MAOMBI YA KUVUNJA MAUTI KATIKA VIBALI

MAUTI NA UZIMA

*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.

ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. Methali 18:21

*Bwana Yesu asifiwe!

√Kitu chochote kilichokuwa na kibali gafla kibali kikafa basi jua ya Kwamba kimetamkiwa mauti wala usihangaike, huo ndio ukweli, nitakufundisha kitu kimoja leo na uweke katika bank yako.Shetani bila dhambi hawezi kukufanya lolote ndio maana anawekeza ili wewe utende dhambi, dhambi ni mlango wa mapepo kupita. shetani akitaka kufunga kibali chako lazima atamke mauti. unajua shetani inawezekana anaitumia biblia kinyume chetu zaidi ya sisi tunavyotumia kinyume chake

√Kila neno kwenye chukulia ya kuwa limetumwa kumfungua mtu sehemu flani. Hili neno lipo kwa ajili ya kutangua mauti! ibilisi anachofanya anatamka mauti tuu, nikupe siri shetani akitaka kukufunga usiwe na kibali atakachofanya hayo mawazo atayaweka kwa makuhani wake yani,wachawi watatafuta uhalali wa kukufunga wewe kwa kupitia dhambi uliyofanya, kupitia iyo dhambi sasa watafanya maagano na kuzimu, yani kuruusu mapepo kukuletea uharibifu.

√(maagano ya kichawi) kwa kufanya kafara au kupitia dhambi hapo ndipo sasa ibilisi hufunga kibali cha mtu. Siri ingine shetani siku hizi hufanya kazi kupitia nje ya mtu, yani si lazima akae ndani wanajua akikaa ndani atakemewa na kuondoka! ivyo wanakujengea ukuta na kufanya kazi yao unashangaa mtu kaokoka na anaishi kwa shida vibali vimeondoka, ndo mana nasisitiza maombi ya namna hii ni bulldozer, Asante Yesu maana anatoa maarifa na hekima za kutosha za kumpindua shetani! ni wakati wa kudili na chanzo cha tatizo! kama wachawi wanafunga kibali kwa kutamka tuu, mapepo yakafunga, pia wewe uliyeokoka unauweza wa kutamka tuu uzima na malaika wa Mungu wakaenda kufungua.

√Bwana Yesu asifiwe! ni wakati kanisa wa kuomba kwa maarifa, nakwambia ibilisi ana hila nyingi ndani ya jina la Yesu siri zote zinafichuliwa na anapigwa anapigiga vizuri tuu na anachia maisha yako na unafanikiwa jina la Bwana libarikiwe. Haya maombi ni ya Roho Mtakatifu ni maombi mimi nayaita BULLDOZER hayaaichi kitu! wewe jaribu tuu kwanza utaona Yesu akibadili ulimwengu wako wa Roho. Halleluyah! Halleluyah!

√Leo tutaenda kutamka uzima katika ndoa, biashara, kazi, vibali, na  mambo yote, na Roho Mtakatifu atatusaidia kuomba tutaingia mpaka ndani kabisa kwa uweza wa jina la Yesu. ibilisi kuna vitu vingi sana kavifunga kupitia vinywa vya wachawi, Biblia inasema ingia mpaka vilindini ukatweke samaki, na leo tutaingia mpaka vilindini kwa jina la Yesu. neno la Mungu ni Roho unapolitamka kwa imani, linakaa attention linasubiri instruction ya pili, unapolielekeza sasa linaenda mpaka sehemu husika, linapoenda hapo linakutana na roho wa mauti amekaa iyo sehemu wale roho wa mauti ni wa giza wanapoona roho wa Mungu wenye mwanga na moto wanakimbia na akisha kukaa sasa uyo Roho wa uzima anaanza kufanya kazi sasa. ivyo amini unapoomba!

√ Tutaomba na tutaenda kumkaribisha Roho wa uzima. Na Roho wa Mungu wako saba (7) waje juu yetu.Hawa Roho wanakaribishwa. Na hawa roho wanapokuwa kuwa juu Yetu basi hakuna tena mauti juu yako na hapo lazima ufanikiwe! Halleluyah! Halleluyah! nampenda Yesu simwachi. Asante Roho Mtakatifu kwa siri hizi.

sema; nampenda Yesu simwachi. alafu tukaombe!

√Baba katika jina la Yesu ninakushukuru kwa kujifunza tena katika neno, mauti na uzima huwa katika uweza ulimi, leo nimetambua ya kuwa kibali huondolewa kwa kutamkiwa mauti! nimegundua pia roho wa uzima ni Roho wa Mungu, roho wa mauti ni roho ibilisi, nimegundua pia jinsi vile roho wa mauti huweza funga kibali, basi pia roho wa uzima ya Mungu hufungua kibali asante Bwana Yesu.

√ Leo hii nakiri kinywa changu kina mamlaka ya mbinguni ya kuruusu mauti na uzima, yani kufungua kibali na kufunga vibali, pia nimegundua pia wanaofunga vibali ni roho wa mauti, wanaofungua vibali ni roho wa uzima! nimejua pia kibali cha mtu kisichoonekana au kilichofichwa au kupotezwa ilo hufanyika kupitia maagano ya kichawi wa roho wa mauti wa ibilisi. Na leo hii kwa neno hili neno la Mungu ni Roho nami nawaruusu Roho wa Mungu kufanya kazi sasa upande wangu, neno la Mungu ni moto naweka moto katika ulimi wangu sasa, neno la Mungu shoka ninaweka shoka katika ulimi wangu, neno la Mungu ni panga ninaweka pango hilo katika ulimi wangu sasa! neno la Mungu ni moto ulao, ninavaa moto ulao sasa, Neno la Mungu hufanya kazi kupitia damu ya Yesu, nami naunganisha damu ya Yesu yenye mamlaka katika ulimi wangu.

√Ee Mungu Baba katika jambo lolote nililokutendea dhambi naomba rehema naomba unitakase kwa damu ya Yesu, unirehemu Mungu katika jina la Yesu! unirehemu Mungu katika jina la Yesu aidha kwa kufungulia mauti katika maisha au yangu au kufunguliwa na watu naomba unisamehe katika jina la Yesu ninamwaga damu ya Yesu ya utakaso katika lango hilo kwa jina la Yesu. Mauti yoyote iliyotamkwa katika kibali changu ninaifuta iyo mauti kwa damu ya Yesu, ninatamka uzima ndani ya kibali changu kwa jina la Yesu. Mauti yoyote iliyotamkwa katika hatua zangu naifuta iyo mauti katika hatua zangu natamka uzima katika hatua zangu kwa jina la Yesu.
mauti yoyote iliyotamkwa katika ndoa yangu naifuta iyo mauti kwa damu ya Yesu, ninatamka uzima katika ndoa yangu kwa jina la Yesu.

√Mauti yoyote iliyotamkwa katika kazi yangu au kazi za mikono,biashara, au huduma yangu naifuta kwa damu ya Yesu, natamka uzima katika kazi zangu kwa jina la Yesu, Mauti yoyote iliyotamkwa katika uchumi wangu naifuta kwa damu ya Yesu, natamka uzima katika uchumi wangu kwa jina la Yesu, Mauti yoyote iliyotamkwa kwangu kunileta taarifa mbaya, hofu aidha nimeona au kusikia ninaivunja kwa damu ya Yesu,  ninatamka uzima ndani yangu wa ujasiri na habari njema kwa jina la Yesu, mauti yoyote iliyotamkwa ya magonjwa tokea kwa wachawi au sehemu yoyote naifuta kwa damu ya Yesu,

√ natangaza uzima wa afya yangu kwa jina la Yesu, mauti yoyote iliyotamkwa ya kunifunga katika vifungo aina yoyote, naifuta kwa damu ya Yesu, natangaza uzima wa uhuru kwa jina la Yesu, Mauti yoyote ya laana katika maisha yangu iliyotamkwa sehemu yoyote naifuta kwa damu ya Yesu, natangaza baraka katika maisha yangu yote kwa jina la Yesu, Mauti yoyote ya maisha magumu, ufukara, kuchanganyi wa, mapooza, utasa, roho ya kuchelewa kufika, roho zozote za ugumu wa maisha za ibilisi nazifuta kwa damu ya Yesu, natangaza uzima katika mpenyo, kufanikiwa, maisha bora, upendeleo wa Ki Mungu, natangaza uzima wa furaha kwa jina la Yesu, uzima wa ama ni, uzima wa kujitosheleza katika mahitaji kwa jina la Yesu, natangaza uzima wa utele kwa jina la Yesu! Asante Bwana Yesu maana  ulimi wangu umekiri hayo! kwa neno ambayo ni roho wa Mungu wameenda kutekeleza sasa kwa jina Yesu.

Bwana Yesu naenda kuwakiri  Roho wako wa uzima sasa!  wawe juu yangu sasa katika jina la Yesu, Na kwa damu ya Yesu! Roho wa uzima wa afya nifuke sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa ndoa nifuke sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa uchumi nifunike sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa kibali nifuke sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa kupiga hatua nifunike sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa amani nifunike sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa kazi, kazi za mikono, biashara, huduma nifunike sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa elimu Nifunike sasa kwa jina la Yesu,

√Roho wa uzima wa ujasiri nifunike sasa kwa jina la Yesu. Roho wa uzima wa kunifanikisha nifuke sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa kiroho nifunike sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa baraka, upendeleo, mpenyo wa ki Mungu nifunike sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa kuzaa, kuongezeka nifunike sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima wa kutengeneza njia nifunike sasa kwa jina la Yesu, Roho wa uzima, Roho wa kumcha Bwana,Roho wa Maarifa, Roho wa ufahamu,  Roho wa shauri  Roho wa uweza, nifuke juu yangu sasa katika jina la Yesu.  Asante Bwana Yesu kwa Roho wako kipitia damu ya Yesu najifunika sasa, wako juu yangu sasa katika jina la Yesu na tokea leo hii nakiri kwamba hakuna roho ya mauti itakayofunika maisha yangu tena kwa jina la Yesu, kwa kuwa sasa nimetangaza na kuwakiri Roho wa Bwana wapo juu yangu sasa, Asante Bwana Yesu imekuwa katika jina la Yesu na damu ya Yesu.

rudia mara 7*

endelea kukiri na kuomba maombi haya kwa mda mrefu

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

  1. Amina kwa maombi mazuri. Naanza kuyafanyia kazi leo,Natarajia ushindi kwa jina la Yesu naamini. Mungu anishindie yote. Barikiwa sana Mtumishi
    .

    ReplyDelete
  2. Asante mtumish kwa Maomb mazuri Mungu na atende sasa nakiri kuvunja roho za mauti. Yesu ni Bwana

    ReplyDelete
  3. Asante sana na roho wa mauti,majeneza na makaburi aondoke kwa jina layesu christo

    ReplyDelete
  4. Haya maombi yananguvu sana roho wa Mungu mwenyewe anashuka. Nimeanza kufatisha niko ofcn nimejikuta nashindwa kutamka nikawa natetemeka sana namshukuru sana Mungu. Mungu akubariki mtumishi

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA