi jua kwanini neno hili leo limekuja.Bwana Yesu asifiwe! ivyo baaada ya maombi haya watu
√wote wabaya watatengwa na wewe, sasa usiwe kinganganizi utajiangamiza mwenyewe.Biblia inasema ibilisi yule baba
√wa uwongo amejaa hila nyingi.
21 Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha. Yeremia 15:21
Tuombe sasa!
Baba katika jina la Yesu asante kwa ufunuo wa kunijulisha kuwa kuna mikono watu wabaya, pia watu wenye kutisha, Leo Mungu neno lako
katika jina la Yesu litaenda kuniokoa na kuniweka huru. maana watu nimezungukwa nao na sijui ndo wale walioandikwa katika Yeremia
15:21, ninao makazini, wapo kwenye biashara zangu, wapo kwenye familia yangu, wapo kwenye ukoo wangu, wapo nyumbani kwangu, wapo kila
mahali na wamenizunguka na si rahisi kuwatambua! isipokuwa kwa neno lako ambalo ni upanga ukatao
kuwili, bila kujua niwafunulia
mipango yangu, nimewashiriki sha mambo yangu, na ndio wamekuwa wakitumiwa na ibilisi, wamekuwa ukuta katika maombi yangu, hatua zangu,
wamenyonya kiroho, kiuchumi, ndio wamekuwa wakinishauri, na mara ingine nimekuwa nikiwaamini sana. Leo Bwana kwa neno lako hili najitenga
nao bila majuto yoyote katika jina la Yesu. Baba nasogea mbele zako leo kwa damu ya Yesu, katika jina la Yesu ninaomba rehema katika
jambo lolote Baba katika jina la Yesu. ninaomba rehema kama mimi mwenyewe kwa namna moja au nyingine niligeuka mtu mbaya mmoja wao! ninaomba
unisamehe unitakase kwa damu ya Yesu, ninaomba rehema kwa kutokusikiza sauti ya roho Mtakatifu, mara nyingi amekuwa akinikanya kwa watu
wabaya au makundi lakini bado sijamtii, leo Mungu ninaomba unirehemu unisamehe katika jina la Yesu, najitakasa kwa damu ya Yesu. naomba
unihesabie haki tena kwa damu ya Yesu. katika jina la Yesu Kristo, sasa Bwana kwa neno lako ninaenda kuwatenga watu wote wabaya katika maisha
bila kujutia kamwe katika jina la Yesu Kristo. Mungu Baba watu wote wabaya wanaotumika na ibilisi au niliwakaribisha wenyewe katika ndoa yangu,
familia yangu, ukoo wangu,
kazini, katika biashara, katika huduma leo hii ninawangoa kwa damu ya Yesu, najitenga nao kwa moto wa roho
Mtakatifu, watu ninaoshirikiana mambo mbalimbali kumbe wana hila na mimi! majirani katika mtaa wangu, majirani nyuma niliyopanga, watu
ninaosoma nao, ninawatenga kwa moto wa Mungu, tunashirikiana katika huduma, au kuabudu nao sehemu moja mapando yote ya ibilisi
ninayangoa kwa moto katika jina la Yesu, ndugu wa upande wa mme au upande wa mke ambao ni mapando ya ibilisi ninawangoa kwa damu ya
Yesu, najitenga nao kwa damu ya Yesu! wote wenye hila na mimi! wote wenye mikono yenye hila, wote wanaotisha najitenga nao kwa damu ya
Yesu, najitenga nao kwa moto wa roho Mtakatifu, ewe rafiki mbaya, ndugu mbaya, mtu yoyote mbaya katika maisha yangu najitenga nawe kwa
damu ya Yesu! kwa moto wa Roho Mtakatifu, Baba kila magu gu watu au mtu ambayo ni ya ibilisi
nayangoa kwa damu ya Yesu. najitenga nao kwa moto wa roho mtakatifu. Katika jina la Yesu. Ameen.
rudia mara 3*
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment